MTAA WA TATU (8)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA NANE
"Shukrani sana ndugu yangu hakika nilikuwa mkosaji sana kwa kufanya vitendo vya kishenzi
kwa wakazi wa mtaa huu sikujali chochote kile
Niliiba nikabaka nikauwa
yote ndani ya wakazi wa hapahapa
wakija wababe kutoka mtaa wa kwanza au wapili tunakuwa wanyonge".....
NIOMBE SAPOTI, BONYEZA TANGAZO LINALOKUJA NA KUJAA KWENYE SIMU YAKO WAKATI UKIFUNGUA SIMULIZI AU LILE LINALOKUWA KATIKATI YA SIMULIZI ZETUKABLA HAUJAIFUNGUA NDANI, PIA KUNA LILE LINAKUJA NA KUNG'ANG'ANIA HAPO CHINI, BONYEZA WALAU MARA 3-4 HIVI HIYO NDIO SAPOTI YAKO KWANGU, TAFADHALI NIPE NGUVU NAKUTEGEMEA SANA MSOMAJI WANGU
SASA ENDELEA...
Hafidhi akauliza
"Inamaana mtaa wa kwanza ni zaidi ya huu mtaa wetu?"
"ndio kaka sisi tupo doro kabisa japokuwa ubabe wetu ni wenyewe kwa wenyewe
Kuna kipindi vijana wa kiume walibakwa mbele ya hadhara tukashindwa kufanya chochote kile.
Yani tukajifungia kwenye majumba yetu tukichungulia madirishani,
hakika ulikuwa unyama wa aina yake
kubakwa mbele ya mkeo au demu wako,
Kuna vijana wawili kukwepa aibu ile wakajinyonga".....
Cholo machozi yakamtoka maana inauma sana hii
"usijali kaka yangu mimi nipo twenzetu nyumbani
Basi
Hafidhi akabeba bage moja
Cholo lingine wakaongozana kurudi kwa kina Cholo njia nzima wakipiga story za hapa na pale'
"Ebwanaee
Cholo kanaswa nini mbona yupo na yule mchina mweusi?"
"Duhuu majanga nilimwambia mimi pitia huku boda akabisha, sasa leo inaitwa ukikimbia nchare ukisimama nchare.
Uchimung'unye uchiteme wala uchimeze
sijui itakuwaje kwa jamaa yetu Cholo".......
ni wale vijana waliokuwa wakicheza draft kwenye
Camp lao.
"sijuI mwanaume ndio anaenda kuliwa mzigo au vipi?"
"Embu acheni uboya wale washapatana na kuwa kitu kimoja"
mmoja kati yao akasema hivyo na kuwaacha wenzie midomo wazi,
"embu rudia tena unasemaje
Issa".........
"Kwani hujasikia au vipi kama masikio yako yapo matakoni bong'oa usikie vizuri bwege wee"
Kitendo cha Issa kumwambia mwenzie vile kikamuuzi yule jamaa kuonyesha kachukia
akalinyanyua
Draft juu na kumpiga nalo kichwani.
Draft lenyewe kwa juu liliwekwa kioo
Issa akapiga kelele za nakufaaa!!!
Kioo kilimchana kichwani na vile kanyowa para.
Shida tupu
yani kitu kidogo tu.
Wanaumizana ikabidi
Issa awahishwe hospitali,
Kila aliyemuona
Hafidhi na
Cholo wakikatiza pande hizo wakabaki na maswali ya kujiuliza
mpaka wanafika nyumbani
kwa kina Cholo kuna mama mmoja akaja mbio
na kumpigia magoti
Hafidhi huku
akisema
"tafadhali nakuomba baba msamehe mwenzio,
Msamehe tu,
Hafidhi akabaki kusikitika tu maana hakuna kitu kibaya kama kupigiwa
magoti na mzazi wako au mzazi wa mwenzako
ni laana ilioje
leo hii si ajabu mama au baba kumpigia magoti mwanae.
Kisa kamkosea siku zote mzazi hata akukosee vipi muombe msamaha wewe sio yeye.
Hafidhi akamnyanyua yule mama na kumwambia
"Mama inuka hutakiwi kufanya hivyo mimi na
Cholo tushakuwa kitu
kimoja sasa"......
yule mama hakuamini na kumuuliza
Cholo
"Eti ni kweli mwanangu"
"ndio mama niko pamoja nae.
Ghafla Hafidhi macho yake yakatua kwa binti mmoja hivi alikuwa anatoka chooni kuoga yani kajifunga kanga moko tu
Ndani hakuvaa chochote kutokana na ile kanga kushikana na maji
Basi mtoto akipiga hatua moja
kitu kinatingishika kama vile mpiga manyanga anavyo yatikisa manyanga yake,
Sijui kwanini dada zetu wakitoka kuoga chupi wanaweka kwenye kopo
na kujifunga kanga tu.
Si kutegana huku
Mtoto akaanza kusugua
Gaga".....
Hafidhi akashtuka baada kuguswa begani na
Cholo kwa kumwambia
"Master karibu ndani"
Hafidhi akacheka kidogo na kusema
"ahaha mimi si master bwana unanipaisha tu,
Cholo akaita
"wee Latifa naona fanya haraka hapo uje kuandaa chakula"....
yule binti akaitikia huku akimalizia kusugua mguu wa kushoto
"Sawa kaka naona umerudi humuogopi tena yule jamaa ehee?"
Binafsi
Latifa tokea atoke chooni hakuweza kumuona
Hafidhi maana alimpa mgongo na kumfanya mwanaume afaidi kucheki zigo na kula kwa
macho.
Mwanaume akaingia ndani na kuanza kupanga mikakati kwanza kabisa ni kuwakusanya vijana wote wa mtaa huu na kuwaunganisha wawe kitu kimoja.
Baada kujiunga na kuwa kitu kimoja
Itabidi tuwape mafunzo ya
Kutosha kuweza kupambana na wajinga wote.
Kingine tujengeane heshima sisi kwa sisi tuwe kitu kimoja.
Yani
Tupendane
Tushikamane
Tusiachane
Tusitengane tukifanya hivyo hakika tutakuwa na umoja wa nguvu, kingine tusisahau masnich yani wasaliti.
Inawezekana hiyo mitaa wakatuma watu wao kuja kutupeleleza nini tunafanya sasa basi tuwe makini"....
Yani Hafidhi akatoa maelekezo ya maana mpaka
Cholo akajiuliza
“huyu jamaa ni Commando nini mbona ana mipango hatari kama vile yupo
Vitani"
Hafidhi akatoka kidogo kwenda chooni
Latifa alukuwa yupo jikoni akipika si akamuona
Hafidhi anamtambua vyema ni adui wa kaka yake
Akapaza sauti kusema
“kakaa....Cholo kimbiaa".....
Huku akienda ndani
Cholo nae akatoka ndani mbio kufika mlangoni wakapigana vikumbo na Dada yake.
Latifa akadondoka chini sema hakujali kama kaumia au laa akajiinua haraka kutaka kuingia ndani.
Cholo akamshika na kumuuliza
“wee Latifa nini kwani?"
Huku akibabaika akajibu
“nimemuona yule jamaa kaingia chooni"...
Hafidhi nae akatoka chooni na kuuliza vipi kuna nini?"
Chollo akabaki kusikitika na kusema
“dahaa wee acha tu ndugu huyu Dada yangu ana Mashetani"
Hafidhi akasogea na kumshika
Latifa kichwa huku akimkazia macho kisha akamwambia
“binti tulia kuanzia sasa nipo pamoja nanyi
Latifa presha ikashuka".....
Salma baada kutimia saa kumi na mbili jioni mtoto wa kike akajiandaa kutoka
Kama walivyo aihidiana yeye na
Sharifa ndani ya saa moja usiku mtoto wakike alikuwa kwenye mduara, akiyakata mauno
“oyaa cheki mitako ile kudadeki nimeitamani kinoma yani".....
“sio peke yako hata mimi kama vipi tumchukuwe tukamfanye asusa".
“si binti kutoka mitaa hii au vipi"
“hapana katokea mtaa wa tatu kwa maboya tu"
Kitendo bila kuchelewa vijana wakaingia kati na kumbeba Salma juu kwa juu na kusepa nae gizani
Salma akajitahidi
kupiga kelele kuomba msaada “jamanii nakufaa nisaidieni"...
Hakuna aliyeshtuka zaidi ya rafiki yake kipenzi
Sharifa akatoka mbio kuwafata na kuwaomba wamuache mtoto wawatu.
“jamani Magoma tafadhali nawaomba muacheni huyo ni rafiki yangu"....
Sharifa aluongea hivyo huku akilia
“sikia nikwambie kitu Dada,
huyu binti ndio kipoozeo chetu ndani ya usiku huu.
Wewe nenda kaendelee kucheza mziki tukimaliza kazi yetu tutamrudisha,
Potea haraka sana tusije tukakujumuisha na wewe"......
Sharifa hakuwa na jinsi zaidi ya kukimbia mbio na kumuacha
Salma akilia wakati huo washamchani dera lake akabaki na Tait tu,
Sharifa akaenda kuomba msaada kwa kaka yake.
“kaka"....
Sharifa akaita kwa sauti
“mbona hivyo sister nini tatizo"
“Salmaa!!!
yani kwa jinsi alivyochoka akaishia kusema Salma,
“kafanyaje huyo Salma sema basi haraka"
“kina Magoma wamemchukuwa na kwenda nae kwenye mjumba kule"....
Ajabu jamaa akacheka kumbe nae ni walewale.
Akasema
“Sharifa Dada yangu wee nenda kacheze mziki hakuna kitu kibaya kitakacho
Mtokea rafiki yako.
Kaenda kuwa starehesha tu"
Sharifa akaona kesi ya mbuzi kaleta kwa kondoo.
Akatoka mbio huku akisema
“hapana kaka".....
Binafsi alidata hakuweza kufahamu ni nani atakaye msaidia rafiki yake
Katika kukimbia akapita kwenye ule mjumba na kusikia jinsi rafiki yake akilia,
Huku washikaji wakisema mtoto mtamu, ingiza mbele niingize nyuma
tufanye kwa pamoja.
Sharifa akili za kutaka kwenda Mtaa wa tatu kutoa taarifa hakuwa nazo
Maana alifahamu fika watu wote wanauwogopa huu mtaa,
Akili ikamjia wacha akajalibu kutoa taarifa,
akatoka mbiombio na kufika nyumbani kwa kina
Salma na kuwakuta kina Beatrice Zay
Bulongo na wengineo
Hafidhi hakuwepo sijui yuko wapi.
Baada kufika hapo akiwa analia
Akasema
“jamani msaada please Salma anabakwa kulee"
hakuna hata mmoja aliyeshituka kwa kutaka kwenda kutoa msaada.
Ndio kwanza kila mtu akaingia chumbani kwake
chezea mtaa wa kwanza wewe
Sharifa akachoka kabisa na kukaa chini huku akilia.
Ghafla akashtuka baada kuguswa begani
Akainua sura yake kumtizama aliyemgusa ni
Hafidhi kwa sauti ya upole akamuuliza
“nini tatizo binti mbona usiku huu upo hapa
Unalia nini?"
Sharifa akajiuliza hata huyu nikimwambia atatoa msaada gani.
Akajitoa mikononi mwa Hafidhi na kuitaji kuondoka
Hafidhi nae hakuwa na jinsi akamuacha aende zake,
Akaingia ndani kufika ukumbini tu
Beatrice akatoka chumbani kwake na kumwita,
“Hafidhi kaka"....
Akageuka na kuitikia
“naamu"
“wakati unaingia humu ndani hujakutana na binti hapo nnje?"
“nimemuona si yule rafiki yake
Salma nimemkuta analia nikamuuliza analilia nini hakunijibu"
“khaa!!! yani ajakujibu chochote, basi kaja hapa na kusema
Salma anabakwa huko"
“What?????
Hafidhi kwa speed kama kiberenge vile akatoka mbio kumkimbilia
Sharifa kwa bahati nzuri akamkuta ajafika mbali akapaza sauti kumwita
“Sharifa!!!....yani sauti yake ile kitu kama upepo hivi ukavuma kuonyesha ana hasira si kidogo
“niambie Salma yuko wapi?"
Sharifa akashindwa kujibu akabaki kimya
Akashtukia akipigwa kibao kimoja tu cha kerbu
yani hakutegemea kupigwa hata siku moja.
“nakuuliza tena Salma yuko wapi"...
Sharifa japokuwa mdomo ulikuwa mzito kujibu na kile kibao alichopigwa
ikawa kama kameza zege
“yuuuu----po....kulee"
Hafidhi akamshika mkono na kumwambia twende unipeleke'
Safari ya kwenda huko ikaanza.
Baada kufika kwenye maeneo hayo
Hafidhi kwa masikio yake akasikia jinsi Dada binamu anavyolia.
Akamuachia
Sharifa na kuzama kwenye mjumba huo
kumbe washikaji washajilia vyao na kusepa
Salma akabaki kajikunyata tu analia dahaa".....
Hafidhi akamsogelea na kumshika
Salma akapiga kelele
“niachenii si mshanibaka kama vipi niuweni kabisa unyama gani mmeniingilia hadi kinyume na maumbile"......
Mwanaume hayo maumivu aliyokuwa nayo moyoni sijui nisemeje yani macho yakawa mekundu kama
Simba, na kumtuliza Dada yake kwa kumwambia
“Salma tulia ni mimi kaka yako nisamehe kwa kuchelewa kufika.
Akamgeukia
Sharifa na kumuuliza
“wee Malaya wako wapi hao kenge blue?"
tukumbuke huyu demu anamtaka kwa hasira zake kampiga kofi kule na sasa hivi anamwita Malaya
Akiwa na hasira
anakuwa yupo Sirius hataki mchezo macho yake tu
yakamtisha
Sharifa na kujibu
“wapo kule kwenye kigodoro"
“twende unipeleke
Sharifa akaongoza njia
Hafidhi akavua jacket lake akabaki na vest kisha akamvisha Salma
huku kigodoro kimenoga balaa
“ebwaee demu mtamu yule
Kitu mnato usipime.
"Kumbe mwanangu mwenyewe umeona ehee"....yani niliingiza kidole kwanza kitu cha motoo"
Vijana wale wenye tabia za kishenzi wakaendelea kupiga story zao
za kijinga tu.
Huku wakivuta misokoto yao ya bange.
Wakati huo mwanaume ndio anaingia.
Kitendo cha kuonyeshwa tu wale pale.
Hafidhi akutaka kuuliza cha nini wala maini
Akaruka kama nyani na kwenda kuachia mateke matatu double,
si
Magoma wala Jimmy wote wakaenda chini, kitendo cha kuinuka kuuliza vipi ngumi za faster faster zikatua usoni mwao.
Ikawa sasa disco kaingia mmasai
Hafidhi alikuwa anapiga yeyote yule
Magoma akapigwa teke moja na kwenda kudondokea
Speaker za mziki.
"Oyaa huyu Billy blanks katokea wapi mbona anapiga hivi"....
Vijana wakaanza kuulizana
NAOMBA SAPOTI, KUNA MATANGAZO(ADS) YANAJITOKEZA KWENYE APP YETU, LIMOJA LINAJAA KWENYE KIOO CHAKO JINGINE LINANG'ANG'ANIA HAPO CHINI KABISA, BONYEZA JAPO MARA 2 AU 3 KILA UKIFUNGUA SIMULIZI HIYO ITANIPA NGUVU YA KUENDELEA ZAIDI NA SIMULIZI ZETU🙏🙏
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA TISA
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni