Notifications
  • MY DIARY (48)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA NANETULIPOISHIA...Familia yangu haikukubali kabisa mimi kuolewa na rangi nyeusi hivyo walinitenga na kusema hawanitambui kuwa mimi ni ndugu yao.Lakini kutokana na mapenzi mazito niliyokuwa nayo kwa baba yake na Leah nilijikuta nipo tayari kwa lolote hivyo nikahama na kwenda kuishi Tanzania.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Katika miaka hiyo tuliyokaa nilibahatika kupata mtoto huyu…
  • MY DIARY (47)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA SABATULIPOISHIA...Lakini ilifikia mahali ndoto hiyo inanijia hata mchana nikiwa nimekaa mahali tulivu.Ilikuwa inanipa taswira nzuri ya sehemu ambayo madini yalikuwepo.Basi nilianza mikakati ya kulitafuta eneo hilo na hiyo ni mara baada ya ushauri wa mpenzi wangu Candy hapo akimaaanisha yule dada aliyekuwa naye pale jukwaaani.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Candy alinisihii sana…
  • MY DIARY (46)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA SITATULIPOISHIA...Nilikuwa kama niliyepigwa butwaa nisiamini nilichokuwa nakiona mbele yangu. Oooooh my God hold me on yalikuwa ni maneno yaliyonitoka kutoka kwenye uvungu wa moyo wangu mara baada ya kumuona James kwa uzuri zaidi na kuamini kuwa yule kweli alikuwa ni kaka yangu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilishindwa kuelewa nini kimetokea mpaka yeye kurudi katika hali yake ya…
  • MY DIARY (45)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA TANOTULIPOISHIA...Ndio niliona hipo haja ya kuokoka na kuishi maisha ya utakatifu kwa maana nishaishi maisha yote ya kuwa mbali na mungu. Nakumbuka nilipokuwa mdogo kipindi hicho naujua mlango wa kanisani tuisahawahi kufundishwa kuwa mtetezi wa kweli wa maisha ya mwanadamu ni Mungu.Na siku zote alaaniwe mtu yule amtegemeaye mwanadamu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Sio kazi ya…
  • MY DIARY (44)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA NNETULIPOISHIA...Yani alianza kutaka uhusiano na mimi tena uhusinao wa mapenzi.Mda wote alikuwa akiniganda kama luba.Na mimi nilikuwa mjanja sana maana nilijifanya sinywi pombe wala kuvuta sigara.Pia baada ya kugundua kuwa wahusika wengine walikuwa wanajiachia niliamua kujifanya mshauri wa mapenzi na mahusiano.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilikuwa nawasshauri sana mshiriki wa…
  • MY DIARY (43)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA TATUTULIPOISHIA...Wakati nabadilisha staili kwa kukichua kile kifaa na kukiweka vizuri huku nikibinya ile switch hili iongeze spidi Mark aliingia. Ni kweli nilimuona ila sasa sikuwa na jinsi ilibidi nimalizie furaha hiyo ya uwongo uwongo. Yaani wazungu jamani sijui walifikiria nini maana kile kifaa ukikiminya kwa juu kinakuwa kinajizungusha chenyewe.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (42)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA MBILITULIPOISHIA...Uzalendo ulinishinda ikabidi nimuulize ni kwanini bado wanatumia njia hiyo ya kizamani kutunza kumbukumbu wakati siku hizi kuna kitu kinachoitwa Human Resource Informaion system ambapo kumbukumbu zote za wafanyakazi kama waliochishwa kazi, wagonjwa, walioenda likizo ,waliopandishwa vyeo na taarifa nyingine muhimu uhifadhiwa kwa kutumia komputa.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (41)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA MOJATULIPOISHIA...Mark anashangaazwa sana na mwanamke huyo lakini kwa kuwa shida yake ilikuwa ni hela anaamua kuachana nae na kuanza maisha mapya hapo jijiini Dar es salaamMaisha yanaendela lakini Mark amekuwa tajiri na mtu mwenye mafanikio sana kiuchumi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Pamoja na mafanikio hayo ni mtu ambaye mapenzi bado yalikuwa yakimuumiza siku hadi siku.Filamu…
  • MY DIARY (40)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINITULIPOISHIA...Alikuwa akinyata kwa kweli. Kweli hata mimi nilimkubali tu siku ya kwanza ingawa bado nilikuwa sijajua ufanisi wake wa kazi.Nilikaa nae hapo kwangu kwa mda wa siki tatu huku asubuhi tukiamka na kuendelea na kazi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Ndani ya mda huo nikagundua kuwa alikuwa na uzorfu mkubwasana hivyo kazi hiyo alikuwa akiimudu kabisa.Hapo sasa nilimkubali sana…
  • MY DIARY (39)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TISATULIPOISHIA...Nilikuwa na furaha sana huku nikiamini kuwa ndoto zangu za kuja kuwa mtu maarufu zinaweza kufanikiwa hata kabla ya kuyapata yale madini. Sikutaka mbwembwe niliamua kuikopi na kuipesti hiyo stori kama ilivyo na kuifowadi kwa Mark.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Baada ya kama lisaa hivi Mark alipiga na kuniuliza kama kweli ilikuwa nai mimi nimetunga hiyo…

TANGA RAHA (39)

SEHEMU YA THELATHINI NA TISA
ILIPOISHIA...
Jamaa wakazidi kunifwata na sikuwa na jinsi zaidi ya kaanza kupiga hatua za hakanyaga maua yaliyopo pembezoni mwa ukuta na kuanza kukimbia kuelekea sehemu yenye msitu,Vijana wa kijerumani naa wakanza kunikimbiza na kadri wanavyo kimbia ndivyo miili yao ikabadilika na kuwa kama mbwa aina ya Bweha(FOX) na kuzidi kunikimbiza.
SASA ENDELEA...
Sikuwa na namna nyingine yoyote zaidi ya kuuparamia mti kwa haraka cha hadi nikakaa juu ya moja ya tawi huku nikihema na jasho jingi lilimwagika.

Mwanga wa mbara mwezi ukanisaidia kuwaona jamaa wakiuzunguka mti huku wakinguruma kwa sauti za kutisha sana.

Mbwa watu wakaanza kutoa vilioa vya ajabu na kadri mawingu yanavyozidi kuufunika mwezi ndivyo wao wanavyozidi kupata shida katika miili yao na ambayo ikaanza kurudi katika hali kawaida hadi wa kawa binadamu wa kawaida ila hakuna aliye kuwa na nguo miomgoni mwao

Kila kitu ambacho kinaendelea sikuwa ninaamini ni kweli na ninayo jionea,nikajilaza kwenye tawi huku nikiendela kuwatazama jamaa na wakabaki chini ya mti wakiwa wananitazama huku wakinisubiria nishuke.

Masaa yakazidi kwenda na kidogo nikaanza kushindana na macho yangu kitika swala zima la usingizi na kila nipojaribu kuyafumbua kwa nguvu zagu zote ndivyo jinsi macho yalivyo zidi kunikatali nakujikuta taratibu nikiyafumba na kausingizi kakanipi-tia.

Nikaanza kuisikia sauti kwa mbali ya Rahma ikiniita na kunilazimu kuyafumbua macho na kukuta mwanga ukiwa umetawala kila sehemu na jamaa sikuwaona,

Nikashuka kwenye mti taratibu hadi ninakanyaga ardhi na Rahma akawa amefika kwenye sehemu nilipo
“Eddy ulikuwa wapi?”

Nikamtazama Rahma kwa macho makali yaliyo jaa hasira na sikumjibu kitu cha aina yoyote zai-di ya kuondoka pasipo kumkibu.

Nikapitiliza moja kwa moja hadi sehemu walipo kuwa wakicheza ngoma zao usiku na kuyakuta mazingira yakiwa kama jana mchana tulivyo yaacha na hapakuwa na hata jani linalo onyesha kuwa limekanyagwa.
“Eddy mume wangu si nimekuuliza ulikuwa wapi hujanijibu kitu au hujanisikia?”
“Pete yanguipo wapi?”
“Ila baby jana si nilikuambia kuwa nimeitupa”
“Nisikikilize wewe mwanamke usitake nikufanyie kitu ambacho sijapanga kukufanyia ninaomba unipe pete yangu kabla sikakuvuruga.”

Nilizungumza kwa hasira huku macho yangu nikiwa nimeyakaza hadi Rahma akaanza kurudi nyuma
“Eddy kwahiyo mimi unanikasirikia?”
“Ninaomba pete yangu”

Nilizungumza kwa hasira huku nikiwa nimemsogelea kwa karibu Rahma hadi akaanza kutete-meka kwa woga.

Nikamuacha na kuingia ndani,kitu cha kushangaza sehemu ambayo jana damu zangu zilimwagika sikuzikuta ila kila kitu tulicho kiacha nikakikuta kama kilivyo ikiwemo dishi la maji na kiwembe.

Wasiwasi ukaanza kunijaa na sikujua ni nini kinacho endelea,nikapitiliza moja kwa moja hadi chumbani na kujitupa kitandani na baada ya muda Rahma akarudi akiwa amechoka na kukaa pembeni yangu
“Baby nimeitafuta ila sijaiona”
“Huo ujinga usiniambie ila kikubwa ninaihitaji peta yangu umenielewa?”
“Ila baby kwani swala la pete si tulisha lizungumza jana na likaisha”
“Nitakunyonga Rahma au ndio umemvisha yule bwege wako jana usiku?”
“Eddy mbona sikuelewi hayo yote yametokea wapi?”
“Sasa hivi unielewei eehee?”
“Ndio Eddy sikuelewi ninaona unanichukia pasipo kuwa na sababu ya msingi....”
“Nisikilize Rahma mimi sio mjinga na kama unahisi kuwa mimi ni mjinga tambua ya kuwa ume-kosea na kamwe usitaraji kuwa mutaweza kuniteka akili zangu wewe na hao mashetani wezako sawa?”
“Eddy mimi shetani?”
“Ndio wewe nishatani tena Shetani mwenye mguu mmoja”

Rahma akaanza kulia kwa uchungu huku akinitazama kwa unyonge
“Tena usijilize kinafki kiasi hichi mimi ninadhani nina mwanamke mtu kumbe unakwenda ku-funga ndoa na majini watu wala wasio eleweka ili sasa iweje au unavyo ona mwenyewe umeni-komoa si ndio?”

Nilizidi kupayuka kwa hasira
“Eddy laiti kama mimi ni jini basi Mungu anilaani sasa hivi na nife ninaapa kwa jina leke mimi siwezi kukufanyia hivyo unavyo fikiria”
“Ahaa kwahiyo jana mimi niliota si ndio....hadi mashemeji zako wakaamua kunilaza juu ya mti?”
“Eddy naomba unisikilize mpenzi wangu........mimi jana usiku niliamka na kwenda jikoni kunywa maji ila nilipo rudi huku chumbani sikukuta kutokana na usingizi mwingi nikajua utakuwa upo bafuni mimi nikaamua kujilaza zangu sasa asubuhi ndio nikaanza kukutafuta na kukukuta ukishuka juu ya mti ila unapo nihukumu nakuniita mimi jini la mguu mmoja unakuwa hujanitendea haki mume wangu....Unavyo niambia hivyo unanipa mimi uchungu mwingi inaonekana kuwa mimi si chaguo lako sahihi.”

Rahma akaendelea kuzungu kwa uchungu huku machozi yakimwagika
“Kwa hiyo niliye muona pale nje sio wewe?”
“Nje wapi mume wangu mbona unaninyanyasa kiasi hicho au kukupenda kwangu ndio kosa?”
“Koma sijazungumzia maswala ya kupendana,mimi ninacho taka kukijua ni kwamba ipo wapi pete yangu”
“Eddy sijui nimetafuta sehemu nilipo itupa jana ila sikuiona”
“Ahaa powa niache nilale....ila kabla sijalala nahitaji kujua mbona jana ulipo iona picha ya mke wa Mzee Ngoda ulistuka?”
“Eddy yule dada nilimuona siku moja nikiwa sijielewi pale nilipo pigwa risasi na baba,alikuwa akinijia katika mazingira ya kuogopesha sana kiasi kwamba nikawa ninaogopa sema sikuwa na uwezo wa kusema kuwa ninaweza kupambana naye.”

Nikajikuta nikikaa kimya huku nikimuangalia Rahma akizungumza huku machozi yakimtiririka
“Kuna vitu ambavyo alikuwa akinionyesha vya ajabu ajabu na akaniambia kuwa mimi ni mfu na sito weza kuishi tena,ila akaniambia kuwa nisipo weza kukubaliana na sharti lao moja basi sino weza kurudi kuishi tena duniani”

Mwili mzima ukazizima huku nikiusikilizia jinsi unavyo nisisimka na kujikuta nikikaa kitako nakumtazama Rahma vizuri na kumsikiliza kwa umakini
“Walikupa Sharti gani?”
“Waliniambia kuwa nifanye juu chini niweze kukuvua pete ambayo ulikuwa umevaa mkononi,na walinipa siku saba za kuishi ndio maana ile siku ya kwanza ulipo kuja nyumbani mimi mwili wangu ulikuwa umesimama nyuma ya mlango na pale kitandani alikuwa amelala Rahma mwengine anaye fanana na mimi na ndio uliye zungumza naye na baada yaw ewe kuondoka mimi mwili wangu ukaingui kwa yule Rahma uliye mkuta kitandani.”

Maelezo ya Rahma yakanichanganya kiasi kwamba nikabaki nikiwa kimya nimemtumbulia mi-macho huku akilini mwangu nikijiuliza kwa maana huyu niliye kuwa naye ni Rahma mfu au asiye mfu
“Kwa hiyo wewe hapo upo upo vipi?”
“Eddy mimi ndio Rahma wako halisi ila Rahma mwengine yupo anaye fanana na mimi na endapo akiingia mwilini mwangu ninakuwa na hasira kama niliyo ishika jana nilipokuwa ninakulazimisha kuweza kuivua pete yako.”

Nikajikuta nikichoka pasipo kufanya kazi,hali ya mashaka ikaanza kunitawala juu ya Rahma huyu ambaye ninaonge.
“Ila Eddy kwa nini ulinificha?”
“Nilikuficha na nini?”
“Hujui kuwa wewe ndio chanzo cha haya yote”

Nikabaki nikiwa ninamtazama Rahma huku nikikosa la kunzungumza na sikjua nimwambie nini juu ya kitu anacho dai mimi ni chanzo
“Rahma unaposema kuwa mimi ni chanzo sijakuelewa una maana gani?”
“Eddy tambua ya kuwa kila ulilolkuwa ukilifanya haya ndio matokeo yake”

Moja kwa moja nikaanza kuhisi Rahma ameingundua tabia yangu ya zamani,ikanibidi niibadi-lishe mada kuepukana na mizozo ya kelele.
“Fanya basi upike msosi baby ninanjaa?”
“Sawa mume wangu ila hiyo mada tutazungumza baadaye vizuri”
“Mume wangu unanichekesha sana”

Rahma alizungumza nyuma yangu na kunifanya nigeuke na kumtazama
“Kwa nini?”
“Kwa maana wewe unajing’ang’aniza kupanda juu ya huo mti wakti unauona ni mkubwa na tangu kule ndani niliikuwa nikikuangalia jinsi unavyo paramia parami”Rahma alizungumza huku akicheka
“Kinacho kuchekesha wewe haswa ni nini?”
“Ninakucheka wewe unaye nga’angana kuapanda hapo”

Nikamtazama Rahma kwa macho ya umakini na kujikuta nikiachia msunyo ulio mnyamazisha kuchela
“Baby jamani mbona unanisunya?”
“Nenda ndani kaniletee maji ya kunywa”
“Sawa mume wangu au umechukia nilivyo kucheka?”
“Hapana”

Rahma akanisogelea na kunibusu shavuni na kuondoka kwa mwendo wa madoido,Sehemu ni-liyo simama nikaanza kuhisi mtetemeko ulio nifanya nitazame chini kwa muda.

Nikajaribu kupakanyaga nikasikia mlio unao ashiria chini yangu kuna shimo.

Nikaanza kuyasogeza majani mengi ya mti yaliyo kauka na nikakuta mfuniko ulio tengenezwa kwa chuma na niimara sana na juu yake ukiwa na mnyororo chakavu ulio unganika kwa pamoja
“Kuna nini hapo?”

Rahma aliniuliza huku akiwa ameshika jagi lenye maji pamoja na kikombe
“Humu ndani sijui kuna nini,ila ninahisi kuna viu muhimu sana”
“Mmmmm hembu”

Rahma akapiga hatua hadi sehemu niliyopo mimi na akanyaga mfuniko kama nilivyo ukanyaga mimi kwa kutumia mguu kisha akanitazama machoni.
“Baby iseje kukawa na madudu ya ajabu ikala kwetu?”
“Madudu gani?”
“Madudu tuu ya ovyo ovyo”
“Hakuna kitu.....Fanya hivi nenda kule jikoni kalete kile kijishoka kilicho ning’inizwa pale ukuta-ni"
“Sawa”

Rahama akakimbia kuelekea ndani na baada ya muda akarudi akiwa ameshika kijishoka nilicho muagiza na kunikabidhi.

Nikaanza kuukata mnyororo kwa kutumia nguvu nyingi ila haukukatika karahisi kama nilivyo tegemea.

Nikaendelea kuukata na Rahma akanipokea kishoka na yeye akaanza kukata,mpaka inafika jioni hatukuweza kuukata mnororo tukaamua kurudi zetu ndani kila mmoja akiwa amechoka kwa kiasi chake.
“Eddy pale wewe uanhisi kuna nini?”
“Mmm sijajua ila kwa historia ya Mzee Ngoda aliniambia kwa hili jumba alikuwa anaishi rafiki yake wa kijerumani so huwezi jua kuna nini?”
“Mmmmm Mungu akibariki kesho asubuhi na mapema tunamkia kwenye ile sehemu”
“Sawa mke wangu”

Tukapika chakula cha usiku na kula,kutokana na uchovu kila mmoja akalala upande wake wa kitanda huku akilini mwangu nikifikiria ni kitu gani kilichopo ndani ya shimo lenye mfuniko wa chuma.

Sikuweza kupata usingizi nikiwa ninashahuku kubwa ya kutaka kujua,masaa yakazidi kukatika hadi inatimu majira ya saa nane usiku nikaanza kuhisi watu wakizungumza nje ya dirisha la chumba chetu.

Nikamtazama Rahma na kumkuta amelalal fofofo,kwa ujasiri mkubwa nikasimama na kuchungulia dirishani na sikuona kitu.

Nikajianza pembeni kusikilizia kama wataendelea kuzungumza wanacho kizungumza kwa lugha zisizo eleweka ila sikusikia tena.Nikarudi kitandani na kujilaza hata kabla sijajiweka vizuri nikasikia tena mazungumzo yao wakiyaendeleza na nikaanza kujiuliza ina maana wananiona ninapo karibia kwenye dirisha au ila nikakosa jibu.

“Nyinyi washenzi hapo nje ninaimani munanisikia hembu niachieni kelele zetu za kijinga”
Nilizungumza kwa kujiamini huku woga kwa mbali ukininyemelea kusikilizia jibu nitakalo pe-wa.

Ukimya ukatawala kama dakika tano hivi nikaamini wameondoka gfla nikaanza kusikia kengele kubwa lenye mlio mithili ya makengele yanayofungwa kwenye minara ya makanisa likaanza kusikika likigongwa kwa nguvu kubwa.

Rahma mwenzangu hana hili wala lile,kwa hasira nikanyanyuka na kuchungulia dirishani sikuona mtu zaidi ya kusikia milele ya kengele.

Nikaanza kupiga hatua za kwenda nje gafla kwenye kona ya chumba akajitokeza bibi ambaye alinitibu kipindi nilipo okotwa msituni,sikustuka sana japo moyo ukanipasuka na kuyabadilisha utaratibu wa mapigo yangu ya moyo

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

18 Simulizi Tanga Raha
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni