DHAMANA (20)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mwandishi: Hassan O Mambosasa
SEHEMU YA ISHIRINI
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Mmoja wa walinzi aliongea kwa sauti nzito huku akiwa ameshika masikio kama ambavyo wenzake wote walivyokuwa wameshika masikio kutokana na kuumizwa na makelele ya Bi Farida, kauli ya yule mlinzi aliposema mchukueni hakuelewa anamaanisha nini na alikuja kuelewa baada ya kujikuta amezungukwa na wasichana watatu wenye urembo wa hali ya juu ambao haikujulikana walifika vipi hapo hadi muda huo.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Akiwa anajiuliza swali hilo wale wasichana walimshika mkono na akajikuta akitokea katika mazingira mengine akiwa pamoja nao hao wasichana, alijikuta akiwa yupo ndani ya chumba chenye mapambo ya kila aina ambacho ukubwa wake kilizidi kumshangaza na kumfanya azubae akishangaa hadi pale alipoondolewa mshangao wake kwa kusikia sauti ya isiyokuwa ngeni masikioni mwake.
"Mama" Ndiyo sauti ya kike aliyousikia ikitokea nyuma yake ambayo ilimfanya ageuke atazame alipoitwa.
"Zayinaa!" Bi Farida alitamka akiwa anaonekana kutoamini macho yake kwa kumkuta Zayina eneo hilo akiwa amevaa mavazi ya kifahari na vito vya thamani na alikuwa akipepewa na wanawake wawili wenye uzuri ambao haukuwahi kuonekana duniani na walikuwa na nywele ndefu na nyeusi kupitiliza.
****
Yule mwanajeshi mmoja aliyetoa ukelele katika kikosi cha kilichotumwa na himaya ya Majichungu alikuwa amezungukwa na mzizi mmoja wa mti ambao ulikuwa ulikuwa unatambaa kama nyoka na kitendo cha kupiga kelele ndiyo ikawa amechokoza nyuki waliofiwa na malkia wao na sasa hasira zote za nyuki zimehamia kwake. Mizizi ya ule mti ilianza kubadilika rangi na kuwa ua rangi sawa na uji wa volkano unaotoka baada ya mlima wa volkano kulipuka, mwanajeshi huyo wa kijini alijikuta akiteketea hadi akawa majivu.
Kelele za yule mwanajeshi kabla hajafa zilifanya eneo hilo la msitu lenye giza kuonekane macho yanayong'aa kama ya macho ya simba yakimulikwa na tochi gizani, macho hayo yalionekana kuwa mengi kila sehemu kuashiria kuna viumbe wengi ndani ya pori hilo walikuwa wamewaona na macho hayo yalizidi kusogea karibu kuashiria kuwa viumbe hao wanasogea karibu.
"Zaghari bekatu mudyosiye jikiteee, zaghari bekatu mudyosiye jikitee. Halkumisate fadyozile gaitak( Washeni nuru za macho yenu muda wa mapambano huu, washeni nuru za macho yenu muda wa mapambano huu. Hakikisheni tunawamaliza tutizimize kazi)" Salmin alitumia lugha inayotumiwa na wanajeshi wa Majichungu pekee ikitokea dharura kama hiyo, lugha hiyo haikuwa inafahamika na kiumbe mwingine yoyote isipokuwa wanajeshi hao.
Wote kwa pamoja waliwasha nuru ya macho yao na kuwafanya waone pori zima kama mchana ingawa ilikuwa ni giza nene lipo porini hapo, hapo waliwashuhudia viumbe wenye maumbo kama miti wakiwa na wanawaangalia na wengine tayari wakiwa wamewazunguka wakiwa na macho yaliyojaa hasira. Viumbe hao walianza kuwashambulia kina Salmin na kupelekea utokee mpambano mkali kwani hadi muda huo tayari kikosi cha Salmin kilikuwa kimeshajianda, viumbe waliopo msituni hapo walijikuta wakipigwa vibaya na kikosi cha kina Salmin kwani nguvu zao ambazo waliamini wanazo wao peke yao walishangaa Salmin akiwa anazitumia baada ya kumgusa jini mojawapo wa himaya ya giza na kuzinyonya nguvu zake. Mpambano ulipowazidia majini wa himaya ya giza mmojawapo alianza kukimbia ili akatoe taarifa ya uvamizi, jini huyo alikuwa ameshaonekana na Salmin ambaye alisoma mawazo yake akamjua lengo lake
Salmin alijigeuza mti kama viumbe wengine kisha akatoa mzizi mmoja mtefu ulioenda kumfunga yule jini halafu akamuunguza kama alivyowaunguzwa yule mwanajeshi aliyekuwa yupo upande wao, alirudi katika hali ya kawaida akaendelea kupambana hadi walipowamaliza majini wote wa himaya ya giza ambao walilala chini kama miti iliyoangushwa katika ukataji miti.
Salmin alianza kuwapiga miale ya radi majini hao mmoja baada ya mmoja na wakabadilika wakawa na maumbo ya majini wa kawaida ambao walikuwa wamevaa sare moja, alimvua mmojawapo sare akavaa yeye mwenyewe kisha akawaamuru wenzake wafanye hivyo. Baada ya muda mfupi wote walikuwa na sare zinazofanana kisha wakasonga mbele kuuvuka msitu huo.
****
Bi Farida alienda kumkumbatia mtoto wake kwa nguvu huku machozi ya furaha yakimtoka akiwa haamini kama angemkuta hapo, alijisahau kabisa kama yupo ugenini katika eneo asilolijua na akajikuta akiwa na furaha ya kumuona aliyesadikika ametekwa.
"Nani kakuleta huku mama?" Zayina alimuuliza mama yake baada ya kuachiana tangu walipokumbatiana.
"mimi ndiyo nimemleta huku" Sauti ya Zalabain ilisikika kisha akajitokeza akiwa ameongozana na mwanamke wa makamo aliyebeba chupa na beseni lenye rangi ya fedha, Bi Farida aliposikia sauti hiyo akageuka nyuma akakutana uso kwa uso na sura ambayo alihisi aliwahi kuiona mahali.
" we ni nani?" Bi Farida aliuliza huku akimkazia macho Zalabain.
"Kaka Jamadin huyo" Zayina alidakia kujibu na kumfanya mama yake ashangae kwani anatambua mwanae huyo alishafariki.
"Fanya kazi yako" Zalabain alimuambia yule mwanamke aliyekuja naye huku akiupuuzia mshtuko wa mama yake, yule mwanamke alimsogelea Bi Farida akampatia chupa aliyokuja bila hata kujali kama itapokelewa au haitapokelewa. Bi Farida aliipokea chupa hiyo akaifungua na akanywa kimiminika kilichokuwa kipo ndani yake hadi akamaliza, alimrudishia kile kichupa yule mwanamke na yule mwanamke akampatia beseni la rangi ya fedha alilokuja nalo.
Bi Farida alipolipokea hilo beseni tu alijikuta akibanwa na kichefuchefu cha ajabu na akainamisha kichwa humo ndani ya beseni akaanza kutapika vitu ambavyo vilimshangaza sana Zayina hadi akageuza shingo pembeni huku akiwa kaziba mdomo, mwisho wa kutapika alitapika kitu cha duara chenye mizizi ambayo ilikuwa inachezacheza kuashiria kina uhai. Baada ya kutapika hicho kitu Bi Farida alizirai papo hapo halafu akazinduka baada ya sekunde kadhaa huku akihema kwa nguvu, alipoinua macho yake akamuona Zalabain na akajikuta akimuita, "Faimu".
"Hapana mama ni Jamadin mwanao" Zalabain alimuambia Bi Farida.
"Mwanangu Jamadin" Bi Farida aliongea huku akiinuka akaenda kumkumbatia Jamadin hadi Zayina akatokwa na machozi.
"Nafurahi mama umetoka katika kifungo kizito ulichokuwa umefungiwa, Zayina njoo na wewe" Zalabain alimuambia mama yake kisha akamgeukia Zayina aliyekuwa akiwatazama, Zayina alisogea akaungana nao katika kukumbatiana.
****
Baada ya kuwamaliza majini wa himaya ya giza waliowekwa kulinda katika eneo la pori hatimaye walilivuka pori hilo na wakatokea katika eneo la mbele la mapango ya Zabakut, walikuta lango la kuingilia katika mapango hayo likiwa limefungwa na pembeni kukiwa na walinzi waliovalia sare kama walizovalia wao. Walitembea hadi kwenye lango hilo ambapo Salmin alitoa salamu ambayo hutumika na himaya hii na wenzake pia wakafanya hivyo, walinzi waliitikia salamu hiyo kisha wakafungua mlango bila kujua wamewaingiza maadui zao ndani ya sehemu yao ambayo hutumika haswa kutengenezea silaha zao hatari na za maangamizi.
Salmin akiwa mbele aliwaongoza wenzake kuingia ndani ya mapango ya Zabakut, waliingia mpaka ndani na wakafuata njia iliyochongwa vizuri kama ukumbi mwembamba wa nyumba unaotengenisha ambao hujulikana korido na waswahili wazungu katika nchi ya waswahili.
Pembezoni ya ukumbi huo katika ukuta kulikuwa kuna mafuvu ya binadamu yaliyokuwa yamepangwa safu moja na yalikuwa yakitoa moto ambao ndiyo ulitumika kama muangaza wa humo ndani ya pango, walitembea hadi sehemu yenye makelele mengi wakakuta lango kubwa sana lililokuwa na mlinzi mwenye kichwa cha nyoka na mwili wa kawaida. Waliposogelea mlango huo yule mlinzi anyoosha mkono na ardhi ya mbele yao kina Salmin ikapasuka na kuacha bonde kubwa na uji wa volcano ukaonekana ndani ya bonde hilo, Salmin aliliruka bonde hilo hadi upande wa pili akamfikia yule mlinzi na kumgusa begani halafu akasogea pembeni.
"Toa utambulisho wako" Yule kiumbe alimuambia Salmin huku akijiweka tayari kupambana.
"Mikaf kama wewe" Salmin alimuambia yule.
"mikaf huwa tunauwezo wa kugeuza ardhi vyovyote, mbona nimepasua hiyo hukuiunga upite" Yule kiumbe alimuuliza Salmin swali ambalo hakulijibu na alijigeuza akawa na kichwa cha nyoka kama yule kiumbe halafu akaiunga njia ile na kupelekea kiumbe yule atabasamu, wenzake walipita wakaja hadi pale alipo.
"Wafanyakazi wapya wa hazina hii, ni wataalam wamekuja kumalizia uundwaji wa silaha zetu" Salmin alimuambia yule kiumbe ambaye alifungua mlango akamruhusu aingie na wenzake akijua ni Mikaf kama yeye mwenye kugawa majukumu.
Mikaf ni majini wa himaya ya giza wenye uwezo wa kuongoza ardhi na udongo na kuupinda au kuufanya watakavyo, majini hawa katika himaya hiyo hufanya kazi ya usimamizi na ulinzi wa sehemu muhimu za himaya ya giza na hutambuana kwa kuoneshana nguvu zao tu. Salmin alivyofika jirani na yule Mukaf anayelinda tayari alikuwa ameshaijua hulka yake kwa kutumia uwezo wa ajabu alionao, pale alipovunja njia aliruka juu na kumgusa begani ambapo alichukua nguvu zake kutokana na uwezo wake alionao na alipoambiwa ajitambulishe ndiyo akaiunga njia akiwa tayari ameuchukua uwezo wa yule Mukaf.
Baada ya kuingia ndani ya eneo hilo kikosi cha Majichungu kiliona chupa mbalimbali zikiwa zimehifadhiwa wadudu wa ajabu wenye mabawa ambao walikuwa wakipiga kelele na kurukaruka, kila chupa ilikuwa imeungamishwa na fito za shaba maalum ambazo ziliingia kwenye mtungi mkubwa wenye kimiminika cha njano.
"wapo kwenye hatua ya mwisho ya ukuaji hawa, walikuwa wakitunzwa kwenye hizi chupa tangu watengenezwe sasa inabidi tumalize kazi yetu tuiokoe himaya yetu. Fanyeni kama nitakavyofanya" Salmin aliwambia wenzake kisha akaenda hadi kwenye mtungi mkubwa akaushika na wenzake nao wakamfuata wakafanya hivyo hivyo, alitoa miale ya radi mikononi iliyoingia humo na wengine nao wakatoa miale hiyo. Mitungi yote iliyowekwa wadudu hao ilipigwa na miale ya radi hadi wadudu hao wakafa wote na makelele ya wadudu hao yakaisha papo hapo kukawa kimya, baada ya kumaliza kazi hiyo Salmin alitumia nguvu za mukaf akakanyaga ardhi ikafunguka akaingia na wenzake wakaingia na kutoroka eneo hilo baada ya kazi yao kukamilika.
Mlio wa maji kumwagika katika nyumba ya Shadii uliisha kuashiria kuwa koki ya maji ishafungwa na maji hayaingii kwenye matanki yaliyojaa, Jamali aliendelea kumsubiri shangazi yake atarudi kwa muda wa saa zima hakurejea na hapo ikamlazimu aende uani kuangalia huenda amekumbwa na tatizo kwani alikuwa hajamaliza kuzungumza naye na hakurejea ndani. Alifika hadi sehemu iliyokuwa na matanki ya maji ambapo kama maji yakijaa na kumwagika basi hujulikana wa eneo hilo kulowana hasa bustani ya maua ambayo imezunguka eneo lenye matanki ya maji, cha ajabu eneo hili lilikuwa kavu kabisa hakuna dalili ya kumwagika maji.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni