MY DIARY (29)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mtunzi: __
SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Hapo sasa nikazidi kuchanganyikiwa ikabidi nimuulize mama huyo alikuwa akifanyia shughuli zake za kujipatia kipato sehemu gani.? Yule dada akanambia kuwa anafanyia soko la ndizi huko Korongoni. Sikuwa na jinsi nilimuomba anipeleke lakini na yeye alisita sita kwa madai kuwa alikuwa na kazi nyingi za kufanya na bado anatakiwa ampeleke mtoto shule.
TUENDELEE...
Haikuwa shida sana nilimuomba anielekeze ili niende mwenyewe. “mimi sipajui na sijawahi kufika ila ananambiaga anafanya soko la ndizi” alijibu yule msichana jibu ambalo lilinishangaza kidogo. Hivi kweli unaishi na binti wa watu alafu hajui sehemu unayofanyia kazi, je likitokea tatizo yeye atafanyaje sasa.
Hapo nikajua kuwa hata nikimsubiri tuende wote haitosaidia kitu. Nikamuuliza swali lingine Yule “ kwa hiyo dada Joyce hakuja hapa jana?” Akanijibu hapana tangia tuondoke naye siku ile hakurudi tena.
Hapo sasa sikutaka kupoteza mda nilianza kuondoka zangu na moja kwa moja nilienda kituo cha polisi. Nilivyokuwa njiani nilikuwa najiuliza nikifika polisi nitoe taarifa gani. Nilivyofika pale niliwaambia kuwa juzi nilikuwa na rafiki yangu tulikuja naye Moshi lakini mimi nilimuacha na kurudi zangu Arusha. Ilibidi nimwache kwa sababu alinambia kuwa alikuwa akimsubiri rafiki wake wa kiume aliyekuwa akitoka South Afrika. Tatizo hapatikani kwenye simu hivyo nimeenda hapo kituoni kutoa taarifa za kupotea kwake. Polisi waliandika hayo maelezo yangu nikaacha na namba zangu za simu wakanambia kuwa kama watapata taarifa yeyote watanipigia.
Basi niliondoka na kwenda huko soko la ndizi ambapo mama yake mdogo alikuwa akifanyia kazi. Nilizunguka sana hapo sokoni kibanda hadi kibanda lakini baadaye nilifanikiwa kumpata. Nilimueleza kitu kilichotokea na hatua nilizochukua ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa polisi.Mama yake mdogo hakuonekana kuwa na presha kwa alinambia hilo sio swala la tukio la kwanza kupotea kwa Joyce kwani kuna mwaka alishawahi kupotea mwezi mzima. Anasimulia mama huyo kuwa tukio hilo liltokea akiwa bado yupoo kwao na tukio hilo liliwatia sana hofu wazazi wake.
Pamoja na historia hiyo na kauli hizo za mama mdogo bado hazikunifanya niwe na amani ya nafsi na kunitoa mashaka niliyokuwa nayo. Basi kwa kuwa nilishatoa taarifa polisi niliamua kurudi zangu Arusha. Nikiwa njiani kuna namba ngeni ya simu tena simu ya mezani ilikuwa ikipiga “Helow, naongea na Leah” iliuliza sauti hiyo? Ndio nani mwenzangu niliuliza. “Napiga simu kutoka Moshi kituo kikubwa cha polisi, sasa kuna taarifa tumezipata kuhusu msichana mmoja mabaye jina lake bado alijatambulika. Hivyo tunakuomba ufike hapa kituoni ukiwa na picha ya huyo rafiki yako”. Alifafanua afande huyo mara baada ya kujitambulisha
Hapo nilichanganyikiwa kabisa nisijue kuwa nishukie njiani nikatoe picha zilizopo kwenye simu au niende mpaka Arusha nikachukue picha ambazo zilikuwa zimesafishwa. Kwa kuwa gari lilishapiata KIA niliamua kuendelea na safari. Tulifika Arusha na sikutaka kupoteza hata dakika moja nilienda moja kwa moja tulipokuwa tunakaa na nikapekua pekua kwenye albamu yake na kuchukua picha zake mbili za hivi karibuni. Sikutaka kupoteza mda nilirudi zangu stendi nikapanda gari la Moshi na safari ikaanza upya.
Niliona kama gari lilikuwa likienda taratibu kutokana na zile taarifa nilizozipokea kutoka polisi. Nilifika Moshi salama na kwa bahati nzuri kituo cha polisi kilikuwa mita chache kutoka stendi ya mabasi. Nilitembea haraka haraka na moja kwa moja nilifika kaunta na kujitambulisha kuwa mimi ndo Leah na nipo hapo baada ya kuambiwa nije na picha. Na hii ni kutokana na taarifa za kupotea za rafiki yangu Joyce nilizowakilisha hapo mida ya asubuhi. Haya lete hiyo picha ya rafiki yako harakaharaka alisema huyo polisi aliyekuwa akinisikiliza.Wakaingia nazo kwenye chumba cha intellegencia.
Nikawa nawasubiri hapo nje kwa maana nilikuwa sijui nini kilikuwa kikiendelea hapo nje. Nilisubiri kama dakika kumi na tano hivi na baadaye niliitwa ndani na kupewa taarifa. Ulisema wewe ni nani yake hilo ndilo lilikuwa swali la kwanza kuulizwa: Mimi ni rafiki yake ambaye nina kaa naye Arusha. Wakaniuliza tena “wewe na Joyce manajishughulisha na shughuli gani?”.Nilimjibu kuwa sisi ni wajisariamali wadogo wadogo. Mnafanya shughuli gani hasa? Tuna saloon ya kike na pia tunaduka linalouza vitu vya urembo vya wasichana. Sasa ndugu naomba unisikilize kwa makini alisema yule polisi mara baada ya kurizishwa na maelezo yangu.
Rafiki yako kwa sasa ni marehemu na mwili wake umekutwa kwenye msitu wa tembo. Uchunguzi wa awali wa kipolisi na kitabibu unaonesha kuwa marehemu aliuwawa kwa kupigwa risasi na kabla ya hapo inaonesha alibakwa na kuharibiwa vibaya sehemu zake za siri. Kwani inaonesha aliingiliwa kinyume na maumbile. Tunaomba uwe mvumilivu kwa taarifa hizi lakini polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa swala hilo. Watuhumiwa wantafutwa kwa udi na uvumba.
Rafiki yako kwa sasa ni marehemu na mwili wake umekutwa kwenye msitu wa tembo. Uchunguzi wa awali wa kipolisi na kitabibu unaonesha kuwa marehemu aliuwawa kwa kupigwa risasi na kabla ya hapo inaonesha alibakwa na kuharibiwa vibaya sehemu zake za siri. Kwani inaonesha aliingiliwa kinyume na maumbile. Tunaomba uwe mvumilivu kwa taarifa hizi lakini polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa swala hilo. Watuhumiwa wantafutwa kwa udi na Mwili ulianza kunitetemeka machozi yakinibubujika kama mtu aliyechomwa na mkuki moyoni.Nilishindwa hata kuongea machungu ya nafsi yalinizidi nikatamani hata nimpige yule polisi aliyekuwa akinipa taarifa. Sikuamini nilichokisikia na niliona ni uwongo tu, Joyce yupo hai huyo wamemfananisha tu. Kufikia hapo machozi yalikuwa yakinibubujika sikuamini nilichosikia. Nilihisi labda nipo ndotoni. Nikamuuliza yule polisi je naweza kuuona huo mwili wa marehemu na mimi nithibitishe kwa macho yangu kuwa Joyce ni marehemu?
“ Kwa sasa mwili wa marehemu umepelekwa hospitalini kwa uchunguzi zaidi” alinijibu polisi huyo. Akageuza kumputa yake na kuonesha na kunionesha picha za marehemu Joyce kisha akachukua zile nilizokuja nazo akaziscan na kuziingiza kwenye program moja ya kinteleginsia hivyo nikaona jinsi wanavyozifananisha.
Teknolojia hii ilikuwa ya hali ya juu sana hivyo sikuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana na ukweli ambao ulikuwa mbele yangu.
Polisi alinambia kuwa nitaendelea kusaidia polisi lakini hawataniweka ndani kwa sababu reflection ya maoch inaonesha mtu wa mwisho kuwa naye alikuwa ni mzungu. Basi nilimpigia mama yake mdogo lakini alikuwa bado hapatikani. Nilimwandikia meseji kumuelezea kilichokuwa kinaendelea. Basi nilielekea huko
hospitali ambapo mwili wa rafiki yangu ulikuwa umehifadhiwa. Tuliongozana na afande huyo ambaye alinipa taarifa na pia alikuwa akinifahamu sana kutona na ile kesi yangu ya kipindi kile ambayo iliniweka ndani kwa mda mrefu sana. Cha ajabu na cha kushangaza sikuwa na namba za simu za ndugu wa Joyce hata mmoja zaidi ya mama yake mdogo. Nikamkumbuka yule mdogo wake lakini sikujua alikuwa wapi kwa wakati huo.
Tulipokuwa hospitalini niliwasiliana na yule wakili aliyekuwa akinisaidia kwenye ile kazi yangu. Nilimueleza kinaga ubaga kitu kinachoendelea. Akanambia yupo Moshi na tukio hilo limemshtua sana hivyo ataacha shughuli zake zote na kuja hapo hospitalini ili aweze kunisaidia kwa sababu polisi sio wa kuamini sana wanaweza kubadilika na kukuweka ndani kwa madai kuwa wewe ni mtu wake wa karibu na lazima ungejua alikuwa na nani dakika chake kabla ya umauti kumkuta.
Nilimwelewa sana wakili lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kuongozana tu na polisi na kwenda nao KCMC. Ndio wangeweza kuniweka ndani ila nilikuwa tayari kwa lolote nisingeweza kukimbia kwenye tukio la rafiki yangu Joyce, ukizingatia mimi na yeye tulishaamua kuishi maisha yetu ya bila ndugu wala nini. Mimi ndi yeye na yeye ndo mimi, wawili kama dunia yetu wenyewe. Madaktari nao walituambia kuwa mwili wa marehemu pia unahitajika kupasuliwa tumboni kwa uchunguzi zaidi. Hapo sasa sikuelewa kwa sababu maelezo ya awali yalisema kuwa aliuawa kwa kupigwa risasi sasa wana mpasua wa nini kwanni aliuwawa kwa sumu?
Haya na maswali mengine magumu ilinibidi nimuulize yule mpelelezi. Na yeye alinijibu kwa kifupi haina shida wacha wafanye kazi yao na ni vizuri kumsubiri mkemia atasemaje ili tujirizishe zaidi. Polisi huyo alinambia kuwa kwa kuwa rafiki yake nimepatikana hivyo basi zoezi la upasuaji litafanyika kesho.
Alinambia niende nikawape taarifa ndugu zake wafanye taratibu za mazishi kwa sababu mwili ukishapasuliwa unatakiwa uzikwe siku hiyo hiyo. Kauli hiyo ilizidi kunichanganya sana nisijue mwili wa Joyce utakwenda kuzikwa wapi.
Sikutaka kupoteza mda nilikwenda moja kwa moja mpaka soko la ndizi mahali ambapo mama yake mdogo na marehemu Joyce alikuwa akifanyia kazi. Nikazidi kupagawa ila sikukata tamaa na kuchoka bali nilipanda gari mpaka majengo. Kwa bahati nzuri niimkuta akijiandaa kwenda kwenye sendoff. Hapo kimoyomoyo nilisema asante Mungu. Alivyoniona alishtukana sana na swali la kwanza aliniuliza mbona macho mekundu hivyo na tena yamevimba.
Hapo akawa amenitonesha kidonda na machozi yakaanza kunitoka huku nikishindwa kuvumilia na kupiga ukunga wa kilio. Kilio hicho kiliwashitua mpaka majirani waakasogea ili kujua nini kilikuwa kimetokea. Kwa ufupi niliwaeleza kuwa Joyce hatukuwa naye tena duniani.Kauli hiyo ilimfanya mama mdogo na yeye ashindwe kuvumilia akaangua kilio. Mama mdogo huyo alilia sana na naweza sema kuwa alichanganyikiwa kwa sababu Joyce pia hakuwa na mahusiano mazuri na ndugu yake kwa sababu tangia mama yake mzazi afariki hakuwahi kwenda kwao hivyo hatukujua mwili utawekwa wapi. Ndugu pekee ambaye Joyce alikuwa akiwasiliana nae na kuelewana nae ni mdogo wake ambaye yupo mwanza.
Huyu ni yule ambaye alizalishwa kipindi akiwa shule na mbaya zaidi mwanaume aliyempa mimba aliikataa. Kwa mujibu wa mama mdogo wake huyo na Joyce aliamua kurudi chuo mara baada ya mtoto wake kufariki. Sikubahatika kuliua hilo mapema ila niliumia pia kusikia mtoto aliyesasabisha yeye kuchukiwa na familia yake alifariki. Sijui familia yao ilikuaje kwa sababu Joyce alitengwa na familia huyo mdogo wake naye alitengwa na familia. Ilibidi nichukue namba za huyo mdogo wake na kumpa taarifa za msiba
Baada ya hapo Nnilimwomba mama mdogo ajikaze na kuwatarifu ndugu wengine habari hizo za msiba.Tulisaidiana hivyo hivyo maana sio siri kila mmoja alikuwa na uchungu sana kutokana na mazingira ya kifo hicho. Habari zilizidi kusambaa kwa kasi na majirani walianza kukusanyika hapo kwa mama mdogo.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni