MZOA TAKA (4)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA NNE
Bibi hakuwa tayari kuinua mdomo wake kuniambia kile ambacho kili mfanya alie
gafla nikasikia honi ikipigwa kwa fujo nikaja kutambua ni gari ikiomba njia nikaenda mbio kuutoa mkokoteni kabla sija ufikia zikashuka njemba mbili mmoja wao mkononi kabeba chenzo
SASA ENDELEA...
Kwanza nikastuka kwa kuya hofia maisha yangu nikarudi nyuma kwa hofu walicho kifanyia mkokoteni wangu dahaa nika baki kutumbua macho tu maana mmojawao kiunoni ana bastora,
nikajuwa bila shaka hawa si watu wazuri nika shuhudia jinsi chenzo ikikata mkokoteni wangu wa mbao si unaipata tair ta gari nazo wakazitoa upepo sijui nime
wakosea nini baada kuona mkokoteni uko nyang'anyang'a yule jamaa akatoa bastora kiunoni na kupiga risasi moja juu
kile kishindo cha mlio wa risasi kila mtu ali tawanyika eneo lile hata mimi nikakimbia na kukatiza vichochoro kazaa nikiwa nahema nikajikuta natokea njia sio
na kuingia uwani kwa watu,
kwanza nikashangaa uwani kukuta purukushani kati ya mwanamke na mwanaume sijui hata wanacho pigania siki fahamu zaidi ya kukuta timbwili tu
tmk kuna vituko usipime kwa watu wanao ishi pande hizo wana fahamu nini namaanisha maana
full ubabe kufumuana tu,
basi yule mwanamke akazidiwa nguvu kwa kukabwa roba yani mtoto wa kiume una suputu kumkaba mwanamke roba kama vile una pigana na kidume
mwenzako ikabidi yule binti aanze kupiga kelele za “jamani!!! nakufaa!!! nisaidieniii hapo kwa papo jamaa akachomoa kisu sijui ali kitoa wapi na kutaka
kumkita nacho yule binti tumboni ikabidi niutumie uwana mume wangu kwenda kuudaka ule mkono wa jamaa nikamsukutua ngumi ya shavu na kujikuta kisu
na yule binti aki viachia maana ali yumba vibaya sana kumbe nina ngumi nzito kidume basi zile kelele za yule binti zika wafanya watu wajazane eneo lile cha
ajabu sasa
amini usiamini kibao nikageuziwa mimi
na kuhisi labda mchezo tuna igiza tu kwakuwa mjumbe wa nyumba kumi alikuwa tayari kesha fika hata alipo uliza kuna nini?"
yule binti akadai mimi nilitaka kum baka ndio gafla akatokea mchumba wake na kumuokoa,
“khaa! wee binti una makengeza au kipofu wewe si ulikuwa una pigwa na huyu jamaa akakukaba roba na kutaka kukuuwa kwa kisu?"
nika jitolea kukusaidia afu eti unasema nili taka kukubaka nikataka kuondoka ila mwenyekiti akaamlisha vijana wani kamate sikuwa mmbishi nitabisha vipi
wakati ishatokea,
baazi ya kina mama wakasema “kijana ni handsome ila anaonekana hana kitu cha kumpa binti yeyote yule mpaka ana fikia hatua ya kutaka kubaka dahaa safari
ikawa moja kwa moja kupelekwa kituo cha police njia tuliyo pita yani kama bahati vile siku zote huwaga upande
wangu tukakutana na kina
Madebe wakiwa katika kukeshiana pesa baada kutoka kwenye mishe mishe zao baada kuniona nimefungwa kamba huku nikisukumizwa wakaja mbio eneo lile
“oyaa vipi mbona mme mfunga kamba dogo langu kama kuku mna mpeleka wapi?"
kuna jamaa akajibu kwa dharau
“una uliza hivyo wewe kama nani kwanza pisheni njia?"
kwa kitendo cha gafla bila kutegemea
Madebe akachomoa kisu na kumchana nacho yule jamaa kwenye mkono maana yeye ndie aliye nishika aka nikata kamba
na kumgeukia Mwenye kiti kwa kumwambia
“sasa sikia nikwambie wee mzee haya mambo yaishe hapa hapa hakuna cha mtu kabaka wala kakatwa oky,
kwa uwoga aliyo kuwa nao mwenye kiti akaitikia sawa!!!
akaniuliza “Salumu kaka wame kukamata kwa kosa lipi hasa?"
nikampa full story washikaji wakasikitika tu na kusema siku zote wanao kwenda jera sio wote wenye hatia,
Madebe akamwambia mwenyekiti hivi “sasa sikia wee mzee huyo binti si kasema ali taka kubakwa sasa leo ndio atabakwa Salumu upo tayari kubaka!!!
nika muitikia ndio niko tayari maana kale kabinti kamenitia hasira tu iwe kama Adhaakanoni tu pale amitha bachan alipo singiziwa kumuuwa amrish poor
akaenda jera
mpaka mkewe na mwanae wakafa siku ya siku anatoka jera katika pita pita zake akamkuta yupo kwenye mkutano sijui marehemu kafufuka au vipi si aka
mkimbiza na kwenda kumuuwa mbele ya mahakama.
ndio mimi sasa huyu binti lazima nimbake
Embu niambie wewe kama ndio umetendewa kitendo kama hiki uta fanyaje maana kumsaidia umsaidie afu aseme eti uli taka kumbaka,
siku zote namfananisha ndugu yangu
Madebe na yule jamaa anae cheza muvi za kibabe akiwa kama teja hivi sijui nani nikimkumbuka nitamtaja
maana tabia za yule jamaa hazi tofautiani kabisa na
Madebe hata kitendo cha kumchana kisu huyu jamaa hakumtishia yeye aka mchana tu,
“sasa Salumu huyu si una mkumbuka kwa sura au?"
“sio sura tu hadi jina namfahamu,'
“anaitwa nani?"
“ni Rahma!!! “ahaa kumbe yule binti wa kipemba wa pale dukani au sio huyo?"
“ndio mwenyewe kaka,'
“oky kitoto white afu kina leta mambo sio sasa Salumu wewe uta mngojea ghetto mi nitamleta afu wewe mwenye kiti na hawa paka wako iwe kimya yeyote
atakaye jaribu kufungua mdomo
atabakwa yeye sawa, baada
Madebe kuchimba biti la maana tuka sepa “Salumu leo benzi yako umeipaki wapi?"
yani mkokoteni wangu washikaji hupenda kuuwita benzi nikamjibu Sheby maana yeye ndie aliye uliza swali lile kwa kumwambia
“mwanangu benzi ipo nyang'anyang'a leo,
“kivipi ipo hivyo nika wasimulia mwanzo mwisho kila mmoja akabaki kushika kichwa tu na kuniomba
niwa peleke eneo la tukio sikuwa na jinsi zaidi ya kwenda nao
temeke tuna ushilikiano basi kila mmoja aka beba kifaa cha mkokoteni tuki ziacha takataka pale
“nikwambie kitu
Salumu,' “ndio niambie kaka Madebe,
“unajuwa wewe ni kama mdogo wangu wa damu kabisa sipendi uwonewe sipendi uumie ndio maana
mpaka time hii nahofia kuku jumuisha katika michongo yetu japo naishi na wewe huku niki fahamu nahatarisha maisha yako
nazunguka kila day kutafuta kazi kwa ajili yako nakosa kwa kifupi tu mimi ni jambazi muuza madawa ya kulevya nakaba nabaka yani kila aina ya unyama mimi
nisha ufanya, kwa yale maneno ya Madebe nikaogopa zaidi"...
Kauli ya madebe kuniambia kuwa yeye ni jambazi muuza madawa ya kulevya na ubakaji ili nifanya nishituke sana. Na kuanza kutetemeka kwa uwoga.
Akaniambia
“Salumu mdogo wangu huna haja ya kuniogopa, kumbuka mimi ndio mtetezi wako. Ngojea nikupe story moja hivi alafu wewe mwenyewe utanipa jibu kwa nini
nimekuwa hivi.
Kipindi natoka kule kijijini kuja town kusaka maisha nilipitia njia nyingi sana za hatari mpaka kufikia hatua ya kuhatarisha maisha yangu niliweza kufikia kwa
jamaa yangu anae kwenda kwa jina la Santos nikawa naishi nyumbani kwake kwa muda tu huku nikisaka michongo ya hapa na pale basi siku moja nikasikia kuna
kazi maeneo flani hivi kwa mchina kwakuwa sikuwa na ishu yeyote nikajihimu asubuhi na mapema. Kwenda kujalibu bahati yangu.nitapatapata hiyo kazi au
vipi".nilipofika nikakuta vijana kwa wazee yani hadi wanawake wapo tukawa tukingojea geti lifunguliwe ili tuingie ndani
basi muda ulipo fika geti lika funguliwa kila mmoja akaingia kwa sie wageni ikabidi tuchaguliwe kuingia kwa bahati nzuri nikawa ni mmoja kati ya walio
chaguliwa kuingia kufanya kazi haikuwa kazi kama kazi zaidi ya kufungua vifuniko vya chupa za maji uhai na kutoa zile nembo zake na kujaza kwenye viroba
kisha kwenda kusagwa kwenye mashine iliyoko humo japo yule mchina alikuwa ana tutukana kwa kiswahili chake kibovu pindi anapo kuona unavuta pumzi au
kunyar
baada hapo tuka hamia kwenye madumu vidumu na ndoo yani takataka za kila aina yani mikojo mavi vyote tunakutana navyo alafu hakuna vitendea kazi kama
groups au viziba pua hakuna basi tukafanya kazi katika mazingira hatarishi ilipo fika time ya kula sikuweza kuamini huo msosi ulivyo pikwa na kuwekwa
kwenye beseni mboga si mboga ipo kwenye kopo binafsi nili shindwa kula
jioni ilipo fika kila mmoja akalipwa kiasi chake cha pesa yani shilling 4000 tu basi siku zikazidi kusonga huku manyanyaso yakiongezeka kule kazini yani huyu
mchina akajiona kama vile yuko nchini kwao anapo jisikia tamaa za kimwili basi atamwita binti yeyote yule kwenye mjumba wake na kumaliza haja zake siwezi
kusahau hii japo ilikuwa ajali kazini lakini ni unyama wa kiasi gani
tukiwa katika mashine ile ya kusaga yale makopo una yaingiza hivi kama kwenye pipa afu una yashindilia kwa kutumia madumu sasa kuna jamaa mmoja hivi ana
itwa Hamisi aka yashika yale madumu na kukandamizia basi ghafla, madumu yakavutwa na upepo wa mashine na kujikuta ana sagwa mikono yake ingekuwa sio
kumvuta sisi angeenda kusagwa mzima mzima akatoka akiwa kibubutu hana tena viganja vya mikono damu zika mwagika maeneo yale tukajitolea kumpa
huduma ya kwanza ili kuzuia damu kuvuja zaidi maana alijikuta anapoteza fahamu kabisa tukapaza sauti kumwita mchina kwa kumfahamisha kuna tatizo huku
dahaa hata hakujali ndio kwaanza yupo ndani ana jilia raha na binti aliye mwita siku hiyo. Ikabidi tujitolee kumuwaisha hospitali mwenzetu
ndugu zake wakafika sisi kurudi kazini tukamkuta mchina anafoka mbaya kwa kuichafua mashine yake kwa damu akaamrisha isa fishwe haraka sana
Salumu kusema kweli ndugu yangu nikaingiwa na hasira sana na kujiuliza huyu ni binaadamu au mnyama hata mnyama hawi na roho kama hii yani baada
kufikilia jinsi gani mfanyakazi wake kapatwa na tatizo yeye anachojali ni mashine yake tu basi ndugu zake Hamisi wakafika na kuja kuzungumza na yule mchina
akawatoa nduki na kuwatishia kuwapiga na bastora.
Mama yake Hamisi akaondoka akiwa analia waende kushitaki wapi wakati watu wenye ngozi nyeupe wana kumbatiwa hapa nchini kwetu hali yakuwa kwenye
nchi zao tunaonekana kama manyani ile hali ika ninyong'onyesha sana,
Nakumbuka siku moja tukiwa tuna piga kazi nikasikia naitwa na yule mchina yani gaidi sana huyu basi nikaenda akanishika mkono hadi chooni nikajiuliza
anaenda kunibaka au".... baada kufika kule nikaweza kuona choo kimejaa mavi mpaka juu ya sinki si akaniambia toa hii nnya shimba simo paye fukiya japo
kiswahili chake kibovu nika muelewa basi nikaomba dhana cha ajabu akaninasa kofi na kusema “fanya hivyo hivyo, kama nataka kazi fanya kama taki kazi nnje
dahaa nikajishika shavuni kwa maumivu wa lile kofi siku zote katika maisha yangu hakuna kitu nisicho kipenda kama kuonewa nilicho kifanya ni kumvamia
tukajikuta tunaenda chini puhu nikawa nampa masumbwi pale chini huku aki jitahidi kujiondoa wapi kumbe sio kila mchina mcheza karate au shaollin huyu
alikuwa mdebwedo tu akaanza kupiga kelele kuomba msaada jameniiiiiiiiii
i,,,,,nisaidieeeeeee,,,,kama haitoshi nikaenda kumkandamiza kichwa chake kwenye sink hasira nilizo kuwa nazo siku hiyo ni kutamani kuuwa tu hasa nikimkumbuka Hamisi japo Mungu ana samehe ila sio kwa mnyama kama huyu, kila aliye fika wakanisihi nimuache kumbe videmu vyake vishapiga cm police nikajikuta nakamatwa na kuvishwa pingu huku mchina akiwa hatamaniki usoni, basi nikapelekwa moja kwa moja ukonga.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA TANO
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni