Notifications
  • MY DIARY (30)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINITULIPOISHIA...Baada ya hapo Nnilimwomba mama mdogo ajikaze na kuwatarifu ndugu wengine habari hizo za msiba.Tulisaidiana hivyo hivyo maana sio siri kila mmoja alikuwa na uchungu sana kutokana na mazingira ya kifo hicho. Habari zilizidi kusambaa kwa kasi na majirani walianza kukusanyika hapo kwa mama mdogo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Msiba ni msiba tu na ukitaka kujua binadamu…
  • MY DIARY (29)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA TISATULIPOISHIA...Hapo sasa nikazidi kuchanganyikiwa ikabidi nimuulize mama huyo alikuwa akifanyia shughuli zake za kujipatia kipato sehemu gani.? Yule dada akanambia kuwa anafanyia soko la ndizi huko Korongoni. Sikuwa na jinsi nilimuomba anipeleke lakini na yeye alisita sita kwa madai kuwa alikuwa na kazi nyingi za kufanya na bado anatakiwa ampeleke mtoto shule.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (28)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA NANETULIPOISHIA...Sisi tumesomea mambo haya bhana waliendela kuzungumza wale walinzi huku wakishuka ngazi kwa polepole. Hapo na mimi nikawa nimejifunza kitu kuwa kumbe unaweza kuingia na mtu guest akakuzuru kisha akaondoka zake.Sasa sijui kwenye zile guest zetu za uswahilini kama wanalijua hili.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi nilala japo usingizi ulikuwa hautaki kuja kwa…
  • MY DIARY (27)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA SABATULIPOISHIA...Alinamba eti hayo ya mimi kuolewa tuyaeke pembeni na kwa nini siku hiyo nisilale Moshi tukumbushie enzi zetu. Mwalimu John aliendelea kusema kuwa amenimiss sana na anomba nisahu yaliyopita na turudie yale maisha yetu ya zamani.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilijifanya simwelewi lakini ukweli ni kwamba nyota ya mwanaume huyu ilikuwa ni kali sana zaidi yangu na…
  • MY DIARY (26)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA SITATULIPOISHIA...Joyce alinambia yeye haendi kujipanga foleni kama makahaba wengine hivyo yeye hufanya biashara hiyo kitaalamu zaidi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Alisistiza pia kuwa eti huwa anatumia kinga kuwakinga wengine. Wakati mwingine alinambia acha awaambukize kwa sababu wanaume wangekuwa na akili basi wasingeenda kununua mwanamke. Anasema kuwa laiti biashara hiyo…
  • MY DIARY (25)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA TANOTULIPOISHIA...Sikuisha hapo pia nilimpongeza kwa kunijali na kunipenda na kuhakisha kuwa siingii kwenye majanga kama yake mara baada ya kutoka jela. Siku hiyo nilimuelewa sana Joyce na nilikuwa tayari kumsapoti kwa lolote ili mradi tu atimize athma yake hiyo ya kuzaa. Tuliongea mengi sana na baadaye alinionesha picha ya mtu ambaye alitaka kuzaa naye.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (24)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA NNETULIPOISHIA...Kwa kweli siku hiyo niliwaza sana na kutafakri vitu vingi. Wale wanachuo wenzangu wamenambia kuwa Msouth alikuwa kwa kimada mwingine na japo stori haikumalizikia ila ukweli ni kwamba alifumaniwa na kupigwa vibaya na huenda walimtupa mahali na ndio maana chanzo cha kifo chake hakieleweki.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilijaribu kuijikontrol ili nisiwaze kitu…
  • MY DIARY (23)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA TATUTULIPOISHIA...Alinisihi sana nisitoe niilee na yeye atatoa huduma zote lakini tuendelee kufanya siri ili tusije tukahatarisha ndoa yake na kusababisha familia yake kuyumba. Kwa kweli sikuweza maana ilikuwa ni kujipa tabu mimi na huyo mtoto atakayezaliwa. Bora ataa ingekuwa ni mimba ya ule mwalimu ambaye hajaoa.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilitamani nimchomekee hiyo mimba…
  • MY DIARY (22)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILITULIPOISHIA...Alitumia vizuri umbo lake la kimiss kutembea kimiss na kuweka mapozi ya maana. Na baada hapo alilala kwenye kile kigodoro na akachojoa vyote isipokuwa kufuli jeupe ambalo nalo alipewa hapo hapo kwa ajili ya kazi hiyo. IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi sikumpa nafasi Joyce niliingilia nafasi yake na kuchukua ule uume wa bandia nikamfuta yule dada.…
  • MY DIARY (21)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJATULIPOISHIA...Nilichomeka simu chaji na kuiweka hewani ili nione kama kutakuwa na sms yeyote iliyoingia.Hofu ilizidi kunitawala na wakati naendela kufikira simu yangu iliita niakzani labda ni Joyce na nilipoiangalia nilimkuta ni Msouth. Sikutaka kuipokea nikaiacha iite mpaka ikate yenyewe.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nikajiuliza kwani amepatwa na nini usiku huo mpaka…

MY DIARY (24)

Jina: MY DIARY
Mtunzi: __

SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE
TULIPOISHIA...
Kwa kweli siku hiyo niliwaza sana na kutafakri vitu vingi. Wale wanachuo wenzangu wamenambia kuwa Msouth alikuwa kwa kimada mwingine na japo stori haikumalizikia ila ukweli ni kwamba alifumaniwa na kupigwa vibaya na huenda walimtupa mahali na ndio maana chanzo cha kifo chake hakieleweki.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

TUENDELEE...
Nilijaribu kuijikontrol ili nisiwaze kitu chochote lakini nilishindwa.Nilimkumbuka sana mama yangu ingawaje sikutaka kumuweka kwenye kundi la wakatili lakini nilijiuliza hivi kweli mama yangu alikuwa akinipenda. Kama ni hivyo mbona imepita miaka yote hiyo hajanitafuta. Hivi kweli unaweza kuzaa mwanao na ukakubli kumuacha kwa baba yake na wewe kurudi kwenu bila kumtafuta kwa kipindi chote kirefu hivyo.

Sasa hapo aligombana na marehemu baba yangu au mimi mwanaye nilijiuliza?Usiku ulishaingia na humo rumande kulikuwa na joto la kutosha giza na kila aina ya karaha. Omba tu kusimuliwa lakini kulala rumande hakufai jamani. Nilijiuliza kwa nini walikataa nisiwekewe dhamana ili hali kulikuwa hakuna ushaidi wa moja kwa moja kuwa mimi nilihusika na mauaji ya Msouth.

Ni wiki ya pili sasa tangia tukio la kufariki kwa Msouth litokee na hakuna dalili zozote za mimi kuachiwa huru. Nimeshahojiwa zaidi ya mara 3 na nimeeleza kila kitu ikiwa ni pamoja na yale maneno niliyoelezwa na wanachuo wenzangu kuwa kijana huyo alikuwa na mahusiano wa kimapenzi na mke wa mtu huko mtaani hivyo hicho ndicho chanzo cha kifo chake.Hata hivyo polisi waliniambia kuwa uchunguzi bado unaendelea. Na kama ushahidi ukikamilika basi kesi itapelekwa mahakamani.

Nilielezwa na mpelezi kuwa mpaka sasa idadi ya watu wanaoshikiliwa na polisi ni pamoja na mwanafunzi mwenzangu yaani MR ambaye yeye ndio chanzo cha ugomvi kutokea kule club na mwingine ni mke wa myu ambaye inasemekana ndo alikuwa awara wa Msouth. Mume wa mke huyo bado anatafutwa na polisi kwa udi na uvumba kwa sababu ametoroka na hajulikani ameenda wapi maaana hata huko anapofanyia kazi haonekani.

Basi siku zilizidi kwenda huku nikisubiri kwa hamu na jamu kesi yetu ipelekwe mahakamani. Joyce alishaangaika lakini wapi kwani inasemekana ndugu wa marehemu walikuwa na uwezo sana hivyo walitumia gharama nyingi sana kuhakiksha kesi haifutwi kirahisi. Joyce kwa kutumia zile hela tulizocheza picha za uchafu aliweza kumpata wakili ambaye alinihadi kunisaidia na alisisitiza kuwa ningeachiwa huru kabla ya miezi 3.

Yaani anaona miezi mitatu ni kidogo nilimlalmikia Joyce.Joyce alinambia kuwa kesi ya mauji ni ngumu sana kwani unaweza kukaa ndani hata zaidi ya mwaka mzima wakati ushahidi ukikutafutwa. Sikuwa na jinsi zaidi ya kuwa mpole maana maji yalizidi unga. Ni siku mbili zimebaki kabla ya kuanza kwa mitihani ya kumaliza semester ya pili ya mwaka wa kwanza. Sikuwa na jinsi zaidi ya kuandika barua ya kuhairisha masomo mwaka huo.Roho iliniuma sana kuona wenzangu wanaendelea na mitihani huku mimi nikiendelea kulala ndani tena kwenye vigodoro vyenye chawa na kunguni. Kweli life is change (maisha yanabadilika) unaweza kulala tajiri na kuamka masikini japo sijui kama kinyume chake yaani kulala masikini na kuamka tajiri ni rahisi hivyo.

Wakili wangu aliapambana usiku na mchana kuhakikisha kuwa naachiwa huru lakini jambo hilo halikuwa rahisi kama nilivyokuwa nafikiria. Siku zilizidi kwenda na tayari miezi sita ilishaisha. Afya na muonekano wangu ukazidi kudorora. Mawazo ya kuendelea na chuo au kusoma nayo yalishapotea kabisa. Kitu pekee ambacho nilikuwa nakitumaini ni kuyatafuta madini yaliyofichwa huko wilayani hai mkoani Kilimanjaro na marehemu baba yangu.

Kwa msaada wa mawakili na wapelelzi ambao nilijenga nao urakifi nilifanikiwa kuachiwa huru. Ushahidi wa kesi ulikamilika na inasemekana kuwa yule Msouth aliuwawa na muwe wa yule mke aliyekuwa akitembea nae. Usiku wa tukio MR alimfuata Msouth na kumtishia kumfanyia kitu mbaya usiku huo.Msouth kwa kuhofia usalama wake aliamua kwenda kulala kwa huyo mke wa mtu.Kwa hiyo kwa namna moja au nyingine Mr naye alikuwa hatianai kwa kutishia kuua na kupelekea kifo chake.

Kwa hiyo siku hiyo Msouth alivyoenda kulala kwa yule mama ndo siku ambayo pia mume wa mama huyo aliaga kuwa anaenda kongo kupeleka mzigo, Si unakumbuka nilikueleza kuwa baba huyo alikuwa ni dereva wa malori yanayoenda nje ya nchi. Kumbe baba huyo hakoundoka na alaikuwa na mpambe wake aliyempa taarifa.Usiku alirejea kwake na kumkuta mwizi wake akiwa ndani akiendelea kula mali zake.

Hali hiyo ilimpandisha hasira na kujikuta akimpiga sehemu za tumboni kwenye bandama na kupelekea damu nyingi kuvuja ndani ya tumbo. Kijana huyo alifanikiwa yaani Msouth alifanikiwa kujikongoja mpaka ghetto kwake na alivyofika alisaidiwa na wenzake na walimkimbiza hospitalini. Walivyomfikisha Hospitali kwa kuwa alikuwa amekunywa pombe manesi hawakumpa huduma yeyote. Kufika asubuhi Msouth alipoteza maisha. Masikini msouth kijana uliyenipenda sana upumzike kwa amani. Umetangulia tu, mbele yetu, nyuma yako.

Ushahidi huu ndio ulioniwezesha kutoka selo na kuendelea na maisha yangu na hiyo ni mara baada ya muaji kupatikana. Nilivyotoka kwa kweli nilikuwa sina pa kwenda kwa sababu chumba changu kilikuwa kimesharudishwa ingawa vitu vyangu viliwekwa mahali salama. Ilinibidi niende Arusha kwa rafiki yangu Joyce.

Ingawa sikupenda kukaa Arusha lakini nilikuwa sina namna ingine nilikubalina na matokea na kuanza maisha mapya yasiyo na mbele wala nyuma.

Kwa rafiki yangu Joyce kulikuwa na kila kitu ila sikuwa na amani ya nafsi kwa sababu hata kufanikisha kunitoa jela ni kwamba alishatumia pesa nyingi sana.

Joyce alitumia hela nyingi sana hivyo ata yeye aliyumba kiuchumi. Kila palipokucha alikuwa akiondoka asubhi na mapema na kurudi usiku.Sikujua alikuwa akienda wapi ila alisisitiza kuwa lazima aangaike ili tuweze kupata hela ya kula. Usiku pia hakusita kwenda kufanya zile shughuli za kujiuza ili mradi tu apate hela.

Kila nilipotaka kumsaidia alikataa katu katu na kuniambia nahitaji mda wa kupumzika tu nile na kurudisha mwili wangu ambao nilikuwa nimekonda sana mpaka nikapoteza uzuri wa shepu langu nilokuwa nalo.Kauli yake ilikuwa na mashiko kwa sababu nilikuwa nimekonda sana na sikuwa tena Bambucha bali kimbaumbau… Si kuna ule wimbo wa jambo squared kimbaumbau kanenepa kawa tukunyema basi kwangu ilikuwa ni kinyume chake yaani tukunyema kakonda na kuwa kimbaumbau.

Siku zilizidi kwenda na kwa msaada wa rafiki yangu huyo mwili ulianza kujirudi na kuwa mzuri kama zamani. Uzuri wangu wa umbo la kibantu ulianza kuonekana na niliendelea kuwa na uzuri wa asili sio wa vipodozi na madawa ya kujichubua. Joyce alinikataza kabisa kujiuza na kufanya yale madili yetu ya zamani na badala yake alinikabidhi saloon na biashara zake zingine. Sikumuelewa kabisa ikabidi siku moja nimkalishe chini na kumuuliza kwa nini yeye anafanya yale madili na hataki mimi niyafanye wakati yana hela za haraka haraka.

Hakuwa tayari kufafanua zaidi ya kusema ananipenda sana hapendi mimi niwe kama yeye. Siku ziliendelea kuyoyoma huku yeye akiendelea kupambana na maisha hayo ya kujikatia tamaa. Siku moja niliona madawa ya kuongeza siku za kuishi na kupunguza makali ya virusi vya ukimwi ambayo alikuwa akiyatumia rafiki yangu Joyce. Hapo nikagundua kumbe alishajikwaa na kwa sasa alikuwa ni muhathirika wa ukimwi. Lakini mbona alinificha hilo ndo swali kubwa lilokuwa likinisumbua. Jambo hilo liliniumiza sana na kujikuta nakosa amani ya nafsi nikajihisi labda na mimi nilikuwa ni muhathirika. Nilitamani kwenda angaza kujitangza lakini niliogopa kwa sababu kwa moyo wangu huu wa plastiki huenda ningekufa hapo hapo baada ya kupewa majibu.

Hapo ndo niliamini kuwa Joyce alikuwa na moyo wa chuma na ndo maana hakutaka nijikwae kama yeye. Lakini pamoja na nia yake nzuri kuwa na mimi nisije kujikwaa bado nilijiuliza yeye alikuwa na uhakika gani kuwa mimi sijahathirika.Siku zote tulihakikisha kuwa tunakula mlo kamili na kufanya mazoezi ikiwa ni mikakati ya Joyce kuishi mda mrefu.

Siku moja tulitoka out nakumbuka ilikuwa ni siku ya jumapili tulivu na tulienda sehemu moja inayoitwa Boatiq Garden hapo hapo Arusha. Siku hiyo Joyce aliniuliza swali gumu sana. Aliniuliza “ hivi rafiki yangu Leah wewe una ndoto gani ambayo ungependa kuitimiza kabla hujafa”. Yaani hapo mawazo yangu yakaenda moja kwa moja kwenye yale madini lakini nilimjibu kuwa ndoto yangu ni kuwa tajiri mkubwa na mtu maarufu zaidi duniani. Kama alikuwa mawazoni mwangu maana alinambia nifafanue nitaweza vipi kuwa tajiri.

Nilimwambia siku zote nayawaza sana madini ya marehemu baba yangu.Joyce akanambia nina mawazo na ndoto kubwa kuliko yeye. Nilimuuliza kwani yeye anataka kuifanyia nini dunia kabla hajafa? Joyce akatabasamu kidogo kisha akanambia ni jambo dogo sana lakini nazani litakuwa na faida sana huko baadaye.

Akaanza kunielezea “ujue kabla mama yangu hajafa alinambia nihakikishe kuwa naweza kuacha mtu wa kumlilia kama mimi nitakavyomlilia yeye siku akifa.

Kwa kifupi nijitahidi kuacha mbegu huku duniani yaani nizaee mtoto.

Mama yangu aliteseka sana mpaka kunizaa mimi na hivyo anaaamini hakuna kitu chenye thamani zaidi duniani kama kuzaa mtoto.Hapo nilimwelewa Joyce kuwa wazo lake kubwa ni kubeba mimba na kuzaa mtoto. Sasa nilijiuliza atazaa na naniili hali yeye ni muhathirika?sikutaka kujiuliza hivyo nilimtupia swali hilo.

Alinambia hataki mwanaye aje ateseke na haya maisha hivyo atamtegeshea kigogo mmoja.
Joyce siku hiyo alinieleza ukweli juu ya afya yake kuwa yeye ni muhathirika wa ukimwi.Na anasema aligundua hali hiyo mimi nilipokuwa rumande na kwa sasa anaishi kwa matumaini kwa kufuata ushauri wa madaktari. Alinambia kuwa pia ana daktari wake maalumu ambaye anamsaidia. Joyce alisisitiza kuwa daktari wake amemwambia kuwa anaweza kubeba mimba na kuzaa mtoto ambaye hana maambukizo ya ukimwi japo hatoruhusiwa kunyonya maziwa ya mama. Nilimuonea sana huruma rafiki yangu kwa sababu alishajikatia tamaa ya maisha na pia nilijionea huruma na mimi pia kwa sababu nilikuwa sina uhakika na afya yangu. Nilimpongeza kwanza kwa kujua hali yake ya afya na pili nilimpongeza kwa kuwa na dhamira ya kuzaa.

Sikuisha hapo pia nilimpongeza kwa kunijali na kunipenda na kuhakisha kuwa siingii kwenye majanga kama yake mara baada ya kutoka jela. Siku hiyo nilimuelewa sana Joyce na nilikuwa tayari kumsapoti kwa lolote ili mradi tu atimize athma yake hiyo ya kuzaa. Tuliongea mengi sana na baadaye alinionesha picha ya mtu ambaye alitaka kuzaa naye.

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
68 My Diary Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni