MUWASHO (11) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumapili, 2 Aprili 2023

MUWASHO (11)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
๐Ÿ“– KUSOMA SIMULIZI
๐ŸŽฌ FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
๐Ÿ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
๐Ÿ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa

Jina: MUWASHO
Mwandishi: Seif Jabu

SEHEMU YA KUMI NA MOJA
ILIPOISHIA...
"Hata funu funu hamna?"

"Fununu zilizopo ni kuwa Monica aliuawa ila hatuna taarifa hizo kiundani zaitukn

"Aliyeongea taarifa hizo ni nani huenda tukimuona tukafanya naye maongezi tutapata muongozo wa kupata ukweli,"

WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
"Tunashindwa kumsema kwa kuwa polisi tunawajua mnavyomchukulia mtu hatua hata kama hana kosa,"

"Basi kama ni hivyo hamtaki kutuambia mhusika tutaondoka na wewe mkuu wa shule mpaka pale upelelezi utakapo kamilika,"

"Mkitaka kufanya hivyo sawa si mko Juu ya sheria,"

"Basi bila kutumia nguvu nyanyuka tuongozane,"

Mkuu wa chuo hakubisha alitii kile alicho ambiwa akaongozana na maofisa wale wa jeshi,

Wakati polisi wakitoka katika ofisi ya mkuu wa chuo tayari huko nje wanafunzi walikuwa na taarifa zote kuhusu mazungumzo yaliyofanyika huko ndani wakajipanga kuzuiya Mkuu wa Chuo asipelekwe polisi,

"Hatukubaliiii……….."

" hatukubaliiii……….."

"Hatukubaliiii……….."

Zilikuwa ni sauti za wanafunzi wakipinga mkuu wao wa chuo kupelekwa polisi,

Polisi baada ya kuona wingi ule wa wanafunzi na kelele zao walitumia hakili ndogo wakafyatua risasi hewani kilichotokea ni kuwa wanafunzi walivaa polisi bila uoga na kuanza kuwapinga huku bunduki zao wakizitupa pembeni na kuziharibu haribu.

Taarifa zilifika kituo kikuu cha polisi FFU wapatao mia moja wakatumwa chuoni ili kutuliza fujo na kuokoa Askari wenzao waliokuwa wakipokea kipigo cha umbwa mwizi.

FFU walitumia nguvu kubwa sana kutuliza gasia katika eneo la chuo ila jitihada ziligonga ukuta kwani wanafunzi walikuwa moto zaidi moto wa kifuu.

Monica alijitahidi ili kuona kama ataweza kufanikisha zoezi lake la kumjeruhi Mernah aliyekuwa ana amini kuwa ndiye aliyetaka kumuuwa,

"Seif naomba tuachane kwa amani wala sihitaji matatizo mengine tena kwani matatizo niliyoyapata kwa sababu nahisi yanatosha."

Dokta Ivete aliingilia kati na kuanza kuongea maneno yaliyokuwa siyo ya kumtia moyo Mernah japo aliyaongea kwa upole na mafumbo.

"Siku zote ngazi ina mwisho na siyo kama tunavyosikia kuwa Dunia haina mwisho, kingine nataka nikwambie kuwa kukata tamaa saa nyongine ni vizuri kuliko kutaka ushindi utakaokuweka katika shimo la Giza milele."

"Asante kwa maneno yako mazuri na yaliyo ujenga moyo wangu kwa zege,"

Baada ya kuongea maneno hayo Mernah aligeuka na kuangalia mlango kisha akajiweka tayari kuondoka ila kabla bata hajapiga hatua alisikia kitu chenye ncha Kali kimemchoma ile kugeuka aliona ni Monica ameshikilia bomba la sindano akajua kuwa kilichomchomo ni sindano,

"Monica siwezi kukuchukia wala kuona vibaya kwani mzigo wa mawazo ulioubeba Juu yangu huna ukweli nao,"

Baada ya kuongea hivyo Mernah aliondoka zake na maumivu yake huku akiwa na mawazo tele Juu ya ya kuvunjika penzi lake na seif.

Mambo yalikuwa mambo mkorogano ulikuwa mkubwa japo Mernah aliamuwa kujitenga Seif ila misuguano bado ilikuwa mikubwa kwani Dokta Ivete aliona bado ana kazi ngumu ya kujihakikishia kuwa Seif ni wake peke yake,

"Seif mbona kama una mawazo ya mbali sana."

"Nitaachaje kuwa na mawazo wakati siku tatu zimekatika bila kujua alipo Mernah,"

"Sasa unataka ujue alipo ili iweje?"

"Ili nijue kama yuko salama,"

"Na ukiisha jua kama Yuko salama inakuwaje?"

"Nitafurahi kama takuwa mzima kwani sipendi apate shida."

"Atazipata tu shida mwaka Juu kwani kakutana na mkono wa Upanga,"

"Hivi kakufanyaje mtoto wa watu mbona unamuombea mabaya,"

"Alichonikosea nakijuwa mwenyewe,

Maisha yaliendelea na hali ya Monica ilizidi kutengamaa na kurudi katika hali yake ya zamani, katika siku alizokaa pale kwa Dokta Ivete alikuwa akimuuliza ni nani aliyemleta hapo,

" Dokta hivi ni nani aliyenisaidia mpaka nikafika hapa ukaanza kunitibu?"

"Tulikuogota Mimi na Seif,"

"Mlipajuaje pale nilipokuwa?"

"Ni hadithi ndefu sana tuyaache tumshukuru mungu kuona unaendelea vizuri,"

Upande wa uongozi ulikuwa ukihojiwa Juu ya taarifa za kapotea kwa mabinti wawili pale chuoni,

"Sema ukweli hatujapata habari yoyote iliyo ya kweli kuhusu walipo Monica na Mernah,"

"Hata funu funu hamna?"

"Fununu zilizopo ni kuwa Monica aliuawa ila hatuna taarifa hizo kiundani zaitukn

"Aliyeongea taarifa hizo ni nani huenda tukimuona tukafanya naye maongezi tutapata muongozo wa kupata ukweli,"

"Tunashindwa kumsema kwa kuwa polisi tunawajua mnavyomchukulia mtu hatua hata kama hana kosa,"

"Basi kama ni hivyo hamtaki kutuambia mhusika tutaondoka na wewe mkuu wa shule mpaka pale upelelezi utakapo kamilika,"

"Mkitaka kufanya hivyo sawa si mko Juu ya sheria,"

"Basi bila kutumia nguvu nyanyuka tuongozane,"

Mkuu wa chuo hakubisha alitii kile alicho ambiwa akaongozana na maofisa wale wa jeshi,

Wakati polisi wakitoka katika ofisi ya mkuu wa chuo tayari huko nje wanafunzi walikuwa na taarifa zote kuhusu mazungumzo yaliyofanyika huko ndani wakajipanga kuzuiya Mkuu wa Chuo asipelekwe polisi,

"Hatukubaliiii……….."

" hatukubaliiii……….."

"Hatukubaliiii……….."

Zilikuwa ni sauti za wanafunzi wakipinga mkuu wao wa chuo kupelekwa polisi,

Polisi baada ya kuona wingi ule wa wanafunzi na kelele zao walitumia hakili ndogo wakafyatua risasi hewani kilichotokea ni kuwa wanafunzi walivaa polisi bila uoga na kuanza kuwapinga huku bunduki zao wakizitupa pembeni na kuziharibu haribu.

Taarifa zilifika kituo kikuu cha polisi FFU wapatao mia moja wakatumwa chuoni ili kutuliza fujo na kuokoa Askari wenzao waliokuwa wakipokea kipigo cha umbwa mwizi.

FFU walitumia nguvu kubwa sana kutuliza gasia katika eneo la chuo ila jitihada ziligonga ukuta kwani wanafunzi walikuwa moto zaidi ya FFU

Hali ilikuja kutulia jioni kabisa majira ya saa saa kumi na mbili pale mheshimiwa Rais alipofika eneo la eneo la chuo na kuongea na wanafunzi wakamshitakia na kumwambia kile wanachokitaka,

"Mnachokitaka tutakifanya kwani inaonesha kuwa polisi ndio wenye makosa cha kwanza polisi walikuja hapa bila kibari, cha pili waliwafyatulia risasi bila kukaa pamoja mkashauriana, kwa tunaomba radhi kama serikali pili tuko hapa kusikiliza kile mlichosema kuwa mnakihitaji,"

Tuna taka wenzetu waliokamatwa,"

"Sawa msihofu dk tano ni nyingi watakuwa hapa,"

Wana chuoni na Raisi walielewana na kweli hali ilitulia na baada ya mda flani wale wanafunzi waliokamatwa waliachiwa,

Askari wawili waliuawa na wengine walipelekwa hospital wakiwa mahututi sana,

Siku zilikatika habari za fujo zilizotokea pale chuoni ikaanza kupotea vichwani mwa wanafunzi na RAIA wanaoizunguuka shule.

Habari za fujo seif alikuwa anazijua vizuri sana na baada ya fujo kumalizika seif alikutana kantini na Skola na walikaa meza moja Skola akamuanza Seif kwa kumsabahi, toka kipindi kile Skola amfumanie Seif akiwa na mernah walikuwa hawakuwahi kusaliama wala kuwa karibu.

"Seif habari yako,"

"Nzuri za kwako?"

"Namshukuru mungu,"

Baada ya salamu kimya kingi kilifuatia kwani kila mmja alikuwa akiwaza aanzie wapi kumsemesha mwenzie, ila siku zote kidume ni kidume tu Seif alianza kutoa maneno machache kwenda kwa Skola.

"Mbona umehadimika sana wangu? Nilijua uliisha maliza mwaka wako hapa chuoni,"

"Nipo nimalize usijue?"

"Nitaambiwa na nani?"

"Mhhh na wengi mnaojuana,"

"Kama nani?"

"Mernah angekuambia,"

"Mhhh… alafu kweli hebu nikuulize swali Skola na unipe ushirikiano,"

"Swali gani?"

"Mala ya mwisho kumuona Mernah wewe ilikuwa link?"

"Ni siku zimepita,"

"Huna fununu fununu labda,"

"Sina Ila nilisikia kuwa aliuawa akiwa na Monica,"

"Si kweli Monica hajauwa wala mernah kwakuwa juzi juzi nilikuwa nao wote na Mernah tukakwazana kidogo akaondoka kwa hasira hata siku tano hazijakwisha toka aondoke kwa hasira,"

"Mhhh ulikuwa umewaficha au ilikuwaje ukawa nao bila watu kujua walipo?"

"Ni story ndefu sana tuyaache hayo,"

"Kwa nini tuyaachie njiani tuyazungumze yamalizike,"

"Kuna yupo Monica anapata matibabu kwani alikuwa amejeruhiwa na muuaji,"

"Muuaji ni nani?"

"Simjui,"

"Hukumuona"

"Monica anadai aliyetaka kumuuwa ni Mermah ila siyo kweli kwani Mtu aliyempa msaada ni Mernah asingekuwa Mernah angekufa kwani mernah ndiye aliyeniita Mimi na kunielelekeza katika hako kapoli,"

"Mhhh hapana inawezeka Monica anachoongea ni kweli kwakuwa walikuwa wao wawili tu."

"Hapana sikubaliani na hilo kama ni hivyo kwanini aliniita ili tumpe msaada,"

"Ni danganya Toto tu ila yeye ndiye muuaji na inabidi umtolee ripoti polisi."

"Mimi mwenyewe namtafta alafu ni mtolee ripoti polisi,"

"Una mtafta wa nini?"

"Namtafta kwa kuwa ni mtu wangu,"

"Ahhhh ila ripoti ni mhimu?"

"Siwezi kumtolewa ripoti kwa kuwa najua hana hatia,"

"Hana hatia wakatia wakati Monica anadai kuwa Mernah ndiye muuaji,"

"Alisemalo halijui,"

"Hali jui wakati yeye ndiye katendewa,"

"Unayo ongea na wewe huyajui?"

"Nayo ongea naongea kutokana na maelezo yako,"

"Tuyaache hayo maongezi maana naona tutafika mbali,"

"Kama atashindwa kutoa ripoti Mimi nitamsaidia kuitoa,"

"Skola ukitaka kutibuana na mimi mguse Mernah utakuwa unatafta mengine,"

"Acha niyatafte alivyonipola wewe anafikili nilifurahi?

"Acha nikupe ukweli ni kuwa hakukupola bali wewe ulitaka kumpola,"

"Seif nilikupenda na nitaendelea kukupenda,"

Seif alinyanyuka akaondoka bila kusema chochote kile ila alikuwa akiwaza cha kufanya Juu ya Skola kwani aliona hana nia nzuri kwa kwa Mernah,

Naapa kutoa damu ya mtu yoyote atakae taka kumtemda vibaya Mernah

Akiwa katika hali ya mawazo alisikia simu yake inaita akaitoa mfukoni kujua nani anamtafta ila alipoangalia alibaini ni simu Monica kwenda Skola kutoka na setting alizokuwa amefanya.

"Halloh Skola ni mimi Monica,"

Jamani like zenu ndogo ndio zinachelewesha hadithi hii. Like na koment yako ndio inaleta hadithi hii.

Endeleaaa….

"Hallow Skola ni Mimi Monica,"

"Mke wangu vipi? Uko mzima?"

"Kiasi chake swty,"

"Kwanza niambie uko wapi jaman nije?"

"Nilipo kufika ni rahisi si unapangumbuka kwa Dado?"

"Ndio,"

"Njoo moja kwa moja nyumba ya tano kutoka hapo kwa Dado, ila Dado hayupo nilienda kumuulizia wakaniambia kuwa alienda uswizi,"

"Nakuja mke wangu,"

Maneno waliyoongea yote Seif aliyasikia akajiuliza afanye nini kumzuiya skola asionane na Monica ila akakosa namna ikambidi atumie mpango wa kuwahi kwenda kuonana na Monica ili ajaribu kumsisitiza asijaribu kumfungulia kesi Mernah,

Akiwa katika mawazo mengi sana akiwaza afanye nini simu yake iliita akayiangalia kisha akaipotezea kwani hakupenda kuingiza mambo mengi kwenye akili yake alitaka awaze afanye nini ili Mernah asishitakiwe,

USIIKOSE SIMULIZI INAYOFUATA

Umeyaona Matangazo?
Yabonyeze Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni