MTAA WA TATU (3)
Zephiline F Ezekiel
5 min read
SEHEMU YA TATU
“Hivi wewe hujui kama huyu ndio
Baba mwenye nyumba, kwanza tokea
lini mtoto wa kiume akapiga
deki.
Wakati basha wako hata kulenga shimo la choo hawezi mikimba inaenda pembeni.
muone kwanza
pua imemkauka kama kikwapa cha mbuzi"
SASA ENDELEA...
Ndani ya nyumba hiyo
kuna mabinti wanaongea hatari tupu mmoja wapo ni Joyce
kisha kuna Beatrice. tisa kumi
kuna Zainabu hakika huyo ni kiboko
ana mdogo wake anaitwa Amina
kama bange basi wanavuta zile mbichi moshi wanatolea makalioni.
Watoto wamedata vibaya mno yani wakasahau kama kuna kufa, baada
Joyce kumchamba yule binti akamgeukia
Hafidhi na kumwambia
“hata usijali kaka yangu wee nenda kaendelee na
mambo yako. Kama kudeki
atadeki yeye kishankupe"
Hafidhi akatabasamu tu na kuingia ndani
Akiwa anakatiza ukumbini
kuna binti akapigana nae kikumbo bila shaka mmoja kati yao
kafanya makusudi
Hafidhi akamtizama yule binti hakika mtoto maishaallah
binti kaumbika si mchezo.
“Mijitu mingine bwana sijui ikoje inatembea macho juu kama vile kabeba jeneza"
Aliongea hivyo huyo binti huku akitoka zake nnje.
Hafidhi nae akamshiti
yapata saa nne Asubuhi ilimkuta
Hafidhi akiwa chumbani kwa bibiye
Beatrice akinywa chai
katika kupiga piga story za hapa na pale
“kwanza asante sana Dada yangu kwa
chai ni watu wachache sana wenye mioyo ya kujitolea kama yako"
“usijali kabisa kaka yangu wee jisikie uhuru tu"
Hafidhi akasema
“kuna story moja hivi naikumbuka kipindi nipo nyumbani kwetu Iringa"....
Beatrice akakaa vizuri na kuomba asimuliwe hiyo story
Ndipo Hafidhi akaanza kwa kusema,
Sauti ya kilio kutoka kwa Binti mdogo iliweza kunishitua kutoka usingizini.
Hakika sauti yake ilikuwa kali sana, binafsi alilia kwa kulalamika msinipige jamani nioneeni huruma".......
Nikabaki kujiuliza huyu binti kafanya kosa gani.
Sikutaka kujiuliza sana zaidi ya kuinuka kitandani na kutoka zangu nnje,
Nilipiga hatua kadhaa na kufika kwenye nyumba moja wapo, nilikuta umati wawatu umejaa
huku msichana mdogo akiwa kabeba mtoto mgongoni, akilia kwa kuomba msaada.
Kuanzia mama mwenye nyumba na watoto wake kama watatu
Wakimtukana na kumpiga masingi yule binti,
Nikataka kufahamu nini chanzo
nini tatizo, nikamsogelea yule
binti na kumuuliza
“Khadija nini tatizo mbona unakifurushi cha nguo umekataa kufua au?"
Hakika binti huyu namfahamu tokea tukiwa wadogo tunasoma shule ya msingi.
Akanitizama huku machozi yakimtoka
kama vile bomba la vua, akaniambia
“Hafidhi kaka yangu tafadhali nisaidie".....
kwa sauti ya huruma yenye kuambatana na kwikwi ya kilio
Khadija aliongea nikamtizama mtoto wake aliyekuwa amelala
mmoja kati ya Mabinti wa mama mwenye nyumba ni Demu wangu.
Akaja na kuanza kubwata
“baby haya mambo hayakuhusu kabisa tuachie mbwa koko wetu".......
Hakika niliumia sana moyoni mwangu kwa binaadamu huyu kumwita mwenzie Mbwa koko.
Kama haitoshi akataka kumpiga kofi kama nisingewai kuudaka mkono wake angeshampiga,
akapaza sauti huku akiruka ruka
“niachee!!!
Sikutaka kumuacha nikamkazia macho nikiwa nina hasira macho yangu yamekuwa mekundu.
Ndipo Khadija akaaza kusimulia"......
“Kwa jina naitwa Khadija Saidi ni mzaliwa kutoka Arusha, wazazi wangu wote walifariki kwa ajali ya gari.
Hakika nilibaki kuwa mtoto yatima tu,
mpaka mzee Kitwana alipotokea kunichukuwa na kuja kunilea
maana yeye alikuwa ni rafiki kipenzi na marehemu baba yangu.
Akanilea na kunisomesha hakika alinipenda na kunithamini kama mwanae wa kunizaa.
Hatimae nimekuwa mtu mzima akaniomba niweze kuolewa na mwanae,
sikutaka kukataa ijapokuwa aliyeniowa nilikuwa namuheshimu kama kaka.
Hatimae nikaolewa
siku si nyingi nikashika ujauzito, na kujifungua mtoto huyu unaemuona,
Hakika baba mlezi alifurahi sana kwa kuitwa babu,
Hafidhi kaka yangu kama ujuavyo juzijuzi tumetoka kumzika mzee wetu,
leo hii nafukuzwa ndani ya nyumba hii.
Nitaenda wapi Mimi".....
hakika history ya Khadija ilinifanya nidondoshe chozi.
Wakati anauliza ataenda wapi yule
mama akapaza sauti kwa kumjibu
“uwende kaburini kwani hujui aliyekufadhiri yuko huko"....
Hafidhi nikafanya tukio ambalo kila mmoja akabaki kinywa wazi,
kwani nilianza kumtandika makofi yule
Mama hakuna aliyesubutu kuingilia kwani nikikasirika nakuwa sishikiki"...
Wakati
Hafidhi anasimulia hivyo
Beatrice akawa anatetemeka mpaka
Hafidhi mwenyewe akashangaa na kumuuliza
“Beatrice vipi mbona hivyo"
Kwa sauti ya uwoga
Beatrice akajibu
“hapana hamna kitu, ehee ikawaje baada kumtandika makofi huyo mama, maana kama ni hivyo mbona mtaani
kwetu tutakoma"......
Hafidhi kuna kitu aliweza kuhisi sema akutaka kuongea zaidi
Nae akauliza
“mtakoma vipi kwani huu mtaa una nini?"
“wee acha tu kaka yangu
sitaki kukwambia chochote wewe mwenyewe utajionea"....
Beatrice alisema hivyo na
kumuacha njia panda Hafidhi j ikram
Kwakuwa chai alishakunywa hakutaka kuendelea na story zaidi ya
kusema ataendelea siku nyingine.
Akatoka mpaka ukumbini na kukutana
uso kwa uso na bibiye
Zulfa
“wee Mwanaume umetoka kufanya nini ndani ya chumba cha ngedere?"
kumbe lile swali
Beatrice akalisikia akatoka na kusema
“ngedere Baba yako mwanaizaya mkubwa wewe,
yani kujipeleka chumbani kwake ile
jana leo hii unajiona ndio
Mother house sio"......
Zulfa hakutaka kuongea sana mziki anaupeleka kwa Joyce
wakati
Beatrice tegemeo lake Zay mbona balaa
yapata saa saba mchana
Hafidhi akiwa chumbani kwake akichezea
Laptop yake sijui anaandika story ya
Chanduka akashtuka
baada kusikia kelele za kama ugomvi hivi
zikitokea nnje,
Siku zote Hafidhi si mtu wa kupenda kufatilia mambo ya watu.
Au kudadisi, sema zile kelele zikamfanya atoke nnje ya Idea,CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akaona si vyema yeye kuendelea kukaa ndani, akaamua kutoka mpaka kibarazani hakuweza kuamini
baada kuona watu
wamejazana pande hizo utasema kuna mechi ya mpira wa miguu.
Au rusha roho kumbe kulikuwa na ngumi baina ya wasichana wawili
“nishakwambia huniambii chochote wee Malaya tu unagawa nyuma na mbele"
“Anaegawa nyuma Mama yako
M****nge wewe
na ukoo wenu wote"......
Sauti za watu zikasikika zikisema
Piganenii",,,,,heshima iwepo
Asha mautupu piga huyoo......."
Ni kauli ambazo zilimshangaza sana
Hafidhi na kuona ni mambo ya kitoto.
Mwanaume akajitosa kati kwenda
kuamulia.
“tafadhalini Dada zangu acheni kutukanana ugomvi sio ishu tumlaani Shetani"
Hafidhi baada kufika pale akaongea hivyo.
Watu wakaanza kumzomea
hiloo,,,,,huyooo,,,,umetokea wapi wewe wa mbwinde nini waache waonyeshane
Kudadeki zako, yule binti mwingine akataka kumvamia mwenzake
Hafidhi akamzuia kwa kumdaka
“wee kaka niachie usinishike wee shoga nini
K***ko zako"
Masikini ya Mungu binti hakuweza kufahamu kama anafanya kosa kubwa sana kumtukania
Hafidhi mama yake kwa kasi ya ajabu binti alijikuta akipigwa kibao na kwenda chini.
Hafidhi nae akashtukia akichotwa zinga la mtama akaenda hewani kimo cha mbuzi.
Akadondoka chini puhuu
kabla hajakaa sawa akiwa pale chini. Akapigwa teke la mbavu mpaka akahisi kutapika damu
hakika mwanaume kimbelembele kilimpoza
Alipigwa vibaya mno,
Watu wakabaki kushangilia tu,
“pigaa huyoo",,,,
ilibidi kina Joyce waingilie kati kuja kumuokoa
“Tafadhali kaka yangu Cholo msamehe
ni mgeni huyu hajui chochote"
Aliongea hivyo
Beatrice kumwambia huyo jamaa aliyekuwa akimpiga Hafidhi,
“pumbavu zake kama mgeni ndio ampige demu wangu sio?"
Akamshindilia na teke la tumbo kisha akamshika demu wake hao wakaondoka huku kila mtu akisema
Lake kumwambia Hafidhi
“karibu sana dogo kwenye mitaa ya
jahannam unabahati
Aisee angekuuwa yule,
Hafidhi akainuka huku akipaza sauti kumwita Cholo “wee bwege nyau kuja hapa".....
na kusema kuwaambia kina Beatrice msinishike
Binafsi Hafidhi akasahau kauli ya Baba yake asijionyeshe yeye ni nani alichokihitaji ni
heshima atapigwaje mbele ya
Mademu ujinga huu"....
“Kaka yangu punguza hasira yule jamaa atakuuwa huwa atanii"
Cholo baada kusikia anaitwa bwege nyau
Akageuka na kuja kumaliza kazi.
Hafidhi kama nyau akatoka mbio tena speed akaruka juu na kuachia
mateke mawili double
yaliyompata Cholo
moja kifuani lingine usoni kidume kikayumba na kwenda chini,
Hafidhi akakunja ngumi
na kumwambia Cholo
“inuka mtoto wa Mama njoo kwa baba yako"....ni kauli ambayo ilimfanya Cholo awe na hasira akajizoazoa pale
chini na kuitaji
kumvamia Hafidhi siku zote ngumi ni mipango sio kuwa na mwili mkubwa ndio kujuwa ngumi
Mcheki yule mchina sijui Jet le jinsi anavyo
wakalisha watu.
Wakati Cholo anakuja kama vile nguruwe pori
Hafidhi aliuvuta mguu wake wa kushoto kwa nyuma kidogo kitendo bila
kuchelewa Cholo akakutana na kifuti cha pua.
Huku ngumi double double zikitua mwilini mwake,
Mwanaume akafanywa Basin beg akapigwa kama mtoto binafsi
Cholo akadebweda hakuna aliyeweza kuamini
Kidume kama Cholo kupigwa na mtu kutoka bush
Kibaya zaidi mbele ya demu wake.
Hakuna kitu kibaya kama kupigwa mbele ya demu wako,
ni aibu kubwa aisee!
kina Beatrice wakaja kumshika
Hafidhi wakimuomba aache
“kaka inatosha basi muache".....
Hafidhi akaona isiwe shida akaingia ndani moja kwa moja chumbani kwake huku akijilaumu kwanini kafanya
vile
Akakumbuka kauli ya Baba yake
na kujiona tayari ni mkosaje.
Kama mwanamke kalala nae tu siku aliyofika, leo hii kashindwa kuzidhibiti hasira
zake mpaka kapigana
(Why".......??
“yani hata siamini kabisa"
“huamini nini Dada Beatrice?"
“yani Cholo ninaemfahamu mimi leo hii kapigwa kama mtoto vile"
“ndio kapigwa siku zote mmbabe anapata
Mmbabe mwezie, kwahiyo sishangai kwa Cholo kupigwa
Alikuwa ni
Beatrice Zulfa Joyce wakiwa na baadhi ya wasichana wengine wakiongelea swala la Cholo kupigwa siku hiyo
“naona mabinti kazi kukalia umbea tu,
Kumdisi Cholo sasa kwa taarifa yenu
mwambieni huyo bwege wenu ajipange.
Kama moto kauwasha ajuwe na kuuzima"...
Ilikuwa kauli kutoka kwa kijana mmoja hivi aliongea hivyo, huku akiingia chumbani kwake.
Nae anaishi nyumba hiyo hiyo,
Beatrice na
wenzake wakaangua vicheko vya kishambenga
“hahahahaa,,,,,utanibeba mieeee ukishindwa nilazeee"......
Zulfa akasema
“eti mwambieni ajipange
Wakati wewe mwenyewe kulenga shimo la choo tu huwezi,
Matokeo yake kila ukinya kitu kinaenda pembeni.
Bila shaka CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Malaya wako anapata shida kukuonyesha
sehemu
ya kipochi manyoya kulenga hujui"....
Vicheko vikazidi kusikika
Jamaa akakunja ndita na kusema
“wewe Zulfa ipo siku yako"
“bwanaee embu nenda zako tutamwita mchina mweusi akufinyange kama
Cholo ohoo"....
“muiteni hivi mnafikilia nani atamuogopa kwanza Cholo mwenyewe ni boya tu ndio maana kapigwa na wabush"
wakati wanaongea
Ghafla yule kijana akakunjwa
“Hivi wewe Bulongo ushaniona mimi wa kunitapeli sio,
yani unishike makalio yangu uingize vidole vyako kwenye kitumbua changu kisha ukaniahidi kunipa shilling elfu
Kumi tokea siku ile mpaka leo unanikimbia
Sasa leo nimekunasa nipe changu"....
NAOMBA SAPOTI, KUNA MATANGAZO(ADS) YANAJITOKEZA KWENYE APP YETU, LIMOJA LINAJAA KWENYE KIOO CHAKO JINGINE LINANG'ANG'ANIA HAPO CHINI KABISA, BONYEZA JAPO MARA 2 AU 3 KILA UKIFUNGUA SIMULIZI HIYO ITANIPA NGUVU YA KUENDELEA ZAIDI NA SIMULIZI ZETU🙏🙏
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA NNE
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni