Notifications
  • THE NIGHTMARE (3)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA TATUILIPOISHIA...Akiwa hewani akikata mawingu kurudi Tanzania, kichwa chake kilikua na mawazo mengi sana juu ya mume wake. Aliikumbuka siku waliyofunga ndoa.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Pia alijua kwanini mume wake alipendelea kufanya kazi uingereza na yeye kumfungulia ofisi huku huku Tanzania. Hakujua kuwa kazi anayoifanya mumewe ni ile ya kutembea na tajiri mkubwa…
  • THE NIGHTMARE (2)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA PILIILIPOISHIA...Khalidi alishangaa kuitwa na mtu asiyemfahamu. Alitoka na kwenda kumuangalia huyo mtu maana kiukweli hakua na ndugu aishie hapa Dar hata mmoja anayemfahamu..IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Alipigwa na butwaa baada ya kumuona Sabra pale.“ahsante mungu.” Aliongea Khalidi baada ya kumuona tu yule binti pale.“pole sasa kaka yangu, nisamahe mie.” Aliongea Sabra kwa…
  • THE NIGHTMARE (1)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA KWANZANi kipindi cha mvua za masika. Upepo mkali, na mvua kubwa iliendelea kunyesha kwa kasi kila kona ya nchi ya Tanzania.Ipo mikoa iliyofurahia mvua hizo kwa kuwa walikua wanaisubiria kwa hamu kwa ajili ya kilimo. Lakini ipo mikoa iliyokua inapata shida kwa uharabifu wa mazingira na mengineyo mengi.Moja ya miko hiyo ni Dar-es-salaam. Watu wanaoishi katika mkoa huo walichukia mvua mfululizo kutokana na sababu mbalimbali. Biashara nyingi…
  • MY DIARY (50)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA HAMSINITULIPOISHIA...Nilimnongo’oneza kuwa atumie kinga ili nisimwambukize ukimwi akanijibu kwa sauti ya mahaba nisiwe na hofu yeye yupo tayari kufa kwa ajili ya penzi langu hivyo hawezi kutumia kinga kwa mke wake aliyemoa tena siku muhimu kama hiyo.Sikutaka kumbishia yeye ndo muaamuzi wa mwisho kuhusu afya yake hivyo nilimuacha aendelee kufanya yake.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Kumbe na…
  • MY DIARY (49)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA TISATULIPOISHIA...Baada ya maneno ya kusilimu ambayo waliambiwa wayatamke kiongozi huyo alisema neno ya mwisho kabla hajashuka.” Kila alie na akili timamu, mwenye busara naa anaetaka haki, na kusimama pamoja na haki, basi akiangalia dunia ilivyo na jinsi inavyokwenda basi lazima kutakuwa na nguvu kuuu nayo ni mwenyezi mungu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Kuna vitu vingi sana…
  • MY DIARY (48)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA NANETULIPOISHIA...Familia yangu haikukubali kabisa mimi kuolewa na rangi nyeusi hivyo walinitenga na kusema hawanitambui kuwa mimi ni ndugu yao.Lakini kutokana na mapenzi mazito niliyokuwa nayo kwa baba yake na Leah nilijikuta nipo tayari kwa lolote hivyo nikahama na kwenda kuishi Tanzania.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Katika miaka hiyo tuliyokaa nilibahatika kupata mtoto huyu…
  • MY DIARY (47)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA SABATULIPOISHIA...Lakini ilifikia mahali ndoto hiyo inanijia hata mchana nikiwa nimekaa mahali tulivu.Ilikuwa inanipa taswira nzuri ya sehemu ambayo madini yalikuwepo.Basi nilianza mikakati ya kulitafuta eneo hilo na hiyo ni mara baada ya ushauri wa mpenzi wangu Candy hapo akimaaanisha yule dada aliyekuwa naye pale jukwaaani.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Candy alinisihii sana…
  • MY DIARY (46)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA SITATULIPOISHIA...Nilikuwa kama niliyepigwa butwaa nisiamini nilichokuwa nakiona mbele yangu. Oooooh my God hold me on yalikuwa ni maneno yaliyonitoka kutoka kwenye uvungu wa moyo wangu mara baada ya kumuona James kwa uzuri zaidi na kuamini kuwa yule kweli alikuwa ni kaka yangu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilishindwa kuelewa nini kimetokea mpaka yeye kurudi katika hali yake ya…
  • MY DIARY (45)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA TANOTULIPOISHIA...Ndio niliona hipo haja ya kuokoka na kuishi maisha ya utakatifu kwa maana nishaishi maisha yote ya kuwa mbali na mungu. Nakumbuka nilipokuwa mdogo kipindi hicho naujua mlango wa kanisani tuisahawahi kufundishwa kuwa mtetezi wa kweli wa maisha ya mwanadamu ni Mungu.Na siku zote alaaniwe mtu yule amtegemeaye mwanadamu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Sio kazi ya…
  • MY DIARY (44)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA NNETULIPOISHIA...Yani alianza kutaka uhusiano na mimi tena uhusinao wa mapenzi.Mda wote alikuwa akiniganda kama luba.Na mimi nilikuwa mjanja sana maana nilijifanya sinywi pombe wala kuvuta sigara.Pia baada ya kugundua kuwa wahusika wengine walikuwa wanajiachia niliamua kujifanya mshauri wa mapenzi na mahusiano.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilikuwa nawasshauri sana mshiriki wa…

MY DIARY (32)

Jina: MY DIARY
Mtunzi: __

SEHEMU YA THELATHINI NA MBILI
TULIPOISHIA...
Lakini kuchepuka kwangu na kuingia mgombani haikumaanisha kuwa sheria ingeniacha hivi hivi.Ilifika mahali ikabidi nizime gari na kutulia tulii kusikilizia nini kitafuata.Tayari nilikuwa nimezungukwa na mapolisi ambao walikuwa wakinifuatilia kwa kutumia pikipiki.Kwa bahati nzuri dereva wa lile gari na yeye alishafika hapo na alishawaambia polisi kuwa mimi naugua ukichaa na nilifufuka kutoka mochwari.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

TUENDELEE...
Kwa hiyo watu wote walozunguka gari walikuwa makini wakiogopa kunisogelea maana mtu kufufuka sio jambo la kawaida. Baada ya kugundua kuwa wananiogopa ilibidi nishuke mwenyewe na kuendelea kufanya vitu ambavyo nilijua kabisa wataamini kuwa mimi nilichanganyikiwa. Nikakumbuka mateso ya selo kipindi kile kwenye kesi ya mauaji ya Msouth hivyo nikaona bila kutumia mbinu lazima watanipeleka polisi.Niliinua mkono wangu mmoja juu na mguu mmoja kama vile nafanya mazoezi.

Bado mbinu hiyo haikusaidia sana kwani kuna mmoja alinifuata a kunikamata akanIfunga pingu na kuniingiza kwenye gari.Nilikuwa mpole na nilishindwa kuelewa kama watanipelka tena hospitali au polisi. Lakini kwa vitu nilivyovifanya walikuwa hawana jinsi ilibidi wanipeleke tu hospitalini. Walinirudisha pale pale KCMC nilipokuwa mwanzo huku nikiwa chini ya ulinzi mkali utafikiri nimetaka kumuua raisi.Magazeti nayo yakapata kitu cha kuandika kuwa msafara wa Raisi waingia doa. Yapo yaliondika kuwa msichana mrembo afufuka na kutia doa msafara wa raisi. Yaani naweza sema nilipata umaarufu kwa mda mfupi sana kwani kila mtu alitaka kujua habari zangu mimi ni nani na ilikuaje mpaka nikapelekwa mochwari.

Basi niliendelea kutibiwa mpaka nikapona na baada ya kupona kabisa nilifunguliwa shitaka la kuendesha gari mwendo kasi na kuvuruga msafara wa muheshimiwa raisi. Kesi iliendelea kuunguruma lakini baadaye kwa msaada wa yule wakili aliyenisaidia kipindi kile kesi hiyo ilifutwa kwa madai kuwa siku ya tukio nilikuwa nimechanganyikiwa. Madaktari nao waliaamua kunisaidia kwa kuandika taarifa kuwa nilikuwa naugua uchizi. Nilimshukuru Mungu kwa yote ambayo yalitokea na kuzidi kufanya kitabu cha kumbukumbu zangu kuwa kikubwa.

Niliendelea na maisha yangu na nilirudi Arusha. Huko nako nilikuta mambo sio shwari ndugu wa marehemu Joyce walichachamaa kutaka ile salooni na kale kaduka wavichukue.Ili kuepusha shari nilikubali kuwaachia vyote na mimi nikaanza upya. Sikuwa na jinsi kwani kuanza upya sio ujinga na kama riziki yangu ipo basi mungu atanijalia nitaipata. Nimepitia majaribu mengi sana hivyo hata hilo niliona kuwa ilikuwa ni muendelezo tu wa historia tata ya maisha yangu. Sikuona haja ya kugombania mali za marehemu maana ilikuwa ni kujitia mikosi tu.Ingawa tulikuwa share hiyo Salooni lakini nilimwachia mungu.

Sikubaki na kitu chochote zaidi ya chumba ambacho tulikuwa tunakaa na Joyce. Niliwaza sana ni kwa vipi nitaweza kuishi Arusha mji wenye gharama kubwa za maisha hili hali sina kitu cha kuniingizia kipato. Hapa sasa nilikuwa sina namna zaidi ya kurudia yale maisha yangu ya zamani maisha ya kutegemea wanaume kwa kujiuza. Ni kazi ambayo marehemu Joyce alinisihi nisiifanyae kwa sababu mwisho wa siku lazima nitaangukia pua lakini sasa ningefanyaje. Ningepata wapi kodi ya kulipia hiyo nyumba.Ningekula nini na je vipi kuhusu mahitaji muhimu ya kike ningeyapata wapi.Ikumbukwe kipindi hicho sikuwa hata na boyfriend wa kunihudumia. Maisha niliyokuwa nikiishi pia yalisbabisha nisiwe na marafiki kabisa wa kike.

Miasha yalibadilka na kuwa magumu na mabaya zaidi. Nikajikuta narudia uelvi na nilikuwa nakunywa pombe kupita kiasi ili kupunguza mawazo. Nilifikiria kujiua na siku moja nilichukua sumu ya panya tayari kwa kujimaliza. Usiku wa siku hiyo niliamaua kujimaliza mara baada ya kuona sina thamani yoyote hapa duniani. Nilisaga vizuri ile sumu tayari kwa kuilamba. Wakati nasali sala yangu ya mwisho kumuomba mungu baba anisamehe kwa makosa yote niliyotenda pamoja na hilo ninalotaka kulitenda la kujitoa uhai nilisikia kama mlango umefunguliwa na mtua akaingia.Ilinibidi nifungue macho na kuangalia ni nani alikuwa ameingia.

Sikuona kitu zaidi ya kusikia sauti yenye mwangwi ya marehmu baba yangu” Leah leahhhhhh leaahhhhhhhhh mwanaaaaanguuuuuuu mwananguuuuuu tafadhaliiiiiiii tafadhaliiiiiiiiiiiiiiiii sanaaa saaanaaaaaaaaa usijiueeeeeeeee kumbukaaaaaaaa baabaaaa aaaa yako nilikuachia chiaaaaaaaaa urithiiiiii thiiiiiiii. Nilitetemeka sana na nilijaribu kupikicha macho ili nione kama nilikuwa naota au ilikuwa laivu. Haikuwa ndoto ilikuwa ni kweli marehemu baba yangu alinitokea na kuniambia nisijiue kwa sababu aliniachia urithi wa madini. Chumba kilikuwa tulivu sana na mawazo ya kujiua yaliniishia.

Nikawasha redio na kufungulia kwa sauti kubwa saana huku hofu ikiwa imenitawala sana.Nilioka nje na kuangalia huku na kule lakini hakukuwa na kitu. Taswira ya utajiri ikanijia na kuanza kujiona ni kama niliyezaliwa upya.Nilipanda kitandani na kulala huku nikimuomba mungu anisaidi kufikia hiyo sehemu ambayo madini yalihifadhiwa na marehemu baba yangu.

Basi maisha ya matumaini yalianza mara baada ya kutokewa na mzuka wa marehemu baba yangu. Siku zikazidi kwenda huku nikiwa napendelea kwenda sehemu mbali mbali za starehe nikihamini kuwa huko naweza kupata marafiki wenye feza. Hali hiyo ikanifanya niwe nakutana na mapedeshee na waliojichanganya nilikuwa nikitembeaa nao kwa kweli. Nitafanyaje sasa maana ingekuwa labda kweteu ni kijiji ningerudi kwenda kushika jembe na kulima lakini nimezaliwa mjini nimekulia mjini na sijui kuhusu kitu kingine chochote zaidi ya kazi ya saloon ambayo na hiyo ndo imeporwa na ndugu wa marehemu yaani baba wadogo wa Joyce.

Sikujibweteka niliendelea kutafuta hela ili nifungue saloon yangu kwa sababu tayari nilishakuwa na uzoefu wa kazi hiyo. Katika harakati hizo ndipo nilipopata nafasi ya kushiriki shindano la miss bonge ambalo lilihusisha wanawake wenye maumbile makubwa hasa makalio.Nilijaza form ya kushiriki mara baada ya kusikia utaratibu ambao ulikuwa ukirushwa kwenye redio ya hapo hapo Arusha inaitwa Triple A. Nilivutiwa na dau neneo la shilini milioni mbili ambalo lilikuwa litolewe kama zawadi kwa mshindi wa kwanza. Nilijiamini kabisa nitashinda shindano hilo kutokana na uzuri wa umbo langu la kibantu. Siku ikafika na shindano likanza huku tukiwa tumevalia mavazi ambayo yalikuwa yakituchora na kuonesha jinsi maungo yetu ya mwili yalivyokuwa. Ni uzalishaji tu sema utafanyaje sasa na ndo ilikuwa ni mwanya wa kuapta hela kiurahisi.

Tofauti na wasichana wengine siku hiyo mimi nilishangiliwa sana kwa sababu nilikuwa ni miongoni mwa wasichana wachache ambao walikuwa hawana vitambi. Ndio wengi waliojitokeza walikuwa na makalio makubwa lakini pia walikuwa na matumbo makumbwa au naweza kusema ni vitambi. Mimi nilionekana mwenye umbo namba nane lenye kuvutia zaidi ya wote walioshiriki shindano lile. Sio majaji sio mashabiki wote waliaamini kuwa mimi nilistahili kushinda shindano lile. Shindano hilo lilikuwa na wazamini wengi sana walowezesha kupatikana kwa burudani mbali mbali zilizowafurahisha watu.

Wakati burudani zikienelea majaji walipiga kura zao zilizowezesha mimi kutangazwa mshindi.Siku hiyo hakukuwa na cha maana sana zaidi ya kujipitisha nyukwaani na kuonesha jinsi gani umejaliwa na mungu kwa kuwa na inye na maungo mengine ya mwili makubwa. Sikuamini kama ningeweza kutangazwa mshindi wa shindano lile kirahisi vile. Nikapewa cheque ya shilingi milioni mbili na zawadi nyingine kama vile simu ya mtandao ambao ulidhamini shindano hilo.

Shindano hilo likanirudisha kwenye ulimwengu wa umaarufu kwa sababu tangia siku hiyo wanaume wengi wakawa wananisumbua kila mmoja akitaka kujiweka. Yaani jamani mwenzenu sijui nilikuwa na nyota gani maana naweza sema ilikuwa ni nyota mbaya ya kupendwa na waume za watu. Maisha yaliendelea huku mawazo yangu yote yakiwa kule kwenye zile Tanzanite ambazo marehemu baba yangu aliniachia kama urithi. Tatizo ambalo lilikuwa likinisumbua Leaha mimi ni kwamba nilipewa jina la kijiji ambako madini hayo yapo lakini sikujua ni sehemu gani hasa yapo.

Ikumbukwe nilishajaribu kwenda sehemu hiyo mara kibao bila mafanikio. Kwa hiyo wazo langu la kurudi kuishi Moshi liliongezeka mara baada ya kuzipata zile milioni mbili. Kwangu ilikuwa ni lazima niishi Moshi ili nifanikishe ndoto yangu ya kuwa tajiri mkubwa sana. Nilifanikiwa kurudi zangu Moshi nikaanza maisha mapya huku nikiwa na wazo la kufungua salooni yangu ya kike.

Lakini hela hile nilishaitumia katika kulipa kodi na mambo mengine madogo madogo ili kufaniksha kupata makazi mazuri maana sikuona haja ya kuishi maisha mabaya hili hali hakuna uhakika wa kuishi miaka mingi.Ilinilazimu kuanza kufanya kazi kwenye salooni za watu lengo ikiwa ni kuonsesha ujuzi wangu, kutafuta jina na wateja na pia kutafuta hela ya kuongezea nifungue salooni yangu

Nilifanya kazi kwa bidii sana jambo ambalo liliniwezesha kupata jina na kuwa maarufu katika fani hiyo ya urembo. Ujue kule Arusha baada ya kutoka rumande Joyce alinipelaka kozi ya Hair dressing and beauty. Umaarufu huo uliniongezea wateja na kujikuta nafanya kazi masaa mengi sana. Wakati naendelea kudunduliza dunduliza likatokea tena shindano lingine la mwanamke nyonga au almaarufu kama inyegwedegwede Kwa mnavyojua tena wanawake wa salooni ndo tunaongoza kwa kupata habari za mjini hivyo basi wapambe wangu walinishauri nishiriki shindano hilo.

Tofauti na lile shindano lilofanyika kule Arusha ili lilikuwa ni shindano la kukata mauno.Yaani ingekuwa ni miaka ya 2015 ningeweza kusema lilikuwa shindano la kucheza ule wimbo wa chekecha cheketua wa Ali Kiba au ule wa nasema nawe wa diamond. Kama kawida sikulaza damu nilijisajili na kuchukua form za shindano hilo na kuzijaza. Na kwa kuwa shindano hilo lilikuwa linahusu kuonesha mauno hivyo nilianza mazoezi ya kucheza musiki hasa ya mwambao kama baikoko, taarabu , kigodoro na mingineyo. Kwa kweli naweza kusema kucheza miziki hii kwangu haikuwa kazi ngumu kwa sababu nilishaanza kuicheza tangia nikiwa mdogo. Siunakumbuka nilishawahi kushinda kashindano kama hako kule club siku ya kwanza kabisa nilipoenda Club nikiwa na mwalimu John.

Nilitafuta CD zilizoonesha watu mbali mbali wakicheza nyimbo hizo. Mbali pia na kuwa na hizo CV pia nilikuwa najitaidi kubuni staili zangu mwenyewe ambazo niliamini kuwa zinaweza kumpagawisha mtu yeyote. Nilikuwa nachanganya staili za kijamaika na hizi za kwetu, sikuacha pia zile za Nigeria hapo nikapata vitu vyangu vya tofauti kabisa. Basi baada ya kujihakikishia kuwa nipofiti kwa mastahili yangu hayo nilisubiri siku ya shindano ifike nikafanye yangu. Siku ya shindano ilifika na mimi nilikuwa miongoni mwa washiriki walioingia tatu bora.

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
68 My Diary Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni