Notifications
  • MY DIARY (33)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TATUTULIPOISHIA...Nilikuwa nachanganya staili za kijamaika na hizi za kwetu, sikuacha pia zile za Nigeria hapo nikapata vitu vyangu vya tofauti kabisa. Basi baada ya kujihakikishia kuwa nipofiti kwa mastahili yangu hayo nilisubiri siku ya shindano ifike nikafanye yangu. Siku ya shindano ilifika na mimi nilikuwa miongoni mwa washiriki walioingia tatu bora.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (32)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA MBILITULIPOISHIA...Lakini kuchepuka kwangu na kuingia mgombani haikumaanisha kuwa sheria ingeniacha hivi hivi.Ilifika mahali ikabidi nizime gari na kutulia tulii kusikilizia nini kitafuata.Tayari nilikuwa nimezungukwa na mapolisi ambao walikuwa wakinifuatilia kwa kutumia pikipiki.Kwa bahati nzuri dereva wa lile gari na yeye alishafika hapo na alishawaambia polisi kuwa mimi naugua ukichaa na nilifufuka kutoka mochwari.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA…
  • MY DIARY (31)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA MOJATULIPOISHIA...“marehemu pia alinieleza kuwa ana miliki duka la vitu vya urembo wa kike ambalo pia Leah analisimamia ila hilo apewe mdogo wake Marry ambaye yupo hapa. Mama mdogo huyo mara baada ya kuyasema hayo alikaa zake chini. Baba mdogo ambaye hakurizika na maelezo hayo alisimama na kusema “kwa hiyo kama marehemu alijua kuwa atakufa hivi karibuni kwani nini hakufuata taratibu za kisheria za kuandika wosia na kurithisha mali.IKIWA UNASOMA…
  • MY DIARY (30)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINITULIPOISHIA...Baada ya hapo Nnilimwomba mama mdogo ajikaze na kuwatarifu ndugu wengine habari hizo za msiba.Tulisaidiana hivyo hivyo maana sio siri kila mmoja alikuwa na uchungu sana kutokana na mazingira ya kifo hicho. Habari zilizidi kusambaa kwa kasi na majirani walianza kukusanyika hapo kwa mama mdogo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Msiba ni msiba tu na ukitaka kujua binadamu…
  • MY DIARY (29)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA TISATULIPOISHIA...Hapo sasa nikazidi kuchanganyikiwa ikabidi nimuulize mama huyo alikuwa akifanyia shughuli zake za kujipatia kipato sehemu gani.? Yule dada akanambia kuwa anafanyia soko la ndizi huko Korongoni. Sikuwa na jinsi nilimuomba anipeleke lakini na yeye alisita sita kwa madai kuwa alikuwa na kazi nyingi za kufanya na bado anatakiwa ampeleke mtoto shule.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (28)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA NANETULIPOISHIA...Sisi tumesomea mambo haya bhana waliendela kuzungumza wale walinzi huku wakishuka ngazi kwa polepole. Hapo na mimi nikawa nimejifunza kitu kuwa kumbe unaweza kuingia na mtu guest akakuzuru kisha akaondoka zake.Sasa sijui kwenye zile guest zetu za uswahilini kama wanalijua hili.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi nilala japo usingizi ulikuwa hautaki kuja kwa…
  • MY DIARY (27)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA SABATULIPOISHIA...Alinamba eti hayo ya mimi kuolewa tuyaeke pembeni na kwa nini siku hiyo nisilale Moshi tukumbushie enzi zetu. Mwalimu John aliendelea kusema kuwa amenimiss sana na anomba nisahu yaliyopita na turudie yale maisha yetu ya zamani.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilijifanya simwelewi lakini ukweli ni kwamba nyota ya mwanaume huyu ilikuwa ni kali sana zaidi yangu na…
  • MY DIARY (26)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA SITATULIPOISHIA...Joyce alinambia yeye haendi kujipanga foleni kama makahaba wengine hivyo yeye hufanya biashara hiyo kitaalamu zaidi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Alisistiza pia kuwa eti huwa anatumia kinga kuwakinga wengine. Wakati mwingine alinambia acha awaambukize kwa sababu wanaume wangekuwa na akili basi wasingeenda kununua mwanamke. Anasema kuwa laiti biashara hiyo…
  • MY DIARY (25)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA TANOTULIPOISHIA...Sikuisha hapo pia nilimpongeza kwa kunijali na kunipenda na kuhakisha kuwa siingii kwenye majanga kama yake mara baada ya kutoka jela. Siku hiyo nilimuelewa sana Joyce na nilikuwa tayari kumsapoti kwa lolote ili mradi tu atimize athma yake hiyo ya kuzaa. Tuliongea mengi sana na baadaye alinionesha picha ya mtu ambaye alitaka kuzaa naye.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (24)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA NNETULIPOISHIA...Kwa kweli siku hiyo niliwaza sana na kutafakri vitu vingi. Wale wanachuo wenzangu wamenambia kuwa Msouth alikuwa kwa kimada mwingine na japo stori haikumalizikia ila ukweli ni kwamba alifumaniwa na kupigwa vibaya na huenda walimtupa mahali na ndio maana chanzo cha kifo chake hakieleweki.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilijaribu kuijikontrol ili nisiwaze kitu…

MY DIARY (26)

Jina: MY DIARY
Mtunzi: __

SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
TULIPOISHIA...
Joyce alinambia yeye haendi kujipanga foleni kama makahaba wengine hivyo yeye hufanya biashara hiyo kitaalamu zaidi.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

TUENDELEE...
Alisistiza pia kuwa eti huwa anatumia kinga kuwakinga wengine. Wakati mwingine alinambia acha awaambukize kwa sababu wanaume wangekuwa na akili basi wasingeenda kununua mwanamke. Anasema kuwa laiti biashara hiyo ingekosa wateja basi hakuna wasichana ambao wangejibweteka na kusubiri kutumia miili yao kama migodi.

Ingawa Joyce alisisitiza kuwa huwa anavaa kinga kila akikutana na mwanaume bado mimi binafsi huwa siamini sana kuhusu mipira hiyo kuhusu kuzuia magonjwa labda mimba. Kwa upande wangu mimi niliendelea kuishi maisha ya kitakatifu. Siku moja niliamua kuja Moshi ili kuanza michakato ya kuyatafuta yale madini ya urithi.Ambalo na amini ndio tumaini langu pekee lilobaki hapa duniani. Wataalam wanasema madini hata yakikaa miaka 100 kama yalihifadhiwa vizuri hayawezi kuharibika.

Hivyo hata mimi sikuwa na hofu kuhusu madini hayo kuharibika au kuharibiwa kwa sababu sehemu yaliyohifadhiwa na katikati ya shamba na kwa mujibu wa marehemu baba yangu hakuna ambaye angeweza kuyafikia hata kama shamba hilo lingeendelea kulimwa. Madini hayo yalikuwa mita 50 chini ya aridhi na sehemu hiyo ilichimbwa kaburi la bandia na kujengewa vizuri kwa juu ili kuwaogopesha watu. Hivyo kwa jinsi Watanzania walivyokuwa wanaogopa na kuyaheshimu makaburi wasingeweza kugusa sehemu hiyo hata kama hilo shamba lingeuzwa kwa watu wengi kiasi gani.

Hivyo vigezo zilinipa ujasiri wa kuamini kuwa hayo madini yananisubiri tu mimi. Nilifanya tena ziara ya kwenda mpaka kijiji hicho na safari hii nilifika kwa katibu kata na nilijifanya kuwa ni mwanafunzi ninayefanya utafiti na lengo langu kubwa ilikuwa ni kutaka kujua kuwa kata hiyo ilikuwa na vijiji vingapi na je kijiji kina ukubwa gani. Na je kijiji kimoja kina ekari ngapi na wakazi wangapi.Hapa nilitaka kufanya mambo kisomi kidogo maana bila hivyo unaweza kujikuata unazunguka kijiji hadi kijiji bila mafanikio.

Nilipelekwa kwa afisa kilimo wa kata ambaye naye alinipokea vizuri akanipa data zote zinazohusu mambo ya mashamba.Basi niliamua kurudi zangu mjini Moshi ili nipande gari la kurudi Arusha. Nilivyofika mjini wakati navuka barabara sehemu moja wanayoiita double road, nilisikia pipiiii na ilikuwa ni mlio wa gari ndo ambayo sikujua ni nani alikuwa ndani.Mara lile gari ndogo iligeuzwa na kuja kusimama mbele yangu.

Sikuamini macho yangu mara baada ya kumuona mtu ambaye nilikuwa nikimpenda sana maishani mwangu na ambaye alikuwa ni mwanaume wangu wa kwanza na si mwingine bali ni mwalimu John. Mtu ambaye alinifundisha mapenzi na kunitoa uanawali wangu. Kwa haraka haraka ilionekana mambo yake yalikuwa ni mazuri kwa sababu alinawiri na kitambi cha nyama na bia kilionekana. Hivyo ni dahiri kuwa alikutana nahela wakati huo.

Basi tulisalimiana na aliniomba tutafute sehemu tuzungumze mawili matatu.Nilimwambia kuwa nilikuwa na haraka kwani nilikuwa nataka niwahi kurudi Arusha. Akaniuliza wa amaki kwani siku hizi haukai tena Moshi.Nilimjibu kwa kifupi kuwa nilishahama siku nyingi sana. Akaangalia saa yake na kuniambia sa hivi ni saa kumi naomba unipe kama lisaa limoja then utapanda gari na kuondoka zako. Nilimshangaa huyu mtu maana tumekutana bahati mbaya lakini alikuwa anang’ang’ania nilimwwambia tufanye siku ingine tena aje Arusha kwa sababu mimi sikuwa na ratiba tena ya kuja Moshi.

Bado hakurizika akanambia kwa kimombo “its ok, but am about to fly to Europe the day after tomorrow( ni sawa lakini kesho kutwa nina mpango wa kusafiri kwenda ulaya).

Mmmmh niliguna na kumwambia “whatever is excellent and its not a big deal we will meet soon after you return back to Tanzania” (vyovote ni sawa ila tutakutana tu siku ukirudi kutoka ulaya) Na mimi nilijaribu kumwaga kimombo kidogo. Akanijibu “ as a good leader, I must be able to use both style of leadership especially when the diplomatic one failed” (nikiwa kama kiongozi lazima niwe na uwezo wa kutumia staili zote za uongozi hasa pale staili ya diplomasia inaposhindikana). So what is your next option( kwa hiyo unataka kufanya nini) nilimuuliza kwa mshangao!!!!!!!!!!!!.

The law of force or dictatorship must be applied( lazima nitumie nguvu) Nikamuuliza how(kivipi). Akanijibu action speaks more than words ( vitendo vitafuata kuliko maneno). Nikaona huyu ni mkorofi kumbe yaani anataka kutumia nguvu kunilazimisha tuende mahali tuakaongee. Nikamwambia am wait your reaction (nasubiri hiyo nguvu unayotaka kutumia). Akanijibu for every action there is an equal and corresponding reaction. Wakati bado nafikiria hiyo sentensi ya kifizikia alinipokonya mkoba wangu na kuutupia kwenye gari.

Nilibaki nimeduwaa nisijue nini cha kufanya maana ndani ya ile pochi yangu kulikuwa na nauli na data zangu nilizozipata huko kijijini.Akashuka kwenye gari akanipa mkono nikamfuata kanifungulia mkono na kuingia kwenye gari.Na tulienda bar moja ambayo ipo karibu na stendi.Tukiwa kwenye gari aliniuliza vipi umeolewa? Nikamjibu wa kumuuliza swali kwa nini umeniuliza hilo swali? Akanijbu na yeye kwa swali kwani mkononi umevaa nini?. Sikutaka kumjibu swali lake hilo kwa sababu ni kweli mkononi nilikuwa nimevaa pete ya ndoa

Na hiyo ndo ilikuwa ni staili yangu mpya niliyoigundua ili kupunguza usumbufu wa wanaume ambao kila siku walikuwa wakinitamani na kunitongoza. Hiyo pete si yeye tu kila mtu niliyekutana naye aliniuliza na ilikuwa ni jibu la moja kwa moja kuwa mimi ni mke wa mtu. Kweli kipya kinyemi ingawa kidonda na siku zote ya kale ni dhahabu niliwaza misemo hiyo maana Ticha John alionekana kabisa kuchanganyikiwa juu yangu. Baada ya kukaa kimya kwa sekunde kadhaa akanambia siku hizi naona umeamua kuwa modo.Hapo nikajua alinipiga dongo kijanja maana mwili wangu siku hizi ulikuwa umepungua japo wengine walisema kuwa ndo nimekuwa mzuri zaidi.

Kama kawaida yake tulivyofika sehemu hiyo aliagiza kuku wa kurosti na bia tena hizi za nje Heinken. Mimi sikutaka mbwembwe na kwa kujichukulia maujiko niliagiza maji kubwa. Na aliponiambia ninywe pombe nilkataa katu katu kwa madai kuwa mimi siku hizi nimeacha pombe tangia niolewe. Ilibidi awe mpole alivyosikia neno kuolewa. Tuliongea mengi sana na alinambia sasa hivi yeye sio mwalimu tena wa sekondari bali ni mwalimu wa chuo. Na alipata chuo cha kufundisha Moshi mara baada ya kumaliza masomo yake ya masters.

Nilimpongeza kwa hatua hiyo ya kimaendeleo katika maisha.Nilimuuliza anafundisha chuo gani akanijibu ni chuo cha ualimu mwenge. Sikusita kumuuliza kama alishawahi kukutana na wale marafiki zake wa kipindi kile.Hapo akanipa habari za kusikitisha kidogo kwani alinambia kuwa wote walishafariki kwa sababu walipata ajali ya gari siku moja usiku wakiwa wametoka kwenye starehe.

Iliniumiza sana habari hiyo lakini kwa upande mwingine nilisema ni bora maana ule ukatili walionifanyia siku zile ulikuwa ni mbaya sana. Si unakumbuka waliniita wakaninulia pombe mpaka nikazima na baada ya hapo walinipeleka mahali na kunifanyia kitu cha kinyama yaani wote watatu walifanya mapenzi na mimi tena bila izini yangu, huwa inaniuma sana kila nikikumbuka. Kitendo hicho huwa kinaniuma sana kwani ni zaidi ya ubakaji.

Nikajisemea kweli malipo ni hapa hapa duniani, kama wao waliamua kuendekeza starehe basi hiyo ndo zawadi ya starehe. Sikuishia hapo nilimuuliza kama na yeye Mwalimu Johna alikuwa ameoa. Hapo aliguna na kuniambia “kwanza nikuombe msamahaa kwa lile tukio lililotokea mlimani city. Kama mnakumbuka siku ile nilivyokwenda jijini kufuatilia mambo ya mkopo nilimkuta akiwa na akiwa na kimwana kingine wakila bata huku wakijiachia ile mbaya.

Nakumbuka nilimfuata walipokuwa wamekaa na nilpomsalimia kwa kumpa mkono alikataa na kunikana kunijua. Kitu kile nacho kiliniuma sana na nakumbuka eti wakati naondoka na yeye alinifuta na kunishika. Palitokea patashika sana siku ile lakini baadaye nilifanikiwa kuondoka na kuendelea na mambo mengine. Tangia siku ile nilitokea kumchukia sana huyu mwanaume.

Nilimwambia nimeshakusamehe japo siwezi kusahau tukio lile na mengine mengi mabaya uliyonitendea. Alinieleza eti yule binti waliachana siku ile ile baaada ya lile tukio pale mlimani city. Nikamwambia nisawa lakini mbona hujanijibu kuwa wewe umeshaowa au la? Akanijibu kwa kifupi kuwa bado hajaoa na alikuwa bado anajipanga kimaisha lakini mambo yake kwa sasa yapo sawa.Kwa hiyo upo kwenye uchumba nilimuuliza?

Mmmmh na wapenzi tu lakini kati ya hao sijaona wa kumuoa alijibu mwalimu John kwa ujasiri.Ilibidi na mimi nigune kusikia wapenzi nikamuuliza kwa hiyo unao wengi? Bado aliendelea kujibu kwa kujiamini ndio kwani wewe unashangaa nini ni kawaida kwa siku hizi mwanaume kuwa na wasichana zaidi ya wawili na bado inapofika mda wa kuoa asione wa kumuoa.

Basi akaendelea kufafanua kuwa kwa mfano yeye ana msichana ambaye ndio amemaliza form four mwaka huo.Sasa je huoni kama ni ndoto kwa mimi kumuoa binti kama huyu aliniuliza mwalimu John. Nikamuuliza kwa nini usimuoe kwani wakati unamtongoza na kufanya nae mapenzi hukulifikiria hilo. Akanijibu eti nililiona ila wakati ingine tamaa za mwili huwafanya wanaume wawatongoze wasichana ambao hawaezi kuwa na future nao..

Hapo nikajifunza kitu na kukumbuka kisa cha baba mwenye nyumba ambaye alidiriki kutembea na mimi na wakati alikuwa na watoto wakubwa zaidi yangu. Basi tuliendelea kupiga stori mbili tatu za hapa na pale na alisisitiza kuwa kama bado sijaolewa huo ni mda muafaka. Nilimjibu kuwa amechelewa na hata kama ningekuwa bado sijaolewa nisingeweza kumpa hiyo nafasi kwa sababu ya bad memory( kumbukumbu mbaya) nilizokuwa nazo juu yake.

Akanambia siku zote nisipende kuishi kwa historia au hisia hivyo basi yakale hayanuki na we should let the past pass( tusahau yaliyopita). Aliendelea kumwaga sera zake eti pamoja nakumwambi kuwa nimeolewa bado hakusita kueleza upuuzi wake.Hapo ndo nikaamini kuwa wanaume ni kiboko. Mbaya zaidi aliacha stori zote na kuanza kuniomba kale kamchezo.Na kwa jinsi nilivyokuwa nimekamiss maneno yake kwa kweli yalianza kuniingia.

Alinamba eti hayo ya mimi kuolewa tuyaeke pembeni na kwa nini siku hiyo nisilale Moshi tukumbushie enzi zetu. Mwalimu John aliendelea kusema kuwa amenimiss sana na anomba nisahu yaliyopita na turudie yale maisha yetu ya zamani.

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
68 My Diary Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni