MY DIARY (30)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mtunzi: __
SEHEMU YA THELATHINI
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Baada ya hapo Nnilimwomba mama mdogo ajikaze na kuwatarifu ndugu wengine habari hizo za msiba.Tulisaidiana hivyo hivyo maana sio siri kila mmoja alikuwa na uchungu sana kutokana na mazingira ya kifo hicho. Habari zilizidi kusambaa kwa kasi na majirani walianza kukusanyika hapo kwa mama mdogo.
TUENDELEE...
Msiba ni msiba tu na ukitaka kujua binadamu wana roho mbaya ni pale tulipowasiliana na baba yake Joyce na kumpa taarifa za msiba.Jibu alilotoa kwa kweli lilikuwa ni la kukatisha tamaa kabisa. “Alituambia tutafute pa kumzika kwa sababu yeye hamtambui kuwa ni mwanaye.
Lakini baba zake wadogo wao walikuja juu mara baada ya kuelezwa habari za msiba na mazingira yaliyotokea. Wao walisisitiza kuwa wanakuja Moshi na watajua nini kifanyike mara baada ya wao kuwasili.Ikumbukwe jambo moja tu ndo lilikuwa linatuumiza kichwa ni kwamba msiba tutaupeleka Arusha au utabaki hapo Moshi kwa mama mdogo. Kuna baba mdogo mmoja yeye alitoa wazo kuwa tuwaombe polisi na madakatri kwamba wasimfanyie upasuaji watupe siku moja zaidi ili tuweze kujipanga kwa mazishi.
Wazo hilo mimi binafsi nililinunua moja kwa moja kwa maana lilikuwa na mashiko. Kwa kuwa mda ulikuwa umeenda sana mama mdogo alivua sare ya send off na taratibu za mazishi zikawa zimeamishiwa hapo kwa mda.Jina la Joyce mtaani hapo alikuwa geni kwa sababu best yangu huyo alishawahi kukaa sana hapo na hiyo ni mara ya mama yake mzazi kufariki na yeye kugombana na baba yake.Historia inaonesha kuwa baba yao na kina Joyce alioa mwanamke mwingine mara baada ya mama yao kutoroka na masharti yalipozidi kuwa magumu Joyce na mdogo wake waliamua kuondoka nyumbani na kuja kuishi kwa mama yao mdogo.
Hapa lazima tujifunze kitu kama wazazi kuna umuhimu wa kuweka misingi mizuri ya kifamilia lasivyo watoto watateseka sana pindi tu wazazi watakapoitilafiana au punde tu mmoja wao atakapoiaga dunia.Ebu fikiria kauli kama hiyo eti baba yake hataki msiba upelekwe nyumbani kwa sababu yeye hamtambui kama ni mwanaye.Ukishazaa umezaa haijalishi nini kimetokea au kilishawahi kutokea damu yako ni damu yako tu. Hii iliniuma sana nikajikuta na mimi naujiuliza maswali hivi na mimi nikifa leo nitaenda kuzikwa wapi. Au nitazikwa kama mzoga usiokuwa na ndugu dini wala kabila.
Sikuwa na majibu ya maswali hayo zaidi ya kububujikwa na machozi. Sikujua nini itakua hatima ya maisha yangu maana Joyce ndo alikuwa rafiki ndugu shoga na muhimili mkubwa sana katika maisha yangu. Hivyo kuondoka kwake duniani ni pengo kubwa zaidi hata ya kufiwa na wazazi. Siku ilisha hivyo na sikuweza hata kula siku hiyo japo nilikuwa sijala tangia asubuhi.Mama mdogo alinisihi sana nile lakini ilishindikana kwa sababu sikuona thamani ya chakula kwa wakati huo.
Asubuhi na mapema baba zake wadogo walishafika na tukaanza kupanga taratibu za mazishi. Walitueleza wazi kuwa wamejaribu kuongea na kaka yao juu ya kupeleka msiba Arusha lakini amekataa katu katu hivyo basi ili kuepuka gharama walisema msiba uletwe hapo kwa mama yake mdogo. Mama yake mdogo alikubali lakini aliuliza huyo mtu atazikwa kwa imani gani? Hapo palikuwa pagumu kidogo kwa sababu mama yake mdogo Joyce alikuwa ni mlokole na Joyce yeye alikuwa ni mpagani maana hakuna kanisa au msikiti aliokuwa akisali. Baba zake wadogo kwa kurahisisha mambo wakasema swala la imani sio tatizo kwa sababu sote ni wamoja na mungu ni huyo huyo yunayemwabudu na kumtumikia.
Ingawa wao walichukulia kirahisi jambo hilo ila mimi binafsi nilijua kabisa jambo hilo lingeleta utata mkubwa..Mama mdogo saa hiyo hiyo akaondoka na kwenda kuongea na mchungaji ili aone kama anaweza kumsaidia kwa jambo hilo.Mchungaji wao naye alitia ngumu kweli kwa madai kuwa hawezi kumzika mtu ambaye sio muhumini na mshirika wao.Akasisitiza kuwa atafanya hivyo kama atapata kibali kutoka kwa mchungaji wa kanisa ambalo marehemu alikuwa akisali hapo alimaanisha Arusha. Mama mdogo ilibidi aniulize mimi “hivi wewe na rafiki yako marehemu huko Arusha mlikuwa mkisali kanisa gani’? Nilimjibu kwa kifupi kuwa sisi ni zaidi ya wapagani kwani huko Arusha hatukujua mlango wa kanisa ulikuwa ukielekea wapi.
Mambo yakazidi kuwa magumu sana na tulibaki tunaangaliana tu.Sikuona mantiki ya mchungaji kumfanyia ukatilii mama mdogo kwa sababu mimi niliamini kuwa ukimzika mtoto wa muhumiini wako ni sawa tu na kumzika yeye.Hapa na mimi nilijifunza kitu kingine katika maisha.Kuwa hizi dini nazo sio za kuzipuuza maana ukifa unaweza kuzikwa kama mzoga tu.Baba yake mdogo akatoa wazo kuwa kuna rafiki yake ambaye ni mchungaji hivyo anaweza kumwomba aje hata amsomee sala ya mwisho. Nia ilikuwa aje tu nyumbani amfanyie sala marehemu kisha tumalize swala hilo.Lakini cha ajabu majibu nayo kutoka kwa mchungaji rafiki yalikuwa ni hayo hayo ya kukatisha tamaa.Hapo nikajua dini nazo siku hizi ni shida.
Muda ulizidi kuyoyoma na watu walizidi kukusanyika hapo na hii ni mara baada ya kupewa taarifa kuwa msiba utaletwa hapo.Baadaye yule mchungaji rafiki yake yule baba yake mdogo na marehemu alipiga simu na kusema ingawa utaratibu hauruhusu kufanya hivyo yaani kuzika mtu ambaye sio mshirika lakini kwa sababu matatizo yametokea na yeye binafsi amebahatika kusoma habari hiyo kwenye gazeti la visa na mikasa hivyo basi ameamua kukata shauri na atakuja kufanya ibada ya mwisho ya kumuaga marehemu.
Taarifa hiyo ilikuwa ni zaidi ya faraja kwa sababu sikupenda au sio jambo zuri kwa mtu kuzikwa kipagani au kienyeji. Sio jambo jema kabisa mtu kuzikwa kama mzoga na hata kama alikuwa hasali bado sio kazi yetu kuhukumu hiyo ni kazi ya muumba mbingu na nchi. Hapo pia tulikuwa tukisubiri majibu ya polisi juu ya maombi yetu kuwa mwili usifanyiwe upasuaji siku hiyo hili kuruhusu ndugu wa marehemu waliokuwa mbali waweze kuhudhuria mazishi hayo.
Nilimpigia tena afande na alinihakikishia kuwa ombi langu limekubaliwa ila tujiandae hela ya kulipia mwili wa marehemu kukaa mochwari. Sikuwa na cha kumpinga na hapo nikakumbuka kuwapigia wale wafanyakazi wake wa salooni na kuwapa taarifa za msiba. Niliwaambia wafunge saloon na waje Moshi kwenye msiba na pia watuletee hizo hela za siku mbili ili zitusaidie hapo msibani. Taarifa hizo ziliwashitu sana hao wadada na walinitupia lawama kwa nini sikuwambia tangia jana. Niliwajibu kwa kifupi kwamba hata mimi sikuwa kwenye hali nzuri cha msingi ni kwamba kwa sasa sio mda wa kulaumiana wao waje tu msibani.
Mdogo wa marehemu kwa jina Marry naye alinipigia simu na kuniambia kuwa tayari alishapanda gari kutoka mwanza na kuja Moshi hivyo atawahi mazishi.
Hapo pia nikamkumbuka Yule kipopa ambaye alizaa na Joyce ingawa walishaachana lakini niliona ni jambo jema kumpa taarifa kwani huyo ni mzazi mwenzie. Naye taarifa hizo zilimshitua sana akanambia atakuja kwenye mazishi na mwanaye ili aje amuage mama yake. Wazo hilo lilinishitua sana kwa sababu mtoto wao alikuwa bado ni mdogo sana ndo kwanza alikuwa Nursery school. Ilibidi nimpigie tena na kumwambia naomba hasije na mtoto kwa sababu atakuwa anamchanganya kisaikolojia. Na yeye alinijibu kwa kifupi kuwa ni wazo zuri kwa sababu hata yeye alifikiria hivyo kabla
Basi tuliendelea na taratibu za mazishi na kesho ikafika marehemu akakamilishiwa taratibu zote za uchunguzi na sisi tukakabidhiwa mwili wa marehemu tayari kwa kuupumzisha kwenye nyumba ya milele. Basi mchungaji yule aliyejitolea kutufichia aibu alifika akamfanyia ibada ya maziko kisha tukampumzisha rafiki yangu Joyce kwenye chumba chenye giza chumba cha sita kwa sita chumba ambacho hakika kila mwanadamu atakipitia. Siku hiyo nililia sana mpaka machozi yalikauka na ilikuwa ni siku ya 3 sasa sijala kitu chochote zaidi ya maji na soda.
Maziko yalifanyika saa saba mchana na tuliamua kuvunja matanga siku hiyo hiyo ili kuruhusu watu watawanyike na kuendelea na shughuli zao. Kwa kweli yule mwanaume aliyezaa na Joyce alitusaidia sana na alitoa hela nyingi sana.Watu walikula vizuri na kunywa vizuri kidogo ikanipa faraja kuwa safari ya mwisho ya Joyce ilikuwa ni ya matumaini. Lazima nimshukuru kwa sababu alituepusha na aibu ambayo ilikuwa itukute. Ilivyofika saa kumi na moja jioni watu walianza kutawanyika na hiyo ni mara baada ya MC kutangaza kuwa msiba ulikuwa umemalizika.
Baadaye Yule mzazi mwenza na marehemu Joyce aliitisha kikao ambacho kilihudhuriwa na mimi, yeye, na ndugu wa marehemu.Yule baba alikuwa na busara sana kwani alianza kwa kusema “nimeona tufanye kikao hichi pamoja kwa sababu nikiwaacha wenyewe nazani mnaweza msielewane. Mimi nimezaa na ndugu yenu na siku zote nilikuwa sijui ndugu wa marehemu zaidi ya Leah.
Lakini leo nimejifunza kitu na kugundua kumbe Leah hakuwa ndugu wa damu wa marehemu bali ni rafiki wa karibu. Aliendelea kuongea baba huyo kwa kusema “Nilikutana na marehemu wiki mbili zilizopita na alinieleza siri kubwa ya maisha yake ambayo hakuna mtu yeyote anayeijua zaidi ya rafiki yake Leah.Hapo
watu wote walinyanyua masikio juu ili kusikia ni nini mtu huyo anataka kutuambia. “Marehemu nilivyokutana naye wiki hizo mbili alinambia kuwa Leah ndo mrithi wa mali zake na ndio atakuwa mama na mlezi wa Lucky mtoto niliyezaa na marehemu.
Hapo ndugu zote wa marehemu walimtolea mimacho na kumshangaa.Akaendelea kusema siri hii hata mama yake mdogo anaijua. Hapo baba mdogo mmoja wa marehemu akamkatiza kwa kumwambia ebu usimsemehe mama yake mdogo kwa sababu yupo hapa hivyo kama ana jambo lolote analijua kuhusu marehemu aseme mwenyewe.Mama mdogo akasimama na kusema “marehemu mwanangu wakati wa uhai wake alinieleza kuwa yeye ni muhathirika wa ukimwi na alikuwa akiishi kwa matumaini. Hapo kila mtu alifunga mdomo kwa sababu mama mdogo alipasua jipu na kukata mzizi wa fitina. Hivyo marehemu alinikabizi akaunti moja ambayo ni fixed deposited account na hiyo alimfungulia mwanaye Lucky. Na alisisitiza kuwa hata baba wa mtoto anatakiwa apewe namba za akaunti ili awe anamuwekea mwanaye akiba.
Pia marehemu alinambia kuwa anamiliki saloon huko Arusha na endapo akifa mda wowote basi salooni hiyo itabaki mikononi mwa Leah ambaye ndio msimamizi na mama mlezi wa mwanaye. Mama mdogo hakuishia hapo aliendelea kwa kusema “marehemu pia alinieleza kuwa ana miliki duka la vitu vya urembo wa kike ambalo pia Leah analisimamia ila hilo apewe mdogo wake Marry ambaye yupo hapa. Mama mdogo huyo mara baada ya kuyasema hayo alikaa zake chini. Baba mdogo ambaye hakurizika na maelezo hayo alisimama na kusema “kwa hiyo kama marehemu alijua kuwa atakufa hivi karibuni kwani nini hakufuata taratibu za kisheria za kuandika wosia na kurithisha mali.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni