MTAA WA TATU (14) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Ijumaa, 19 Juni 2020

MTAA WA TATU (14)

UMEWAHI KUONA AU KUSIKIA KUHUSU PICHA ZA AI?
Sasa naomba nikufundishe bure kabisa nawewe uzitengeneze kirahisi kabisa

Mwandishi: Hafidhi J Ikram

SEHEMU YA KUMI NA NNE
Ikiwa ishakatika wiki moja sasa tokea
Hafidhi afanye mauwaji na kukimbilia maeneo ya Keko luanga akaweza kupata
Hifadhi kwa jimama moja hivi.
Na kuishi hapo kwa kujificha
“Hivi Zuwena hiyo tabia ya kutoka na vitoto vidogo utaacha lini?"

NIOMBE SAPOTI, BONYEZA TANGAZO LINALOKUJA NA KUJAA KWENYE SIMU YAKO WAKATI UKIFUNGUA SIMULIZI AU LILE LINALOKUWA KATIKATI YA SIMULIZI ZETUKABLA HAUJAIFUNGUA NDANI, PIA KUNA LILE LINAKUJA NA KUNG'ANG'ANIA HAPO CHINI, BONYEZA WALAU MARA 3-4 HIVI HIYO NDIO SAPOTI YAKO KWANGU, TAFADHALI NIPE NGUVU NAKUTEGEMEA SANA MSOMAJI WANGU
SASA ENDELEA...
Mama Asia aliulizwa hivyo
na rafiki yake kipenzi
basi akajibu kwa kubetua midomo juu.
“kwani wewe inakuhusu nini?"
Kwanza mtoto kwa mama yake au
ujui kama mtoto wa mwenzio kwako ni mkubwa mwenzako.
Kwanza hanipwelepweti bibi wewe
kitu kinakaza penyewe
Kama unamavi kanye kichaka kile pale
ha!ha!ha!ha!ha
wakati wanaongea
Hafidhi nae akatoka ndani na kusema
“baby natoka kidogo naenda hapo kati"

“sawa my dear angalia wasije kukuiba
Handsome wangu nikaja kufa kwa presha bure".....
Hafidhi akacheka na kuondoka zake
alikuwa katinga pamba kali si mchezo
tena kanyoa kiduku,
Wakati anaingia katika mtaa mmoja
akashangaa kumuona
sijui bibi au msichana akiwa kalala kwenye kibaraza cha nyumba moja.
Akashikwa na shahuku ya kutaka kufahamu yule mtu anaumwa au vipi
akapiga hatua na kusogea eneo lile
pembeni ya yule mtu kulikuwa na machicha ya nazi yani kama vile kawekewa kuku
Basi akatoa sauti kwa kusalimia
“shikamoo bibi"
yule mtu akageuza shingo yake kumtizama huyo anaemsalimia,
na kuitikia japo kwa sauti ya chini sana.
“hapana mimi sio bibi kaka yangu
ni maisha tu haya yamenifanya niwe hivi
tafadhali nisaidie"...
Mtu yule aliongea maneno hayo huku
machozi yakimtoka
kwanza meno yake yalikuwa ya njano kuonyesha kwa jinsi gani
ajapiga mswaki kwa muda mrefu kinywa chake kilitoa harufu mbaya
N'zi hawakucheza mbali na eneo hilo
Hafidhi akatambua bila shaka huyu mtu anaitaji msaada mkubwa sana.
Basi akakaa karibu yake zaidi na kumuuliza
“Dada nini shida? nini tatizo?
Binti yule akajiinua japokuwa alikuwa hawezi
Hafidhi akamsaidia na kumuweka sawa.
Mara kuna sauti ya binti ikasikika ikisema
“mimi kesho sipeleki ng'oo mtu ananuka kama nini bwana"
basi akatokezea kisichana kimoja kishombe
shombe bila shaka anajipenda vibaya
mno, mkononi kashika bakuri
ndani yake kuna machicha ya nazi
si akamuona Hafidhi akapaza sauti kuita
“mamaa".....
“abee Sikitu unasemaje?
“njoo uwone huku"
Hakuja mama yake pekee akaja na mabinti kama wawili hivi.
Wote wakashangaa na kutoa macho
“wee mkaka unakaa na huo mzoga usikii harufu mbaya kweli?"
mmoja kati ya wale mabinti akauliza hivyo.
Hafidhi akawatizama na kuwaambia
“wekeni mlicho mletea"
wote wakatema mate chini pohoo"...
Sikitu akaenda kumimina yale machicha kwenye lile bakuri, wakaondoka zao,
Kitendo cha kuwekwa yale machicha yule binti
Akaanza kuyala
Hafidhi akamshika mkono na kuipiga teke ile bakuri.
Binti akalia na kusema
“tafadhali kaka yangu niletee hiko ndio chakula changu"...
Sauti yake haikuwa kubwa japokuwa alijikaza kuongea sema alishindwa
“tulia Dada yangu hustahili kula
machicha wewe si mnyama wala si ndege.
Niko hapa kukusaidia niambie matatizo yako yote nitakusaidia"
Hafidhi aliongea hivyo huku
machozi nae yakianza kumrengarenga.
“samahani kaka yangu siwezi kukwambia chochote kile wee nenda tu
maana kila niliyemwambia kuhusu matatizo yangu
waliishia sehemu mbaya
Wengine wakanibaka pasipo
kuhofia hali yangu
Please wee nenda tu,
Hafidhi hakutaka kuondoka.
Binti akaanza kutoa
full story
Kwajina naitwa
Habiba Khatibu ni mzaliwa kutoka mkoani Lindi,
ni mtoto wa kwanza kati ya watoto wanne wa mzee Khatibu naweza kusema familia yetu ilijaaliwa furaha na upendo
wazazi wangu walimiliki mashamba ya mtama takribani eka
Hamsini Baba na mama walikuwa na juhudi kubwa sana,
Katika kufanya kazi ya kilimo cha mtama, ufuta, kunde, mbaazi, na halikadharika.
Pia nyumbani tulikuwa na mifugo
ya aina mbalimbali kama vile
Mbuzi, kondoo, kuku, na bata.
Maisha yatake nini tena kwetu"...

Hakika tulikuwa na furaha sana
basi nakumbuka siku moja ndani ya kijiji chetu kulikuwa na ugomvi
Mkubwa sana baina ya baba yangu, na mzee mmoja anaekwenda kwa jina la mzee Kambangwa
Walikuwa wakigombea mashamba
kila mmoja akidai lile eneo ni lake.
Baba akamtishia mzee
Kambangwa kumuuwa kwa kumwambia
“nakuapia Wallah juwa la kesho hutoweza kuliona kamwe"
sijui alitamka hivi kama vile yeye Mungu
au vipi ni kweli kesho
yake mzee yule hakuweza kuamka
kitandani ikasadikika amekufa.
Baba akaonekana ndio aliyehusika na kifo hicho si alisema, na kweli imekuwa
Matatizo yakaanza kuikumba familia yetu,
Tukaanza kuitwa sisi ni wachawi
kumbe siku zote
ukigombana na mtu usitoe kauli
za vitisho kama alivyotoa baba
inawezekana pembeni kuna
adui yenu ataitumia nafasi hiyo kuwaangamiza. Baba hakuhusika na kifo cha mzee
Kambangwa kauli yake mwenyewe ikawa kama kawasha moto kwenye nyasi kavu,
basi furaha ikatoweka
kijiji kikatutenga hata shuleni
sikuweza kwenda nikiingia darasani tu wanafunzi wote
wanatoka nnje kuogopa kukaa na
Mchawi,
siku moja nikiwa natoka kisimani nikaweza kusikia sauti kama za watu wakipanga jinsi ya kuiteketeza familia yetu.
Sikutaka kuchelewa nikawai nyumbani haraka kutoa taarifa kwa baba,
hatukuwa na namna ni kukimbia
Kijiji tukizubaa tutakufa, tuliacha nyumba yetu.
Mashamba yetu, mifugo yetu na kukimbia sisi kama sisi,
kipindi hiko nilikuwa ndio kwanza ni binti mwenye umri wa miaka kumi tu.
Tulipita pori kwa pori
msitu kwa msitu hatimae tukaja kutokezea barabarani,
tukaanza kutembea kidogo kidogo
maana tulikuwa tumechoka sana.
safari ilikuwa ndefu nisijuwe wapi tunaenda,
kila mmoja alikuwa kimya
tukafika sehemu moja hivi inaitwa hoteli tatu.
tukaweza kupata usafiri kumbe,
njaa nayo ilikuwa inatuuma
ajabu baba alikuwa na pesa nyingi sana kwenye kibegi alicho
kibeba tukafika Kilwa masoko gari ikasimama tukaingia hotelini na kupata chakula
Baba akasema hii safari tunaenda mjini kwa shangazi yenu,
Kuhusu mashamba na nyumba si kitu mbele ya uhai wetu.
Hizi pesa ni akiba ya kila mauzo sijui tukiuza mtama mbuzi basi pesa naweka
kwenye akiba,
Nilifurahi sana kupata baba mwenye akili kama huyu
tofauti na wengine wakipata
pesa kazi kunywa pombe au kuhonga Wanawake,
hatimae safari ikaendelea na kufika jijini
Dar es salaam,
Tukaenda mpaka nyumbani kwa shangazi tukapokelewa kwa furaha kubwa
Shangazi alikuwa kajenga nyumba yake kubwa tu maeneo ya
mtoni kwa Aziz Ally, tukaishi hapo nikapelekwa kuendelea na masomo katika shule ya msingi
Temeke mwisho, furaha ikarudi upya tukasahau kila kitu kuhusu shida
baba alifungua
biashara za hapa na pale
“mke wangu mpendwa hatimae nimenunua nyumba yetu"
Baba alitamka hivyo wakati tukiwa
sebuleni tukipata chakula cha usiku
kila mmoja hakuweza kuamini,
Shangazi akamuuliza
“unasema kweli kaka au unataka kufurahisha baraza tu?"

“ni kweli dada yangu kama hamuamini tuombe uzima kesho
Asubuhi na mapema twende mukaiyone"...
Kila mmoja alifurahi nikasema
huyu ndio baba yangu wa pekee hakuna kama yeye hapa duniani,
Kesho yake tukaenda kuitazama hiyo nyumba mama alifurahi
mpaka furaha yake ikapitiliza na kulia
Maisha yakaanza tukiwa kwenye nyumba yetu nakumbuka siku
moja wakati natoka shule niliweza kumuona baba
Akiwa amekumbatiana na mwanamke sikuweza kufahamu yule mwanamke ni nani yake,
Basi nikamezea rohoni na kurudi zangu nyumbani, nilitaka kumwambia mama
sema nafsi ikawa nzito kutamka kitu kama
hiko, nikabaki kimya
Ghafla furaha nyumbani ikaanza kutoweka
niliweza kugundua hilo
baada kuliona tabasamu la
mama sio lile nililolizoea yani
alikuwa akitabasamu kwa kujilazimisha tu,
“mama mbona unaonekana kama hauna furaha vile, vipi unaumwa? au kuna tatizo?
Mama hakunijibu kitu zaidi ya
mchozi kumtoka nikamfuta kwa kutumia kiganja changu cha mkono
“basi usilie mama yangu tambua mimi kwasasa sio mtoto tena nishakuwa niambie tu".....
Akanishika kwenye paji langu la uso na kuniambia
“Habiba mwanangu tambua kitu kimoja
wewe ni bado binti mdogo sana
usiombe ukikuwa ukaja kukutana na matatizo kama haya.
Hakika ni mateso makubwa sana moyo wangu unaungua
mwanangu, mama akaanza kulia
nilitumia nafasi hiyo kumbembeleza
hali ya mama ikaanza kuwa mbaya
akakonda
siku moja nikiwa ndio najiandaa kufanya mtihani wa taifa darasa la
Saba mama akaniita chumbani kwake
na kuniambia
“Habiba mwanangu tambua kitu kimoja mama yako sina muda wa kuishi tena hapa
duniani please mwanangu
shika hii bahasha ndani yake
kuna barua usiisome mpaka siku
Ambayo utakuja kupata mume
au siku ambayo utakuwa umeingia Reba
kwenda kuzaa please nakuomba
tafadhali usisome kwa sasa".
Baada kuniambia vile nikamuahidi sitoisoma
akaomba kupumzika,
nikamfunika shuka vizuri sikufahamu kama ameomba kupumzika milele
laiti ningejuwa nisingemuacha mama ndani peke yake"...
Hihihihihihi!!!
haaaaaaahii".....

Mpaka kufika hapo
Habiba akaanza kulia, japokuwa sauti yake ilikuwa bado ipo chini sana ilisikika vyema masikioni mwa Hafidhi, akamshika na kumbembeleza
“pole sana Dada yangu usilie yote ni mipango ya Mungu
sote kwake tutarejea endelea kunisimulia"...
binafsi Habiba akafahamu ni kweli
Hafidhi anania ya kumsaidia.
Akaendelea
“basi nilitoka chumbani na kwenda kuhifadhi ile barua sehemu salama,
nikaenda zangu kucheza
Mdako na marafiki zangu kina
Sara, Zuwena, Jasmin, yani nilikuwa na marafiki wengi tu, mpaka ikatimia saa nane mchana nikarudi nyumbani kupika
ugali nikaanda kila kitu nikaenda kumtizama mama chumbani kwake
nikamkuta bado kalala vilevile
nikamsogelea na kumuamsha ikawa ndio amsha na wewe kumtikisa na kumwita
kote mama hakuweza kushtuka
hata kidogo.
Nikatoka nnje na kumwita shogaake kwa kumwambia
“mama Jasmin mbona mama yangu hataki kuamka"....
Nae haraka akaingia ndani na kuanza kumtikisa kwa kuita
“mama Habiba, wee mama Abdully
amkaa"...mwisho akaangua kilio
nilijiuliza sana kwanini analia kumbe mama yangu kashaiyaga dunia.
tulilia sana hasa baba
ndio alikuwa ashikiki kwa kulia, ndani ya
msiba huo sikuweza kuwaona ndugu zangu yani wadogo zangu
si Abdully wala
Mariam hakuwepo hata mmoja
tukaenda kumzika mama yangu mpendwa,
Mitihani ya kumaliza darasa la saba sikuweza kuifanya, ikatakiwa nirudia mwaka unaofata
walimu na wanafunzi wenzangu walinipa pole.
hata haijafika wiki moja tokea tumzike mama baba akaleta mwanamke
mwingine ndani na kunitambulisha ndio atakuwa ni mama yangu mpya,
nilijiuliza sana
inakuwaje hata machungu bado hayajapoa leo hii baba kaleta mrithi wa mama ndani.
Sikuwa na jinsi kukubali matokeo
maisha yakazidi kusonga
“hivi baba kwani kina Abdully wako wapi
mbona uliwachukuwa ukidai wanaenda kusoma shule ya boarding mpaka leo
siwaoni
hata kwenye msiba wa mama hawakuja?"
Nilimuuliza hivyo baba
ajabu hakunijibu kitu akaninasa kibao
“Shika adabu yako maswali
gani hayo ya kijinga, wee
Fatuma huyu mtoto umfundishi adabu ehee?"
Baada kunipiga alimuuliza hivyo mama wa kambo basi akatoka jikoni akiwa kashika
mwiko akaja kunichapa nao.

NAOMBA SAPOTI, KUNA MATANGAZO(ADS) YANAJITOKEZA KWENYE APP YETU, LIMOJA LINAJAA KWENYE KIOO CHAKO JINGINE LINANG'ANG'ANIA HAPO CHINI KABISA, BONYEZA JAPO MARA 2 AU 3 KILA UKIFUNGUA SIMULIZI HIYO ITANIPA NGUVU YA KUENDELEA ZAIDI NA SIMULIZI ZETU🙏🙏

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO



USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA TANO

Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni