MZOA TAKA (3)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA TATU
“Vipi tena mwenzetu una tembea macho juu juu una tatizo gani?"
sikuweza kumjibu kitu zaidi ya mchozi kunidondoka pasipo
kujitambua akanishika mkono na kuniomba niingie kwenye gari
aina ya Benzi.
SASA ENDELEA...
Nikazunguka upande wa pili wa gari ili nipande nafsi yangu ikasita baada kuona kwa jinsi ile gari ilivyo kuwa safi wakati huo Joyce kashapanda akaniuliza “vipi
tena mbona hauwingii kwenye gari?"
nikamjibu “kusema kweli siwezi kupanda nitakuja kuchafua siti bule!!! akacheeka na kuniambia embu
Salumu acha ushamba bwana ingia twenzetu kama viti vikichafuka vitaoshwa tu wee usijali ingia tu,
basi nikapanda ndani ya ndika yenye kiyoyozi sijui mnaita kipupwe huku mziki laini kutoka kwa west life unao kwenda kwa jina la my love ukilindima na
kunifanya nijisikie burudani, kila mmoja akawa kimya sikuweza kufahamu
Joyce anawaza nini zaidi ya kuwa makini kuendeesha gari basi safari ikazidi kusonga nisijuwe wapi tunakwenda na kigiza nacho ndio kina jongea, tukafika
sehemu moja
sijui hotelini au vipi akabaki gari maana hiyo sehemu kulikuwa na magari mengi tu yakishua basi tukashuka na kuingia ndani ya hoteli hiyo
“whaoo
Joyce huyoo, ni sauti ya binti mmoja akija mbio kumkumbatia Joyce
hakuwa peke yake kulikuwa na kikundi wanaume kwa wanawake basi
Joyce akafanya kunitambulisha ya kwamba mimi ni rafiki yake basi kila mmoja akanipa mkono wa bashasha nikaweza kukaa na kuagiza kile ambacho kina nifaa
furaha ikaongezeaka zaidi na kunifanya niweze kusahau mawazo ya kuachwa na Mwanaidi
kuna muda Joyce akanyanyuka sijui kwenda chooni au vipi mi sijui zikapita dakika kama tatu hivi tokea Joyce ainuke pale nikajikuta naguswa begani kucheki ni
muhudumu wa hoteli ile nikamuuliza “nikusaidie nini Dada yangu?"
akanijibu ya kwamba “unaitwa kule nnje na mwenyeji wako,"
nikajuwa bila shaka Joyce anaitaji tuondoke basi nikajinyanyuwa na kuwaaga wale nilio kaa nao meza moja nikatoka nnje nikakuta hali ya ukimya flani hivi
nikaisogerea gari kitendo cha kuifikia tu gafla nikapigwa na kitu kizito kichwani kikitokea nyuma yangu nikayumba yumba huku nikiona dunia inazunguka
mwishoe nikaenda chini
nisijuwe kinacho endelea,
ni sauti ya watu wakiulizana na maji kunimwagikia ndio ikanifanya nifumbuwe macho yangu japo kwa shida sana maana maumivu ya kichwa yalikuwa bado
hayajapoa nikajaribu kujinyanyua hamadi Mungu wangu nina bokxa tu mwilini mwangu sina nguo nyingine yeyote ina maana baada kupigwa nilivuliwa nguo au
wali nitupa vibaka ndio wakanisaura sikuweza kupata jibu zaidi ya mchozi kunitoka tu nikajiinua huku nimeshikilia sehemu zangu za sili huku nikitetemeka
kuna baazi ya watu wakasema mchawi kila mmoja akasema lake mwisho wakajadiliana nipelekwe kituo cha police,
nikanyanyuliwa msobe msobe huku nikipigwa mikofi ya maana na vijana wenzangu wasio kuwa na utu hata chembe “kijana mdogo unakuwa mchawi oyaa huyu
sio wa kumpeleka police dawa yake ni moto tu nikawashwa ngumi mitama na makofi nilipigwa kwa kugombewa kama vile mpira wa kona bahati nzuri police
wali shapewa taarifa kwa kukamatwa mchawi maeneo yale wakaja kunitoa mikononi mwa wananchi wenye hasira kali nikapigwa pingu damu chapa chapa ziki
nivuja nikapelekwa kituo cha police pale manzese na kusweka ndani hata huduma ya kutibu majeraha yangu sikupewa nikabaki kuugulia maumivu tu huku
nikijiuliza maswali mengi pasipo kupata majibu,
why me?" kwa nini mimi?
eee Mwenyezi Mungu ni kipi nimekosea katika dunia hii ni dhambi gani kubwa niliyo ifanya mpaka nateseka hivyo
furaha yangu ya muda mateso yangu yasio fika kikomo why?"
nilijiuliza maswali tu,
Salumu nililia maumivu yakazidi kunizidia Joyce nimekukosea nini mimi je nilifanya makosa kukuokotea kipochi chako na kukuletea
hii ni mara ya pili sasa napigwa Joyce nijibu basi unaitaji nife?"
nilijiuliza mwishoe mchozi unanimwagika dahaa yapata saa kumi alasiri nikasikia afande akilitaja jina langu kwa kuniita nika jinyanyua kiuvivu uvivu na
kwenda karibu na nondo za sero sikuweza kuamini macho yangu baada kuwaona washikaji zangu wakiongozwa na
Madebe wamefika pale kituoni hata wao wakastuka baada kuniona nikiwa katika hali ile,
Madebe midomo ikawa inamtetemeka kwa hasira huku akitamani kupiga hata afande basi nikatolewa
nikiwa ndani ya boksa tu iliyo lowana damu alicho kifanya
Madebe ni kuivua jeanse yake akabaki na bukta aina ya jenzi akanipatia ile suruwali niivae nikaivaa kisha
Sheby akavua T-shirt yake na kubaki na vest akanipa T-shirt nivae baada maandikishiano wakaondoka na mimi ndani ya daladala nikawapa mkasa mzima huku
nikimtupia kila laana Joyce na kumuuliza
Madebe wamejuwaji kama mimi nimekamatwa na tena nipo kituo cha police manzese?"
Madebe akajibu unajuwa jana usiku tulikuwa tushajiandaa kwenda kumteka yule boya sasa tukiwa tushakusanyika pale maskani tukawa tunakungojea wewe tu
muda ukazidi kwenda pasipo wewe kutokea tukaona kama vipi tukutimbie maguu mpaka maghetoni baada kufika pale tukakukosa tukachekecha akili pasipo
kupata jibu,
na tusingeweza kufanya uvamizi pasipo kuwapo wewe tukarudi maskani yapata saa tano hiyo baazi ya washkaji wakasepa kwenda kulala huku wakisema ishu
imebuma
baada kukaa kitambo kidogo tukaona kuna gari ikija kwa kasi pale maskani tukajuwa labda maafande kila mmoja akasepa kimtindo wake ila mimi na
Shaibu tukanyuti chemba kidogo ile gari aina ya benzi macho ya paka ikafunga break kwa kasi sana tukaweza kumuona msichana mmoja hivi akishuka huku
akipiga kelele “jamani!!! salumu nisaidieni!!! salumu jamani anakufaa!!!!
baada kusikia akitaja jina lako
Salumu na akisema unakufa tukaamua kujitokeza baada kutuona akaja mbio na kutuambia “twendeni mkamsaidie
Salumu watamuuwa jamani!!! tukapanda kwenye gari yake kwa kasi akaendesha mpaka kwenye hoteli ya ubungo plaza pale baada kupaki tukashuka kucheki eneo
la tukio hakuna kitu kwa hasira zangu nikamkunja yule msichana na kumuuliza ni nani kamfanyia kitendo hicho
Salumu?"
maana kengere ya hatari ilishanigonga kichwani na kuhisi utakuwa
Salumu ni wewe tu hakuna mwingine,
kwa uwoga akanitajia
“kusema kweli mi sijui ila nahisi atakuwa Tonny tu ndio kafanya hivi,"
“Tonny ndio nani na anahishi wapi?"
“ni mpenzi wangu anaishi ilala,
“haya tupeleke kwa huyo kibwengo nikawapigia cm wana wafanye mchongo tukutane ilala hakuna aliye uliza maana kila mtu alishajuwa kimenuka
tukafika ilala boma kabla hatujashuka kuna gari akaja kupaki na kushuka jamaa flani hivi kisharo kikiwa kinaongea na simu ndio mchinjeni kama vipi huyo boya
mshamba hawezi kuja pale na demu wangu chinja kabisa sikutaka kusubili kuambiwa ndio yeye au sio nikashuka kwenye gari na kwenda kumtia roba ya mbao
akajitahidi kukuruka wapi akaishia kujamba tu nikaenda kumtia kwenye buti ya gari yake nikapanda safari ya kumpeleka chimbo ikaanza tukapishana na wana
wakiwa ndani ya tipa tukawapa ishara warudi basi baada kumpa kibano cha maana akawapigia cm vijana wake na kumtajia wapi wamekutupa basi tukamuachia
kwa makubaliano ya kwamba iwapo tukakukuta umekufa na yeye ajichimbie kaburi mapema
tukaja pande za manzese baada kuulizia ulizia tukatonywa upo kituo cha police pole sana kaka,
wakati
Madebe ananisimulia ile story ndani ya daladala kuanzia abilia konda hadi dereva mchozi ukawatoka na wengine kusema “sijawai kuona marafiki wenye
kupendana na kusaidina kama nyinyi ni moja kati ya vijana wa kuigwa sana poreni sana
Aseee!!! dahaaa kila mmoja akatupa pore baba mmoja akajitolea kutulipia nauli daladala nzima maana dahaa
sikuweza tena kurudi kwenye ile nyumba ya mama
Mwanaidi nikawa naishi kwa Madebe maana ni zaidi ya ndugu japo kuwa ni rafiki yangu tu baada kupita siku kama nne hivi nikaingia kitaa na mkokoteni wangu kusomba taka Madebe yeye
ana mishe mishe zake tu anazielewa mwenyewe nikiwa bado nazisomba taka na kuzipakiza kwenye mkokoteni nikasikia vicheko vya kimbea tu “ohoo jamanii
hahahaha mzoa takataka utazoa hadi mavi mwaka huu, japo sikutaka kuwatizama wale mabinti wanao sema vile ila sauti ya mmoja wao sio ngeni masikioni
mwangu hakuwa mwingi ni
Mwanaidi nikainua uso wangu na kumtizama tulipo tizamana tu akaibetua midomo yake na kutema mate chini huku akiachia zinga la msonyo “nyooo*** lione
sura mbayaa kaa tako la mzee," leo hii Mwanaidi ananiambia mimi hivi dahaa nikashika mkokoteni wangu na kusonga nao mbele kufika sehemu hivi nikasikia
kama kelele za ugomvi hivi nikasimamisha mkokoteni wangu nikanyata kwenda kufahamu washkaji wanagombania nini hasa nikasikia
“oyaa acha uboya ujuwe unajuwa mpaka sasa nimepoteza shi ngapi broo?"
“hiyo pesa yako ya madafu tu unitishi lolote dogo kwanza yule
Mwanaidi nishamuendea kwa babu kashafanya yake kwa kumuweka kwenye kifuu yule boya mzoa vinyesi sijui nini kabwaga kama zigo la kuni
nikastuka kusikia vile!!!,
Kitendo cha kusikia ya kwamba yule akijitapa na kujisifu kuwa
Mwanaidi kasha muweka kiganjani kwa kumuendea kwa babu sijui huko tanga ndipo nikaweza kupata picha
Mwanaidi ninae mfahamu mimi sio huyu wa sasa ime kuwaje abadilike ghafla vile na kuniona mie ni kinyaa si lolote si chochote,
nikajiuliza maswali mengi sana pasipo kupata jibu hata moja nitawezaje kurudisha penzi langu kwa
Mwanaidi liwe kama zamani nikajiambia habari hizi nimfikishie ndugu yangu Madebe huwenda ata nishauri nini cha kufanya nikaufata mkokoteni wangu niweze
kusonga na njia kitendo cha kupiga hatua kazaa tu nikakutana na yule bibi akiwa ana okota chupa za maji uhai kwa kuzitia kwenye kiroba,
nae baada kuniona akaja kwa mwendo wa kujikongoja na kuniuliza “vipi mjukuu wangu hujambo?"
nikamjibu “sijambo bibi shikamoo, “marhabaa mjukuu wangu basi nakumbuka majuzi tu uli nipa msaada kwa kuni peleka kwa mama ntilie kule yani sina cha
kukulipa baba yangu ila shukrani sana akubaliki sana mjukuu wangu, baada kusema vile akakiinua kiroba chake cha makopo na kuanza kuondoka nikabaki
kumtizama tu huku niki tingisha kichwa
kwa masikitiko moyoni nikaingiwa na imani kwa kumuita “bibi!!! aka geuka kuni tizama nikaenda mbio kumfata binafsi nikaweza kuona kwenye paji lake la uso
mchozi ukimdondoka,
“bibi mbona unalia?" nili muuliza hivyo huku nikimfuta chozi kwa kiganja cha mkono wangu, kitendo cha kumuuliza ni kama nime fungulia bomba la vua
nikajisahau kabisa kama mkokoteni nime usimamisha balabalani
“bibi niambie kinacho kuliza ni kitu gani?"
nieleze bibi hakuwa tayari kuinua mdomo wake kuniambia kile ambacho kili mfanya alie
gafla nikasikia honi ikipigwa kwa fujo nikaja kutambua ni gari ikiomba njia nikaenda mbio kuutoa mkokoteni kabla sija ufikia zikashuka njemba mbili mmoja wao mkononi kabeba chenzo
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA NNE
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni