Notifications
  • THE NIGHTMARE (3)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA TATUILIPOISHIA...Akiwa hewani akikata mawingu kurudi Tanzania, kichwa chake kilikua na mawazo mengi sana juu ya mume wake. Aliikumbuka siku waliyofunga ndoa.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Pia alijua kwanini mume wake alipendelea kufanya kazi uingereza na yeye kumfungulia ofisi huku huku Tanzania. Hakujua kuwa kazi anayoifanya mumewe ni ile ya kutembea na tajiri mkubwa…
  • THE NIGHTMARE (2)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA PILIILIPOISHIA...Khalidi alishangaa kuitwa na mtu asiyemfahamu. Alitoka na kwenda kumuangalia huyo mtu maana kiukweli hakua na ndugu aishie hapa Dar hata mmoja anayemfahamu..IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Alipigwa na butwaa baada ya kumuona Sabra pale.“ahsante mungu.” Aliongea Khalidi baada ya kumuona tu yule binti pale.“pole sasa kaka yangu, nisamahe mie.” Aliongea Sabra kwa…
  • THE NIGHTMARE (1)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA KWANZANi kipindi cha mvua za masika. Upepo mkali, na mvua kubwa iliendelea kunyesha kwa kasi kila kona ya nchi ya Tanzania.Ipo mikoa iliyofurahia mvua hizo kwa kuwa walikua wanaisubiria kwa hamu kwa ajili ya kilimo. Lakini ipo mikoa iliyokua inapata shida kwa uharabifu wa mazingira na mengineyo mengi.Moja ya miko hiyo ni Dar-es-salaam. Watu wanaoishi katika mkoa huo walichukia mvua mfululizo kutokana na sababu mbalimbali. Biashara nyingi…
  • MY DIARY (50)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA HAMSINITULIPOISHIA...Nilimnongo’oneza kuwa atumie kinga ili nisimwambukize ukimwi akanijibu kwa sauti ya mahaba nisiwe na hofu yeye yupo tayari kufa kwa ajili ya penzi langu hivyo hawezi kutumia kinga kwa mke wake aliyemoa tena siku muhimu kama hiyo.Sikutaka kumbishia yeye ndo muaamuzi wa mwisho kuhusu afya yake hivyo nilimuacha aendelee kufanya yake.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Kumbe na…
  • MY DIARY (49)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA TISATULIPOISHIA...Baada ya maneno ya kusilimu ambayo waliambiwa wayatamke kiongozi huyo alisema neno ya mwisho kabla hajashuka.” Kila alie na akili timamu, mwenye busara naa anaetaka haki, na kusimama pamoja na haki, basi akiangalia dunia ilivyo na jinsi inavyokwenda basi lazima kutakuwa na nguvu kuuu nayo ni mwenyezi mungu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Kuna vitu vingi sana…
  • MY DIARY (48)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA NANETULIPOISHIA...Familia yangu haikukubali kabisa mimi kuolewa na rangi nyeusi hivyo walinitenga na kusema hawanitambui kuwa mimi ni ndugu yao.Lakini kutokana na mapenzi mazito niliyokuwa nayo kwa baba yake na Leah nilijikuta nipo tayari kwa lolote hivyo nikahama na kwenda kuishi Tanzania.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Katika miaka hiyo tuliyokaa nilibahatika kupata mtoto huyu…
  • MY DIARY (47)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA SABATULIPOISHIA...Lakini ilifikia mahali ndoto hiyo inanijia hata mchana nikiwa nimekaa mahali tulivu.Ilikuwa inanipa taswira nzuri ya sehemu ambayo madini yalikuwepo.Basi nilianza mikakati ya kulitafuta eneo hilo na hiyo ni mara baada ya ushauri wa mpenzi wangu Candy hapo akimaaanisha yule dada aliyekuwa naye pale jukwaaani.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Candy alinisihii sana…
  • MY DIARY (46)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA SITATULIPOISHIA...Nilikuwa kama niliyepigwa butwaa nisiamini nilichokuwa nakiona mbele yangu. Oooooh my God hold me on yalikuwa ni maneno yaliyonitoka kutoka kwenye uvungu wa moyo wangu mara baada ya kumuona James kwa uzuri zaidi na kuamini kuwa yule kweli alikuwa ni kaka yangu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilishindwa kuelewa nini kimetokea mpaka yeye kurudi katika hali yake ya…
  • MY DIARY (45)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA TANOTULIPOISHIA...Ndio niliona hipo haja ya kuokoka na kuishi maisha ya utakatifu kwa maana nishaishi maisha yote ya kuwa mbali na mungu. Nakumbuka nilipokuwa mdogo kipindi hicho naujua mlango wa kanisani tuisahawahi kufundishwa kuwa mtetezi wa kweli wa maisha ya mwanadamu ni Mungu.Na siku zote alaaniwe mtu yule amtegemeaye mwanadamu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Sio kazi ya…
  • MY DIARY (44)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA NNETULIPOISHIA...Yani alianza kutaka uhusiano na mimi tena uhusinao wa mapenzi.Mda wote alikuwa akiniganda kama luba.Na mimi nilikuwa mjanja sana maana nilijifanya sinywi pombe wala kuvuta sigara.Pia baada ya kugundua kuwa wahusika wengine walikuwa wanajiachia niliamua kujifanya mshauri wa mapenzi na mahusiano.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilikuwa nawasshauri sana mshiriki wa…

AISEE KUMBE RAHA (18)

Mwandishi: Pablo

SEHEMU YA KUMI NA NANE
"Haina haja hata ya kuwakaribisha licha ya kuwa nimewaita sasa basi twende moja kwa moja katika lengo la kukuita kuwa kwanza mwanao tumeshamfuta hapa chuoni."
"Whaaaaaaaaaaaat.!!!!

SASA ENDELEA...
Baba akajikuta akipandwa na hasira za ghafla na kupiga ngumi ile meza iliyokuwepo pale ambapo nyuma yake alikuwepo mkuu wa chuo na Mbele yake tulikuwepo sisi.Kupiga meza ile kwa hasira ilikuwa ikiashiri kutoamini kile ambacho mkuu wa chuo alipomwambia kuwa nimefutwa jina chuoni ikiashiria kwamba nilikuwa nimefukuzwa.

"Unasemaje mkuu wa chuo Mwanangu nini."Baba akaongezea huku akimuangalia yule mkuu ambaye kidogo alianza kuonyesha hali ya uoga fulani baada ya baba kupigwa ile meza kwa hasira.Wakati huo mimi nilikuwa kimya kijasho chembamba kikianza kunitoka kwa sababu nilishaanza kuhisi kuwa kosa la kufukuzwa chuo lilikuwa ni zile picha ambazo nilizopigwa nikiwa mtupu na kutangazwa katika mitandao ya kijamii kuwa mimi ni shoga na nahitaji Mtu.
"Mzeee tulia ukileta jazba zako hapo kumbuka kuna maaskari tutakusaga kituoni bure kwani wewe ujui Mwanao alichofanya au kilichotokea Maana chuo hiki kizima kinajua alichofanya Mwanao na si chuo kinakaribia sasa tanzania nzima au dar-es-salaam nzima hii."Mkuu wa chuo akaongea kwa jiamini na kusababisha mpaka baba kumuelewa alichokuwa anakimaanisha na kusababisha Baba atulie Maana tayari alikuwa ameshasimama huku viganja vyake viwili alikuwa ameshavikunja na kutengeneza Ngumi nzito ambayo kama kweli ndio anampiga mtu basi lazima angesababisha mauwaji.Baada ya Maneno yale ya mkuu wa chuo baba akarudi na kuketi katika kiti chake kisha akanigeukia mimi nakunikata jicho kali sana huku akihema kwa shauku kubwa ya kutaka kujua kilichosababisha mpaka mwanae nimefutwa chuo.

"Haya nambie mkuu mwanangu amefanya kitu gani mpaka mumfukuze chuo maana nimelipa milioni moja na nusu nimeipatia shida sana licha ya kuwa pesa ndogo lakini kutokana na hiyo ningeongezea hata kwenye mtaji wangu pumbavu."Baba akaongea tena kwa jazba na kusababisha yule mkuu wa chuo amuangalia kwa uoga uoga kisha taratibu mkuu wa chuo ambaye aliulizwa swali na baba akazama mfukoni mwake na kutoa simu yake aina ya tecno p5 ambayo nilikuwa naijua kutokana na umbo lake kisha akaanza kubonyeza bonyeza na kusababisha presha ianze kupanda na kushuka na kujikuta nikihaha pale hadi kumshangaza baba ambaye akaacha kumuangalia yule mkuu wa chuo na kuniangalia mimi kwa hasira ya juu.
"Enhee unatoka majasho eeee leo lazima nikutafune Mwanahizaya wewe na wewe mkuu tunapotezeana muda pumbavu zako nambie Mwanangu amefanya nini Maana nakuona unabonyeza bonyeza simu nitakuzingua ujue."Presha ikazidi kumpanda Baba ambaye akajikuta akimkalipia tena yule mkuu wa chuo ambaye baada ya kukalipiwa nikamuona akibonyeza simu yake haraka haraka vile akionyesha kama Mtu ambaye alikuwa akitafuta kitu fulani vile.Baada ya dakika kama moja kupita kwa Macho yangu nikashuhudia mkuu wa chuo akimpa Baba simu yake ya mkononi ile tecno ambayo mara ya kwanza Baba alisita kuipokea.

"Mimi simu ya nini.??"
"Mzee mtata kweli pokea simu uangalie utumbo wa Mwanao." Baba akaipokea ile simu na kuangalia kioo cha ile simu ambayo ilikuwa inawaka waka tu na kujikuta akiganda Baada ya kuangalia kile kitu ambacho hakikutegema kabisa kikiona katika macho yake.
"Mzee wewe ukiona umemaliza kuangalia ya kwanza kibonyeze tu kioo itakuja picha Nyingine." Mkuu wa shule akaongezea Na Baba akafanya kama alivyoambiwa huku mdomo wake ukiwa wazi kwa mshangao.katika hali ya kutoamini baba akazama mfukoni na kutoa kitambaa na miwani yake kisha akajifuta machoni na kufuta ile miwani nakuangalia zile picha ambazo mimi sikuziangalia pale lakini nilikuwa nishagundua kuwa zilikuwa ni zile picha ambazo alinipiga suzan.
"Weee huyu nani mbwa wewe." Ghafla baba akanigeukia na kunionyesha picha ambayo hata mimi niliishangaa kwa sababu ilikuwa picha ambayo ilikuwa imeeditiwa na kuongezewa maneno.
"Jamani mimi shoga nina hamu kweli kama unajiweza nitafute kwa Namba."yalikuwa ni maneno yalioandikwa katika ile picha nakuambatanishwa na namba yangu ya simu kabisa hali ambayo ilisababisha nitoe macho.

"B.aa...b.aa s...io...........Paaaaaaaaaaaaaaaaa" Nikiwa nasusua kujibu swali ambalo baba aliniuliza Ghafla kofi zito la uso likatua barabara katika uso wangu kutoka kwa Baba nakusababisha niachie ukelele wa nguvu ambao hakusaidia chochote.
"Mkuu ahsante naomba hizo picha nirushie katika namba yangu uliyonipigia maana nimejiunga whatsapp sawaaa."Baba akamwambia mkuu wa chuo ambaye alibaki kimya akimuangalia Baba alionekana kuchanganyikiwa kwa hali ambayo alikuwa kama ukimuangalia Macho yake yalibadilika kabisa na kuwa mekundu kama mtu aliyekuwa amevuta sigara.
"Wee Mbwa leo nakuua." Baba akaniambiaa kisha akaniongeza kofi zito ambalo nililikwepa lakini likanipata maeneo ya kichwa Haraka baba akanisogelea na kunishika mkono kisha akaninyanyua kwa kutumia Nguvu zake zote na mimi nikanyanyuka na Moja kwa moja tukaanza kutoka huku Baba akiwa amenishika Mkono.
"Mzee Barua hii."
"Fala wewe mkuu wa chuo gani boya wewe barua ya nini mimi kachambie chooni."Baba akamjibu kwa hasira mkuu wa chuo ambaye hakuwa na la kuongeza akabaki kimya tu anatusindika kwa Macho.

"Shogaaa huyoo!!!,shogaaaa!!!!!,shogaaaa huyo sio riziki huyo."Yalikuwa ni maneno yaliyopenya Barabara katika masikio yangu Baada ya kutoka katika Chumba cha mkuu wa chuo Ambapo ile tunatoka tu Mimi na Baba tukakumbana na wanachuo wenzangua ambao nilikuwa nasoma nao Katika darasa moja.Lakini Hali iliyonichanganya na kunishangaza na kunihuzunisha ni ile Baada ya kutoka na Wale wanachuo wenzangu kuniambia Maneno yale ambayo yaliniumiza mimi na Baba ambaye baada ya kusikia zile huku akiwa amenishika mkono akaniachia mtama mzito ambao ulinipeleka chini na kujikuta nikiangukia Mbavu na kusababisha nianze kulalamika lakini Baba akujali akaninyanyua kama mwizi na kuanza kwenda na Mimi na kusababisha wanachuo wengi kuniangalia Huku wengine wakitoa simu zao nakuanza kurekodi tukio lile la kupelekwa msobe msobe na Baba.

"Eeee Mungu Nimefanya nini mie Mbona nadhalilika mimi."Nilijikuta nikilalamika mwenyewe tena kwa kusema kwa nguvu Baada ya kuingia katika lile gari la Baba ambaye maneno yangu wala hakuyajibu au kuniangalia Machoni yeye haraka akaanza kuendelesha gari kwa kasi ya ajabu hadi kuniogopesha mimi na kujikuta nikitaka kumuambia baba apunguze mwendo lakini Mdomo wangu ukawa mzito kumuambia Maana nilikuwa katika wakati ambao wala sikujua kama nitakuwa mzima.Safari yetu Mara ya kwanza ikagonga katika moja ya duka ambapo baba akashuka na kufunga gari kisha akaenda pale dukani ambapo mimi nilikuwa namshuhudia kupitia kioo tu cha gari kisha akageuka na kurudi kwenye gari huku mkononi akiwa na chupa mbili za pombe kali aina ya konyagi.Kama kawaida yake akafungua Mlango wa gari nakukaa pale kwa dereva kisha akang'oa gari na kuanza kuendesha kwa kasi kuwahi nyumbani huku mkono mmoja akihimili usukani na mwingine akiwa anagugumia konyagi mdomoni mwake.Sikuwa na la kusema kwa sababu ujanja wangu wote ulikuwa mfukoni kwa wakati ule ambao bado niliendelea kutetemeka kama paka aliyemwagiwa Maji majasho yalikuwa yakinitoka Moyo ulikuwa unanidunda kama saa mbovu.
"Eeee Mungu nisaidie."Nikajikuta nikimuomba Mungu aniokea katika janga lile baada ya macho yangu kushuhudia kuwa tulikuwa tumeshafika Nyumbani na Baba akafunga breki na kupaki gari lile sehemu ambayo Mara nyingi alikuwa anapakigi kisha akaifungua konyagi yake ya pili akaanywa yote Haraka haraka safari akiwa ananiangalia Kwa hasira kali sana......

Hakika kweli hakuna marefu yasiyokuwa na ncha Mambo yote niliyofanya ya kijinga sasa leo Mungu alikuwa akinifundisha adabu.kuingia katika mikono ya baba niliona kabisa ndio ulikuwa mwisho wa jeuri zangu kutokana na baba yangu nilimjua vizuri mambo yake yakutojiuliza mara mbili katika sekta yake ya kuamua maamuzi.Baada ya kuinywa ile konyagi yake huku akiniangalia kwa hasira akafungua milango yote ya gari.
"Naomba utoke ueleke mwenyewe Mlangoni pale ole wako ukimbie mtoto wa juzi wewe unishindi lolote."Baba akaniambia kwa hali ya kujiamini na Mimi sikuwa na budi nikatoka taratibu hakika sikuwa na ujanja wowote maana kukimbia matatizo sio njia nzuri ya kuondoa matatizo ambayo yanakukabili kwa mwendo wa haraka haraka nikakimbilia Mlango wa ndani kisha nikaufungua nakutanguliza kumuomba mungu kisha nikazama mpaka sebuleni lakini nikakaribishwa na hali ya utofauti kabisa nikakuta kilio kikubwa pale sebuleni na nilipoangalia vizuri nani aliyekuwa akilia vile hakuwa si mwingine bali ni Mama ambaye alikuwa amejiinamia huku akilia kwa nguvu na kuniogopesha sana.Akili ikaniruka haraka nikamsogelea Mama mpaka pale nakumshika.
"Mama kuna tatizo gani mama angu mama mbona unalia mama kuna nini.??"Nikajikuta nikimwambia mama kiunyonge nakusahau yote yale ya mimi na baba ambaye alishuhudia picha zangu nikiwa mtupu na akili yote ikahamia kwa mama ambaye alikuwa akilia kama kulikuwa na msiba.
"Tokaaa hapa mwanaharamu mkubwa hivi wewe una akili kweli wewe yani kwanini unaiaibisha famili yetu kwa nini sasa ndugu wote wananitumia mimi picha zako za utupu ukijitangaza kabisa kuwa wewe ni shoga kwani umekosa nini wewe hapa mpaka ukaamua vile umekosa nini umekosa nini au nikuue nikuue."Yalikuwa ni maneno ya mama huku akilia na mikono yake ikiwa shigoni mwangu akinikaba huku akiniambia maneno yale yaliorudisha sekeseke zima la nyuma.Machozi yakaanza kunitiririka baada ya kugundua kuwa hadi mama naye alirushia vile picha na alizishuhudia hakika nguvu zikaniisha kabisa sikuwa na la kuongea nikabaki kumuangalia mama ambaye baada ya kuniona mimi nimetulia akaacha kunikaba na kubaki akihema huku akiniangalia kwa hasira kali sana.Ghafla nikasikia mlango ukifungulia na baba akaingia pale sebuleni uso wake ukiwa umezidi kuwa na hasira hakika ilikuwa ni majanga zaidi ya majanga.

"Piga magoti bwege wewe."Baba alipofika akanirushia teke zito lililotua barabara tumboni nakusababisha maumivu ambayo yakapelekea nijishike nakutii amri yake ya kuniambia nipige magoti.
"Hivi wewe umekosa nini mpaka kwenda kujitangaza wewe shoga na kujipiga na picha kabisa na ukichelewa kunijibu ninayokuuliza basi nakushushia kipigo mpaka nakuua."Baba akaniambia nakuniachia na kofi zito la mgongo kisha akarudi pale kwenye kochi na kukaa karibu na mama.
"Hee kumbe na wewe mume wangu usharushia utumbo wake mama hapa hatuna mtoto nyie uwiiii."mama akasema kwa mshangao baada ya kugundua kuwa na baba naye anajua lile sekeke ambalo hakika wala sikutegemea katika maisha yangu kuwa yangekuja kunitokea mimi.
"Mke wangu wee nyamaza weee jibu swali haraka pablo maana nataka kwanza nijue michezo ile umeanza lini kabla sijatumia mbinu zangu za kijeshi nikuue."Baba akaniuliza tena na alipoona nimechelewa kujibu akanyanyuka na kuninyanyua kama mzigo na kunikunja maeneo ya shingoni kwa kutumia shati langu nililovaa akaninyanyua na haraka akaanza kunitandika ngumi kali za tumbo ambazo hakika ziliingia kweli kweli na kujikuta nikianza kugugumia kiume bila ya kutoa makelele hakuishia hapo baada ya kunitandika ngumi zile mbili akaongeza na kichwa kimoja cha kichwa ambacho kilisababisha nidondoke chini mzima mzima na kusababisha pale aliponipiga kichwa kuvimba na kuota nundu.hakika ile ilikuwa ni siku ambayo sitakuja kuisahau kwa sababu ndio siku ambayo nilimshuhudia mama yangu akikosa huruma kabisa ya kunitetea wakati makosa ambayo baba alikuwa akinishambulia mama anakuaga mstari wa mbele kunitetea lakini siku ile alikuwa kimya kama sio yeye naye alikuwa na hasira kama baba vile.

"Haya tunataka jibu kwanini umefanya vile na michezo ile umeanza lini wewe mimi nikajua nimepata dume la mbegu kumbe hakika Mungu akupi vyote yani."baba akaniuliza swali tena huku
Akiongeza msisitizo mkubwa na mimi nikanyanyuka na kukaa sawa huku nikimuangalia Mama na baba ambao walikuwa wakiniangalia mimi kwa hasira kali.
"Baba yangu na mama yangu hakika nimewakosea sana na pia nakutunguliza msamaha kwa kile ambacho kimetokea Kumbukeni kuwa anayefanya kosa anastahili kusamehewa na mimi nimefanya kosa nahitajika kusamehe ila kiukweli kabisa mimi sio shoga kama maelezo ya kwenye picha zile picha nimepigwa na msichana ambaye namfahamu kabisa msichana ambaye nililala naye kimapenzi ndio akanipiga zile picha wakati nimelala amua kunidharirisha vile Baada ya kuhisi kuwa mimi nimevujisha picha za rafiki yake ambaye hapa juzi kati nilikuja kuchukulia na mapolisi na kusingiziwa kesi hiyo ambayo baada ya kutopata ushahidi wa uhakika nikaachia na nilikuwepo na mama kituoni hapo."Maneno yale yalimshtua kidogo baba ambaye akaniangalia kwa umakini kisha akageuza macho kumuangalia Mama ambaye naye sura yake ya hasira ikageuka na kuwa ya wasiwasi na upole baada ya kusikia maneno yale na kumuangalia baba ambaye akamkata jicho mama.

"Mama pablo mbona mimi ukuniambia sakata hili la kukamatwa."
"M..ume wangu nilisahau na niliona kama kukwambia ningekusumbua huko safarini."Mama akamjibu baba ambaye hasira zake zikashuka taratibu na kuniangalia mimi.
"Sasa pablo kwanini mwanamke huyo mshenzi amekufanyia hivyo bila ya wewe kujijua.??"
"Ndio hivyo baba sikutegemea lakini akanipiga picha na yeye ndio amezisambaza baba."
"Tatizo hakuna ushahidi wa kutosha wa hilo tungeenda kumshtaki lakini mwanangu pablo umezidi sana mpaka inafikia hatua hiyo mwanangu na Mara kibao nilikuwa nakukanya hawa wanawake wa siku hizi sio sasa Aibu gani hii katika familia maana ndugu zote washajua aibu gani hii Mwanangu."Yalikuwa maneno ya mama ambaye aliongea kiunyonge na kusababisha Baba ainamishe kichwa chini na kujikuna huku akiwa anafikiria kitu na kubaki mimi nikiwaangalia kwa makini.
"Kiufupi nikiongea kama baba Mwanangu hii aibu hatuwezi kuivumilia na tunatakiwa kuiyepuka mapema Mwanangu maisha ni popote nikisema hivyo ujue namaanisha nini Mwanangu naamanisha kwamba unatakiwa uhamu dar-es-salaam na uendee kukaa morogoro kama miaka miwili ili vuguvugu liishe kabisa huko pia nitakutafutia Chuo."Maneno ya Baba yaliniacha nikiwa sina cha kusema nikajikuta nikibaki Namuangalia baba huku nikiwa siamini kama nimeweza kuwaelewesha baba na Mama bila ya kutumia Nguvu nyingi bila ya wao kunikazia sana.Na hakika sikuwa na La kuongea baada ya baba kuniambia nikaanze maisha mapya morogoro kwa sababu ya ile soo ya mimi kupigwa picha..............

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO



USIKOSE SEHEMU YA KUNI NA TISA

Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
4 Aisee Kumbe Raha Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni