MTAA WA TATU (27)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA
Hata sijui hivyo vitu kanunua muda gani
Akatoa mavazi meusi na kuvaa kisha akafungua begi na kutoa visu na star
Yani zile nyota kisha akatoka nnje sijui usiku ule wa manane mwanaume anaenda wapi
NIOMBE SAPOTI, BONYEZA TANGAZO LINALOKUJA NA KUJAA KWENYE SIMU YAKO WAKATI UKIFUNGUA SIMULIZI AU LILE LINALOKUWA KATIKATI YA SIMULIZI ZETUKABLA HAUJAIFUNGUA NDANI, PIA KUNA LILE LINAKUJA NA KUNG'ANG'ANIA HAPO CHINI, BONYEZA WALAU MARA 3-4 HIVI HIYO NDIO SAPOTI YAKO KWANGU, TAFADHALI NIPE NGUVU NAKUTEGEMEA SANA MSOMAJI WANGU
SASA ENDELEA...
Kwanza alikuwa yuko faster
kwa kutembea akafika sehemu
moja hivi parking ya magari kama kawaida yake akaiba pikipiki na kuondoka kwa speed
huku akiacha vilio kwa walinzi,
Ndoto ilikuwa imemzindua
Mwanaume na hiyo safari ndio mwanzo wa kuuwa tu,
Njia panda ya Ubungo yeye akiwa anatokea
Mabibo hostel akakunja kuifata barabara ya Mwenge
Usiku huo magari na pikipiki sijui bajaji zilionekana moja moja tu, kufika
Mwenge akakunja kushoto kuingia
Lugalo, ndani ya makongo
Mwanaume akazama kwenye vichaka fulani
Taa ya pikipiki kaizima tokea
Mwenge akashuka kutoka kwenye pikipiki na kuanza kukimbia kwa kasi kuzisogelea baadhi ya nyumba,
Kama vile nyau akaruka samasoti na kwenda kutua kwenye moja ya nyumba,
Zote mbinu za kininja ogopa sana
Mwanaume kuvamia kambi ya Jeshi.
Kwa uwangalifu zaidi akafungua mlango kwa kutumia funguo malaya akaingia ndani
Dakika kama tano akatoka na kuondoka eneo hilo.
“oyaa Bonge hii pikipiki si ndio iliibiwa ile jana usiku au sio hii?"
“ndio kaka mwenyewe si
Suma"...
“sasa imekuwaje imerudishwa au mwizi kaogopa kurogwa nini!"
“ina wezekana maana Suma kwao Tanga yule"....
“ehee umenikumbusha kitu kaka unajuwa kuna jamaa yangu mmoja anaitwa Shaha
Sasa huyu jamaa yangu yeye ishu
zake ni uchomaji mkaa na kubeba mbao.
Basi ikawa kila akisafirisha kuzipeleka jijini
Dar kama sio pale Kibaha basi popote anadakwa na maafande wale
Maliasiri,
Anapigwa faini kubwa tu.
Sasa siku moja akaenda kwa babu yake kufanyiwa mambo
yani hivi ninavyokwambia jamaa anasafirisha hadi mizigo ya watu magunia ya mkaa mbao polisi wakimdaka kufungua
Kontena wanaona mikungu ya ndizi tu"
“ha!ha!ha!ha!
Ebwana noma yani baada kuona magunia ya mkaa na mbao wanaona
Ndizi?"
“ndio maana yake huko Tanga ni noma
Asikwambie mtu"
Wakati walinzi wale wakipiga story
Asubuhi ile wakisubiri kukabidhi
vitu vya watu kwa wenyewe
Ndipo wakasikia taarifa ya habari ikitangaza tukio la mauwaji
“bwana Franck ambae ni Kostebo
katika kikosi cha JWTZ amekutwa ameuwawa kwa kuchinjwa
Ni tukio ambalo limetokea jana usiku
Chanzo cha mauwaji hayo bado hakija fahamika",,,
Hakika lilikuwa ni bonge la pigo kupitia kwa kikosi kizima cha Jeshi ukizingati
marehemu alikuwa ni mmoja kati ya
Makamanda wenye kutoa mafunzo kwa vijana wote
“hakika tumepata pigo kubwa sana kwa kuondokewa na Kamanda
wetu sijui kawakosea nini walimwengu mpaka wameamua kumuuwa kikatili namna hii!"
Yani kachinjwa kama kuku kusema kweli hatutoweza kukaa kimya katika swala hili
huyo muuwaji au wauwaji
Lazima tuwasake popote walipo.
Mmoja kati ya makamanda
Aliongea hivyo kwa hasira
Asubuhi ile
Hafidhi alikuwa akiosha vyombo taarifa za mauwaji zikisambaa kama umeme.
“mambo vipi my dear?
Naona unajipa tabu baby wangu hutakiwi kuosha vyombo wakati Mimi nipo"
Amina aliongea hivyo baada kufika na kumkuta Hafidhi akiosha vyombo
“wala usijali baby mbona kawaida tu,
Hivi jana ulikuwa wapi?"
Ni swali ambalo lilimfanya Amina ainamishe kichwa chini ni aibu kumwambia mpenzi wako kwamba umebakwa.
“Amina si nakuuliza wewe inamaana unatunga uwongo wa kunidanganya sio?"
Amina mchozi ukaanza kumtoka
Hakupenda kuongea uwongo
Akaogopa kuongea ukweli akihofia kuachwa.
Hafidhi akainuka na kujifuta mikono
Na kumshika kipenzi chake
“niambie nini tatizo mbona unalia?"
“sina budi kukwambia ukweli Eddy sijawai kukudanganya kamwe
Ile jana nilikuja mpaka pale maskani na kukuulizia kwa Pengo
akaniambia umekuja nyumbani nikatoka mbio kukuwai kufika
pale kisimani nikaitwa na Ashirafu nikaenda kumsikiliza ajabu kufika tu akanikamata kinguvu na kwenda kunibaka"....
(What!) nini?.....
“Eddy please usiniache"
Hafidhi akamfuta machozi na kumwambia
“usijali kipenzi changu siwezi kukuacha
Naomba uoshe hivyo vyombo kisha utanipikia kitu mseto wacha mi nikaoge naitaji kwenda town kucheki
Michongo ya kazi"
Basi Amina akatabasamu na kuanza kuosha vyombo,
Mwanaume hakuchukuwa dakika nyingi akatoka na kwenda zake town
baada kupita mitaa miwili mitatu kuna maneno akaongea
“kama unyama wacha uwe unyama tu huyu bwege nae aende kubakwa huko kuzimu
Akaingia ndani ya Gym moja haiko mbali na kitaa hiko.
“ohoo karibu sana kijana naona umekuja kupasha sio".....
Ashirafu baada kumuona
Hafidhi kaingia humo akaanza kumshobokea
Mwanaume akafanya kama anataka kuondoka hivi yani kumpa mgongo Ashirafu
“vipi tena dogo mbona unaondoka
Ghafla
Ashirafu akashtuka baada kuona jamaa kachenji mavazi faster yani kufumba na kufumbua kawa Ninja
ndani ya Gym kila mmoja akashikwa na kiwewe,
Sema wanaume wakajipa moyo na kuitaji kupambana nae wee
Ilikuwa hatali ndani ya Gym kichapo kikaanza kutembea Ashirafu alipigwa kifuti cha kifua na kwenda kudondokea kwenye chuma kimoja kikafyatuka na kumkita tumboni, basi alicheuwa kila kitu mpaka nyongo vioo vilivunjika watu walitupwa huku na kule,
Mwanaume alikuwa hashikiki kabisa utasema Ninja mask au
Ninja suit, akaenda kukamata chuma kimoja akachomoa yale mataili ya train
Akabaki kaishika nondo
Ashirafu hakuweza kuinuka tena akabaki kutambaa tu mara nondo ikakita mgongoni mwake na kutokea tumboni
Damu hadi utumbo ukamtoka na kuwa kimya wasalimie kuzimu"
Ndio kauli aliyoitoa Hafidhi ile anageuka tu
sauti ya ving'ora ikasikika"......
Kabla mwanaume ajajiuliza sana gari za polisi hizo hapo nnje tena kwa speed yote wakafunga break tangazo likatolewa
“Kijana usitake kushindana na mikono ya sheria utakuja kuumia
Tunakuomba ujisalimishe mwenyewe
hii ni amri"
Baada agizo lile kutoka kwa kiongozi wa msafala. Mwanaume akatoka akiwa kaweka mikono juu, kufika nnje polisi walikuwa ni wengi kila mmoja yupo makini na siraha yake.
Basi akaambiwa apige magoti chini.
Ajabu upepo ukaanza kuvuma vumbi likatimka mpaka polisi wengine wakafumba macho ndani ya dakika mbili upepo ulivuma, kuja kutulia
Mwanaume hayupo kashapotea mbele ya upeo wa macho yao.
Sema hawakutaka kukata tamaa wakatawanyika kumtafuta huku na kule hawakuweza kumuona.
Upande mwingine tunamuona.
Amina baada kuosha vyombo akajiandaa kupika kabla ya kufanya hivyo akafagia mule chumbani akatandika kitanda na kukusanya nguo chafu.
Sema kuna begi akaweza kuliona na kujiuliza kuna nini humu kama ujuavyo
siku zote kitu ukikitilia shaka utaitaji kukichunguza.
Basi Amina akafanya kulibeba na kuliweka kitandani
Na kufungua zipu laa haula hakuweza kuamini macho yake kwa kile alichokiona ndani yake yalikuwa maburungutu ya pesa
Akabaki kukodoa macho tu
Wazo likamjia akimbie nazo, akashikwa na kiwewe si mchezo.
Ni zile million mia saba Hafidhi kaziweka ndani akalifunga bagi na kulivaa mgongoni ile anafungua mlango tu kuna kitu kikamgonga kichwani, na kuanza kuona kizunguzungu bibiye akaenda chini na kuwa kimya.
Mlango ukajifunga huku Amina akibaki chumbani kalala chini hajitambui,
Kwa upande huu ndani ya uwanja wa ndege kuna mabinti watatu matata yani kwa jinsi wanavyoonekana tu wapo kikazi zaidi.
Basi wakapokelewa na wenyeji wao wakaingia ndani ya gari aina ya Vogue
safari kwenda makao makuu ya Jeshi ikaanza
“Yusra unakumbuka nini baada kurudi nchini Tanzania?"
“nakumbuka vitu vingi sana mkuu"..
“kama vipi embu vitaje!"
“nakumbuka siku ambayo mgombea wa Uraisi alidondoka wakati wa kampeni kwenye viwanja vya jangwani.
Kingine nakumbuka siku ambayo mabomu yalilipuka kule mbagala kuu,
“kumbe una kumbukumbu nzuri sana Yusra,
Je Vivian nawe unakumbuka kitu gani?"
binti anaekwenda kwa jina la Vivian hakujibu kitu zaidi ya kukaa kimya tu,
Binafsi alikuwa yuko mbali kimawazo akiwaza kuhusu jukumu zito walilo kabidhiwa na muheshimiwa Raisi juu ya kumsaka muuwaji wa kutisha
Anae wapa jambajamba jeshi la polisi nchini.
Moyoni mwake akajiambia ni kazi ndogo tu kwani washafanya kazi nyingi na nzito kama hizo.
Hawajawai kufeli.
“Wee Vivian!!!
Mwenzake akamshtua kutoka kwenye dimbwi zito la mawazo, akaitikia
“abee unasemaje Mariam?"
“mkuu amekuuliza unakumbuka nini baada kuiyona nchi yetu ya Tanzania maana tuliondoka tokea tukiwa wadogo?"
Basi akajiweka sawa na kusema,
“kiukweli sina kumbukumbu yeyote ile kwa kifupi nawaza kuhusu hicho kikundi cha watu wenye kufanya mauwaji tu"...
Mkuu wa msafara akatabasamu na kumwambia
“Vivian binti yangu naona ushaanza kuingiwa na hofu kubwa ndani ya moyo wako.
Binafsi hicho sio kikundi cha watu huyo ni mtu mmoja tu, kibaya zaidi ni mtoto wa mkuu wa majeshi bwana J Ikram
Sema amri imetoka kwa Muheshimiwa Raisi kijana atafutwe popote alipo
Akamatwe akiwa mzima"
“ha!ha!ha!ha! Kila mmoja akaanza kucheka si
Mariam wala Vivian na Yusra wote
wakabaki kucheka, mpaka mkuu wao akabaki kushangaa na kuuliza
“vipi mbona mnacheka?"
Vivian kwa sauti ya kicheko akasema
“unajuwa nini mkuu sisi tulidhani tunakuja kupambana na kikosi kikubwa cha
watu kama elfu kumi hivi tukajiandaa kibabe zaidi. Kumbe kijitu chenyewe ni kimoja
tu, mi naona hii kazi niachiwe mimi peke yangu"
“Vivian tambua kitu kimoja usimdharau
mtu usiemjuwa kwa kifupi jamaa ni hatali kuweni makini"
Gari ikaingia ndani ya jengo moja hivi lipo nnje kidogo ya jiji kisha dereva akapaki
Na wao kushuka
ile wanapiga hatua kadhaa tu
Kwenda mbele ghafla kikatokea kitu ambacho hakuna aliyeweza kukitegemea baada kuibuka kiumbe kimoja kutokea kwenye vichaka siku zote mdharau mwiba
mguu huota tende
Mwanaume alikuwa akimfatilia mkuu wa msafara tokea uwanja wa ndege
Akachumpa na kwenda kumshika kwa nyuma huku siraha yake aina ya
Mundu ile ya kukatia majani ikiwa shingoni kwa mkuu, yule
Akajifanya mjanja kutaka kuitoa
Mwanaume akacheza na shingo,
Yusra akaruka na kupiga mateke
ya haraka haraka mwanaume akapanchi
Kisha akamdaka na kumuwekea mundu shingoni
Wenzake vijasho viliwatoka na kubaki kutetemeka.
“tulieni mabinti tulizo la moyo wangu, naomba niwaambie kitu kimoja hii ngoma sio yakitoto kama mnavyo fikilia nyinyi sasa basi nawaomba mrudi mliko toka
Msije mkafa kizembe sipendi kuuwa
Wanawake mkikaidi amri itabidi nifanye hivyo, ukiona mtu anafanya kitu kama hiki
Basi tambueni kuna jambo nyuma ya panzia"...
Baada kuongea vile akamzungusha tena Yusra na kumsukumiza kwa wenzake kisha akapotea kwa kuchumpa kwenye
Majani.
Mabinti nao wakaingia kwenye gari
Vivian akakamata usukani na kuizungusha gari kwa kasi
Mariam akifungua briefcase na kutoa siraha zake
Yusra nae akafanya hivyo ndio kwaanza wanaingia nchini na kukalibishwa kwa chai ya kikubwa, ndani ya nnje kidogo ya jiji ikawa balaa
Hafidhi akiwa ndani ya pikipiki
NAOMBA SAPOTI, KUNA MATANGAZO(ADS) YANAJITOKEZA KWENYE APP YETU, LIMOJA LINAJAA KWENYE KIOO CHAKO JINGINE LINANG'ANG'ANIA HAPO CHINI KABISA, BONYEZA JAPO MARA 2 AU 3 KILA UKIFUNGUA SIMULIZI HIYO ITANIPA NGUVU YA KUENDELEA ZAIDI NA SIMULIZI ZETU🙏🙏
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni