MAMA MWENYE NYUMBA (63)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA SITINI NA TATU
Alisema bwana Magige akiwa na uakika kabisa mke wake hato elewa kitu, huku ana fungua sms nyingine toka kwa AnifahSASA ENDELEA...
‘Sijawai kukutania toka ume nisusa, lakini ukweli ndio huo, demu wako kicheche,’ alimaliza kuisoma na kuifuta, huku moyoni akiuguria maumivu ya wivu akiisi kuwa mida hiyo Rose ana shughulika na mtu mwingine, yani wivu ulio mpata kuliko angekuwa amesikia kuwa mke wake ndie anamsalitiBaada ya pewa maagizo na mkuuwake wakazi, moja kwamoja Said akaelewa mkuu wake huyo anamaanisha nini, maana alikuwa anaujuwa huusiano haramu wa mkuu wake na mrembo Rose ambae kwa upande mwingine nayeye ni afande wake pia, Said ambae mida hiyo alikuwa ndani ya nyumba yake line Polisi quarters (kotaz), akaondoka mala moja akiwa amevalia kptulah yake ya kaki, na tishert ya man chester united, akaenda kituoni aliko liweka gari la boss wake, safari za kumsaka Rose ambae ndie afisa wa zamu, kituo cha kwanza kabisa kilikuwa ni polisi wilaya, jirani na uwanja wa maji maji, akashuka kwenye gari na kuwa kuta wakina Anifah na mwenzie wakiendelea na kazi, ambapo zamu yao ingeisha saa nne usiku, na hao wote ni askari wa chini yake, wakamsalimia kijeshi, na yeye akaitikia
“Vipi jamani asfisa wa zamu waleo amesha pita hapa?” aliuliza Said, “amesha pita nazani ameelekea benk, maana ailtokea upade huu na ameelekea huku” alijibu yule askari wa kiume, huku Aifah akiwa kimya anafurahi kimoyo moyo akijuwa kuwa Saidi amesha tumwa kumfwatilia, “ok! nina maagizo yake wacha nimfwate” alisema Said akitaka kuondoka, “yupo na gari lake lile jeusi, ukiliona tu ujuwe kuwa ni yeye” aliongea Aifah akiwa na maana ya kumpa msaada zaidi Said wa kumpata afande Rose, hapo ndipo Said alipo ondoa gari kuelekea benk, dakika kumi mbele alikuwa anafika benk, akumkuta Rose wala gari lake, akaulizia akaambiwa kuwa ametoka mda mfupi ulio pita, wakimwonyesha njia aliyo elekea, kitendo bila kuchelewa Said akaondoa gari, na kendelea kuzunguka kumtafuta afande wake Rose, ambae ni nyumba ndogo ya afande Magige Chacha, huku njiani akipokea simu na sms toka kwa boss wake akiulizia maendeleo ya msako wa Rose
Baaada ya kuzunguka vituo vitatu vya ukaguzi wa afisa wa zamu, Saidi wakati ana elekea kituo cha nne ambacho lazima afisa wa zamu akitembelee, ikulu ndogo ya mkoa, atua chake kabla ajakifikia aliliona gari la afande Rose, likitoka maali hapo na kurudi katikati ya mji, akaanza kuli fwatilia Toyota Harrer, kwa umakini mkubwa, kule liliko elekea, huku Said akitoa taalifa kwa boss wake kuwa amesha liona gari la Rose na sasa analifwatilia, “yupo na nani?” aliuliza afane Magige, “bao sija mwona mtu alienae kwenye gari na sija juwa kama anamtu, lakini nalifwatilia” aliongea Said, “ok! akiksha una fwatillia kila kitu” alisisitiza boss Magige, Said aliendele kulifwatilia gari la Rose, kila lilipo elekea, wakikata kushoto nayeye anao , wakikata kulia yumo, mpaka alipo waona wana ingia kwenye viwanja vya hotel moja kubwa Nyumbani Peace Lodge, ni sehemu iliyo changamka sana
Upande wanje walionekana watu wengi sana wakiwa wame kaa kwenye viti vyao wamezunguka meza zilizo tapakaa vinywaji mbalimbali, Said aliliona gari la Rose likisimama kwenye maegesho ya hotel hiyo yeye akisimama upande wapili wa barabara, nakushuka kishaakaelekea kwenye ile hotel, macho yake yakiwa kwenye gari la Rose, akaona mlango wa upande wa abiria ukifunguliwa na akashuka kijana mmoja mdogo, na kuufunga ule mlango kisha akaelekea ndani ya ile hotel, said kwa kujificha sana asionekane na Rose, alimfwatilia yule kijana kule ndani, bahati ikawa upande wake, alimkuta yule kijana akiulizia vyumba “kuna vya elfu ishilini na tano, na vya hamsini elfu, nani kunakila kitu, na asubuhi una pata kifungua kinywa” aliongea dada muhudumu wa vyumba, huku Said akiwa amesha sogea karibu kabisa, kama vile na yeye ni mteja
“Vya elfu hamsini vipoje, na vya elfu ishilini na tano vipoje?” said alimsikia yule kijana akiuliza, “vyote vina vitu vinavyo fanana, tofauti ni kwamba, cha elfu hamsini, kina chumba na sebule” alijibu yule dada huku akimgeukia Said “samahani anko wacha nimalizane na huyu nitakusikiliza” alisema yule dada, “hakuna shida dada, endelea nae mimi nasubiri” alisema Said akijiwa anesimama pamoja nao, pasipo Yule kijana ambae ni Edgar kujuwa kama anafwatiliwa, “ok! naomba cha elfu ishilini na tano” aliongea Edgar, kisha akaingiza mkono mfukoni na kutoa kiasi cha pesa za kulipia chumba, huku yule dada akitoa kitabu cha kuandikisha wageni wanao lala hotelini hapo
“Ok! anko nawewe unaitaji cha bei gani?” aliuliza yule dada akimwambia Said, huku anapokea fedha toka kwa Edgar, kisha aka mpa kiabu aandike, “ngoja amalize ksha tutaongea maana mimi naitaji shot time” aliongea Said akitazama kwa makini sana maandishi ya Edgar, “hapa kwenye namba ya chumba niandikeje?” aliuliza Edgar akimtazama dada mhudumu, “ebu kwanzaaa... andika namba sita B,” alisema yule dada huku akiangalia kwenye sehemu ya kutundika funguo, kisha akaitoa funguoa moja yenye kibao kido kilicho andikwa 6 B, juu yameza kubwa ya pale mapokezi, mala simu ya Said ikaanza kuita “nakuja mala moja dada yangu” alisema Said akitoa simu yake huku akiogea pembeni, ambapo aliona Edgar asinge sikia maongezi yake
“Ndio boss... ndio nipo hapa Nyumbani peace... ndio wanachukuwa chumba, ndiyo ndiyo... nakuja sasa hivi kukuchukuwa.. nimeishika mpaka namba ya chumba... nakuja sasa hivi sawa boss nawapitia.. we wapigie kabisa..” alimaliza kuongea Said, nakukata simu, kisha akaanza kurudi mapokezi “samahani dada nakuja nime pigiwa simmu naitajika sehemu mala moja,” alisema Said huku akimshuhudia yule dada mhudumu, akichukuwa funguo za chumba kutoka mezani, nakuongozana na Edgar kwenda kuonyeshana chumba, said akaondoka zake na kuelekea nje, akitokeza kwenye sehemu ambayo watu walikuwa waejaa wakiendelea na starehe zao, akanyoosha moja kwa moja kuelekea nje ya eneo ilo akilifwata gari leke alipo liegesha
Mida ya saa nne za usiku Suzane na Seline walikuwa wamesha maliza kula mapocho pocho waliyo andaliwa nyumbani kwa mzee Haule na mkewake, japo haya kunoga sana kutokana na tukio la Edgar kukamatwa na polisi, Suzane na Selina wakaaga huku mzee Haule akisisitiza kuwa wasubiri hiyo kesho wajuwe kinacho endelea, ikiwezekana waende wakambe shauli hilo liwe la kifamilia zaidi, na kuliondoa polisi, nusu saa baadae Suzane na Seline walikuwa wamesha fika nyumbani kwa Seline, huku mda wote Suzane akinung’unika juu ya matukio yanayo mkuta mpenzi wake, huku akizingatia alitegemea sku waleo kufaidi dudu aliyo ikosa si zaidi ya tatu, maana toka akutane na Edgar Suzane hakuwai kuikosa dudu atasiku moja, tena alikuwa anapewa zaidi ya mala moja kwa siku, ukiachia siku tatu alizo wai kuingia kwenye sikuzake kabla hajashika ujauzito
“Ngoja kesho nikatoe kisi chochote cha fedha wamwachie Eddy wangu” aliendelea kunung’unika Suzane, “tena yule mwanamke mwenye vinyota ana roho mbaya yuleeee, yani nimemchukia ghafla” aliongea Suzane kabla ajastuliwa na simu yake iliyo ita, akaitazama namba iliyo mpigia ilikuwa ngeni, akaipokea “hallow..” aliongea Suzane baada ya kupokea na kuweka simu sikioni, “shikamoo dada Suzie” ilikuwa ni sauti ya Joyce, “malahaba Joyce mambo?” walisalimiana vizuri kisha Joyce akamsimulia Suzane kuwa amekutana na Sophia na Sophia anaonekana kuchukia kuondoka kwao yeye na Edgar, huku Joyce akificha wasi wasi wake juu ya Sophia kumtaka Edgar, “achana nae huyo, wewe ukiwa na lolote nijulishe nahii namba yako nina isave”
Sophia kiukweli taalifa ya Suzane kuama dar ilimchanganya sana, “inamaana ndio na mkosa Edgar hivi hivi?” aliwaza Sophia akiwa chumba kwake amekaa kitandani huku meza ndogo ya chumbani kwake ime zungukwa na chupa nyingi za bia juu na chini, na chupa kadhaa zikiwa zimesha nyweka, “lakini atakama nikiwa nae si nitakuwa na share na mama” aliendelea kuwaza Sophia, “lakini bola alivyo ondoka, maana mwisho wasiku mimi na mama tunge kuwa vimada wa mwanaume mmoja, na kwanjisi mtoto alivyo mtamu yule sidhani kama mama ange kubari kuniachia” aliwaza Sophia huku akichukuwa simu yake na kuandika ujumbe, ‘Edgar na Suzane wame amia Songea’ kisha akaituma kwa mama yake’......
Sms hiyo ilimkuta mama Sophi akiwa pembeni ya kitanda cha mumewe pale Tumbi Hospital, “pumbavu, huyu Suzie anawazimu nini? kwanini ame amkimbiza Edgar, anataka sisi wenzake tukose utamu, ngoja nitajuwa lakufanya” aliwaza mama Sophia baada ya kuisoma sms ya mwanae Sophia, mama Sophia ambae alikuwa anasubiri asubuhi ifike amchukuwe mume wake waondoke kuelekea nyumbani, ambako ane uguziwa hapo, aliendelea kuwaza namna atakavyo weza kuonana na Edgar, “nita mpata tu” liwaza mama sophi akimtazama mume wake ambae alikuwa amejilaza kitandani amepitiwa na usingizi
Said baada ya kutoka ndani ya Hotel na kuingia kwenye gari, mala simu ikaita akaitazama alikuwa ni mzee Magige, akaipokea, huku macho yake akielekeza kule Hotelini, akamwona Rose akishuka kwenye gari na kuelekea ndani ya Hotel huku akiwa kwepa watu wawili mschana na mvulana waliokuwa wameshikana kimahaba, huku wakiyumba kwa ulevi “naam boss” aliitikia na mzee magige akamwambia kuwa amesha wataalifu askari watano kule line polisi, awapitie atawakuta kituoni wakimsubiri, “sawa boss, tena namwona Rose anaingia hotelini, wacha nifanye haraka ni wa pitie kisha nije nikufwate”
Aliongea Said huku akimwona Rose akipotelea ndani ya jengo la Hotel, huku akizibwa zibwa na wapenzi wawili ambao nao walikuwa wananaingia humo ndani huku wakiwa wame shikana mikono wakipepesuka kwa ulei, lakini aikumzuwia Saud kumwona Rose alie kuwa amevalia sale za kazi, akakata simu na kuwasha gari kisha akaondoa gari kwa fujo akinusulika kuligonga gari moja Toyota Harrer jeusi kama la Rose lililo kuwa linataka kuingia Nyumbani Lodge, nusu saa baadae alikuwa pembeni ya kituo cha polisi cha wilaya akiwa chukuwa askari watano wenye maumbo ya ki bouncer kweli kweli, walio vallia sale zao za polisi, bila kuchelewa wakajaa kwenye Land cruzer V8, safari ikaanza ya kuelekea nyumbani kwa mzee Mgige
Wakati huo bwana magige alikuwa sebuleni na mke wake, “haaaa kazi nyingine hizi ni usumbufu sana” alisema mzee Magige akisimama huku akijisonya sonya
NAOMBA SAPOTI, KUNA MATANGAZO(ADS) YANAJITOKEZA KWENYE APP YETU, LIMOJA LINAJAA KWENYE KIOO CHAKO JINGINE LINANG'ANG'ANIA HAPO CHINI KABISA, BONYEZA JAPO MARA 2 AU 3 KILA UKIFUNGUA SIMULIZI HIYO ITANIPA NGUVU YA KUENDELEA ZAIDI NA SIMULIZI ZETU🙏🙏
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA SITINI NA NNE
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni