MY DIARY (27)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mtunzi: __
SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Alinamba eti hayo ya mimi kuolewa tuyaeke pembeni na kwa nini siku hiyo nisilale Moshi tukumbushie enzi zetu. Mwalimu John aliendelea kusema kuwa amenimiss sana na anomba nisahu yaliyopita na turudie yale maisha yetu ya zamani.
TUENDELEE...
Nilijifanya simwelewi lakini ukweli ni kwamba nyota ya mwanaume huyu ilikuwa ni kali sana zaidi yangu na ningekuwa nimekunywa pombe mambo yangeweza kuwa rahisi kwa upande wake.
Kama aligundua vile akamwita muhudumu na kumwambia aniletee Saint Anne wine kama ile aliyoninywesha siku ya kwanza ya mimi na yeye kufanya mapenzi. Kwa wale wasiokumbuka ilikuwani Tanga hiyo tulipoenda kufanya ziara ya utalii kwenye mapango ya amboni. Niliendelea kusimama na msimamo wangu kuwa mimi sinywi pombe na natakiwa kuondoka nimuwahi mume wangu. Mwalimu John akasema hata kama hunywi mletee chupa nzima ataibeba.
Basi nikaletewa chupa nzima ya wine. Mmmmh uzalendo ulinishinda nikajikuta naomba glass na zoezi la kuponda mali kufa kwaja likaendelea. Wakati tukiendelea waliingia watu wawili ambao walionekana kama mume na mke hivi. Na kwa kuwa sehemu nyingi zilikuwa zimejaa waliamua kuvuta kiti na kukaaa pembeni yetu yaani tulikaa meza moja. Kuangalia vizuri walikuwa ni Mary na Joseph wanafunzi ambao tulikuwa tunasoma nao darasa moja nilipokuwa chuoni.
Kwa kweli ilikuwa ni zaidi ya furaha na hapo nikaamini msemo wa Kiswahili usemao milima haikutani bali binadamu wanakutana.Tulisalimiana kwa kukumbatiana na kumwacha mwalimu John akishangaa.
Hawa watu walikuwa wakipendana sana na tulipoingia tu chuoni wiki ya kwanza mahusiano yao ndo yalianza. Basi furaha ikaongezeaka kwa meza na pombe zikaendelea kunyweka. Sikujua nini itakuwa hatima yangu usiku huo je nitaenda Arusha au nitachukua chumba na kulala Moshi au nitaenda kulala na mwalimu John.
Wazo la kulala na Mwalimu John nilikuwa silipi nafasi kwa sababu moyo wangu ulikuwa na kinyongo kikubwa kutokana na mabaya aliyonitendea. Basi katika stori za hapa na pale Joseph akampigia rafiki yake ambaye na yeye tulisoma nae na pia yeye alikuja na demu wake. Nikajisemea tazama ilivyo vyema na kupendeza ndugu wakikaa pamoja kwa upendo na amani. Basi stori za kukumbushia maisha ya chuo ziliendelea. Stori hizo zilinitia machungu kwa sababu sikubahatika kumaliza masomo ya chuo kutokana na majanga ya maisha yalitotokea
Saa yangu ya mkononi ilionesha kuwa ilikuwa ni saa tatu usiku na bado athma yangu ya kwenda Arusha ilikuwepo pale pale. Nilijua kabisa ikifika saa nne naweza kupata magari yanayotoka mbeya kwa maana ndo magari yaliyokuwa ya mwisho kupita moshi. Mwalimu John kweli alikuwa na hela maana hizo raundi alizokuwa akizipiga wewe acha tu. Kitu kinachoitwa sifa ni kibaya sana huku duniani. Mara Mwalimu akatoa wazo tuhame, alisemaa “ jamani leo kuna mahali wanapiga laivu bend kwa nini tusiende huko tukamalizie hii siku ya furaha kwa marafiki kukutana” Alisema hivyo mara baada ya kuona wahudumu walikuwa wakisua sua. Ikumbkwe na mimi wakati ho nilishabadilisha kinywaji na nilikuwa nakunywa zile bia zangu za bei mbaya.
Kosa kubwa lilofanyika mwanzoni mimi nilimtambulisha mwalimu John kama mme wangu ili angalau na mimi nionekane kuwa nipo kwenye sytem. Hivyo nikawa na shindwa kuaga na kuondoka maana sasa utaondokaje na kumuacha mumeo. Hoja ile ya kuhamia sehemu ingine iliungwa mkono na watu wengi.
Joseph aliunga mkono hoja kwa kusimama na kumpa mkono Marry wake, na Marry akasimama tayari kwa kuondoka. Basi wote wakasimama tayari kwa kuondoka nikabaki mimi tu ndo nimekaa.
Huyu mwalimu John alikuwa ni mjanja sana yeye alijifanya kwenda chooni.Hapo nikazidi kuchoka zaidi ukizingatia walijua kabisa alikuwa ni mume wangu.
Nikajiuliza sijui nimzalilishe tu kwa kumkataa au niende nikale bata na baadaye nichukie chumba na kulala mwenyewe. Basi niliaamua kukata sahuri la kubaki na nikaamua kumwandikia Joyce meseji na kumwambia kuwa siku hiyo sitarudi kwa kuwa asubuhi nataka nirudi kule kijijini hivyo nimelala Moshi.
Hapo Joyce alinipiga kabisa tukaongea kwa kirefu. Alisisitiza kuwa niwe makini na nisikubali kulala na mwanaume kama tulivyokubaliana mpaka hapo nitakapo pata mwanaume wa kunioa. Yaani huyu mwanamke alikuwa na machale sana sijui halihis nini.Nilimwahakikishia kuwa sitaweza kufanya ujinga wa namna yeyote ili na mimi nisije nikajikwaa kama yeye na kupata hili gonjwa lisilo na tiba. Basi kwa kuwa kila couple ilikuja na gari yake ndivyo tulivoondoka na kwenda sehemu moja iliyoitwa Mr Price City.
Hiyo sehemu nazani ilikuwa ni mpya kwa sababu mimi na ujanja wangu wote nilikuwa sijawahi kufika. Tulipanda ngazi kwa sababu sehemu hiyo ilikuwa ni ghorofani. Tukapata sehemu nzuri tukaaa huku tukiendelea kunywa vinywaji huku tukiburudishwa na burudani nzuri ya live bend. Mawazo ya kurudi Arusha yalishatoweka na hapo ikawa ni kula bata tu. Baadaye mida ilivyokwenda watu wote waliondoka na tukabaki mimi na mwalimu John. Akaniuliza tunaenda kulala kwangu au tuchukue chumba na kulala mjini?
Hapo nilimcheka sana na kumwambia hivi yeye haoni aibu kusema upuuzi huo mbele ya mke wa mtu. Hapa nikawa nimempandisha hasira zake. “Yaani kama ulikuwa unayajua yote hayo ulikuwa unasubiri nini kuondoka ukakaa mpaka usiku huu.” Alilalamika mwalimu John. Nilimjibu kwa kumwambia ndo hivyo niliamua kukutunzia tu heshima kwa sababu ya wale marafiki zangu. Nikaongeza kumwambia kuwa “ na una bahati sana ingekuwa na wao sio mke na mume ungenikuta nishafika Arusha’
Sawa nimekuelewa sasa na wewe unaenda kulala wapi? Aliuliza mwalimu John.Nikamjibu popote tu ambapo kuna vyumba vya kulala wageni. Alikaaa kimya kama dakika mbili kisha kuniambia “ mimi ni msomi bhana siwezi kulazimisha mapenzi kwa hiyo twende nikupeleke Dar Street maana kule ndo kuna guest nyingi sana. Nikamwambia huko mbali sana twende nipeleke hapo KNCU kuna room nzuri hata kama ni ghali nitalipa ili nilale tu. Akanambia sawa anaheshimu mawazo yangu kwa kuwa mimi ni mtu mzima.
Nikamwambia kwanza kutoka hapo tulipokuwa hadi KNCU si mbali hivyo yeye aniache tu mimi nitachukua bodaboda. Msimamo huo ulimshangaza sana maana alishazoea kuwa nikinywaga pombe nakuwa mjinga mjinga. Hakuamini kilichokuwa kinatokea na nilivaa sura ya kazi. Nilimuonea huruma sana lakini sikuwa najinsi nikikumbuka yale yote mabaya aliyonifanyia. Ndio nilikuwa na ugwadu wa mda mrefu lakini sikutaka kujirahisisha hasa kwa mtu ambaye alishindwa kunisaidia wakati wa shida hasa kodi na kusababisha nikaangukia kwenye mikono ya baba mwenye nyumba.
Tulishuka ngazi na tulivyofika nje mimi niiita tax.Kitu hicho hakikumfurahisha kabisa ikabidi atumie nguvu kuniingiza kwenye gari lake. Sikukata niliingia na kumwambia nipeleke CRDB bank nikatoe hela. Na yeye kwa kuwa alikuwa amekasirika hakutaka kubishana na mimi alinipeleka na nikatoa hela. Tukaingia kwenye gari na badala ya kunipeleka hotelini yeye alinyoosha na kunipitiliza. Nikajua kuwa alitaka kutumia nguvu kunipeleka nyumbani kwake. Nikamwambia hata akitumia nguvu na kunipeleka kwake ajue kuwa hataweza kufanya mapenzi na mimi kwa kuwa nilikuwa katika siku zangu za gari la mshahara.
Kauli hiyo ilimuingiza upepo na kuniambia “ ujue sa hivi ni usiku wa saa nane hivo ananooenea huruma kuwa nitapoteza bure hela yangu kwa kulipia chumba. Nikamjibu kwa kumwambia afuate ninanvyo mwambia kwa kuwa popote atakaponipeleka nitawapigia simu polisi na hatoaamini kitakachotokea. Kwa nini usiwe muelewa niliendelea kuongea kwa jazba.Basi ukijumuisha na zile stori za mimi kwenda rumande na hivi wale wanachuo walikuwa wanasema kuwa kilichoniweka huru ni umaarufu wangu ilibidi mwalimu John awe mpole na kugeuza gari kisha kuipeleka sehemu niliyohitaji. Tulivyofika getini alipaki gari lake kisha mimi nikashuka na kumuaaga kwa kuwambia asante na unaweza kwenda.
Bado sijarizika unaweza kukosa chumba na ikumbukwe na mimi ndio nilikuchelewesha na kukuharibia ratiba zako kwa hiyo tatizo lolote litakalotokea ni mimi wa kulaumiwa. Kwa kuwa aliongea point sikutaka kumkatilia tukapanda nae lift hadi reception. Nikalipia chumba na bado lakini mwalimu huyu bado aliaamua kuning”ang’ania kwa madai kuwa alitaka kukiona hicho chumba kilivyo. Nikaona isiwe tabu tukaenda naye na baada ya kukifungua hicho chumba tukaingi wote na mimi nilisimama mlangoni nikamwambia sitayari aondoke. Cha ajabu alikataa kuondoka na kuniambia hapo ndo amefika mwisho wa reli kigoma.
Kwa jinsi alivyokuwa mkorofi Ticha John akajimwaga kitandani kama mtu aliyekuwa na furaha ya kuhamia nyumba mpya. Nikamwambia nampa dakika tano na hasipo ondoka napiga simu polisi au kwa walinzi waje wamtoe kwa nguvu. Nikaingia chooni maaana kilikuwa ni chumba cha self container. Nilijifungia kwa ndani lakini wapi yule mwanaume hakutaka kuondoka aliendelea kunisubiri. Zilipita dakika kumi nikaamua kutoka na kukimbilia simu ya mezani. Akaanza kunizuia kwa kutumia nguvu ili nisiipige. Nikamwambia basi yeye alale hapo kitandani na mimi naenda kulala chooni.
Nikachukua shuka nikaingia nalo chooni na kujifungia. Kwa bahati nzuri vyuo vya hapo vilikuwa ni visafi sana hivyo niliweza kuvumilia kukaa hapo kwa dakika kumi zaidi. Baadaye nilimsikia akifungua mlango na akaondoka zake. Nilitoka kwa haraka na kufunga chumba changu huku nikisema asante mungu kwa kunijalia ujasiri huo nilioufanya. Nilioga na kisha nikajimwaga kitandani. Dakika chache baadaye huku nikiwa nipo uchi nilisikia mlango wangu ukigongwa. Sikutaka kuiitikia zaidi ya kujifunika shuka vizuri na kufumba macho.
“Samahani dada mimi ni mlizi” ilisikika sauti nje ya chumba. Niwasaidie nini niliuliza kwa mshangao. ‘ Huyu kaka uliyeingia naye tumruhusu aende’ waliuliza wale walinzi. Nikajibu kwa kujiamini ndio. Nilisikia mwalimu John akisema haya lala salama mke wa mtu usisahau kushuka neti.Hapo kicheko kilinijia lakini nilijikaza nisicheke kwa nguvu hivyo kuzidi kujikunyata kwenye lile shuka nililokuwa nimejifunika. Nilisikia pia wale walinzi wakimwambia usichukie kamanda hizi ni taratibu za kiusalama.
Kuna mtu hapa alikuja mwaka jana akamua mpenzi wake aliyekuja naye akataka kuondoka kwa staili kama hiyo yako tukamkamata., wale walinzi waliendelea kumuelewesha mwalimu John. Sisi tumesomea mambo haya bhana waliendela kuzungumza wale walinzi huku wakishuka ngazi kwa polepole. Hapo na mimi nikawa nimejifunza kitu kuwa kumbe unaweza kuingia na mtu guest akakuzuru kisha akaondoka zake.Sasa sijui kwenye zile guest zetu za uswahilini kama wanalijua hili.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni