SORRY MADAM (76)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA SABINI NA SITA
ILIPOISHIA...
Nilizungumza kwa sauti kubwa, huku nikiendela kukikandamiza kisu kwenye tumbo la Dorecy ambaye muda wote machozi yanamwagika, kwa ishara Khalid akawaamrisha watu wake kutupisha, tukapita katikati yao huku muda wote nikiwa makini sana, nikiwatazama watu wa Khalid
“Ila Eddy unacheza makida makida kwenye nyaza za umeme”
NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
Khalid alizungumza kwa kujiamini sana, sikujali maneno ya Khalid zaidi ya kumuamrisha Dorecy kutembea kuelekea nje.Tukafunguliwa mlango na walinzi wake baada ya Dorecy kuwaamrisha waweze kufanyan hivyo.
“Magari yenu yapo wapi?”
Nilimuuliza Dorecy kwa sauti ya ukali, taa kubwa lililopo katika jumba hili likawa na kazi ya kutumulika kila sehemu ambayo tunakwenda, macho yangu yote yakawa na kazi ya kutazama kila sehemu ya jengo hili kuangalia walinzi walio jipanga huku wote bunduki zao zikiwa kwetu, Dorecy akanionyesha moja yan jengo ambalo aliniambia kwamba ndipo yalipo magari, kwa hatua za umakini tukatembea hadi lilipo jengo hilo na kuingia ndani, ambapo nikakuta magari mengi ya kifahari takiwa yamepangwa kwa mpangilio mzuri.Macho yangu yakatua kwenye gari aina ya BMW inayo endana na gari ya Sheila aliyo pewa na wamarekani alio cheza nao filamu ya ngono.Nikaisogela huku nikiwa ninaendelea kumshika Dorecy shingo yake, nikajaribu kufungua mlango wa gari na ukafunguka, kwa bahati nzuri nikakuta funguo ikiwa kwenye siti ya dereva.
“Eddy si umesha fika sehemu uliyokuwa unahitaji, niachie sasa”
“Bado unakazi na mimi”
“Kazi gani jamani Eddy?”
“Utaijua mbele ya safari”
Nikamshukumiza Dorecy kwenye siti ya pembeni na mimi nikaingia, nikaiwasha gari na ikawaka pasipo tabu yoyote, cha kushukuru MUNGU mafuta ya gari yamejaa vizuri kwenye tanki lake, nikashusha pumzi nyingi huku nikijifunga mkanda wa gari
“Eddy Khalid atakuua”
Dorecy alizungumza kwa sauti ya chini huku, machozi yakiendelea kumwagika, sikutaka kumsikiliza sana Dorecy, nikairuduisha nyuma gari na kuiweka sawa kuelekea kwenye mlango wa kutokea kwenye jumba hili ambao ni wambao.
“Funga mkanda”
Nilimuamrisha Dorecy na akatii, nikaknyaga mafuta pamoja na breki na kuifanya matairi ya nyuma ya gari kuserereka kwa nguvu, nikaachia breki na kuifanya gari kuanza kwenda kwa mwendo wa kasi, nikaubamiza mlango na gari ikapita kwenye mlango bila ya shida.Taa kali zikapiga kwenye kioo cha gari langu na kunifanya nisione mbele vizuri, nikajikuta nikikanyaga breki kwa haraka, huku macho yangu yakikitazama ‘Kifaru’ kikubwa kilichopo mbele yatu.Nikatazama pembeni na kuona kuna bustani ya maua ambayo gari linaweza kupita pasipo shida yoyote.Nikatazam kifaru hichi ambacho mara nyingi hutumika jeshini katika vita.Mwanga wa Helcoptar ukaendelea kumulia kwenye gari letu,
“Shiti”
Nikakanyaga mafuta kwa haraka, kugeuza gari kwa kasi na kuuelekezea kwenye bustani ya maua, risasi nyingi za walinzi wa Khalid zikaanza kupiga kwenye gari yetu cha kushukuru Mungu hakuna risasi hata moja ambayo inaingia kwenye gari, nikaendelea kuipitisha gari kwenye bustania ya maua hadi nikafika kwenye barabara kubwa iliyopo ndani ya hili jengo la Khalid
“Njia hapa ya kutokea ni ipi?”
“Wewe nyoosha tuu mbele”
Dorecy akanipa ushirikiano mzuri paiso kupinga, nikazidi kunyoosha kwenye barabara aliyo seme Dorecy, huku mfululizo wa risasi ukizidi kuniandama kwa nyuma, mwanga wa Helcoptar ukazidi kutumulika
“Kunja kushoto”
Dorecy alizungumza na mimi nikafanya kama alivyo seme, kazi yangu kubwa ikawa ni kubadilisha gia kwenye gari na kuongeza mwendo kasi wa gari
“Kulia”
Nikakunja kulia kwenye kibarabara kidogo ambacho kwa mbele yake kuna geti dogo lililo wazi, nikazidi kuongeza mwendo kasi wa gari na kutoka kwenye ngome ya Khalid.Tukatokea kwenye barabara iliyopo kwenye kilima, huku pembeni ya barabra kukiwa kuna maporomoka marefu mithili ya barabara ya mlima Kitonga uliopo Mkoni Iringa nchini Tanzania.
“Unaijua hii barabara?”
“Ndio wewe twende”
Umakini wote nikazidi kuuweka kwenye barabara, kwani ina kona nyingi, na endapo nitafanya ujinga wa aina yoyote gari itabingiria kwenye maporomoko na ndio utakuwa mwisho wa maisha yangu na Dorecy.Helcoptar ya watu wa Khalid ikazidi kutufwata kila sehemu ambayo tunaelekea, kutokana na uzoefu wangu wa kuendesha gari kwenye barabara zenye makona mengi, haikuwa nguma kwangu kuhimili kona za hapo kwa hapo ambazo ni nyingi sana.
“Ukimaliza kona mbili hapo mbele kuna mporomoko mrefu kuwa makini”
Dorecy alizungumza, ushirikiano wake sikuuamini sana kutokana na yote aliyo nifanyia, nikazidi kuongeza mwendo kasi wa gari huku miguu yangu, ikiwa na kazi ya kucheza na breki.Tukafika kwenye kiporomoko ambacho Dorecy anazungumza kwa mbali kidogo nikaona taa za gari kwa haraka haraka zinapata kumi zikiwa zimeziba njia, kwa jicho langu la kushoto nikamuona Dorecy akitabasamu hapo ndipo nikagundua amaniuza, kwa kutumia kisukusuku changu cha mkono wa kushoto, nikambamiza nacho Dorecy pembeni ya shingo yake na kumfanya atulie kimya na kupoteza fahamu.Nikafunga breki za gari langu, umbali kidogo kutoka zilipo gari za watu wa Khalid, nikatazama kushoto kwangu ambapo kuna maporomoko marefu, hapakuwa na nyia ya aina yoyote.Kulia kwangu kuna ukuta mkubwa wa mlima, Helcoptar ikasimama na kuzidi kutumulika,
“Nitafanyaje?”
Nilijikuta nikijiuliza swali mwenye pasipo kupata jibu, kwa kutumia kioo cha pembeni nikaona gari nyingi zikija kwa kasi nyuma yangu, huku zikaanza kushuka kiporomoko ambacho ndipo nilipo.
“Bwana Eddy jisalimishe, wewe mwenyewe”
Niliisikia sauti ya Khalid ikitokea kwenye kipaza sauti juu ya Helcoptar yake,
“Siwezi kufa kijinga”
Nilizungumza mwenyewe huku nikiitazama Helcoptar ambayo inaendelea kumulika mwanga kwenye gari yetu
“Moja jisalimishe”
Khalid alianza kuhesabu, nikatimaza pembeni upande wa kushoto nikaona tobo kubwa kwenye gemo kubwa la mlima, gari za mbele yangu zikaanza kupandisha kilima huku za nyuma zikishuka kwa kasi, nikakanyaga mafuta, pamoja na breki zote kwa pamoja na kuyafanya matairi ya nyuma yakiserereka kwa nguvu gari za nyuma zilazidi kunisogelea katika sehemu ambayo nimesimama, kwa kasi nikakunja kulia na kuifanya gari yangu kuelekea kwenye tobo lilipo kwenye gemo la mlima, sikuamini kama gari yangu inaweza kuingia ndani ya tobo hili, sikumini macho yangu baada ya kukuta barabara iliyo chongwa ndani ya shimo hili, ambayo ipo ndani ya mlima
“Waoooo”
Nilijikuta nikipiga kelele a furaha baada ya kufanikiwa kuingia ndani ya shimo hili, japo kuna giza jingi ila taa gari langu zikanisaidia kuona mbele vizuri sana.Gari za watu wa Khalid zikaendelea kunifukuzia kwa nyuma jambo lililo anza kunipa wasiwasi mwingi
“Wakinikamata watanila nyama”
Nilijisemea kimoyo moyo, nikamtazama Dorecy na kumkuta akiwa bado amepoteza fahamu, upana wabarabara hii iliyo chongwa ndani ya mlima ikazipa upenyo gari za watu wa Khalid kutanda njia nzima, huku baadhi ya gari zikijari kunipita ila niliwazui kwa kuwazibia njia kwa mbele.Wakaanza kunipiga risasi kwenye kii cha nyuma cha gari langu, nikazidi kuongeza mwendo wa gari langu, mbaya zaidi barabara hii haina hata kona zaidi ya kunyooka.
Risasi zao nyingi zikafanikiwa kutoboa kioo cha nyuma cha gari na kuzidi kunichanganya akili yangu, nikazidi kukanyaga mafuta hadi mshale wa spidi mita ukagota kwenye spidi ya mwisho ambayo ni mia mbili na hamsini.Nikazidi kwenda mbele, gafla nikakutana na kona ambayo kwa mwendo ambao ninao nikashindwa kukunja na kuisababisha gari kupiga kweney ukuta na kuvunja ukuta huu wa udongo, kufumba na kufumbua nikajikuta gari ikielea hewani, na kuanza kwenda chini kwenye miamba mikubwa ya mawe jambo ambalo lilinifanya niaanze kusali sala yangu ya mwisho kwani, ikitua chini mimi na Dorecy wote tutakuwa maiti
Gari ikazidi kwenda chini kwa kasi, gafla nikastukia gari ikiwa imekwama huku, tawi kubwa la mti likiwa limeingia dirishani la nyuma la gari na kuifnya iendelee kuninginia kwenye mti, nikashusha pumzi taratibu huku nikitazama chini, cha kumshukuru MUNGU, kutoka sehemu tulipo ning’inia hadi chini si mbali sana, nikaufungua mkanda wa gari nilio jifunga, nikamtazama Dorecy na kumuoana akiwa anainyanyua nyanyua shingo yake, akizinduka kutoka usingizini.Akanitazama kwa macho yakuchoka
“Eddy”
“Nini?’
“Yupo wapi Khalid?”
“Wee mwehu nini, jiulize mwenyewe”
Nilizungumza kwa hasira huku nikiufungua mlango wa gari, kuna tawi lipo karibu na mlango wangu, nikapiga makadirio ya macho na kuona ninaweza kuruka na kulikanyaga pasipo na wasiwasi wa aina yoyote
“Eddy unataka kwenda wapi, kwani hapa wapi?”
Dorecy alizungumza huku akitazama chini
“Hapa tupo mbinguni mama yangu”
“Mbinguni……!!?”
“Unauliza tena, hapa ukifungua mlango tuu umeshafika kwa sir God”
Nilizungumza kwa dharau, nikaruka kwenye tawi la mti, kwa bahati nzuri nikatua vizuri na kujiweka sawa mwili wangu, nikashuka kwenye mti taratibu na kufika chini pasipo shida ya aina yoyote, gafla nikasikia kelele za Dorecy akiniita jina langu, ikanilazimu nimtazame nikamuona akiwa ananing’inia, huku ameushikilia mlango wa gari uliopo upande wa siti yake
“Eddy niokoe mwenziooo, ninakufa mimi”
“Ukijiachia tuu unafika mbnguni, hapo tulikuwa kwenye geti la kuingilia mbinguni”
Nilizungumza huku nikimtazama Dorecy jinsi anavyo ning’inia huku akiirusha rusha miguu yake hewani
“Eddy nakufa mimi”
Dorecy aliendelea kuzungumza kwa sauti ya kilio, huku akiendelea kuning’inia hewani, nikatafuta sehemu yenye jiwe lililo kaa vizuri, nikakaa na kuendelea kumtazama Dorecy anaye endelea kuninginia hewani
“Eddy niokooe”
“Nikuulize kitu Dorecy?”
“Ehee” Alijibu huku akiwa amening’inia
“Hivi huku ulifikaje?”
“Nikuulize wewe, tumefikaje huku?”
“Ahaa unaniuliza mimi tena kwamba tumefikaje huku, unadhani kwamba mimi nilikuwa ni ndege iliyo kufikisha kwenye hii nchi?”
“Eddy tuachane na hayo, ninakuomba unisaidiea”
Dorecy alizungumza kwa sauti ya unyong, akiashiria kwamba amechoka sana
“Madini yangu yapo wapi?”
“Edd siwezi kukujibu hadi nishuke”
“Basi wewe si mjeda wa mzee Godwin, jishushe mwenyewe”
Nilizungumza huku nikinyanyuka kwenye jiwe, nikiendelea kulichunguza aneo zima la hii sehemu, nilipo hakikisha lipo salama na hakuna uwezekana na watu wa Khalid kufika katika sehemu tulipo nikarudi sehemu alipo Dorecy akiendelea kuning’inia huku akitoa kilio kwa mbali akilalamika kwamba anakufa
“Jiachie”
Nilizungumza huku nikiwa nimesimama chini yake nikimtazama
“Ehee?”
“Hujasikia, jiachie nitakudaka na hilo jitumbo lako”
“Kweli Eddy?”
“Kama hutaki basi bwana”
“Basi najiachia”
Nikaitega mikono yangu usawa wa sehemu anayo ning’inia Dorecy, nikahesabu moja hadi tatu, Dorecy akajiachia na kutua kwenye mikono yangu, cha kushukuru MUNGU ametua vizuri kwenye mikono yangu, nikamsimamisha chini na kumuacha akiendelea kuhema kwa nguvu, kama bata mzinga.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni