MAMA MWENYE NYUMBA (51)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA HAMSINI NA MOJA
Ambao wame amuwa kupumzika hapa ili kesho mapema waendelee na safari, wao walielekea moja kwa moja upande wa sehemu yakupata huduma ya chakulaSASA ENDELEA...
“Ningekuwa peke yangu sijuwi inge kuwaje” alisema Rose wakati wanaingia mle ndani na kuchagua sehemu nzuri ya kukaa, na kuagiza chakula
Tumbi hospitali Sophia alikuwa anarudi toka kibamba kituo cha polisi, baada ya kuagizwa na mama yake aende akaliangalie begi la baba yake, akiamini kuwa yeye akuweza kuliona labda ni kwasababu alikuwa amechanganyikiwa, lakini Sophia nayeye hakuliona kabisa ilo begi, ambalo analifahamu vizuri sana, akiwa anaingia pale hospitali taratibu huku akitafakari kilicho mtokea baba yake huku mawazo ya kuwa mama tyake pia ametembea na Edgar yakimjia kichwani, kiukweli alizidi kuchanganyikiwa binti huyu, anakujikuta akimvaa mgonjwa mmoja aliekuwa anapishana nae
“We! dada vipi ebu tazama mbele bwana”alifoka dada mmoja ambae alikuwa na mgonjwa alie mgonga Sophia, bila kusema kitu Sophia aka mtazama yule mgonjwa alie msukuma, alikuwa ni mwanamke ambae alionekana kupatwa na hajari, au kupigwa usoni, kutokana na bandeji alizo zilibwa kwenye paji la uso, na kwenye pua “samahani dada, ilikuwa bahati mbaya” alisema Sophia kwa sauti ya upole huku bado amemtazama yule mgonjwa, ambapo yule mdada aliyekuwa nae, alimshika mkono na kuanza kuondoka zao
“Mh! kama namfahamu huyu dada,” aliwaza Sophia kisha akawasoglea, “samahani dada,” alisema Sophia akimtazama yule alie mshika mgonjwa, nao wakasimama, “eti huyu dada kama na mfahamu, lakini sikumbuki nilimwona wapi?” alisema Sophia akijaribu kmtazama yule dada mgonjwa, “mh! kwani wewe unakaa wapi?” aliuliza muuguza mgonjwa, “nakaa mbezi” alijibu Sophia, “ok na sisi tuna kaa mbezi, inawezekana ulituona hapo asa kama unapenda kutembelea full dose” alisema yule dada muuguzaji, nakumfanya sophia astuke kidogo, “ok! inawezekana, maaa hapo natembeleaga sana, poleni sana” alisema Sophia huku akiaga na kuondoka zake, akajichekea moyoni, “shenzi kabisa Malaya we!” alikuwa ni queen au ni binti wa jana, ambae alilazwa pale hospitali, baada ya kupigwa na chupa usoni, nampigaji akiwa ni Sophia mwenyewe, Sophia alienda moja kwa moja mpaka kweny chumba alicho lazwa baba yake, akamkuta mama yake akiwa na mgonjwa lakini mgonjwa bado alikuwa ame kata moto, kutokana na mituko ya mala kwa mala, walicho amua madoctor ni kumvizia atakapo zinduka wa chome sindano ya usingizi, maana ile kuzimia zimia ni hatari sana kwa mgonjwa, Sphia akatoa riporti yake kuwa hakuna kitu kwenye gari
Leo usiku bwana kazole na mke wake walikuwa wamelala kwenye chumba ambacho miaka iliyopita kilikuwa cha watotot wakike, bado walikuwa wanaongea ili na lile, huku bwana Kazole akijitahidi kumuweka sawa mke wake na kumsaaulisha kipigo na usaliti wa siku tatu zilizopita, “hivi mzee ameuza mashamba ya wapi?” aliuliza Bwana Kazole wakiwa wame jilaza kitandani na mke wake, “mashamba wapi? ni Edgar huyo nasikia amewatumia mifedha mingi, ameoa mwanamke mwenye mihela mingi sana, tena anafanya kazi benk” hapo bwana kazole akawa amepata jibu la swali lake, “umewai kuongea na Edgar siku mbili hizi,” aliliza kwa shahuku bwana Kazole, haaaa! wapi, nitaanzaje kwanza, yani atakurudi hapa nyumbani ilikuwa ni bahati mbaya tu, naonaje aibu” alisema mke wa bwana Kazole akivuta shuka safi na zuri lililopo pale kitandani, nakujifuika mpaka kifuani, “weweeee ukiendekeza aibu, utakufa masikini, changa mka, kumbuka vikoba bado unadaiwa” alisema bwana Kazole huku mke wake akijigeuza na kumwonyea mume wake mgongo, kichwani mwake akitafakari maneno ya mume wake
Huku ruhaha Edgar na Rose walikuwa wamesha maliza kupata chakula, na Edgar akalipa chakula cha wote wawili, “hivi Edgar, unaonaje tuki lala hapa, maana kusafiri usiku nivibaya” alishauri Rose, na Edgar akaunga mkono, “ni kweli alafu kesho saa kumi namoja tuna endelea na safari” baada ya makubaliano hayo, “Rose akashauri waamie kwenye bar, wakachangamke kidogo, wakiwa wana fanya utaratibu wa kupata vyumba vya kulala, walielekea upande wa bar, na kutafuta sehemu nzuri wakakaa, sehemu hiyo ilikuwa ime changamka sana, watu wengi walikuwa wakipata vinywaji, huku wakiudumiwa na waschana warembo, kama mmoja aliewafwata mala tu baada ya kukaa, “ni wahudumie tafadhari,”
Hapo wakwanza kuagiza alikuwa Rose naomba bia ya.. light., wewe Edgar utakunywa nini?” aliuliza Rose baada ya kutaja kinywaji anacho kiitaji, “mimi naomba mvinyo mwekundu,” alisema Edgar akiingiza mkno mfukoni akitaka kutoa fedha, “hapa Edgar, zamu yangu,” alisema Rose akimzuwia Edgar kutoa fedha, kisha yeye akafungua mkoba wake na kutoa pochi ndogo alafu akatoa elfu kumikumi tatu, akampa yule dada, “achana na light, lete huo mvinyo chupa mbili, alafu tuitie na mhudumu wa vyumba” alisema Rose kisha akamtazama Edgar
“Kwanini unapenda mvinyo mwekundu?” aliuliza Rose bado amemtazama Edgar huku akitabasamu, “ndiyo pombe yangu ya kwanza kuanza uinywa” nime jikuta naizowea hiyo hiyo” alijibu Edgar akikwepesha mcho yake yasi kutane na macho ya Rose, ambe alikuw amekaa upande wapili wa meza nakuufanya watazamane, “mh! unaijuwa kazi yake?” aliuliza Rose, “si kilewa? au kuana nyingine” aliuliza Edgar huku pembeni yao akisimama mwana dada, akiweka tray yenye chupa mbili za mvinyo, na grass mbili tupu mezani, “wa vumba anakuja” aliongea yule dada akifungua chupa moja ya mvinyo
“Ok! asante” alijibu Rose na yule dada ondoka zake, na kabla hajafika mbali alipishana na kijana mmoja ambae aliongoza moja kwa moja, kuifwata meza yao, alipo fika aka wasalimia na kujitambulisha kuwa yeye ndie msimamizi wa upande wa uduma za vyumba, “ok! tunaitaji vyumba viwili, mna fanyaje” aliongea Rose, huku Edgar akimimina mvinyo kwenye grass yake na kisha kwenye grass ya Rose “kwanza kabisa poleni sana, chunba kilicho baki ni kimoja tena singo, yani cha kitanda kimoja, nachumbachenywe tulimwekea mteja mbae, alikuwa anatokea arusha, sasa ameghairi amepitia dar usiku huu, na mkichelewa kinaweza kuchukuliwa” alongea yule kijana akionyesha msisitizo, Rose akatabasamu na kumtazama Edgar usoni. Edgar akakwepesha macho yake, Rose akamtazama yule kijana na kumwambia
“Eti! akuna guest nyingine ya jirani?” yule kijana mhudumu wa vyumba aliwatazama kwa zamu, “ vyumba hapa ni mpaka comfort, hukoooo kitonga, kwani nyinyi siyo wa penzi, mpaka mna tafuta vyumba tofauti?” aliongea yule kijana akiendelea kuwa tazama kwa zamu, Edgar na Rose wakacheka kidogo, “kwani unatuonaje anko, tuna endana?” aliuliza Rose huku akiinua grasi ya mvinyo, na kuiweka mdomo kupiga funda moja laini, “mh! yani nilivyo waona nika shangaa sana, lakini uwezi kujuwa labda...” alishindwa kumalizia yule kijana, Rose akacheka kidogo na kumtazama Edgar, “eti! Eddy una semaje, utaweza mzungu wa nne” aliuliza Rose na Edgar akajibu, “Usijari nita lala kwenye gari” alisema Edgar akiinua grass nay ye na kuiweka mdomoni
“Ok! anko bei gani?” aliuliza Rose akifungua pochi yake, “elfu hishilini na tano tu!” Rose alitoa fedha hiyo na umpatia yule kijana ambae aliondoka akiagiza kupitia ufunguo mapokezi na kusaini kitabu cha wageni, “unaogopa nini kulala chumba komoja na mimi?” aliuliza Rose baada ya kuakikisha yule kijana amesha ondoka, “mh! unazani ni kazi lahisi kulala na mwanamke mlembo kama wewe,”alijibu Edgar na wote wakacheka, “kwani nikiwa mrembo ndio nini, si tuna lala na nguo zetu” alisema Rose, huku wakiendelea kunywa mvinyo mwekundu, “au unaogopa nita kubaka?” aliuliza Rose wakacheka tena, “unibake au ukibake kibakio?” alisema Edgar huku wakiendelea kucheka, “ok! kama auogopi kitu basi mimi sikupi ufnguo wa gari, tuna lala wote chumbani” alisema Rose akitazama chini, akishindwa kumtazama Edgar ambae sasa alikuwa anaweza kumtazama Rose, sijuwi kwaajiri ya kinywaji
“Rose utanitafutia kesi, kwa jinsi ulivyo mzuri alafu tulale chumba kimoja, lakini poa mimi nitalala chini” aliongea Edgar huku wakiendelea kupiga kilaji chao taratibu, kwakifupi maali hapa watu uwa wanakesha wakipiga mtungi na wengine lala kwenye magari, wakiwa wame opoa wanawake ambao walikuwa weni sana pale mbuyuni, ukiachilia wahudumu wakike pia kuna wana dada ambao walikuwa wana kuja kwa kuatafuta watu wa kuondoka nao, wakiwa na nia ya pata fehda toka kwa madereva hao wengi wao wakiwa ni wa magari makubwa, “kwahiyo tume kubaliana tuta lala wote, alafu itakuwa lahisi kuamshana mapema, kesho asubuhi” aliongea Rose akijaribu kumtazama Edgar usoni, “poa aina tatizo,” alijibu Edgar akiendelea kukamua mvinyo, Rose akaachia tabasamu
Tumbi hospital Sophia na mama yake walikuwa wame kaa pembeni ya kitanda alicho lala mzee Mashaka, ilikuwa saa tano za usiku mama Sophia alikuwa anasinzia, japo Sophia alikuwa anajitahidi kumsemesha semesha, ili mama yake asilale asilale, “Sophia bola ungeenda kupumzika alafu mimi kesho, uni letee chakula asubuhi” aliongea mama sophia na Sophia akaunga mkono, japo moyoni alikuwa anajambo ambalo lilikuwa linamsumbua sana juu ya namba ya Edgar kuseviwa saloon kwenye simu ya mama yake, nambaya zaidi alipoipiga, Edgar alipokea na kumuita mke wetu, njiani sophia alikuwa akiwaza
“Kwa maana hiyo Edgar anatembea na mama, ebu ngoja” alisema Sophia huku akichukuwa simu yake kwenye dash board na kuitafuta namba ya Edgar kisha akaipiga, simu iliita kidogo ikapokelewa “hallow sophi vipi kunakitu ume sahau?” mh! sauti aikuwa ya Edgar , ilikuwa ni sauti ya mama yake, “haaaa, mama nimekosea, kunamtu nilikuwa nampigia” aliongea Sophia akakata simu, “mbona nashindwa kuelewa, inamaana atasimu yake anayo mama, au amesha fukuzwa kwa Suzan?” alijiuliza Sophia wakati akiwa anaendelea na safari yakeakataka kupitia kwa Suzan akajuwe kulikoni, lakini akaona itakuwa ngumu sana kutokana na yaliyotokea asubuhi, akaona labada ampigie simu, akaona ndiyo kabisa aitapokelewa, akaamua kuendelea na safari
Mama Sophia baada ya kupokea simu ya sophia, kwenye simu aliyozani ni simu ya mume wake, maana ata jila mwanae lilikuwa lime andikwa Sophia, aka iweka simu kwenye mkoba wake, kisha akenda kukaa kwenye kiti cha mataili maalumu kwa wagonjwa (wheel chair) kilichopo mle ndani akaa na kuanza kupitiwa na usingizi
Ilikuwa saa sita usiku, ndipo Edgar na Rose walipo shauliana wakapumzike chumbani, maana mida ilisha watupa mkono na safari yao bado ilikuwa ndefu sana
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA HAMSINI NA MBILI
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni