MUWASHO (12) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumapili, 2 Aprili 2023

MUWASHO (12)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
๐Ÿ“– KUSOMA SIMULIZI
๐ŸŽฌ FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
๐Ÿ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
๐Ÿ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa

Jina: MUWASHO
Mwandishi: Seif Jabu

SEHEMU YA KUMI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Akiwa katika mawazo mengi sana akiwaza afanye nini simu yake iliita akayiangalia kisha akaipotezea kwani hakupenda kuingiza mambo mengi kwenye akili yake alitaka awaze afanye nini ili Mernah asishitakiwe,

WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Simu iliita tena kwa awamu tatu bila Seif kuipokea ila baada ya kukatika alisikia SMS inangia kwenye simu, afadhali kusoma SMS kulikoni kupokea simu

Seif aliishika simu kisha akaifungua SMS ile ila alipoisoma alioneka kupagawa akainuka haraka alipokuwalipofikaakatoka nje huku anakipimbia kama mwehu, SMS hiyo ilikuwa ikisema kuwa, Nakupigia simu hupokei wakati unajua kazi uliyonipa? Mernah nimemuona nikajaribu kumzubaza ili nikupigie simu, nakupigia simu hupokei sasa hiyo itakuwa kazi kweli Mimi Niko hapa kichangani na nimemuona mazingira haya haya?

Seif aliongeza spidi ya miguu yake ili aone kama anaweza kuwahi kuonana na Mernah, alipofika barabarani alichukua Piki Piki ili awahi,

"Dereva wahi vuta moto vuta moto baba,"

Dereva Piki Piki wanavyopenda kukimbia na yeye kweli alivuta moto Piki Piki ikawa inatereza Juu rami utafikili inataka kupaa,

Upande wa pili.

Uoande wa pili Monika alikuwa akipiga story na Dokta Ivete ila baada ya mda wakasikia kengere ikiita kumanisha kuna mtu nje anabisha hodi,

"Kuna mgeni sikia kengere hiyo,"

"Ngoja nikafungue,"

Aliyekuwa anagonga mlango hakuwa mwingine alikiwa ni Monica,

"Karibu mgeni bila shaka wewe ndie Skola"?

" ndio,

"Karibu Monica yuko ndani,"

"Asante,"

Skola aliingia ndani ila akaonana uso kwa uso na Monica hakuamini kumuona akiwa mzima alimuangalia mala mbili mbili kisha akamkumbatia huku akisema,

"Mke wangu pole sana….."

"Asante vipi wewe umzima?"

"Mimi mzima kabisa ila nilikumisi nikamisi zaidi penzi lako mpenzi wangu,"

"Ndio hivyo na Mimi yalinikuta ya kunikuta nikachomwa chupa sehemu za siri ila mungu akanisimamia,"

"Pole sana mamyto, ila nani alifanya haya yote?"

"Mernah kwa ninavyoelewa na kwa nilivyosikia,"

"Huyu Mernah tumfanye nini?"

"Aaahh…. Ni kumuachia mungu tu,"

"Khaaaa kumuachia mungu?"

"Ndio,"

"Sikia Skola Mimi nikimuona nitamuulia mbali,"

"Khaaa usifanye hivyo Skola,"

Wakiwa wanaongea Dk Ivette alikuwa akiwasikiliza tu ila walipofika kwenye suala la kuuwa aliingilia kati na kusema,

"Mbona mliisha muuwa mnappresha gani?"

"Tumeisha muuwa?"

"Ndio,"

"Kivipi?"

"Siku ya kesho hataimaliza duniani atakuwa amekwisha tayari kwani sumu aliyonayo mwilini mwake ni kali sana,"

"Sumu,"

……………. ………. ……………

Upande wa pili self alijaribu kuwahi eneo aliloambiwa kuwa Mernah alionekana mda siyo mrefu,

Alipofika aliangaza huku na kule bila matumaini yoyote yale akaamuwa ampigie simu yule jamaa aliyekuwa amempa kazi,

Hallow niko maeneo haya uliyoniambia"

"Njoo kwa mangi mchoma mbuzi,"

"Sawa,"

Alijisogeza kwa mangi na kweli akamuona wakakaa wakaanza kuongea,

"Niambie vipi umemuona wapi mernah"

"Brother kabla ya yote nikwambie kitu kimoja,"

"Kipi?"

"Yule binti ni wa kufa leo au kesho kwa hali aliyonayo,"

"Unasemaje?"

"Kama ulivyosikia…"

"Kwani yukoje kiafya,"

"Kachoka sana arafu yuko kama ka data kiaina,"

"Hapana…."

"Kingine nikuwa masera wamekuwa wakijipigia tu kwani hana akiri vizuri,"

"Kujipigia nini?"

"Wanafanya naye mapenzi,"

"Etiiii?….

" isitoshe mpaka masera wenye ngoma wamepita naye bila kings,"

"Kheeeee……,"

Seif alitaka kuchanganyikiwa baada kusikia kuwa kwa sasa Masera wanajipigia Mernah kilichomuuma zaidi ni pale aliposikia kuwa mpaka masera wenye ukimwi wamepita bila kinga,

"Acha niendelee kumtafta si umesema kaelekea huku?"

"Ndio,"

Seif alianza kuyipiga mitaa kumtafta Mpenzi wake msichana aliyempenda sana ila tamaa na ngono vikawatengamisha ili hali bado anampenda.

kweli nilikukosea Mernah ila nahitaji msamaha wako kwani sijielewi mpaka sasa, matatizo yako yote yanayokukabili naamini mimi ndie chanzo umekuwa mwenda wazimu kwa sababu yangu, sura yangu niifiche wapi? Mbona naona Dunia imenikasirikia?

Seif na yeye taratibu alianza kudata na akajikuta anaanza kuongea peke yake barabarani bila kujitambua,

Akiwa katika tembea tembea alimuona msichana aliyefanana na Mernah akamkumbatia kwa nguvu huku akisema,"

"Mernah wangu kwanini ulinikimbia? Kwanini uliniacha peke yangu?"

"Eehh mwehu nini? Hebu niachie,"

Kazi haikuwa rahisi kumzuiya Seif asimnganganie binti huyo aliye mfananisha na Mernah wake, zilipita dakika kumi kasheshe ikiwa inaendelea mpaka alipofika yule kijana aliyekuwa amepewa kazi ya kumtafta mernah,

"Oyi brother umekuwaje wewe mbona unafakamia watu usio wajua,?

" aaahhh kumbe ni wewe, hebu sema ukweli huyu siyo Mernah wangu?"

"Siyo yeye"

"Ahhh kumbe siyo yeye?"

"Ndio siyo yeye huyu,"

"Oky acha niendelee kumtafta,"

"Pouwa,"

Seif alitia huruma alikuwa kama kadata vile kwani mambo yote aliyofanya yalikuwa ya kichizi chizi tu,

Baada ya seif kuondoka yule Dada aliyefananishwa na Mernah alimuuliza yule kijana,

"Kwani huyu kijana kawaje?"

"Alikuwa na Mpenzi wake ila Mpenzi wake kwa Sasa ni chizi yaani mwenda wazimu na afya yake haiko vizuri wakati wowote ule anaweza kufa,"

"Unaweza kuwa unaijua historia yawo?"

"Hapana ila kuna anaijua aliniambia kuwa anasoma na seif chuo kimoja,"

"Naomba unikutanishe Naye,"

"Sasa twende kijiweni maana jamaa anakujaga kijiweni kuchukua ngada,"

"Sawa,"

Upande wa seif aliendelea kuhangaika kumtafta Mernah wake kwani aliamini bila Mernah hawezi kufanya chochote kile,

Mernah umekwenda wapi mbona mboni zangu zinahitaji kukuona ili macho yangu yapate nuru ya kuona?

"

"Sumu?"

Wote walisitaajabu kusikia sindano ya sumu,

"Ndio sindano ya sumu, namaanisha kuwa ile sindano uliyomchoma siku ile wakati nakutibu ilikuwa ina sumu kali ndani,"

"Khaaa Mimi Monica nimeuwa?"

"Ndio, kwa hiyo dhamira yenu imekamilika,"

"Ila sikutaka iwe hivyo,"

Skola aliingilia kati akanena maneno yake kwa furaha sana,

"Raha iliyoje jamani kusikia habari nzuri kama hii,"

"Skola usifurahie kifo cha Mernah kwani kumbuka na yeye anahitaji kuishi,"

"Ndio hivyo kuishi imeshindikana Sasa unata tufanyeje tuongee na mungu?"

"Imeniuma sana kuona mkono wangu umefanya hivyo,"

"Isikuume potezea tu Mpenzi wangu."

Upande wa pili Mernah alionekana akiwa amelala katika ya barabara magari yakashindwa kwenda watu wakamzunguuka kujua kulikoni,

Watu walikusanyika kujua kipi kimemkuta binti huyo ambaye ni Mernah,

"Jamani kawaje huyu binti?"

"Na sisi hatujui,"

"Huyu binti ni kichaa,"

"Mhhh jamani hata kama ni kichaa ndio hivyo barabarani?"

"Jamani anaweza kuwa kichaa ndio ila inaonesha amefariki,"

Kila mmoja alikuwa akiongea la kwake kama ujuavyo kwenye mkusanyiko wa watu wengi kukiwa na tukio kila mmoja anaongea la kwake,

Wakati yote yakiendelea hayo alitokea kijana mmoja mtanashati mwenye muonekano mzuri mbele ya macho ya wengi akamuangalia sana Mernah na kwa umakini kisha akamsigelea akambeba kwa mikono yake miwili kisha akaanza kuzipiga hatua kuelekea kwenye gari yake watu wakabaki midomo wazi huku wengine wakijinongoneza,

"Huyo ndugu yake au msamalia mwema?"

"Mhh sijui labda nduguye mbona kamchukua kimya kimya?"

Wengine nao walikuwa wakisema yao,

"Inawezekana kweli akawa nduguye?"

"Labda anamchukua kwa ajiri ya kafara huyo maana watu tuko tofauti kifikira na mtazamo,"

Minongono ilizidi maneno mengi yakasemwa na machache akayasikia ila akapotezea akaendelea na mambo yake.

Upande wa pili Seif alizidi kuranda randa mtaani akimtafta Merinah wake asijue kuwa merinah ameogotwa na mtu asiye julikana na haijulikani mtu huyo amempeleka wapi,

Akiwa katika hangaika ya kumtafta Mernah alipoteza simu akabaki hana mawasiliano yoyote na mtu,

Seif alipotupa jicho upande wa pili alimuona msichana aliyefanana na scola akamva na kuanza kumpiga makofi yule binti akapiga ukelele wa kuomba msaada huku akisema,

"Mwiziiii…….mwiziiiii…..mwiziiii.."

Kelele zile zilizuwa taflani kubwa na watu wakaja wamejaa jazba wakaanza kumpiga Seif bila kumuhurumia nazani na wewe unajua vizuri jinsi mwizi anavyokabiliwa na raiya.

"Jamani habari za seif kuna mwenye nazo? Maana kakaa kimya sana,"

Monica alihoji kuhusu seif na wote wakawa kama wametoka usingizini,

"Mhhhh unajua kweli Seif hatuna habari zake hebu skola mpigie simu,"

"Ngoja nifanye hivyo,"

Walipiga ila simu haikuja na majibu yoyote yale.

"Mbona hapokei simu?"

"Mhhh… Dokta hebu jaribu wewe kumpiga,?"

Dokta naye alipiga ila yeye akawa na bahati ikapokelewa japo haikupokelewa na Seif,

"Hallow… Habari yako?"

"Nzuri wewe nani unapokea simu ya mume wangu?"

"Hunijui ila fanya haraka njoo hapa mtaa wa idirisa ka/koo mumeo anapigwa na nzengo anatuhumiwa wizi,

"Nini wewe unachosema?"

"Kama ulivyosikia, wahi"

Dokta alikata simu akawambia wenzie,

"Twendeni nyie Seif anakufa huko?"

"Kuna nini tena,"

"Nitawambilia kwenye gari,"

Safari ilianza ya kwenda huko aliko elezwa Dokta ila Monica na skola walikuwa wakitoa macho sana wakijiuliza kuna nini?"

"Twambie basi presha zitatuuwa,"

"Seif anashambuliwa na nzengo,"

"Kwa kosa gani?"

"Wizi wa kupora."

"Wizi wa kupora mbona vioja hivi tena?"

"Siyo vioja anaweza kuwa amesingiziwa,"

Seif alizidi kushambuliwa na wananchi na pale alipojitetea kuwa siyo mwizi hakuna aliyemuelewa.

Kipigo kwa seif kiliendelea kuwa kikali sana mpaka ikafikia hatua ya kuonekana anaenda kuyiaga dunia,

Tairi na mafuta vililetwa ili kumchomelea mbali Seif aliyekuwa anatuhumia kwa wizi, alivikwa tairi na kumwagiwa mafuta ila kabla kiberiti hakijahusika kuwasha moto mlio wa risasi ulisikika watu wote wakashituka kana kwamba walikuwa usingizini,

Aliyetokea kutoa msaada hakuwa polisi hakuwa mgambo wala mwanajeshi bali alikuwa ni binti mdogo mwenye miaka 19 mwenye asili ya kihindi,

Risasi ya pili ilisikika na kufanya watu kuanza kusambaratika kwa kuogopa kufa,

"Wote tokeni hapo atae pinga nitampiga risasi,"

Baadhi ya vijana wanaojiita wababe wa kitaa walijifanya hawasikii amri ile na kuendelea kubaki pale pale, binti wa kihindi alipoona wanasita kutoka alimpiga mmoja wao risasi ya mguu hapo ndipo wakaona kuwa kweli binti huyo yuko siriasi wakakimbia wote,

Baada ya kutawanyika binti huyo aliwatishia vijana wawili kwa bastora na kuwambia wamuingize kwenye gari yake,

Baada ya patashika za hapa na pale yule binti aliondoka eneo hilo akiwa na Seif ndani ya gari,

Scola, Monica na Dokta walifika eneo la tukio ila hawakumkuta Seif eneo hilo,

USIIKOSE SIMULIZI INAYOFUATA

Umeyaona Matangazo?
Yabonyeze Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni