MAMA MWENYE NYUMBA (49)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA AROBAINI NA NNE
Alitembea mpaka, kwenye kiuo cha daladala za kwenda kibaha, yani upande wa morogoro, akaingia kwenye gari (coster) la kwenda msata, akakaa kwenye siti yap eke yake, na kuliweka lile begi la mzee Mashaka chini ya sitiSASA ENDELEA...
Dakika kumi natano mbele alikuwa amesha fika mzani wa zamani, wa kibaha maili moja, akashuka baada ya kulipa nauli kwa kondakta, nakulitelekeza lile begi la mzee Mashaka, ilisha timia saa saba kamili za mchana, hapo Edgar akasogea pembeni kabisa ya barabara pana ya eneo lile, na kutulia macho akiwatazama polisi ambao walikuwa wame tanda pale wakikagua magari yenye makosa, Edgar aliwatazama wale polisi akijaribu kumchagua ambae angeweza kumsaidia kumtafutia usafiri wakumfikisha Songea, akiamini anaweza kupata atakama ni gari kubwa la mizigo, maana kwa bus mida hii ata kwabahati mbaya usingeweza kulipata, mabus ya Songea uwa yanapita kuanzia saa kumi nambili na nusu adi saa moja kasolo asubui, macho ya Edgar yalituwa kwa mmama mmoja polisi, alie onyesha kuwa na mtumima wa kuweza kuwa mama yake kabisa“Yule anaweza kunisaidia” aliwaza Edgar huku akitembea taratibbu kumfwata yule mama mtu mzima, “shikamoo mama,” alisalimia Edgar baada tu ya kumfikia yule mama” kabla hajaitikia yule mama akageuka kwanza, nakumtazama msalimiaji,” malahaba mwanangu vipi unashida” aliuliza yule mama kwa sauti ya upole, hapo Edgar akaanza kujieleza, kuwa yeye anaitaji usafiri wa kwenda Songea mana alikuwa anasoma chuo, amesha maliza mitihani, na amesha kabidhi chumba alichokuwa anakaa, kwasababu kodi ilisha kwisha, sasa ameona bola asafiri mchana hule, “ok mwanagu kakae bale kwenye benchi, tubahatishe” aliongea yule mama akimwonyesha Edgar kwenyebenchi moja pembeni ya barabara chini ya mti, “asante sana” alishukuru Edgar akienda kukaa kwenye bechi
Hapo sasa Edgar alishuhudia magari yakipita, na masaa yakienda aliona yule mamama akijaribu kuomba mala gari hili mala lile lakini yote haya kuwa na safari ya Songea, toka saa saba msaa tisa kasolo, huku mda wote akiwa ame jawa na hofu ya tukio alilo toka kuli fanya maana taswila za wale watekaji wake zilikuwa mbaya sana, aliwaacha wana fanana na mazombi, ndipo alipo shuhudia gari moja ndogo aina ya Toyota harrier likisi mama karibu na yule mama tena bila ata kusimamishwa, kika shushwa kioo cha upande wa habiria, pasipo kusikia sauti ya yule mama, lakini alimwona akiongea kwa kufurahi na vicheko vidogo vidogo, akionyesha kufahamiana na mmiliki wa gari ambae alikuuwa bado ajamwona, maongezi ya yule mama polisi na mwenye gari yali dumu kwa dakika tano, kisha akamwona yule mama akimwonyeshea ishara ya kumwita, hapo Edgar akusuburi aitwe mala mbili, maana hofu yake kubwa ilikuwa ni kulala dar, alipaona ni pachungu sana, aliinika haraka na begi lake na kukimbila kwenye lile gari
“Haya ingia muwai maana Songea ni mbali sana” aliongea yule mama HUKU Edgar akikfungua mlango wakati kati wa lile gari, “hapana ingia huku mbele, tena afadhari maana ningekuwa peke yangu mpaka Songea” Edgar alistuliwa nasauti tamu yakike tena ilipenya vizuri masikioni mwake, Edgar aka funga mla ngo alio ufungua na kufungua wa mbele, akaingia nndani ya gari nakufunga mlango, “asante mama” alishukuru Edgar huku gari likiondolewa, “funga mkanda anko” ile sautiya kike ili penya tena masikioni kwa Edgar, hapo akakumbuka kumtazama dereva wake, “mama yangu” alilopoka Edgar alihisi mapigo ya moyo wake yakisimama kwa sekunde chache, kutokana na uzuri wa mschana alie kaa pembeni yake, tena alionekana mrembo aswaaa, na mbaya zaidi Edgar alishusha macho kutazama jisi alivyokuwa amekaa kwenye kiti cha dreva na kusaba bisha msambwana uenee kwenye kiti chote, huku hips za wastani zilizo fichwa kwenye jinsi la brue lakubana, alilo vaa binti huyu zikionekana vyema
“Anko umenisikia?, funga mkanda” aliongea yule binti akionyesha kugundua kuwa abilia wake anamshangaa. maana yule mschana alimwona jinsi Edgar alivyo kudoa macho, kutazama majaliwa yake, ambayo kila wakati anashuhudia midume yenye uchu iki mkodolea macho, asa anapo pishana nao, lazima wageuze shingo zao kuangalia mgongo wake, lakini licha ya kumwona Edgar alivyo kodoa macho, ila aliona wazi kuwa kijana huyu ambae anakaribiana nae umri, akiwa na dalili za uoga wakuto jiamini, “ume ssema una enda Songea, kwani nikwenu huko?” aliuliza yule mwanamke huku Edgar akifnga mkanda wa kiti cha gari, (seat belt) “ndiyo ni nyumbani, huku nilikuwa nasoma” alijibu Edgar akitazama mbele kuangalia wanako elekea, alifanya hivyo kwa sababu mbili
Kwanza nikuepusha tamaa ya mwili wake maana kilicho mkuta ilikuwa sili yake, pili kwa mwonekano wa yule binti alijuwa hakuwa na uwezo wa kumchukuwa, maana licha ya kuwa mrembo kama Suzan, lakini kutokana na muonekano wake alionekana kamabinti mdogo, alafu mwenye uwezo mkubwa wakifedha, na matumizi mengi sana ya fedha, ukimtazama alivyo vaa kuanzia viatu vilivyoonekana vina samani kubwa sana, tishert na jinsi, pia shingoni alining’niza cheni ya dhahabu, na vidoleni ndiyo husiombe kasolo kkidole gumba tu vidole vingine vyote vili tawaliwa na pete za dhahabu tupu, hivyo akaona atajitesa bule nafsi yake bola atazame mbele, kuangalia maloli makubwa na ma bus toka morogoro yanavyo ingia mjini dar kwa mbwembwe
“Ok! ameniambia yule afande, hivi ulikuwa unasoma chuo gani?” aliuliza yule dada huku akikanyaga mafuta, nakulifanya Toyota Harrier lizidi kutimua mbio kuiacha kibaha, “likuwa nasoma chuo cha habari pale kibamba” alijibu Edgar, huku bado akiwa ametazama mbele, kukwepa asimtazame huyu dada, “ok! kwahiyo wewe ni msanii?” aliongea yule dada mwenye mwonekano kama watu flani hivi wa kaskazini, wanaitwa wa Iraq, kama sija kosea, huku akicheka na kmtazamakidogo Edgar ambae alikua ametazama mbele, huku akiachia tabasamu kidogo, “siyo msanii, mimi naitwa mwana Sanaa” alijibu Egar kwa sauti ya upole, na yule binti akacheka tena, huku na yeye anatazama mbele kuangalia barabara, “ok! sawa mwana Sanaa, sasa wewe Sanaa yako nini,” aliuliza huku akimtazma kidogo Edgar kisha akatazama mbele
“Nina fani tatu, kwanza nimsanifu wa michoro mbali mbali, kama majengo, ramani za garden, pia michoro ya nguo zakike na kiume, mabago ya matangozo na elekezi, fani ya pili nimwongozaji filamu, na fani ya tatu na buni visa na kuchora katuni” alieleza Edgar kwa sauti ile ile ya upole, “nikipajiau umejifunzia chuo hapo hapo?” aliuliza yule binti mrembo, mwenye umbo matata, huku akinyoosha mkono wake mmoja kwenye redio ya kwenye gari na kubonyeza kidude flani, kuruhusu mziki uanze kusikika, mle ndani yagari
“Nimejifunza tokanikiwa shule, nikaendelea seminalini, ambako nili pata msaidizi mmoja shilikani kwetu, alinielekeza mengi sana, huku chuo nime kuja ku tafuta cheti tu” alisema Edgar bado macho yapo mbele, “he! kwahiyo nipo na padre mtalajiwa?” aliuliza yule dada akionyesha mshangao, “hapana nimwezi wa tatu sasa toka nimeachana na mambo ya upadre” alijibu Edgar kwa sauti yake tulivu, “ok! naona ata upadre bado aujakutoka, maana unaonekana mpoleee, mimi naitwa rose wewe je unaitwa nani?” alijitambulisha yule mdada huku wakicheka kidogo, “naitwa Edgar” alijibu Edgar na Rose akaomba asimuliwe mkasa ulio mtoa Edgar seminalini, hapo Edgar akaanza kusimulia kile kisa cha kupigana na mwanafunzi wa chuo cha ualimu, huku safari ikishika kasi na mziki mzri uki wa sambamba na sauti ya mwanamziki wa reggae, Don Carlos kwenye wimbo wake wa seven day a week, ukiwaburudisha
Huku kimbamba mloganzila nako, kumbe baada ya Edgar kutimka na kuishia zake baadhi ya wananchi wa eneo lile walisogea kwenye tukio, wapo walioona tukio la ngumi, lakini walikuwa mbali kidogo hivyo hawakuweza kuelewa vizuri kilicho tokea, hapo kila moja alikuwa anaongea la kwake, huku wengine wakipiga simu kituo cha polisi ilikuja kutoa msaada wa haraka, baada ya mda mfupi polisi walifika eneo la tukio nakuanza kuwa kagua majeruhi, wakakuta mmoja tayari amesha kufa, na mmoja anaangaika na jicho lake nan die aliekuwa na uafadhari, wengine wawii walikuwa wamezimia, hapo wale polisi wakawaachukuwa wale watatu akiwemomzee Mashaka, na vijana wawili na kuwa pakiza kwenye gari lao huku malehemu akilaazwa nyuma kabi na polis wawili waka baki na lile gari la mzee Mashaka kwaajili ya kufanya utaratibu wa kulipeleka kituoni, mpaka mwenye atakapo pona au ndugu na jamaa watakapo patikana, waje kuli chukuwa
Njiani wale polisi waliwakagua wakina mzee Mashaka kama kuna kitu kitakcho weza kuwa saidia kumpata mtu wa karibu wa watu wale, ndipo kwenye mfuko wa suluali wa mzee Mashaka wakakuta simu, wakatafuta namba simu adi walipo mpata mkewake wakampigia simu kuwa alipoti kituo cha polisi kimbamba kwa maelekezo zaid, huku wakimpa maelekezo ya mwanzo kuwa mume wake inaisiwa mume wake akiwa na wenzake amevamiwa na watu wasio julikana na kufanyiwa shambulio baya sana, maana aikuwa hajari kutoka na na mwone kano wa gari, ila ni kipigo kitakatifu, aikuchukuwa ata nusu saa mama sophia alikuwa kituo cha polisi kibamba akilikagua gari la mume wake, jinsi lilivyo chakazwa vioo, nakutapakaa damu kama bucha la ng’ombe, hayo yalikuwa ni maelekezo ya mkuu wakitu baada ya mamasophia kufika na kujitambulisha, akaambiwa alikague gari ili kuakiksha kama vitu vilivyomo vinaifadhiwa vizuri na vinavyo bebeka aondoke navyo baada ya kupekua pekua, alifanikiwa kukuta laki tano kwenye mkebe wa gari pamoja na simu, ambayo aliitambua mala moja, akizani amesha wai kumwona nayo mume wake
Lakini ikweli ni kwamba alimwona nayo Edgar, mume wake mdogo, baada ya kuakikisha ame sha maliza kukagua, akaanza safari ya kuelekea Hospital, huku njiani akimpgia simu mwanae Sophia, kumweleza kilicho tokea, nayeye akaaidi kumfata mida hiyo hiyo huko Hospital, naam mama Sophia alifika hospital salama na kukuta mme wake akiendelea kupatiwa matibabu, baada ya kuwa amesha pata fahamu kwa msaada wa mashine za kubust (jina la kitaalamu silijuwi), masaa matatu baadae mgonjwa alitolewa kwenye chumba cha upasuawaji akiwa amesha shughulikiwa vyema, mguu uli shonwa naukiwa umesha wekewa vyuma vya kusaidia, pia shavuni napo alishinwa, akapatiwa kitanda kwenye chumba kimoja chenye hadhi ya VIP, kwa maelekezo ya mkewake, pia na wale vijana wawili walipatiwa matibabu, kama ilivyokuwa kwa mzee Mashaka, nao wakalazwa kwenye chumba chao wawili, nayule mwingine nae akiwa amelejewa na fahamu lakini bado hajitambui
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA AROBAINI NA TANO
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni