MZOA TAKA (2)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA PILI
Sikuweza juwa kilichoendelea nikaja kustuka baada kumwagiwa kitu cha baridii nikaweza kufumbua macho yangu na kuhisi maumivu kila maeneo nikicheki pembeni nikaweza kumuona Mwanaidi akiwa ameshika bakuri na kitambaa kumbe nilikuwa nipo chumbani kwangu nimelala chini ya mkekaSASA ENDELEA...
Baada Mwanaidi kuniona nimefumbua macho ndipo akatabasamu huku akijifuta machozi akapaza sauti kwa kuita "Madebe kaka,' mlango ukasukumwa ndipo akaingia Rafiki
yangu kipenzi Madebe ndio ambaye alinichukuwa kule kwa Sele nikaenda kuishi geto kwake mpaka siku niliyo amua kujitegemea kwa kuondoka kwake japo
hakupenda kwa kuniambia "kaka bado hujapata mchongo wa maana mi naomba ukae tu hapa mpaka unnue godoro kitanda na vinginevyo ndipo uame,'
nikamwambia usijari kaka hata chini nitalala tokea niondoke kwake tukawa tukikutana kijiweni na kupiga story za hapa na pale sasa leo hii washkaji wanashuhudia niko hoi sio kitandani bali kwenye mkeka Madebe akanisogelea na kuniuliza
“Salumu kaka ni nani amekutendea hivi?"
nikawa sina jibu zaidi ya mchozi kunichuruzika tu kwani sauti haikutoka japo nilijitahidi kuzungumza nikashindwa Madebe kwa hasira alizokuwa nazo akaishia
kupiga ngumi ukutani kwa kusema "shit! kudadeki mshkaji hawezi kuzungumza kitu kubabeki tungewafahamu hao waliomtendea hivi jamaa yetu. Wallahi
kingenuka leo hii
Nikiwa nimelala chini ya mkeka siwezi kunyanyuka wala kupapasa popote kwani mikono ilikuwa mizito sana mpaka nikajishangaa wale vibaka wamenipigaje
mpaka nimekuwa hivi yani nisiweze hata kunyanyua mdomo. Kuzungumza na mtu marafiki zangu kina madebe wakishilikiana na Mwanaidi waliendelea
kunitizama na kunipa huduma za hapa na pale kila siku niliweza kumsikia Madebe akisema "one day jamaa atapona tu na siku atayo nyanyua mdomo na kuwataja
walio mtendea hivi nitakufa na mtu siku hiyo hiyo
siku zikakatika yapata mwezi sasa nikiwa kitandani kwani madebe hakupenda nilale chini ya mkeka akaniletea kitanda cha 5x4 ndio nikawa nalala hapo siku hiyo
Asubuhi nikaweza kusikia mabishano nnje kati ya Mwanaidi na mama yake huku mama yake akisema
“utake usitake utaenda kama mimi ni mama yako niliekuweka tumboni miezi 9 utaenda tu nyau wee!!!
"hata kama umeniweka tumboni mgongoni au wapi siwezi kuolewa na Mwanamme nisiempenda na tena ukiendelea kunilazimisha huyo mwanaume ataipata pata
naweza nikamkata kata hiyo anayo jivunia kuitwa mwanaume"
“thubutu uwezo huo huna huyo nikidume shababi sio huyu mzoga wako ulio lala kitandani!"
dahaa mchozi ulinitoka kwa kusikia naitwa mzoga jamani binaadamu ndivyo walivyo,
“sikia wee mzee nikwambie kama mzoga ni mumeo na wazazi wako,' "haa yani Mwanaidi umefikia hatua ya kumwita baba ako na bibi na babu yako mizigo sio
wee mtoto ntakuachia radhi Ohio",,,,, nikasikia vishindo vya kukimbizana kikili kakala huku Mama Mwanaidi akipiga kelele "jamaniiii majilaniii nakufaa njoeni
mnisaidieee!!!
nikatamani kutoka kwenda kusaidia nikashindwa ndipo sauti zikasikika za majilani
"wee Mama Mwanaidi vipi embu fungua mlango kwanza, "sifungui Mwanaidi anataka kuniuwaa kusikia eti Mwanaidi anataka kumuua mama yake
nikajikakamua kusimama mpaka nikaweza cha ajabu nikasimama kabisa nikapiga hatua mbili tatu na kupaza sauti kwa kuita "Mwanaidiiiiiii
iii...huku nikitoka kufika mlangoni tukagongana vichwa puhuu kumbe yeye baada kuisikia sauti yangu akawa anakuja mbio tukabaki kutizamana kila mmoja
akihema si tukaanza kucheka,
Ha!ha!ha!ha! Akaniuliza
“baby ni wewe au?"
“ndio mimi dear tukakumbatiana kwa furaha huku machozi yakitutoka binafsi hakuna aliye tegemea mi kupona ghafla vile wakati
Madebe anahangaika kutafuta pesa nipelekwe hospital kwani pesa haikuwepo nikaenda kuoga nikaandaliwa chakula nikala
Mwanaidi akaniita Salumu my dear" nikaitikia,
“naamu Mwanaidi niambie”
akawa anajing'ata ng'ata kucha huku akilembua macho yake kisha akanitamkia
"nakupeenda naitaji uwe baba wa watoto wangu Salumu!"
kwanza nikashituka si akaja kunikumbatia na kukutanisha midomo yetu dahaa toto midomo lainiiii kama naramba sufi vile ghafla mlango ukasukumwa wote
tukageuza shingo zetu kuangalia mlangoni.
Majanga hakuwa mwengine
zaidi ya Madebe
akataka kurudi nnje maana alicho kiona hakuamini
macho yake.
Yani mgonjwa
aliye muacha kitandani hawezi kusimama wala kuongea
leo hii kama miujiza anamkuta yupo kifuani kwa Mwanamke anazinyonya chuchu,
nikainuka kutoka
pale kitandani na kwenda kukumbatiana nae maana alikuwa anafikicha fikicha macho
“eee Mungu baba kila jinsi ya sifa njema ni zako tunakushukuru kwa kuweza kujibu maombi yetu japo hatuingi Msikitini kufanya ibada yeyote ile ila
umeyapokea maombi yetu",,,,,
ni maneno
ya Madebe
huku machozi
yakimtoka
nikamfuta machozi na kumwambia
“hakika Mungu ni mwema sana!"
Tukakaa chini na kuanza kuwapa full story kwa kile kilicho nitokea,
“dahaa pole sana kamanda wetu ila kisasi lazima kifanyike. Usiku huu huu tunamteka yule boya kisha tunamzamisha kwenye Mjumba ataeleza tu cha kwanza
ataje pesa ziko wapi kingine awataje wenzie wote kuanzia sasa tunakinukisha kitaa au sio?"
Nikaitikia,
“ndio kaka" basi kila mmoja akagonga tano na kusepa zao. Ndani ya chumba nikabaki mimi na Mwanaidi tukabaki kuangaliana kama vile, majogoo yanayo
tamaniana kupigana"
nikamtekenya kwenye mbavu mtoto wa kike akashituka huku sauti ya kuguna ahaaaaa,,,mi stakiii
nikamshika kiunoni na kumtekenya zaidi siwezi kukwambia nili enjoi vipi tunda la binti yule kigori usiku kucha ali
lala kwangu,
maana mama yake hakuwepo siku hiyo nikawa mimi ni kama baba mwenye nyumba
wapangaji walio
tuona nikienda bafuni
kuoga na
Mwanaidi wakabaki kusonya tu huku wakipindisha midomo yao kama kishuzi.
Siku hiyo nikiwa kitaa cha temeke mikoroshini
nazoa takataka kusema kweli sikuwa na vitendea kazi
kama Groups au choteo
la kuzolea taka zaidi ya kunyanyua migunia viroba na matenga nikiwa nishajaza rumbesa la taka huku njaa ikiniuma vibaya sana maana mpaka saa saba mchana
sikuweza kutia chochote kitu tumboni kwangu.
Nikiwa najikakamua kusukumiza mkokoteni. Ghafla nikasikia sauti nyuma yangu
“za saa hizi mjukuu wangu?"
nikasimamisha mkokoteni na kumuangalia huyo anaye nisalimia ni nani?.....
kabla ya kumuitikia alikuwa ni Bibi kikongwe sana maana hata kusimama vyema hakuweza zaidi
ya kuupindisha mgongo wake sijui kiuno kinamuuma au. Mkononi ame beba mkongoja pamoja na kimkoba flani hivi, nikamuitikia
“sijambo Bibi yangu shikamoo!!!
akaitikia “marahabaa Baba nilikuwa naomba msaada wako baba hapa unionapo tokea jana usiku sijatia chochote kitu tumboni kwangu
nahisi utumbo
una nikata kata!"
nikabaki kumkodolea
macho tu na kuwaza hapa nilipo mi mwenyewe mfukoni nina shilling mia tano tu kingine
sijala tokea Asubuhi
sasa huyu bibi nitamsaidia vipi"......
nikamtizama
vizuri na kuona
maeneo ya tumboni kwake
kafunga jiwe kwa ajili ya kuzuia njaa
nafsi ikanisuta kwa kuniambia
Salumu embu mpe msaada huyo bibi
ndio wewe una njaa ila hukufunga jiwe kuzuia njaa tena unasukumiza mkokoteni wenye mizigo mizito
huyo bibi kashindwa
kustahamili mpaka kafunga jiwe,
nikajikuta namwambia “bibi nifate japo alitembea kwa shida sana akanifata mpaka kwa mama Somoe na kumuonyesha sehemu ya kukaa baada Bibi kukaa huku
akipepesa macho na kujiramba ramba kwa kutamani msosi maana aliwakuta wateja wengine wakigonga menu
nikamshika mkono mama
Somoe na kwenda nae chemba kidogo
“ehee vipi tena baba wewe mbona tunavutania pembeni?"
“ahaa hamna kitu sema nini!!!
“ndio nakusikiliza boss wangu,
“sasa mimi hapa sina kitu mfukoni nina jero tu so kama vipi mpatie msosi yule bibi kisha jioni nitakucheki,
“hamna shida boss wangu,
basi akaenda kumuandalia chakula na kumtengea yule bibi
binafsi alikuwa na njaa sana akakifakamia chakula chote,
nikaondoka na mkokoteni wangu kwenda kumwaga takataka dampo
yapata saa kumi na moja jioni niko masikani na kina
Madebe huku tukipiga story za hapa na pale
“oyaa Salumu kaka ule mchongo wetu tumeupanga leo lazima ufanyike time ya kama saa nne usiku hivi tunavamia pale na kumchomoa yule dogo kitu
nitakacho mfanyia atajuta kwa nini kazaliwa mwanaume
pumbavu zake,
ni maneno aliyo kuwa akiyatoa
Madebe mpaka mwili ukanisisimka kwa vitisho vile,
nikatoka zangu maskani na kurudi zangu ghetto cha ajabu nikakuta chumba changu kufuri sio ile ya kwangu nikatoka mpaka uwani na kumkuta
Mwanaidi akiwa amelala mapajani
kwa Mwanaume huku akimchezea kidevu na yeye akichezewa nywere na kushikwa shikwa katika maungo yake nilibaki kuduwaa tu
na hata alipo niona
Mwanaidi hakustuka wala kujali lolote
nikasikia sauti ya kicheko
cha kimbea kikitokea nyuma yangu
“aha!ha!ha!ha warereeee!!! utaishia kula kwa macho tu mnuka uvundo,
ni maneno ya mama
Mwanaida na kunipushi huku akisema “embu nipishege mie!!!
nikayumba kabla ya kuushikilia ukuta
Mwanaidi kwa kuniumiza roho zaidi akanyonyana denda na yule jamaa mbele ya macho yangu
aseee!!!
dahaa inauma sana hii kidume nikajikaza baada kuikumbuka
kauli ya mama akiniambia
“mwanangu
Salumu katika dunia hii usimuamini mtu yeyote yule zaidi ya mimi mama yako na tambua ya kwamba wanawake ni kama nyoka muda wowote ule anaweza
kukubadirika
kwahiyo kuwa makini sana mwanangu,
nikatoka nikiwa sijui naenda wapi maana binafsi nilikuwa nime changanyikiwa si kidogo
nikastushwa na mlio waoni maana nusu nusu nigongwe nikajikuta nadondokea kwenye mtaro wa maji machafu kwa presha dereva wa ile gari aina ya Benz
macho ya paka
akafunga break gafla
akijuwa tayali
kashauwa akashuka na kuja mbio kwenye mtaro nikawa ndio natoka macho yetu yaka
gongana na binti mrembo huwa na penda kuwaita
Jacklin wolper maana hapa kwetu sijaona dada mrembo kama huyu sijui wewe katika macho yako unamkubali nani ila wolper kauteka moyo wangu,'
binti huyu hakuwa mwingine bali ni
Joyce hata yeye alipo niona akabaki kushangaa “whao!!! si
Salumu wewe?" Nikamuitikia kwa kichwa huku nikijiandaa kutoka kwenye mtaro akanipa mkono kwa ishara ya kunivuta nikampatia ile ananivuta tu nikajikuta
namvuta yeye
na yeye akaja vupuu kwenye mtaro na kujikuta mimi juu yeye chini huku face zetu zikiwa karibu zaidi akaanza kujichekesha kwa aibu watu walio weza
kushuhudia mchezo ule wakahisi muvi zetu za kibongo
tu maana gari hata haijanigusa
nimechumpa mtaroni wakabaki wakicheka tu kidume nikatoka na kumpa mkono
Joyce akatoka huku akisema
“kweli nimeamini Mwanaume ni mwanaume tu mi baada kukuvuta wewe kumbe navutwa mimi,
tukabaki kucheka tu kabla ya kuniuliza
“vipi tena mwenzetu una tembea macho juu juu una tatizo gani?"
sikuweza kumjibu kitu zaidi ya mchozi kunidondoka pasipo
kujitambua akanishika mkono na kuniomba niingie kwenye gari
aina ya Benzi.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA TATU
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni