Nyumba ya Wachawi (4)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mtunzi: Denis Benard
SEHEMU YA NNE
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
‘’Rafiki yangu vipi mbona sikuelewi?nimekutafuta tuje kunywa chai sijakuona na pia nikiangalia sura yako naona kama huko mbali sana?sikiliza hiki si kipindi cha kuwa mbali hivyo kimawazo,kwa maaana utakuwa unakaribisha vitu vinginee ambavyo kimsingi vitakuletea matatizo sana katika afya yako,kua makini sana na maisha yako yanayokuja basi na vitu vingine’’ aliongea Elly kwa uchungu sana.
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Yale maneno yalimfanya Faluu atulie pale,lakini hakuwa na jibu la kumueleza Elly kwa wakati ule na badala yake aliondoka tu na kuingia ndani .Hali ile ilimpa wakati mgumu sana Elly na akaona haitakuwa nzuri kama hatashindwa kumueleza mama yake juu ya kila kitu kinachoendelea kwa rafiki yake…
‘’Mama mimi nimekuja kukueleza kitu kimoja hapa’’ aliongea Elly
‘’Kitu gani hicho mwanangu ?’’aliuliza mama yake Elly.
‘’Unajua Ulipotuandalia chai muda Faluu hakuwepo ndani na nilijaribu kumtafuta sikumuona kabisa,mimi nikanywa hivyohivyo,lakini wakati natoka ndani saa hizi nimekutana nae mlangoni hapo,lakini nilivyomuona tu nikajua namna anavyohisi,Faluu hayuko sawa kabisa mama yangu na tukichelewa tutampoteza’’ aliongea Elly kwa msisitizo zaidi.
‘’Sasa tutafanyaje mwanangu?’’aliuliza mama yake.
‘’Daah!!mimi sijui hata tunafanyaje,lakini kikubwa naona ipo haja ya kumkalisha chini na kumshauri,maana bila hivyo sijui hata itakuaje’’ alijibu Elly
‘’Kweli mwanangu,maana hatuna jinsi’’ aliongea mama yake Elly.
Wakati wakiongea kule,Faluu alikua ndani akiwa ametulia mwenyewe huku akiwa na msongo sana wa mawazo na hasa mawazo yake yalikua juu ya nini msaada wa maisha yake.
‘’Nitafanya kitu gani juu ya maisha yangu ya baadae?? Na nani atakae nisaidia kulifanikisha swala hili??,Mungu wangu mbona kama hauko na mimi?nisaidie Mungu wangu maana sijui ni kwanini mama yangu kafariki katika mazingira haya’’ Faluu alikua akifikiria sana.
Wakati akiwa katika mawazo yale,Ghafla aliona hali ya chumba kile alichokuwepo ikibadirika na kulitokea na upepo mkali sana na baada na muda mfupi kulikua shwari kabisa,kitendo ambacho kilimfanya awe na wasiwasi zaidi.
‘’Mmmh,haya mambo gani tena humu,jamani mbona kama mnanifuatilia??mama yangu mumembeba na mimi tena??nimewafanyia kitu gani? Haya njooni mnichukue basi ili mfurahi’’ Faluu aliongea kwa uchungu sana.Sauti ile ilisikika nje walikokuwepo Elly na mama yake,sauti ambayo iliwafanya washtuke na kutaka kufatilia ili wajue nini kinaendelea..
‘’Wwe Elly embu ingia ndani uangalie nini kinaendelea,mbona mwenzio anaongea hivyo,wahi bhnaa’’ aliongea mama yake Elly.
‘’Kweli mama,ngoja nimuangalie’’ alijibu Ellyn a baadae alikimbia kuingia ndani alikokuwepo Faluu ili akathibitishe ajue nini kinaendelea.
Alipofika alimkuta Faluu akiendelea kuongea yale maneno na cha ajabu,Elly alianza kuangalia huku na kule ili ajue ni nani atakua akiongea nae..
‘’Faluu ndugu yangu,wewe ni ndugu yangu sasa,naomba utambue hauitaji kunificha kitu chochote sasa hivi,embu niambie,unaongea na nani?? Na mbona unakua katika hali hiyo??punguza mawazo kaka ‘’ aliongea Elly
Katika kipindi chote hicho Faluu hakuwahi kuongea kitu chochote kilichokua kikimsibu,Lakini baada ya kusikia maneno kutoka kwa rafiki yake Elly ilibidi aongee kitu…
‘’Ni kweli ndugu yangu unayoyazungumza,lakini kuna wakati nafikiria najiona kama niko peke yangu na sina msaada kabisa maisha yangu’’ aliongea Faluu huku akilia.
‘’Kwanini unasema hivyo?’’ Elly aliuliza.
‘’Kwasababu siku ile wakati niko shambani,kuna sauti niliisikia katika masikio yangu ikinieleza kua,baada ya mazishi ya mama nilitakiwa nihame hapa,niende kijiji cha jirani,ndivyo alivyoniambia’’aliongea Faluu.
Maneno yale yalimshtua sana Elly na kujikuta yakimkumbusha siku alipomuona Faluu porini …
‘’Aisee,rafiki yangu pole saana,najua namna unavyoumia,lakini pia kuna maelekezo nilipewa kwamba ;Pole saana kijana,nimefatilia sana namna unavyoteseka na naomba uamini kua mtu mnayetaka kumtafuta nimzima kabisa na muda si mrefu utamuona,lakini swala ambalo napenda sana umfikishie ni hili,naomba umwambie kua katika maisha yake atateseka sana,lakini lazima awe na matumaini ya kufika kule anakotakiwa kufika’’aliongea yule mtu pale na baadae alipotea…
(Kwa mshtuko mkubwa sana ,Faluu aliongea)
‘’Nitateseka?? Sasa ndio maisha gani? Na pia ni mtu gani huyo aliyekueleza maneno hayo’’
‘’Aisee,rafiki yangu pole saana,najua namna unavyoumia,lakini pia kuna maelekezo nilipewa kwamba ;Pole saana kijana,nimefatilia sana namna unavyoteseka na naomba uamini kua mtu mnayetaka kumtafuta nimzima kabisa na muda si mrefu utamuona,lakini swala ambalo napenda sana umfikishie ni hili,naomba umwambie kua katika maisha yake atateseka sana,lakini lazima awe na matumaini ya kufika kule anakotakiwa kufika’’aliongea yule mtu pale na baadae alipotea…
(Kwa mshtuko mkubwa sana ,Faluu aliongea)
‘’Nitateseka?? Sasa ndio maisha gani? Na pia ni mtu gani huyo aliyekueleza maneno hayo’’Aliongea Faluu
‘’Unatakiwa utulie kwanza na upunguze wasiwasi sawa,ila kiukweli mtu huyu si mfahamu na namna alivyotokea pale nilipokua katika msitu ule sijui hata nikueleze nini,embu tuanze maisha mapya sawa ndugu yangu’’Aliongea Elly.
‘’Sawa rafiki yangu,nimekuelewa sana,lakini nitahitaji sana msaada wako’’Aliongea Faluu
Baada ya kukubaliana pale,Elly alimchukua na kumpeleka moja kwa moja kwa mama yake,ili na mama naye aongeze maneno yake,maana waswahili wanasema,maneno ya mtu mzima ni dawa kutokana na hekima iliyopo ndani yake. Mama alipomuona alifurahi sana ..
‘’Karibu mwanangu,jisikie nyumbani ‘’aliongea mama
‘’Asante sana mama yangu’’alijibu Faluu
‘’Mama nimemleta Faluu kwako na nimemweleza kila kitu,kikubwa nataka kushirikiana naye’’aliongea Elly.
‘’Sawa mwanangu,lakini napenda kuongea neno moja kwako mwanangu,Maisha yetu binadamu,yana mambo mengi,hususa ni furaha ,amani na wakati mwingine maumivu,hayo ndiyo maisha yetu wanadamu,kikubwa katika ni uvumilivu na kujua kua hayo yote ni maisha sawa mwanangu,tutakua wote hapa usijali,Nakupenda sana mwanangu’’mama yake Elly aliongea.
Maneno yale yalimfariji na kumfurahisha sana Faluu na kujiona kama maisha ameyashinda tayali.Faluu alianza maisha yake kwa moyo na akajikuta akiwa na furaha sana na siku zilizidi kwenda.Baada ya miezi kadhaa Faluu alianza akijishughulisha na biashara ndogondogo ya kuuza nyanya akiwa na rafiki yaake Elly ambaye ndiye aliyemchukulia kama ndugu,kwa maana akuwa na ndugu mwingine tofauti na familia aliyokua akiishi kwa kipindi hicho.
Biashara yao ilizidi kukua siku hadi siku na alizidi sana kuyapenda maisha yale aliyokuwepo.Lakini siku moja akiwa amekaa sokoni anaendelea na biashara yake,Elly alikua ametoka kidogo ameenda kufatilia mzigo mwingine,Faluu alijikuta mawazo mabaya yakimjia katika kichwa chake,yalikua ni mawazo juu ya maisha yake yaliyopita na zaidi ya yote ilikua ni kumbukumbu juu ya mama yake na wakati huo huo akiwa katika mawazo hayo alijikuta yale maneno aliyoambiwa kipindi akiwa shambani siku mama yake anafariki yanamjia…
‘’Baada ya mambo yote ya msiba kuisha hakikisha unaenda kwa mjomba wako,hayo ndiyo maneno ya mwisho nilioachiwa na mama yako’’ Maneno haya yalifanya hali yake kubadirika na kua na majonzi sana.
Wateja walipokua wakifika kutaka huduma walishangaa sana,maana hawakumzoea akiwa katika hali ile,wengine walijaribu kumuuliza..
‘’Faluu kaka mbona kama unaonekana hauko salama leo,kulikoni ndugu yangu’’ aliuliza dada mmoja..
Lakini cha ajabu siku hiyo Faluu akuwa na maneno mengi zaidi ya kutoa huduma tu kwa wateja na kuendelea na hali yake.Ilikua nikipindi kigumu sana kwa Faluu na kulikua na swali ambalo lilikua likimsumbua zaidi…..
‘’Kwanini mama yangu alinitaka niondoke hapa baada ya kumaliza mazishi??, hivi inawezekana kweli?? Na kwanini??’’ lakini kwa upande wake alikua akikosa majibu maalumu yakujijibu..
Baada ya muda Elly alifika na kujikuta akipigwa na butwaa baada ya kuona hali ile kwa Faluu,maana ile hali muda mrefu sasa kuiona kwa rafiki yake,
‘’Ndugu yangu vipi?, mbona hivyo kaka’’aliuliza Elly
‘’Samahani kaka naomba nikuache,nikapumzike kidogo nyumbani,siko salama sana,nakuomba’’hayo ndiyo maneno aliyoongea Faluu na baadae aliondoka na kuelekea nyumbani.
Elly alibaki njia panda pale,maana Faluu hakumfungua kujua nini ni nini kwake na wakati mwingine alifikiria kama yeye ndiye sababu ya hali aliyokua nayo Faluu..
‘’Mmmh,kwanini hali hii ghafla??kulikoni??lakini labda’’alifikiria na baadae aliamua kuachana nayo na kuendelea na biashara pale sokoni…
Baada ya Faluu kufika nyumbani,alipitiliza hadi katika chumba wanacholala na kupumzisha mawazo yake kidogo,lakini pia wakti akiwa ndani amelala,yale maneno yalimjia tena na kusumbua akili yake,alijikuta akishindwa kuvumilia..
‘’Jamani nitaisha hivi mpaka lini ??,basi ngoja nifanye mnavyotaka basi’’yalikua ni mawazo yake Faluu na baadae aliamka na kuanza kukusanya nguo na baadae aliondoka bila kutoa taarifa na kuelekea katika kile kijiji alichoambia aelekee baada ya mazishi ya mama kama maagizo kutoka kwa mama yake ………………..
Faluu aliondoka na kuelekea katika kile kijiji alichoelekezwa na ile sauti aliyoisikia shambani.Wakati akiwa njiani alikua na mawazo mengi sana na hasa alikua akitafuta sababu ya kwanini aende kwa mjomba wake katika hicho kijiji.Alipokua amefika katika mti mmoja mkubwa uliokuwepo pembezoni mwa njia aliyopita,upepo mkali sana ulianza kuvuma ghafla tu,hali ambayo ilimfanya aingiwe na hofu..
(Huku mapigo yake ya moyo yakiwa yamebadirika,mawazo yalimjia)
‘’Mmh! Hii nini sasa na kwanini hivi,mbona nateseka saana??’’ alikua akiwaza huku machozi yakimtoka,hali ile ilimuumiza sana..
Baada ya Elly kukaa muda mrefu sokoni bila majibu yoyote ya rafiki yake,alianza kujisikia vibaya na kujikuta akiingiwa na hofu sana na kwa vile alikua amezoea kua naye sokoni alijkuta akikosa amani na hivyo akaamua kufunga ili aende akamjulie hali yake nyumbani.Alipofika nyumbani alimkuta mama jikoni akiwa anapika,mama alipomuona alibaki akimshangaa tu kitendo ambacho kilimpa wasiwasi Elly..
‘’Mama mbona unaniangalia sana kulikoni’’ Elly aliuliza.
‘’Nakushangaa wewe hapo,’’ mama alijibu.
‘’Unanishangaa?? Nini tena??’’ Elly aliuliza
‘’Sasa mbona huko peke yako? Rafiki yako yuko wapi?’’ mama aliuliza
Swali lile lilimshtua sana Ellyn a kumfanya hautupe ule mfuko aliokua amebeba…
‘’Peke yangu?mbona Faluu amekuja huku muda mrefu sana,maana muda Fulani ametoka sokoni akiwa analalamika hajisikii vizuri,mimi nikamwambia aje apumzike,kwani wewe hujamuona?’’ Elly aliongea huku akiwa na amepagawa.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni