MY DIARY (25)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mtunzi: __
SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Sikuisha hapo pia nilimpongeza kwa kunijali na kunipenda na kuhakisha kuwa siingii kwenye majanga kama yake mara baada ya kutoka jela. Siku hiyo nilimuelewa sana Joyce na nilikuwa tayari kumsapoti kwa lolote ili mradi tu atimize athma yake hiyo ya kuzaa. Tuliongea mengi sana na baadaye alinionesha picha ya mtu ambaye alitaka kuzaa naye.
TUENDELEE...
Nilishituka kwa sababu mtu huyo alikuwa ni maarufu sana hapa mjini Arusha kwa sababu baba yake alikuwa anamiliki maghorofa makubwa na hoteli za kitalii.
Ilibidi nimulize Joyce kwa nini amemlenga huyo na sio wengine? Akanijibu kuwa hataki mwanaye aje apate shida huku duniani. Kimoyomoyo nikajisemea angejua hata mimi nilizaliwa kwenye familia tajiri lakini leo hii nateseka na shida za dunia asingekuwa na mawazo hayo. Lakini sasa Joyce utampataje huyu mwanaume hili hali hamfahamiani ilibidi nimuulize Joyce. Joyce akacheka na kuniambia “nimeshapewa sehemu na viwanja anavyopenda kukaa hivyo nitamwinda mpka nimpate.
Basi tulirudi nyumbani kwake na maisha yakaendelea. Maisha yetu yaliendelea hivyo hivyo kwa yeye kwenda kwenye shughuli zake na mimi kwenda salooni.
Siku moja nikiwa zangu home nimechoka na miangaiko ya salooni alinipigia simu mida ya saa mbili usiku. Akanambie niende Ngurudoto hotel lakini nivae kimtego mtego na nikifika hapo nje nimpigie na atanambia cha kufanya. Sikutaka kumkatalia lakini nilimuuliza sasa niavaaje?. Akanambia vaa kimini au pigo lolote ambalo mwanaume yeyote akikuona lazima atakuangalia mara mbili mbili.
Nikajiuliza sijua ana dili gani huyu wakati siku zote ananikataza hizi kazi nisije na mimi nijikwaa na umeme kama yeye. Lakini kama unavyojua mimi kwake huwa sina kipingamizi kutokana na historia yetu na utu aliouonesha kwangu kipindi chote nikiwa kwenye matatizo. Kumbe yule mtoto wa kigogo anayemwinda azae naye alikuwepo hapo. Basi nilifika sehemu hiyo na kuanza kung’aa sharubu nisijue nielekee wapi. Wakati naendelea kufikiria nini cha kufanya mara simu yangu ikaita. Na nilipoangalia ilikuwa ni meseji ndefu kutoka kwa Joyce. Meseji ilinielekeza nisamame hapo hapo na niendelee kubofyabofya simu huku nikionekana kama mtu aliyepoteza dira
Na kuna gari ya yule jamaa anayetaka kuzaa naye anakuja hapo kuspend.Na nyuma ya gari hilo kuna gari la lingine la kijana mtanashati ambaye yeye amemtuma. Hivyo chochote atakachonifanyia huyo kijana niwe mvumilivu it’s a deal.Meseji ndo ilimazia kwa kusema kuwa ni dili tunacheza hapo. Mara likaingia gari la kwanza na la pili kwa mpigo, wakati wale waliokuwa kwenye gari la mbele hawajapaki na kushuka pale getini alishuka kijana mmoja sharobaro na akanifuta kwa shari na kuanza kuniambia “ Kwa nini unanisaliti mpaka uanze kutembea na vigogo” kabla sijajibu kitu Yule kijana alinizaba kibao.
Mweeeeh hapo nilisikia uchungu nikaanza kupiga mayowe ya kupigwa. Yule kijana akaendelea kunitukana na kuniita Malaya. Sikujua niimbie au niendelee kusubiri kipigo kingine. Wakati anaendelea kunitukana Yule mtoto wa kigogo alishuka kwenye gari na kuwaambia walinzi wamshike Yule kijana kwa sababu anachofanya ni uzalilishaji. Basi kwa ustaarabu akanifuata mimi ambaye nilishachuchumaa na kujiinamia na kuniiunua na kuniambia pole dada kuna mtu ulikuja kuonana naye? Nikamjibu kuwa ndio alafu huyu kaka mimi simfahamu.
Wakati naendelea kujieleza kumbe Joyce alikuwa sehemu ya juu ya hotel hiyo akishuhudia kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Alishuka huko kama mbogo na kuja sehemu tulipokuwepo nay eye akawasha moto. “ Yaani mda wote huo mimi nakusubiria kumbe unagombania wanaume huku nj?” Ilibidi Yule mtoto wa kigogo ajishushe na kutumia ustaarabu na busara na kusema “ samahnai dada huyu ni nani yako?” Huyu ni mdogo wangu kabisa nashangaa mda wote hafiki kumbe huku nje kuna matatizo alisema Joyce kwa sauti ya upole.
Sawa basi punguza jazba huyu mdogo wako hana shida bali huyu kijana ndo mkorofi alisema Yule mtoto wa kigogo. Sawa usijali nitamalizana naye huyu ni mdogo wangu kabisa alisema Joyce. Akawambia walinzi “ naomba uwaambie wahudumu waniletee bili yangu niondoke zangu siwezi kukaa hapa tena. Wakati mlinzi anapiga hatua kumfuata muhudumu, mara akamwambia au chukua hii. Akafungua pochi yake na kutoa dola za kutosha kisha akmpa Yule mlinzi.Alimpa nyingi mpaka Yule mlizi akashangaa.
Ikabidi mlinzi akamwambia “ hapana dada mbona umenipa nyingi sana wakati umekunywa maji tu. Kwa dharau akamwambia zingine utatumia kwa matumizi yako. Yule mlinzi bado alikataa ofa hiyo nahissi ni kwa kumuogopa boss wake ambaye ndo huyo mtoto wa kigogo. Basi ilinibidi niingilie kati kwa kutoa noti ya elfu tano na kumpa mlizi kisha nikazichukua zile dola na kuziweka kweneye pochi yangu. Joyce akanambia haya twende turudi nyumbani out imeishia hapa.
Wakati tunaondoka Yule mtoto wa kigogo alitoa businesscard yake na kumpa Joyce akamwambia pole sana kwa yaliyokukuta naomba ukitulia unitafute.
Tuliondoka na kuingia kwenye bonge la gari alilokuwa amekuja nalo Joyce. Nilijiuliza maswali mengi sana ikiwa ni pamoja na kujiuliza hilo gari alilipata wapi.
Nikajijibu mwenyewe kweli huyu ni kiboko ya mujini. Nilimpigia saluti kwa sababu hakuna jambo aliloamua hapo mjini akashindwa. Tuongee ukweli Joyce wewe ni mwisho wa reli kigoma ilinibidi nimwambie. Alicheka na kuniambia hiyo ni hatua moja bado ya pili ya kumuingiza laini. Nikamsifia kwa kumwambi wewe tena ukishapata namba zake kwisha habari yake. Akanambia usijali thi is our new mission( huu ndo mpango mpya).
Kweli ni new mission lakini kle kibao kiliniumiza sana mpaka sa hivi nakisikilizia. Akacheka na kuniambia pole ngoja turudisha gari la watu tukae mahali tule na kunywa ujipooze.Kwanza usiku huu nipo na dili na mzungu kwa hiyo tuatenda mahali kula bata na baada ya hapo nitakurudisha nyumbani maana situlishakubali wewe usijiusishe kabisa na shughuli hizi hili usije na wewe kwenye janga la maradhi. Aliendelea kusema best wangu huyo ambaye siku hiyo alikuwa na furahaa sana.
Alafu siunajua tena wewe ndo unatakiwa unilelee mwanangu. Basi tulirudisha gari sehemu ambaye alikuwa amekodisha. Baadaye tuliingia mahali na kuazna kula baata mpaka kuku wakaona wivu. Wale wazungu alikuwa akiwasema walikuja na baada ya usiku kuwa mkubwa waliamua kunurudisha nyumbni na wao kuendelea na kile kinachoitwa kifuatacho ITV. Nilila huku nikiwa mwenye upweke kwa maana na mimi ilikuwa nimemiss sana kale ka mchezo. Yaani huwezi amini ilikuwa ni mwaka mzima umeshapita bila kumjua mwanaume.
Mawazo ya bailoji ya olevel ilinijia eti ile theory ya use and dis use of organ ambapo inaelezea kuwa kama kiungo ukikitumia vizuri ndivyo kinavyokuwa kikubwa na kuwa imara nakama usipo kitumia kinakuwa dhaifu na kinawez kupotea. Nilikuwa nawaza ujinga lakini nakumbuka mifano ya mwalimu wangu wa bailoji ambayo alikuwa akiitoa enzi hizo kwa mfano alituambia eti nyoka zamani alikuwa na miguu na twiga hakuwa na shingo ndefu ila kutokana na harakati za kutafuta majni kwenye miti mirefu ndo ikawa hivyo.
Lakini pamoja na mawzo hayo ya kijinga bado msimamo wangu wa kuvumilia mpaka hapo nitakpopata mwanaume wa kunioa ulikuwa pale aple. Sio kwamba wanaume walikuwa hawanisumbui. Walikuwa wakinisumbua sana lakini nlikuwa siwahamini nab ado niliamini kuwa wao ni wakatili sana. Wakati mwingine nilitaka kumpa nafasi Yule wakili aliyenisaidia kutoka rumande lakini bado nilikuwa simwamini kabisa. Na pia hakuonesha nia ya kunioa zaidi ya kutaka mzigo
tu.
Nikajisemeha lakini angenikuta enzi zangu ningempa na kumchuna hela zake.Niliwaza sana kuhusu maisha yangu lakini bado niliendelea kumtegemea mungu na kuamini kuwa ipo siku atanifungulia njia kwa kuwa yeye ni muweza wa yote. Najua ndugu msomaji umesema Amina. Siku zilizidi kwenda huku Joyce mambo yake yakizidi kunyooka kwani alishafanikiwa kumwingiza laini Yule mtoto wa kigogo.Hapaana chezea mtu anayeitwa Joyce jamani.
Siku moja tukiwa nyumbani nilimuona Joyce akiwa anatapika tapika huku hali yake ikibadilika badilika kila siku.Nikajua tayari mambo yalishakuwa mambo kurubembe alikuwa amepatikana na nilopomuuliza alikiri kwa kinywa chake kuwa alikuwa ni mjamzito. Nilimuuliza mimba ya nani akanambia huwa hafanyi makosa katika kutimiza ndoto zake, ile mimba ilikuwa ya yule mtoto wa kigogo.
Miezi ilisogea na kitumbo kilianza kuonekana.Ilivyofika miezi minne kasheshe ndo ikaanza.Joyce alianza kuumwa na tulivyofika hospitali tuliambiwa kuwa mimba ilikuwa imetunga pembeni ya uji wa uzazi. Joyce alikuwa akitapika kila anapokula kitu. Akawa mtu wa kutundikiwa drip tu. Kwa kweli alikonda sana mpaka nikajua safari yake ya kifo ndo imefika. Madaktari walishauri aitoe hiyo mimba lakini alikataa kwa madai kuwa hata mama yake alipata tatizo kama hilo pindi alipokuwa amebeba ujauzito wake.
Aliendelea kuishi katika hali hiyo na baadaye tuliamishiwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC. Miezi ilizidi kwenda na madaktari walimuahidi hali itatengemaa pindi mimba itakapofikisha miezi 6. Basi niliendelea kumuhudumia huku nikupewa sapoti ya pesa na yule kigogo aliyempa mimba. Kweli madaktari wana nafasi yao hapa duniani kwani baada ya miezi sita Joyce alipona kabisa na kurudi katika hali yake ya kawaida
Tuliruhusiwa na kurudi Arusha ambapo tuliendelea na maisha yetu kama kawaida.Joyce alitakiwa kila siku kufanya mazoezi ya kutembea kwa miguu umbali fulani. Na tulifuata ushauri wa madakatari na mambo yalienda vizuri. Hatimaye miezi tisa ilifika na Joyce alijifungua salama kabisa.Alijifungua mtoto wa kiume na akampa jina la Lucky yaani bahati.
Ndoto zake zilikuwa zimetimia na alikuwa akifuata ushauri wa kitatibu ili kuhakikisha mtoto huyo hasipate maambukizo ya ukimwi. Mungu aliweka mkono mtoto huyo akaendelea kukua na hatimaye alikuwa mkubwa kabisa na alipopimwa alionekana kuwa ni mzima wa afya.Siku, mwezi na hatimaye miaka zilipita na mtoto akawa mkubwa na alipelekwa shule ya English medium.
Sisi tuliendela na shughuli zetu maana mtoto huyo alipelekwa shule ya gharama na baba yake na alikuwa boding na baba yake alimuhudumia kwa kila kitu.
Mwanaume huyu aliyezaa na Joyce alikuwa na mke na watoto wengine hivyo hawakuweza kudumu na Joyce. Ikumbukwe na hata hiyo mimba ilibebwa siku ya kwanza tu walipokutana na Joyce hakufanya makosa. Joyce hakuacha ule mchezo wake wa kufanya biashara haramu ikiwa ni pamoja na kuuza mwili wake. Nilimsihi sana aache kufanya hiyo kazi kwani alikuwa akisambaza ukimwi kwa watu wasio na hatia.
Joyce alinambia yeye haendi kujipanga foleni kama makahaba wengine hivyo yeye hufanya biashara hiyo kitaalamu zaidi.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni