Notifications
  • THE NIGHTMARE (9)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA TISAILIPOISHIA...“mmenifananisha, mimi ndio kwanza naigia ofisini mida hii.” Aliongea yule afande na kuigia kituoni.“sasa aliyekuwa anatuhoji ni nani kama sio huyo?”Alijikuta anajiuliza mwenyewe swali lililompa utata mkubwa kichwani mwake.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Wakati wakiwa hawajui hili wala lile, walishangaa kuona maaskari wakijazana pale na ambulance ikafika…
  • THE NIGHTMARE (8)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA NANEILIPOISHIA...Walipofika feri, walipewa nahodha mwingine tofauti na yule aliyemuota na boti ilikuwa ndogo tu ya kawaida tofauti na ile aliyoiota.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Sharji alijikuta anapiga makelele baada ya kumuona Balqis akiwa amejaa damu mdomoni huku ametoa makucha yake akimfata kwa nia ya kumdhuru.“AAAAAAAAAAAGH”Sharji alipiga kelele na kukurupuka.…
  • THE NIGHTMARE (7)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA SABAILIPOISHIA...“kha!!!!”Ulikua mshangao mkubwa kwa watu karibu wote baada ya kumuona Sharji akiwa na taulo akitoka chumbani kwa Balqis.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Wengine walicheka na kaka yake alionekana kutoifurahia hali ile.“sasa wewe unatutia wasi wasi bure, si ungesema tu kama unaenda kulala kwa huyu dada?” aliongea kaka yake na kukirudia kile chumba alichompangia…
  • THE NIGHTMARE (6)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA SITAILIPOISHIA...“toa loud speaker bwana.”Aliongea Balqis baada ya Sharji kubonyeza kitufe cha kupaza sauti.“kwanini hutaki nisikie maongezi yenu?” aliongea Karimu kwa sauti ya ukali kidogo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...“kwani kuna ubaya mimi nikiongea private na mdogo wako?” alijibu Balqis baada ya kuisikia sauti ya Karimu.“hakuna ubaya.” Alijibu Karim kwa sauti ya…
  • THE NIGHTMARE (5)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA TANOILIPOISHIA...Alijikuta outomatic akijisemea kwa mshangao baada ya kumuona dada mmoja mrembo mwenye asili ya kiarabu akiingia mule ndani. Hakuvaa ushungi kama alivyowazoea kuwaona waarabu wengi ambao alikutana nao. Huyu alivaa suruali ya jeanz nyeusi na juu akiwa na kikoti chake cheusi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Kati kati kulikua na nguo Fulani nyeupe iliyonakshiwa…
  • THE NIGHTMARE (4)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA NNEILIPOISHIA...Aliongea Khalidi na kuufungua mkanda wa suruali yake na kuanza kumtandika Karim.“unanipiga mimi?...utaona!”IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Aliongea Karim na kuondoka huku analia.*****************************Zilipita wiki mbili bila ya Karim kuonekana nyumbani kwao. Sabra alisikitika kidogo kutokana na kuwapenda sana watoto wake japokuwa huyo mtoto mkubwa hakuwa…
  • Fumanizi la Mchepuko Mwizi😂 | Comedy
    Mume amefuma viatu vya mchepuko wa mke wake mlangoni lakini akakosea kuingia ndani kabla aweke umakini kwenye hivyo viatu mwisho wa siku akaibiwa na vyake😂Hili tukio lazima lichukuchekeshe sana hata kama ulikuwa haujataka kuchekaItazame kisha nipe like na ukinipa maoni kwenye comment nitashukuru sanaUsisahau kubonyeza Subscribe kama haujajiunga na fungua #ChekanaZephiline kupata video zangu zote ambazo zipo mtandaoniNashukuru sana kwa wewe ambaye unanipa nguvu ya kuendelea kuwaletea kazi nzuri…
  • THE NIGHTMARE (3)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA TATUILIPOISHIA...Akiwa hewani akikata mawingu kurudi Tanzania, kichwa chake kilikua na mawazo mengi sana juu ya mume wake. Aliikumbuka siku waliyofunga ndoa.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Pia alijua kwanini mume wake alipendelea kufanya kazi uingereza na yeye kumfungulia ofisi huku huku Tanzania. Hakujua kuwa kazi anayoifanya mumewe ni ile ya kutembea na tajiri mkubwa…
  • THE NIGHTMARE (2)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA PILIILIPOISHIA...Khalidi alishangaa kuitwa na mtu asiyemfahamu. Alitoka na kwenda kumuangalia huyo mtu maana kiukweli hakua na ndugu aishie hapa Dar hata mmoja anayemfahamu..IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Alipigwa na butwaa baada ya kumuona Sabra pale.“ahsante mungu.” Aliongea Khalidi baada ya kumuona tu yule binti pale.“pole sasa kaka yangu, nisamahe mie.” Aliongea Sabra kwa…
  • THE NIGHTMARE (1)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA KWANZANi kipindi cha mvua za masika. Upepo mkali, na mvua kubwa iliendelea kunyesha kwa kasi kila kona ya nchi ya Tanzania.Ipo mikoa iliyofurahia mvua hizo kwa kuwa walikua wanaisubiria kwa hamu kwa ajili ya kilimo. Lakini ipo mikoa iliyokua inapata shida kwa uharabifu wa mazingira na mengineyo mengi.Moja ya miko hiyo ni Dar-es-salaam. Watu wanaoishi katika mkoa huo walichukia mvua mfululizo kutokana na sababu mbalimbali. Biashara nyingi…

MY DIARY (34)

Jina: MY DIARY
Mtunzi: __

SEHEMU YA THELATHINI NA NANE
TULIPOISHIA...
Hapo nikakumbuka kuwa zile zana zangu za kazi nilikuwa nazo ni vile vifaaa vya kupimia ukimwi ambavyo huwa navitumia kabla ya kukutana na mwanaume yeyote nisiyemfahamu. Nikaamua kumkubalia huku nikiamini kuwa hiyo ndo kinga yangu pekee iliyobaki kama mwanaume huyo atataka kuzini na mimi usiku huo.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

TUENDELEE...
Basi tuliondoka na kwenda sehemu ambayo mwanaume huyo alikuwa amefikia .Kwa bahati mbaya au nzuri Mark alinipeleka kwenye hile hotel ambayo huwainanikumbusha mambo mengi sana hasa mwanume wangu wa kwanza yaani mwalimu John. Yaani sijui kwa nini hoteli hii nilikuwa nikiletwa mara kwa mara na cha ajabu Mark alikuwa amekodi chumba namba 10 chumba ambacho pia mwalimu John alikuwa akikipenda sana.Kama kawaida yangu tulipoingia tu chumbani mimi nilikimbilia bafuni na mbaya zaidi niliingia na pochi yangu kitu ambacho kilimshangaza Mark. Nilijisafisha vizuri kisha nikava ile kondomu ya kike. Baada ya kuhakisha nimevaa kinga vizuri nikachukua kile kipimo cha ukimwi na kukiweka juu kabisaya pochi.

Nilitoka huko mawaliwatoni na kumkuta mkaka huyo amewasha laptop yake akissoma emaili zake.Basi na yeye akatumia nafasi hiyo kwenda kuoga. Aliniwekea clips za vichekesho na kuniacha nikiendelea kuburudika.Yaani japo nilikuwa nimechoka lakini mara baada ya kumuona Erick Omond mchekeshaji maaarufu kutoka nchini Kenya uchovu wote uliisha. Mimi jamani ni miongoni mwa Watanzania wachache ambao walikuwa wakimfuatilia sana mchekeshaji huyo hasa kutokana na tabia yake ya kurudia rudia nyimbo za msanii maarufu Tanzania yaani Diamond Platunzmz. Yaani huyu mchekeshaji ni kiboko ule wimbo wa nasema nawe eti yeye kaubadilisha na kuwa nabeba mawe. Basi Mark alirudi na kupanda kitandani na tofauti na mimi nilivyofikiria kuwa mwanaume huyo atakuwa na papara sana kutokana na tabia yake ya uchu aliyoionesha tulipokuwa kule kwenye shindano la mwanamke nyonga.

Mark alianza kujitambulisha upya kuwa yeye ni mwandaaji na mcheza filamu. Filamu maarufu ambayo ilimwingiza na kumfanya awe maarufu kwenye tasnia hiyo ni ile filamu ya MY WIFE TO BE.Mark alinieleza kinaga ubaga kuwa amevutiwa sana na mimi na anataka kunioa. Hapo mimi ilinibidi nicheke kwa sababu sikuwahi kuwaza kuolewa hivi karibuni. Alafu pia mtu tumekuatana leo alafu anatangaza nia ya kunioa jamani si masihara haya. Mimi kwa kweli sikuwahi kuwaza kuolewa nilichokuwa nikiwaza ni jinsi gani nitafanya ili kukamilisha ndoto yangu ya kuboresha maisha yangu kupitia yale madini. Niliendelea kumsikiliza Mark huku akiongea kwa utulivu sana huku akionesha kama mtu anyemaanisha kitu anacho kiongea. Alinambia kuwa anataka kuniingiza kwenye tasnia ya filamu.Ilibidi nimuulize kwani anavyoniona mimi naweza kuwa na kipaji cha kuiigiza?

Yeah kwa jinsi ninavyokuona una vipaji vingi sana na kama utapewa nafasi ya kupata mafunzo kidogo unaweza kuwa bonge la superstar alisema Mark kwa kujiamini. Ilibidi nimshushue kwa kumwambia sikiliza Mark uzuri wa umbo na sura sio kigezo cha kucheza filamu. Mark akacheka na kuniambia mimi sijasema uzuri wako ndo utakuingiza kwenye filamu ila nimegundua kuwa unavipaji vingi kama unaweza kucheza na mashabiki jukwaani basi hutoshindwa kucheza na kamera wakati wa kushuuuti filamu. Basi nilimuambia hilo la kuingia kwenye filamu sawa ila hilo la kunioa hapana.

Tatizo nini kwani hujajipanga kuolewa au hautaolewa maishani mwako aliuliza Mark kwa upole. Ujue Mark mimi na historia nyingi sana ambayo kama nikukueleza kamwe hutoweza kukaa karibu yangu. Historia yangu ni ndefu sana na bado inaendelea na hata mimi kukutana na wewe sehemu kama zile sio kwa sababu nilipenda kushiriki mashindano kama yale basi tu ni hali ya maisha.Pia historia yangu bado haijakamilika labda mpaka hapo nitakapo pata madini aliyoniachia marehemu baba yangu kama urithi wangu. Najua historia yangu haitakusitua sana kwa sababu ni mambo yanayotokea duniani lakini historia yangu ya uhusiano na mapenzi ni ngumu sana.

Kwa kifupi kaka yangu kwa sasa hutoniweza kwa sababu nishazoea starehe, yaani mimi sio mwanamke ambaye unaweza niweka ndani nikawa mkeo. Yaani sijui kama eti nitaweza kumtunza mwanamme kumfulia kumpikia na mambo mengine muhimu.Ilibidi nimwekee vikwazo ingawa nilijua kama nitapata mwanaume atakayenipenda na kunijali ningeweza kubadilka na kuwa kama wanawake wengine.Mark alikuwa akinisikiliza kwa umakini sana huku akitingisha kichwa kuonesha huenda mimi sijielewi.

“Ujue sisi ni watu wazima kwa hiyo sioni kama kuna haja ya kujadili historia zetu kwa sababu ni vitu ambavyo vilishatokea na vilitokea kwa sababu na bila hivyo pengine mimi na wewe tusingeweza kukutana alisema Mark.Kwa hiyo nitakuwa ni mwanaume wa ajabu sana kama historia yako ya mapenzi itakuwa kikwazo cha mimi kuwa na wewe. Kwa kifupi naweza kusema sihitaji kuijua historia yako ya mapenzi kwa sababu hata mimi ya kwangu sio nzuri aliendelea kufafanua Mark. Kauli hiyo sihitaji kujua historia yako kwa kuwa hata ya kwangu sio nzuri ilinifurahisha sana.

Ikabidi nimuulize kwani historia yake ya uhusiano na mapenzi kwa kifupi ipoje.? Marka akajibu kuwa eti historia yake ni ndefu sana pengine kuliko ya kwangu ila kwa kifupi kwa sasa anataka kuanza upya na kuwa na familia.Nikabidi nitumie ladies power nikamwambia niambie basi hata kidogo babee. Bado alisita hapo nikaamua kumsogelea zaidi na kumuekea kichwa change kifuani mwake.Basi Mark akaanza kunisimulia “ ujue nilikuwa nikifikiria kuwa ukitaka kuoa mwanamke ambaye hatokusumbua basi ni lazima uende kuoa kijijini. Basi mimi nilifanya hivyo kwa kwenda kijijini na kuoa binti ambaye alikuwa ni mshamba kabisa. Nikamtoa kijini na kumelta jijini ambapo tulianza maisha.

Na kwa kuwa alikuwa ameishia form four basi mimi niliamua kumtafutia chuo ili ajiendeleze.Na kwa kuwa alikuwa akipendelea sana mambo ya utalii basi nilimpeleka pale chuo cha utalii cha taifa.Basi maisha yakaendelea na kutokana na maji ya chumvi ya Dar basi uzuri wake ukaanza kuonekana.Mtoto akang’aa na kuwa kivutio cha wanaume wengi. Siunajua tena rangi nyeupe jinsi zinavyokuwaga hasa zikipata matunzo.Baadaye akalijua jiji na hata mavazi yake yakaanza kubadilika. Baadaye akaanza kubadilika na tabia akawa haoni tena thamani yangu kwake. Mbaya zaidi walikuja wazungu hapo shuleni kwao na yeye akawa miongoni mwa wanafunzi walifaziliwa kwenda kusoma nje ya nchi.

Nilitumia nguvu zangu zote kumzuia asiende lakini ilishindikana.Na alianza kunichukia kwa madai kuwa mimi sipendi maendeleo yake.Nikaona isiwe tabu mwache tu aende akasome.Na mimi nilikuwa namzuia si kwa nia mbaya eti sipendi asome la hasha bali ni kwa sababu tayari alikuwa na ujauzito wangu aliendelea kufafanua Mark.Nilitega masikio vizuri maana nilihisi stori imekuwa tamu huku nijisemea hapa asije akaikatisha na kusema Iitaendela kesho.

Basi binti huyo akaondoka huku akiwa na kihoro cha kwenda kusoma ulaya aliendelea kusimulia Mark.Basi akiwa ulaya tuliendelea kuwasiliana kwa kutumia mitandao ya kijamii hasa ule wa Skype. Siku zilizidi kuyoyoma huku nikiamini kuwa mimba yake iliendelea kukua na itakapofikisha miezi 8 atarudi nchini ili aje ajifungulie huku. Mbaya zaidi ilipofika hiyo miezi bado hakurudi na aka niblock kwenye mitandao yote ambayo tulikuwa tunatumia kuwasiliana naye.Akafunga akaunt zake za zamani kuanzia WhatsApp, facebook, twiter, instagram, tango, na skype.

Sikujua nini kimemsibu lakini kila siku iendayo kwa mungu niliendelea kutumia juhudi zangu zote kuhakikisha nampata hewani.Mwaka mzima ulipiata bila mawasiliano na mimi nikawa nimekataa tamaa kabisa na haya maisha.Siku moja nikiwa zangu jengo la kitega uchumi nilimuona mtu kama yeye akiingia supermarket. Kwa sababu nilikuwa location tukishuti filamu nilishindwa kumfuata ila alikuwa na rafiki yake kipenzi.Hivyo niliamua kumpigia Yule rafiki yake na nilipomuuliza kuwa yupo wapi akanambia yupo jengo la kitega uchumi. Hapo nilikuwa sina haja tena ya kutafuta ushaidi niliendelea na kazi ambayo ilinipeleka pale. Niliamua kumpotezea kwa sababu nilijua nikifanya makosa tu nitaharibu kwa sababu hiyo sehemu tulipewa kwa mbinde sana na tulipewa kwa mda mfupi sana.

Hivyo niliona kuwa ni bora niendelee kufanya kazi na baada ya hapo ningemtafuta na kwa kuwa nilikuwa na namba ya huyoo rafiki yake sikuwa na hofu sana. Aliendelea kusimulia Mark stori iliyonifanya usingizi wote uniishe na kufuatilia kwa umakini ili niweze kujua nini ulikuwa mwisho wao. “Wewe naye una moyo mgumu sana yaani uone kitu chako tena cha ndoa ambacho mlikuwa hamjawasiliana mda mrefu ukiache hivi hivi nilimwambia kuonesha kuwa namsikiliza kwa umakini sana.

Yeah nilikua sina jinsi kwa sababu kazi ndio msingi wa maisha na mimi ndo nilikuwa director pale kwenye ile movie. Kwa hiyo tuliendelea na kazi na tulifanikiwa kumaliza salana japo sikuweza kufanya ile kazi kwa ufanisi wangu wa siku zote. “Kwa hiyo nini kilitokea baada ya hapo ilibidi nimuulize swali mara baada ya kumuona ametulia tulii kama mtu aliyewaza kitu kingine wakati akisimulia”. Niliona macho yake yalikuwa yametua kwenye mapaja yangu ambayo kwa bahati mbaya khanga niliyojifunga ilikuwa imejiachia hivyo kufanya sehemu zile za mautamu kuonekana kidogo.

Baada ya kuakamilisha ile kazi niliondoka na nilivyofika nyumbani nilimpigia simu yule rafiki yake na nikaomuomba tuonane siku iliyofuata.Kwa kuwa rafiki yake alikuwa ni mtu mwelewa sana peace and love alikubali na tukaonana siku iliyofuata.Nilitumia mda mwingi sana kumdadisi kuhusu rafiki yake na baaadye alikubali kuniambia ukweli. Biblia inaseam ijue kweli na kweli itakuweka huru hivyo ukweli huo hata mimi uliniweka huru. Nasema ukweli uliniweka huru kwa sababu nilijua mambo mengi ambayo nilikuwa siyafahamu na ambayo pengine yalikuwa ni fumbo kubwa sana kwangu aliendelea kusimulia Mark.

Kwanza niliweza kugundua kuwa Yule mwanamke ile mimba aliitoa hata kabla hajapanda ndege jambo hili lilinifanya niumie sana na kupata uchungu ambao kwa kweli hauzungumziki alisema Mark. Hapo ilinibidi nimwambie jamani pole. Pili niliambiwa kuwa alipata bwana mzungu ambaye walifunga naye ndoa na sasa ana mimba yake. Tatu niliambiwa kuwa ndugu zake na wazazi wake walihusika kwenye mipango hiyo hivyo walibariki kabisa huyo binti kuniacha mimi mumewe wa ndoa na kuamua mtoto wao aolewe upya. Nne ni kwamba huyo mzungu amewaamishia wazazi wake mjini na amewajengea nyumba ya kifahari.

Kwa hiyo mimi ninavyowapigiana simu na kuwajulia hali kumbe wenzangu huwa wananichora tu.

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
68 My Diary Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni