Notifications
  • MY DIARY (36)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA SITATULIPOISHIA...Sasa wewe fikiria mimi niliyeletewa zawadi sikujua ni zawadi gani lakini yeye tayari alishafungua na kuchungulia na kujua nini kilifungwa huko ndani.Basi nikaendelea kumuhudumia yule mama huku na yeye akiniambia kuwa itabidi nikimmaliza hizo zawadi tusifungue hapo hapo na waniimbie wimbo wa happybirthday.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Tuliendelea na stori mbili…
  • MY DIARY (35)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TANOTULIPOISHIA...Tatu niliambiwa kuwa ndugu zake na wazazi wake walihusika kwenye mipango hiyo hivyo walibariki kabisa huyo binti kuniacha mimi mumewe wa ndoa na kuamua mtoto wao aolewe upya. Nne ni kwamba huyo mzungu amewaamishia wazazi wake mjini na amewajengea nyumba ya kifahari.Kwa hiyo mimi ninavyowapigiana simu na kuwajulia hali kumbe wenzangu huwa wananichora tu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (34)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA NANETULIPOISHIA...Hapo nikakumbuka kuwa zile zana zangu za kazi nilikuwa nazo ni vile vifaaa vya kupimia ukimwi ambavyo huwa navitumia kabla ya kukutana na mwanaume yeyote nisiyemfahamu. Nikaamua kumkubalia huku nikiamini kuwa hiyo ndo kinga yangu pekee iliyobaki kama mwanaume huyo atataka kuzini na mimi usiku huo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi tuliondoka na kwenda sehemu…
  • MY DIARY (33)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TATUTULIPOISHIA...Nilikuwa nachanganya staili za kijamaika na hizi za kwetu, sikuacha pia zile za Nigeria hapo nikapata vitu vyangu vya tofauti kabisa. Basi baada ya kujihakikishia kuwa nipofiti kwa mastahili yangu hayo nilisubiri siku ya shindano ifike nikafanye yangu. Siku ya shindano ilifika na mimi nilikuwa miongoni mwa washiriki walioingia tatu bora.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (32)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA MBILITULIPOISHIA...Lakini kuchepuka kwangu na kuingia mgombani haikumaanisha kuwa sheria ingeniacha hivi hivi.Ilifika mahali ikabidi nizime gari na kutulia tulii kusikilizia nini kitafuata.Tayari nilikuwa nimezungukwa na mapolisi ambao walikuwa wakinifuatilia kwa kutumia pikipiki.Kwa bahati nzuri dereva wa lile gari na yeye alishafika hapo na alishawaambia polisi kuwa mimi naugua ukichaa na nilifufuka kutoka mochwari.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA…
  • MY DIARY (31)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA MOJATULIPOISHIA...“marehemu pia alinieleza kuwa ana miliki duka la vitu vya urembo wa kike ambalo pia Leah analisimamia ila hilo apewe mdogo wake Marry ambaye yupo hapa. Mama mdogo huyo mara baada ya kuyasema hayo alikaa zake chini. Baba mdogo ambaye hakurizika na maelezo hayo alisimama na kusema “kwa hiyo kama marehemu alijua kuwa atakufa hivi karibuni kwani nini hakufuata taratibu za kisheria za kuandika wosia na kurithisha mali.IKIWA UNASOMA…
  • MY DIARY (30)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINITULIPOISHIA...Baada ya hapo Nnilimwomba mama mdogo ajikaze na kuwatarifu ndugu wengine habari hizo za msiba.Tulisaidiana hivyo hivyo maana sio siri kila mmoja alikuwa na uchungu sana kutokana na mazingira ya kifo hicho. Habari zilizidi kusambaa kwa kasi na majirani walianza kukusanyika hapo kwa mama mdogo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Msiba ni msiba tu na ukitaka kujua binadamu…
  • MY DIARY (29)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA TISATULIPOISHIA...Hapo sasa nikazidi kuchanganyikiwa ikabidi nimuulize mama huyo alikuwa akifanyia shughuli zake za kujipatia kipato sehemu gani.? Yule dada akanambia kuwa anafanyia soko la ndizi huko Korongoni. Sikuwa na jinsi nilimuomba anipeleke lakini na yeye alisita sita kwa madai kuwa alikuwa na kazi nyingi za kufanya na bado anatakiwa ampeleke mtoto shule.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (28)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA NANETULIPOISHIA...Sisi tumesomea mambo haya bhana waliendela kuzungumza wale walinzi huku wakishuka ngazi kwa polepole. Hapo na mimi nikawa nimejifunza kitu kuwa kumbe unaweza kuingia na mtu guest akakuzuru kisha akaondoka zake.Sasa sijui kwenye zile guest zetu za uswahilini kama wanalijua hili.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi nilala japo usingizi ulikuwa hautaki kuja kwa…
  • MY DIARY (27)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA SABATULIPOISHIA...Alinamba eti hayo ya mimi kuolewa tuyaeke pembeni na kwa nini siku hiyo nisilale Moshi tukumbushie enzi zetu. Mwalimu John aliendelea kusema kuwa amenimiss sana na anomba nisahu yaliyopita na turudie yale maisha yetu ya zamani.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilijifanya simwelewi lakini ukweli ni kwamba nyota ya mwanaume huyu ilikuwa ni kali sana zaidi yangu na…

RANIA (40)

JINA: RANIA
SEHEMU YA AROBAINI
ILIPOISHIA...
Daah..Dom aliumia sana moyoni mwake...machozi yalimtoka kwa kasi.

Utapona tu Rania.. Naamini utaweza kusema tena.. Alisema Dom huku amemuweka Rania kifuani kwake machozi yakimtoka.

SASA ENDELEA..
Dom umeshamwona Rania?.. Nasikia ameamka..aliuliza Fasha kwa pupa lakini Dom alionekana mnyonge sana.

Nini tatizo kwani?..aliuliza Fasha baada ya kuona Dom amepoa.

Rania ni kweli amezinduka..lakini.. Alisema Dom kisha akasita.

Nini kwani?... Mbona umesita?..aliuliza Fasha.

Hawezi kuongea.. Alisema Dom.

Fasha alishangaa sana na kuhuzunika..haraka alikwenda alikokua Rania ili ajihakikishie.

Rania... Aliita Fasha kwa sauti ya upole.

Rania alitabasamu tu na kuitika kwa kutikisa kichwa.

Fasha aliumia sana...alijua yote Haya yamempata Rania kwa ajili ya nchi.. Kwa upendo alisogea ba kumkumbatia huku akimpa maneno ya faraja.

Upande wa Rai pia hali haikua nzuri sana..alikua mzima sehemu zingine lakini hakuweza kutembea.

Yalikua maumivu ndani ya ile familia.. Dom na Fasha walikua mbele ya mama yao wakimwangalia kwa huruma machozi yakimtoka kila mmoja wao.mama yao alijitahidi kuwafariji akiwaambia hatachukua muda mrefu atapona.

Muda huo Mars alikua ameshafika Tharia lakini hakuweza kuja ikulu kumwona Fasha maana aliogopa kwakua aliwahi kua msaliti akishirikiana na Suya. Kwahiyo alikua amekaa mtaani yeye na vijakazi wake wote kwa muda.

Baada ya masaa machache kupita habiri alikua na watoto wake akiwaeleza mambo yalivyokua kipindi kirefu kilichopita.

Aliwaeleza jinsi kundi lao la wafanyabiashara lilivyoangamia kwa ajali..watu watatu tu walipona akiwemo yeye.baada ya yeye kupona mbele alikutana na muuaji alietumwa na Suya kumuua ili asije akavujisha habari za Fasha maana alikua alishaanza kujua kuhusu Fasha.

Hata hivyo muuaji yule alimhurumi na kumwacha aende zake ika asirudi Tharia asije akauawa na Suya.

Sasa baba wewe ulijuaje yaliyokua yanaendelea huku?.. Aliuliza Fasha.

Nilikua na kijakazi wangu ambae ni mtumishi wa Suya kwahyo aliniambia yote.. Hata hivyo kwa sasa hayuko duniani...alisema habiri

Upande wa Rai na Dom wao hawakutafutwa wauawe maana Suya alizania kua wako nchi ya mbali.

Upande wa Suya na watu wake walikua wanajipanga kuvamia mara ya mwisho kabisa ili waone huenda wakashinda maana walizania kua mfalme wa Tharia na lazi wameshabweteka kutokana na ushindi walioupata.

Kwa upande wa Suya mwenyewe. Yeye kama yeye hakuona umuhimu wowote wa ile vita..siku zote lengo lake kubwa ni kupata kiti cha kifalme ili kukamikisha nguvu zake ili awapige maadui Zake wa baseki..sasa kwa muda huo suya hakua na nguvu zake za miujiza kwahiyo vita haikua na maana kwake ila hata hivyo alishiriki tu kuwaunga mkono Faritha na watu wake.

Habiri na wanae wakiwa wanaongea mara ilikuja taarifa kua watu wa Suya na Faritha wamefanya mashambulizi tena.

Hapo jeshi zima la Tharia na lazi yaliamka..Fasha na Dom nao waliondoka kwenda vitani pia..wanajeshi walikua wameshapungua hivyo hata wananchi wa kawaida wanaojiweza walihamasishwa kusaidia nchi.

Katika wanajeshi hao wa kujitolea..Namadi pia alikua miongoni mwao.

Vita ya mwisho kabisa ilipiganwa..jeshi la upande wa Suya likikua dogo kuliko upande wa wafalme. Licha ya hivyo vita ilikua nzito bado.

Katika kupigana.. Fasha alikutana na Suya ana kwa ana.

Suya alionekana anapata udhaifu juu ya kumshambulia Fasha.. Fasha alihofia.. Alizani ni mbinu tu ya Suya ili ampumbaze.

Walipigana kwa muda mrefu sana.. Suya alikua vizuri sana kwenye haya mambo licha ya kua Fasha alikua zaidi yake.

Umeshafanya mengi mabaya sana Suya.. Husitahili kushinda hii vita..alisema Fasha.

Kwanini vitani ni mahali patakatifu?..kwamba waliofanya mabaya hawapati ushindi?.. Aliuliza Suya.

Hakuna marefu yasiyo na ncha..mwisho wako umefika sasa..alisema Fasha.

Acha kuongea sana vitani.. Utapoteza nguvu na umakini wa kupigana na utampa nafasi adui.. Alisema Suya.

Kwahiyo unanipa mbinu?..Aliuliza Fasha.

Mganga alipoona kua Fasha amevaana na Suya aliamua kurusha mkuki kumuua Fasha.Fasha hakuona maana alikua amemtega mgongo Dasu.

Suya aliuona mkuki ule ukija kwa kasi.. Fasha akiwa haelewi lolote lile alivutwa na Suya kwa kasi na kugeuzwa.

Ile anatahamaki kuona nini kinaendelea Suya tayari alikua chini alitokwa na damu nyingi sana maeneo ambayo mkuki ule ulimpata.

Fasha aliishiwa nguvu na kujikuta yupo chini amepiga magoti.

Suya alikua akimwangalia Fasha huku akitabasam kwa mbali.. Fasha alibaki ametumbua macho ya mshangao na mshtuko.hakuamini kama suya ndo wakujitoa uhai kwa ajili yake.

Suya akiwa hali mbaya alianza kuongea.

Hata mimi suya niliwahi kua Mtu asie na hatia kabla dunia haijanibadilisha na kunifanya Suya huyu aliepo hapa..niliwahi kua Mtu mwema eti..

Fasha alishindwa kujua alie au afurahi.

Fasha..naweza nikawa nimekudanganya mengi maishani mwako..lakini upendo wangu kwa nchi hii ya Tharia ulikua wa kweli..pia upendo wangu kwako ulikua wa Kweli.. Nilipanga kua ukipata kiti cha ufalme nikuue lakini sina uhakika hadi leo kama ningeweza...alisema suya kwa taabu.

Ma..m..a...aliita Fasha kwa kigugumizi.

Baseki.. Nchi ya Baseki iko mbioni kuiangamiza Tharia baada ya vita hii...chukua hii...alisema Suya huku akitoa kitu kama kisu ila kinang'aa sana na kumpa Fasha.

Ukifika ikulu kivunje hiki..matunda yake utayaona tu... Tharia iwe salama mikononi mwako Fasha.. Alisema Suya akiwa ana hali mbaya sana.

Mama.....aliita Fasha huku machozi yakimlengalenga.

Muda huo Dom alifika pale... Suya kwa taabu alimwangalia Dom halafu akasema.

Kaka yako anaonekana ni mtu mwema..Tharia itakua salama mikononi mwenu..alisema Suya. Dom alishangaa... Hakujua kama suya tayari ameshmjua vyema.

Dada...dadaaa..kwanini lakini?.. Aliia Dasu akiwa mbele ya Suya.

Nisamehe mdogo wangu.. Hajawahi pata faida ya kufuata amri zangu.. Nimeharibu maisha yako..nisamehe sana.. Dada yako nakupenda sana Dasu... Alisema Suya.

Dasu alilia sana

Taratibu suya alianza kuaga dunia hii...

Nitakukumbuka sana mwanangu huku ninakoenda...nisamehe sana Fasha.. Nisamehe sana mdogo wangu dasu kwa kukuacha mwenyewe..

Hayo yalikua maneno ya mwisho ya Suya na akapoteza maisha muda huohuo.

Dasu aliinuka kwa hasira kutaka kummaliza Fasha lakini Dom alimzuia.

Baada ya kushindwa vita ile Faritha aliamua kujiua..wapambe wake pia walifuata nyayo.

Dasu alikimbia..yeye hakufa vitani.. Kiapo chake kilikua ni lazima amuue Fasha.

Fasha akiwa njiani yeye na Dom wakielekea kambini kwa ajili ya maandalizi ya kuondoka mara ulitupwa mkuki tena...

Fasha alivutwa kichakani na mtu asie mjua...Dasu alipoona kua Fasha hajafa aliamua kujitokeza kumshambulia ana kwa ana..alikutana na moto mkali wa Dom na alikufa ndani ya dakika chache.

Fasha alipogeuka kuona nani amemvuta alikuta ni mkewe Mars.

Mars!!.. Aliita Fasha kwa mshangao.

Haraka twende.. Hapa huenda sio salama kwako... Alisema Mars huku akimwonesha Fasha Farasi ila Fasha alikataa maana alihofia kumwacha Dom peke yake.

Baadae Mars alikutana na baba yake na kumwomba msamaha... Baba yake alimsamehe na kumtakia maisha mema na Fasha kama ikiwezekana..Mfalme wa Lazi alikuja na kumwona Rania katika hali yake mbaya akahuzunika sana.. Alimwombea apone haraka kisha akaenda lazi kwa amani.
*****

Siku mbili baadae Fasha alifika ikulu na kukivuja kile kijiti kama kisu alichopewa na Suya.

Kile kijiti kilipovunjika kulitokea vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Baseki.. Walipigaba sana na kudhoofisha jeshi lao kitendo kilichorahisisha Tharia kuisambaratisha baadae.

Fasha alikua akikubuka maneno ya Suya "Acha kuongea sana vitani.. Utapoteza nguvu na umakini wa kupigana na utampa nafasi adui" ..alijikuta anatabasamu kwa huzuni.

Mwaka mmoja baadae matatizo yote yaliisha na kukawa na utulivu..wazazi wa Rania wakiwa na Namadi na Hanna na Lau walihamia ikulu.

Walifurahi kuhamia hapo maana waliweza kumwona Rania mara nyingi.

Mfalme wa Tharia siku moja aliondoka na Fasha kwenda kuzuru kaburi la Suya

Sijui nilie au nisilie..ila yote kwa yote naweza kusema wewe ni shujaa wa Tharia.. Umeiokoa Tharia mkononi mwa Baseki Mara mbili..alisema Mfalme mbele ya kaburi la Suya.

Fasha bado unamchukia suya?.. Aliuliza Mfalme.

Simchukii..hata kidogo... Alisema Fasha.

Baada ya siku mfalme wa Tharia alimwambia viongozi wote wa Tharia kua Fasha si damu yake na akawatambulisha wazazi wake ambao ni Rai na habiri pamoja na kaka yake Dom.

Aliwaeleza yaliyotokea yote nyuma na kuomba radhi kwa kuwaficha..kila mtu alishngazwa na habari ile.

Hata hivyo haikumwondolea Fasha haki ya kua mtawala maana ni damu ya Mfalme halali wa Tharia.. Mfalme kelkuni.

Uchaguzi wa mrithi wa kiti cha ufalme ulifanyika na Dom akaonekana kua anafaa sana maana ni mkubwa kiumri kuliko Fasha.. Kila mtu alikubaliana hata Fasha mwenyewe aliridhika na uteuzi hio..

Lakini Dom wala hakukubali..alidai hajui mengi kuhusu utawala.. Aliomba sana kwa wazee wa baraza na mfalme ku Fasha ndie awe mrithi..maoni yake yalisikilizwa na baada ya mjadala mrefu Fasha alichaguliwa kua mrithi.

Miezi michache baadae mfalme alikufa kwa maradhi na Fasha akatawala

Bakanga mdogo wake Mfalme alikua hai muda wote huo.. Alitoroka punde tu vita ilipoanza.

Aliposikia Fasha anatawala alitokomea mbali na hakuwahi kurudi.

Miaka mitano ilipita bila Rania kuweza kuongea..Rai yeye alikua ameshapona.

Anatakiwa kuwa sehemu tulivu sana huku akitumia dawa hii...sehemu tulivu sana ambayo haina kelele za watu...alisema Rai.

Dom,Fasha Namadi na Hanna wote walikua hapo pamoja na Rania na Rai.

Inabidi mmoja hapa aondoke na Rania na kwenda nae huko patulivu...alisema Rai.

Mimi hapa... Alidakia Hanna.

Namadi alimwangalia jicho la kuibia Hanna.

Hapana nitaenda nae mimi..alisema Dom.

Walibishana hapona mwisho wa siku Dom akashinda..

Hanna ulikua unataka kumwacha mmeo sio..alisema Namadi wakiwa wawili.

Ulinioa lini we nae... Alisema hanna.

Kuanzia sasa... Nimeshakuoa...kwani hutaki?..alisema Namadi.

Hanna alitoa tabasamu la sitaki-nataka.

Kesho yake Dom na Rania walikua tayari kwa safari na walikua wakiagana na watu wao.

Ufalme mzima uliwatakia safari njema.

Hakikisheni mmerudi salama...alisema Fasha.

Bila shaka tutarudi...alisema Dom.

Rania na Dom waliondoka huku Fasha akiwasindikiza kwa macho hadi wakaishia mbali.

Dom na Rania walielekea eneo moja mlimani wakiwa wawili tu..walikaa huko kwa muda.

Dom alikua akijitahidi siku zote kumfurahisha Rania akiamini itasaidia kupona kwake kwa haraka zaidi.Rania alikua na furaha sana kua karibu na Dom ingawa hakuweza kuongea.. Aliishia kutabasamu tu.

Mara kwa mara familia ya Rania na ya Dom walikua wakija kuwatembelea huko walikokua na Fasha pia alikuja.

Unajua nilikua nimekukumbuka sana Fasha... Nilitamani kurudi ila niiogopa...alisema Mars alipokua anaongea na Fasha.

Sikuwahi kujua kama ushaingia moyoni mwangu,nilizani nipo hapa kimasrahi.nisamehe sana.hata kama sio leo..hata siku zijazo naomba ujitahidi unisamehe....alisema Mars.

Fasha alimshika Mars mkono kisha akasema:

Wala sijawahi kukuchukia.naomba tu uwe na amani.. Nilijua tu unadanganywa na ipo siku utarudi..alisema Fasha.

Nashukuru sana Mfalme wangu.. Alisema Mars.

Fasha alikua akipata wakati mgumu pale anapokumkumbuka Rania.. Aliumizwa sana na ukweli kua Rania hatakuja kua wake..ila alijikaza maana hakutaka kuleta sintofahamu kati yake na Dom.

Rania akiwa amekaa na Dom wanapunga upepo mara Dom alisikia kama Rania ameongea vile.. Alihisi ni fikra zake tu,akapotezea.

Dom...aliita Rania.

Dom aligeuka na kumtazama Rania kwa mshtuko kidogo.

Nimechoka kukaa nje.. Alisema Rania.

Dom alihisi ndoto.. Alilipuka kwa furaha akajikuta abamkumbatia Rania kwa nguvu huku machozi ya furaha yakimtoka.

Haraka alimbeba na kumrudishs ndani ilihali Rania alikua anaweza kutembea vizuri tu.

Rania... Ongea tena... Alisema Dom.

Sitaki kurudi kule ikulu.. Tuishi tu huku sisi..alisema Rania.

Dom alifurahi sana Rania kupona.. Alifurahi mno.

Sasa furaha yangu umekuja.. Nimesubiria upone kwa muda mrefu.. Rania asante kwa kupona..alisema Dom.

Rania alitabasam tu.

Muda mfupi baadae walikuja ndugu kuwaona...familia nzima ya Rania na ya Dom walikuja.

Ilikua ni furaha kubwa waliyokua hawajaitegemea kwa Rania kupona.

Basi sasa twende ikulu... Alisema Rai kwa pupa.

Nisamehe sana mama..sihitaji kurudi huko.. Naomba mnipe nafasi niishi huku na Dom... Alisema Rania.

Wote waliangaliana asipatikane wa kutoa ruhusa hiyo.

Yote ni sawa tu..ilimradi muwe na Furaha... Alisema Fasha.Rania alifurahi waziwazi.

Baade Fasha na Dom walikua wakiongea.

Nakutakia furaha ukiwa hapa na Rania....hongera kwa kunyakua hisia za Rania..anatamani ningekua mimi vile..Alisema Fasha huku alimpigapifa Dom kwenye bega.

Haha..we nae.alisema Dom kwa masihara.

Na wewe uwe na furaha na malikia Mars.. Uiongoze vyema nchi... Alisema Dom.

Walikumbatiana kwa muda mrefu sana..kila mmoja alitamani kuendelea kua na mwenzake.baada ya hapo Fasha alikwenda kumuaga Rania.

Rania.. Nafurahi umepona..nafurahi sana...alisema Fasha.

Na mimi ninafurahi kwakua wewe unafuraha..alisema Rania.

Nimeshahisi kilichokufanya ukatalie huku... Alisema Fasha.

Nini?...aliuliza Rania.

Umenikwepa...alisema Fasha.

Kidoogo..ni kweli ila sio sana.. Alisema Rania.

Walicheka wote na wakaagana.

Familia zote ziliwaaga Rania na Dom na kuwatakia maisha mema..

Dom na Rania walibakia wenyewe.

Mmh..midomo yako mbona imekauka...inaonesha utakua na mimba baada ya siku mbili wewe...alisema Dom huku akimchunguza chunguza Rania huku akimsogelea

Nini?? mimba??..aliongea Rania huku akirudi nyuma nyuma.

Dom alimvuta na kumkumbatia kwa nguvu... Rania pia alitoa ushirikiano huku akiwa na tabasamu la kutosha.

*********MWISHO*********
NAWASHUKURU SANA KWA USHIRIKIANO WENU 🙏🙏🙏🙏

TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
3 Rania Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni