MAMA MWENYE NYUMBA (70)
Zephiline F Ezekiel
4 min read
SEHEMU YA SABINI
“Afadhari, dah! alitaka kuni changanya huyu kichaa” alisema Suzane akimwambia Edgar, ambae mda wote alikuwa anaendesha gari huku akifwatilia maongezi ya mke wake, “nani huyo sophia?” aliuliza EdgarSASA ENDELEA...
“Ndiyo eti alisema anataka kuamia Songea,” hapo Edgar na yeye aka cheka kidogo, una cheka unazani mazuri hayo?” alisema Suzan akimpiga kikofi kidogo Edgar, kwenye bega lake la kushoto, Edgar akaachia tena kicheko “kwahiyo mwezi wa tano tunafunga ndoa?” aliuliza tena Edgar baada ya kumaliza kucheka, “ndio, una taka mpaka tupate mtoto mwingine akute bado atujafunga ndoa, alafu mwanamke wako amejifungua mtoto wa kiume” aliuliza Suzane huku akifungua data, kwenye simu yake, zikaanza kuingia messeji za whatsap kwenye simu yake, akaanza kuzi soma na kuzi jibu, nyingi zilikuwa za kumpongeza, kutokana na kujifungua, kasolo moja tu! ilitoka kwa Joyce, ikimjulisha kuwa amejifungua mtoto wa kike, Suzane akaisoma kimya kimya pasipo kumjulisha Edgar, zaidi ya hapo mpaka wanafika nyumbani Suzane alikuwa ajapokea messeji ya picha toka kwa Sophia, nyumbani walipokelewa vizuri pia walikuta seline amesha wapokea wazazi wa Suzane, waliotokea Iringa kuja kumtazama mjukuu wao
Wazazi wa Suzane walikaa hapo siku tatu yanne wakaondoka kurudi Iringa wakipanga kurudi miezi mitatu ijayo kwaajiri ya kudhuria sherehe za harusi ya binti yao Suzane, kutokana na kuwa busy na mtoto Suzane akajikuta akikosa mda wa kutumia simu, na kutoka na utokuwa na tabia ya kuingia sana kwenye internet akuwa ame washa data kwa mda wa siku zote nne tokea atoke Hospital, siku hiyo baada ya Edgar kurudi stend kuwasindikiza wakwe, akamkumbusha jambo Suzane “hivi Sophia alikutumia picha?” aliongea Edgar akionyesha shahuku ya kutamani kumwona mwanae alie zaa na Sophia, “ok! ngoja niwashe data, alafu unajuwa kuwa Joyce amjifungua mtoto wa kike?” aliongea Suzane huku akichukuwa simu yake na kuwasha data
“Mh! kwa huyo.. mefukuzana,” aliongea Edgar kwa mshangao, huku akikumbuka kuwa mama sophia nae alisha waiuanguka nae mala kibao, lakini akuwa na taalifa nae, “sasa je? unzani mzigo ulio utunza miaka yote hiyo utamwacha mtu salama?” alisema Suzane huku messeji za whatsap zikiingia mfurulizo mpaka kale kamlio kaka taka kustuck, hapo Suzane akaanza kuitafuta namba ya Sophia, akaipata akaona kuna picha nne zimetumwa, akazifungua, macho yake yakakutana na picha ya watoto wawili wanaofanana sana huku mmoja akiwa amevalishwa kigauni cha pink, kuonyesha ni wakike, na mwingine akiwa amevalishwa kikaptula na tishet
“Mh! kwani amejifungua mapacha?” aliuliza Suzane, huku Edgar akichungulia zile picha, ni watoto wawili waliofanana na mwanae aliezaa na Suzane, huku picha nyingine pia wakiwa moja moja wame shikwa na mzee Mashaka, “ebu subiri” aliongea Suzane akionekana kubadirka sura, na kuwa mwenye wasi wasi, akapiga simu kwa Sophia, “hallow kwani ume jifungua mapacha” aliuliza Suzane bila salamu, “mh! best ata salamu, huyo mwingine ni mtoto wa mama” hapo suzane akamtazama Edgar usoni, huku simu bado hipo sikioni, “hallow, hallow Suzie unanisikia?” ilisikika sauti ya Sophia, huku Suzane akiwa bado ame iwka simu yake sikioni anamtazama Edgar, kisha akamtazama mtoto wao ambae alikuwa amelazwa kwenye kakitanda kake kenye neti, alafu akamtazama tena Edgar, huku macho yame mtoka kama ameona kitu cha hajabu usoni kwa Edgar
“Ina maana mama nayeye....” aliongea Suzane, na Sophia akadakia, “ndiyo amejifungua, si’nilikuambia” Suzane akuwa na maana hiyo, “sawa msalalimie mpe hongera yake, alisema Suzane kwa sauti ya unyonge, “tena amesema tuta ongozana wote kuja kwenye harusi ya yenu” kauri hiyo ilimchanganya sana Suzana, japo aliji taidi kujibu, “karibuni sana” hapo Suzane akakata simu huku anamtazama Edgar kwamacho yaliyo jaa uzuni, alifanya hivyo kwa sekunde kazaa, kisi cha kuanza kumwogopesha ata Edgar mwenyewe, lakini ghafla Edgar akamwona Suzane akingua kicheko kikubwa sana, Suzane alicheka kama dakika nzima hivi na kumfanya Edgar anayeye atabasamu, lakini tabasamu la wasiwasi, mwisho suzane akatulia kidogo, “samahani kama nitakuwa nime kukosea mume wangu, hivi ulilala na mama Sophi,?” aliuliza Suzane, akimtazama Edgar usoni
Hapo Edgar akaitikia kwa kutikisa kichwa juu chini, akimaanisha kuwa ndiyo, “mh! hivi awa ni vichaa kweli, kwahiyo walikuona wewe ndie mtuwao wakuwaburudisha?” alisema Suzane huku akitikisa kichwa kwa masikitiko, “lakini sizani kama itajirudia tena, sasa siwezi kuingia kwenye mitego kizembe zembe” alijibu Edgar kwa sauti nzito yenye utulivu, happo Suzane akamkumbatia Edgar “nakuamini mume wangu, lakini husiwe lege lege mpaka ile mimama inakubaka” wote wakacheka kidogo, “ila wewe unge kuwa padre unge wabaka masister, siyo kwa usongo huo, ulio kuwanao” alisema Suzane kisha wote wakacheka sana
Naam miezi mitatu mbele Edgar na Suzane walifunga ndoa, katika kanisa la mtakatiffu Teresia la Matogoro mjini Songea, ikifwatiwa na sherehe kubwa sana, iliyo fanyika katika ukumbi wa NYUMBANI PEACE VILLAGE, iliuzuliwa na watu wengi sana, wakiwepo wakina Joyce na Rafiki yake Nancy, Sophia na mama yake, ambao wali fikia nyumbani kwa Suzane huku Suzane na Edgar wakiamia kwa mda nyumbani kwa mzee Haule, pia waliudhuria wakina Rose na polisi wenzake wengi sana ambao kwa kiasi kikubwa walishirikiana na wafanya kazi wa benk, ya wananchi, walio ongozwa na Seline, kufanikisha sherehe hii kwa michango na mauzurio ukumbini na kanisani
Upande wa mzee Mashaka ambae alikuwa anampango kabambe sana wa kulipiza kisasi kwa kijana Edgar, alishindwa kufanya hivyo baada ya kupata tatizo la kudumu la mguu, na kugunduwa kuwa Suzane na Edgar wame amia Songea, japo baada ya mke wake kujifungua na mtoto kufanana na mtoto wa Sophia, alianza kuisi kuibiwa, maana mwanzo kabisa mke wake alimjulisha kuwa amepata ujauzito wake, kutokana na tendo walilo fanya siku moja kabla ya siku ya balaha, lakini akajipa moyo kuwa kufanana mtu na mjomba wake siyo vibaya kwasababu ni damu yake mzee Mashaka akawa mtu wa kutembelea magongo na kiti cha matairi, huku ofisi zake akiamishia nyumbani, akuweza tena kwenda Full dose kumvizia binti wajana, ambae na yeye baada ya kutoka Hospital, alipata bwana ambae alimpatia mtaji wa ubuyu na bisi, sasa anauza pale mbezi mida ya jioni, lakini siku moja moja akipata bwana anamshughulikia
Edgar na mke wake wana ishi vizuri na kwa amani kubwa sana, huku wakipeana mapenzi ya mke na mume, dada zake wawili Edgar mwishoe walkubari matokea, na kuishi vizuri na kaka yao na wifi yao, Bwana kazole alifukuzwa kazi kutokana na ulevi wakupindukia na kurudi kwao Rukwa, Sophia alipata mume na kuolewa huu mwanae akimwacha kwa bibi yake, akicheza na mama yake mdogo, Joyce alimaliza chuo na kuajiriwa, na sasa ana mchumba na wanatarajia kufunga ndoa, Rose yeye ataki kuolewa wala mchumba, bado anadowea ndoa ya Edgar na Suzane
Nime lazimika kukata baadhi ya matukio kutokana na urefu wa hadithi, lakini hipo siku utaisoma vizuri katika mwonekano mpya kabisa
HAPO NDIO MWISHO WA KISA HIKI CHA MAMA MWENYE NYUMBA NA MPANGAJI WAKE
NAOMBA SAPOTI, KUNA MATANGAZO(ADS) YANAJITOKEZA KWENYE APP YETU, LIMOJA LINAJAA KWENYE KIOO CHAKO JINGINE LINANG'ANG'ANIA HAPO CHINI KABISA, BONYEZA JAPO MARA 2 AU 3 KILA UKIFUNGUA SIMULIZI HIYO ITANIPA NGUVU YA KUENDELEA ZAIDI NA SIMULIZI ZETU🙏🙏
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

MWISHO
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni