MY DIARY (33)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mtunzi: __
SEHEMU YA THELATHINI NA TATU
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Nilikuwa nachanganya staili za kijamaika na hizi za kwetu, sikuacha pia zile za Nigeria hapo nikapata vitu vyangu vya tofauti kabisa. Basi baada ya kujihakikishia kuwa nipofiti kwa mastahili yangu hayo nilisubiri siku ya shindano ifike nikafanye yangu. Siku ya shindano ilifika na mimi nilikuwa miongoni mwa washiriki walioingia tatu bora.
TUENDELEE...
Basi ilivyofika zamu yangu ya kufanya vitu vyangu nilipanda jukwaani huku nikiwa nimevalia kivazi ambacho kilitosha kabisa kunipa ushindi kwani ukumbi wote ulizizima kwa makelee ya kunishangilia.Nilivyovyaa kwa kweli ilitosha kuwachengua mashabiki ambao wengi walikuwa ni wanaume tena wenye uchu wa mambo hayo ya kukata mauno.Sikutaka kupoteza mda nilianza kazi yangu kwa makeke ili hali nikijua kabisa watu wote waliokuwa wakinitizama walikuwa wanaumia roho kutokana na mvuto wa umbo langu niliokuwa nao.
Nilisikia mijibaba miwili ikiulizana hivi lile wowoo ni la kwake au ni la mchina? Mmoja wao akaropoka “wee kitu original hicho, kwani umemsaahau huyu binti tulishakutana nae kule Arusha mpaka tukambatiza jina la soda kubwa tena ya fanta yaani BAMBUCHA.?” Yeah nimekumbuka alidakia mwanaume wa tatu waliokuwa nao.
Akaongeza basi huyu tusimwite tena BAMBUCHA bali tumpe jina la bia kwani inaonesha thamani yake ni kubwa zaidi. Basi wote kwa pamoja wakacheka.
Wakati nikiendelea kutingisha makalio yangu ambayo kiukweli yalikuwa yakitetemeka kama mawimbi ya bahari, yule aliyetoa hoja akapendekeza jina linalofanana na bia eti kutokana na uzuri niliokuwa nao aliniita HAINKEN WOWOWO.
Ilinibidi nicheke kwa nguvu kitu ambacho kiliwashitua mashabiki wangu waliokuwa wakinifuatilia, hawakujua nilikuwa nikicheka nini wakajua labda nilifurahishwa na ule wimbo wa kanga ndembendembe laki si pesa. Wakati nikiendelea kuzungusha nyonga yangu kwa ufundi wa ajabu niliokuwa nao niliendelea kufuatilia mazunguzo ya wale watu waliokuwa wamekaa meza ya karibu na jukwaa. Niliendelea kuzungusha nyonga na kwa wale ambao ndo ilikuwa ni mara yao ya kwanza kuniona walishangaa sana.
Lakini kwa wale ambao walishaniona kwenye shindano la miss bonge kule Arusha wasingeshangaa sana kwani kile ndo kipaji nilichojaliwa na mwenyezi Mungu. Nilizungusha kisawa sawa huku nikirembua macho yangu kitu ambacho siku zote kilikuwa nikiwaumiza wanaume wenye tamaa. Kwa ufundi wa ajabu nilio kuwa nao niliendelea kufuatilia wimbo niliowekewa huku nikilitegeza sikio langu moja kwenye ile meza iliyokuwa karibu yangu. Wale wanaume waliendelea kunitumbulia macho huku wakiendelea kubishana juu ya jina gani wangenibatiza kulingana na uzuri wangu.
Nilibahatika kumsikia mmoja akimwita muhudumu kwa fujo na kumwambia “inaelekea wewe hujui majukumu yako, mbona bia imeisha na umekaa mbali?
Dada kwa heshima kubwa na kutambua kuwa walikuwa wameanza kulewa alimjibu kwa kumwambia samahani kaka” Sitaki samhani yako niletee bia inayofanana na huyo dada kwenye jukwaa. Yule muhudumu alibaki ameduwaa asijue nini cha kufanya. Akauliza jamani kaka mbona sikuelewi nikuletee kinywaji gani? Kaka kwa ukali akamwambia kinachofanana na huyo dada.
Muhudumu akaenda kaunta na alipokuja alikuja na soda kubwa iliyojazia yaani BAMBUCHA. Watu wote kwenye meza yao walishangaa yaani mtu alikuwa anakunywa bia na sasa ameletewa Bambucha. Ili bidi wapigwe na butwaa, yule jamaa akamuuliza yule muhudumu kwanini umeleta hii soda? Muhudumu kwa kujiamini alisema ‘Ni kwa sababu huyo dada anaitwa BAMBUCHA.Basi watu wote pale mezani waliangua kicheko.
Basi kwa kuwa kila mtu alipewa nyimbo tatu kuonesha maujuzi ya kuzungusha nyonga na kuchezesha makalio, hivyo mimi niliwekewa wimbo wangu wa mwisho. Huku nikibadilisha staili na kucheza ile matata ya kulala chini kisha kuzungusha kama vile upo juu ya mwanaume. Nilimsikia yule mteja akimwambia muhudumu niletee HAINKEN WOWOWO na wakati Yule dada akitafakari Heinken wowowo ni ipi, kwa macho yangu ya wizi nilimwona yule kaka akifungua pochi yake na kutoa hela na kila kwenye noti ya elfu kumi alikuwa akiandika kitu.
Sikujua alikuwa akiaandika nini nitakwambia nikishuka jukwaani. Basi nikaamua kuendelea kufanya yangu na nilikuwa namalizia na ile staili ya mdembwedo.
Hii staili ni mbaya sana kwani unakuwa kama unajizalilisha, hapa wapambe wangu walinimwagia maji kwenye makalio hivyo kuwa ndembendembe. Nilitumia vizuri vidole vyangu kuviingiza sehemu ambazo kwa kweli naogopa kusema. Yule kaka akashindwa kuvumilia akanifuata na kunimwagia zile noti za elfu kumi kumi.
Sikujua alinipa shiling ngapi kwa kuwa haikuwa kazi yangu kuokota hela ila kwa utundu wangu niliivuta moja kwa kutumia vidole vya miguu yangu. Nilifanya hivyo kwa sababu mara nyingine huwa tunazulumiwa na pia nilitaka kujua yule kaka aliandika nini kwenye zile hela.Mda wa mimi kuendelea kukaa jukwaani ulimaliika basi nikashuka chini huku mashabiki wakinipigia mayowe na makelele ya shangwe
Nilikwenda moja kwa moja kwenye chumba cha kubadilishia nguo na wasiriki wengine waliendelea kufanya mambo yao.Baadaae washiriki wote walimalizika na muda wa kutangaza mshindi ulifika. Nakulikuwa hakuna haja ya kupepesa macho mimi nilitangzwa mshindi jambo ambalo lilifanya ukumbi uzizime kwa kuraha. Ikabidi mashabiki waniombe nicheze wimbo mmoja ambao ungewafurahisha nakusindikiza ushindi wangu.Kinyume na walivyotarajia mimi sikuwekewa tena wimbo wa taarabu bali niliwekewa wimbo wa kinaigeria nakuanza kufanya vitu vyangu.Maneno ya wimbo ule ndo huwa unanipa maksi sana “ baby pull over, show me your particular, revese, back, right. Left and front”
Hapo sasa mimi kweli nikawa naonesha vitu vyangu vya mbelee, nyuma kushoto na kulia ili mradi kumtukuza mungu kwa kazi nzuri ya uumbaji.Kweli mungu alinipa kipaji maana staili yangu yauchezaji iliwafanya watu kufungua pochi zao na kuja kunitunza. Nlipata hela nyingi sana ambazo hata mimi mwenyewe sikuzitarajia. Tamasha likaisha kihivyo na kila mtu akaendlelea na ratiba zake.Leah alipewa hela zake zote alizotunzwa pale jukwaani akaendelea na furaha ya yake ya kushangilia ushindi.Kabla sijaondoka nikakumbuka zile noti za kwanza ambazo nilipewa na yule kaka ambaye alinibatiza jina la Heinken wowoo badala ya Bambucha. Kweli kuna watu wana akili huku duniani kwa sababu zile noti ziliandikwa namba za simu.Niliziangalia zile noti nikatabasanmu na kujisemea kweli wanaume wana mbinu nyingi sana duniani.
Basi mara baada ya kuhakikisha kuwa zile hela zangu na cheque niliyopata ipo sehemu salama niliamua kumtafuta yule kaka. Nilichukua simu yangu na kumpigia simu yake iliita mpaka ikakata bila kupokelewa.Nikaamua kumtumia ujumbe mfupi wa maneno “mshindi wa mwanamke nyonga hapa” Yule jamaa mbona alipiga simu mwenyewe na swali la kwanza aliloniuliza ni kuwa nipo wapi.Ilibidi nimjibu kuwa nipo nyumbani.Yule kaka ambaye mimi nilikuwa namjua kabisa kuwa ni star wa bongo movie aliniuliza kuwa eti tunaweza onana usiku huo kwa sababu kesho anaondoka alafu alikuwa na jambo la muhimu sana kuhusu maisha yangu.Yaani kusikia jambo muhimu kuhusu maisha yangu kwa kweli nilichanganyikiwa. Ilibidi nimjibu kinyonge sasa tuataonana wapi usiku huu. Basi Yule mkaka akanambia kuwa wanaelekea club na kama sitojali niungane nao kwa kuwa anaamini kuwa huko tutapata mda wa kuongea zaidi.Kwa kuwa mimi nilitambua ustaa wa kaka yule nikaona hakuna haja ya kulaza damu huwezi jua labda anataka kuniingiza kwenye tasnia ya filamu. Nilimuhadi kuwa nitafika maeneo hayo tuliyokubaliana mda mfupi baadaye.
Kwa kuwa nilikuwa na hela nikaona isiwe tabu ngoja niende zangu home nikaweke hela kisha nivaee nguo za club nikale raha mie mtoto wa watu. Nilichukua tax kwa kiburi ya hela zile za kutunzwa. Uzuri safari hii nilikuwa naishi katikati ya mji.Mimi jamani napenda sana mziki kwa sababu ndo ilikuwa ni starehe yangu ninayoipenda hivyo msinishangae kabisa mimi kukubali kwenda club kirahisi hivyo. Nilijipara kisha nikaondoka zangu na kwenda eneo la tukio na nilivyofika bado sikutaka kutumia hela yangu kulipa kiingilio.
Basi nilimwandikia sms na kumuueleza kuwa nilishafika eneo la tukio.Sikuwa mbali sana na fikra zangu kwa maana baada ya dakika mbili tu mwanaume huyo alitoka na kuja nje mahali ambako nilikuwa nimesimama.Hakutaka kupoteza mda akanilipia kiingilio kisha tukaingia ndani. Tulipitia kaunta na akanambia nichkue kinywaji ninachopenda. Tulikwenda pembeni mafichoni kidogo sehemu ambayo tungeweza kuongea bila kuwakera wengine. Tulikaa sehemu ambayo sauti ya mziki ilikuwa sio kubwa ili tuweze kuongea. Naitwa Mark alianza kwa kujitambulisha staa huyo wa filamu hapa nchini.Na mimi nikamwambia naitwa Leah japo wengine wananifahamu kwa jina la Bambucha.
Hatukuweza kuongea sana kwani kampani ya Mark ilisogea karibu yetu hivyo tukawa wengi na stori zikabadilka na kuanza kupiga storiza club na mziki. Na kwa bahati nzuri wanaume hao wote walikuwa na mademu zao kwa hiyo aliyefurahishwa na mziki aliamka na kwenda kucheza. Na wengine walicheza palepale pembeni ya meza. Mark nae hakujivunga alinipa mkono na kwenda kusasambua. Kama kawida yangu ikija swala la kucheza mziki basi ndo ujue kuwa umenifikisha mahali pake. Sikujivunga kwa kweli nilionesha yale maujuzi yangu na hivyo nikawa kivutio cha watu waliofika eneo hilo. Ilifika wakati watu wote waliacha kucheza na kunitazama mimi nikifanya vitu vyangu. Mambo yaliendelea na Dj uzalendo ulimshinda ikabidi atoe tu zawadi.Sikushangaa kwa sababu haikuwa mara yangu ya kwanza kupewakuponi ya kuingia bure club mara baada ya kutawala stage
Baadaye mda ulienda sana na nilikuwa nimechoka sana hivyo nilimuaga Mark kuwa nahitaji kuondoka na kwenda kupumzika.Cha ajabu Mark alikata kuwa nisondoke na aliniomba tuende kulala nae kwa sababu alikuwa bado hajaniambia kitu ambacho yeye alitaka kuniambia na pia isitoshe yeye kesho anaondoka na kwenda Nairobi kwa ajili ya kazi zao hizo za filamu. Aliniweka njia panda kwa kweli kwa sababu ndo ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kukutana na mwanaume huyo kivipi nitamwamini na kuenda kulala nae.
Nilimueleza ukweli kuwa hiyo ndo siku yetu ya kwanza kukutana sasa ni kwa vipi tunaweza aminiana na kwenda kulala wote. Pamoja na vikwazo vyote hivyo bado Mark alisisitiza kuwa kuna jambo la muhimu anataka kuongea na mimi. Hapo nikakumbuka kuwa zile zana zangu za kazi nilikuwa nazo ni vile vifaaa vya kupimia ukimwi ambavyo huwa navitumia kabla ya kukutana na mwanaume yeyote nisiyemfahamu. Nikaamua kumkubalia huku nikiamini kuwa hiyo ndo kinga yangu pekee iliyobaki kama mwanaume huyo atataka kuzini na mimi usiku huo.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni