MY DIARY (5)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mtunzi: __
SEHEMU YA TANO
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Akanisimamisha na kuanza kuiuliza maswali mengi yasiyo na maana huko akionekana kutojiamini. “samahani dada, sijui unaelekea wapi”? Nikamjibu dukani. Akavuta pumzi ndefu na kuniambia ok, nisaidie namba zako za simu. Nikamwangalia juu na chini nikwambaia nimezisahau na simu nimeiacha ndani nikirudi ndani nitakuletea..
TUENDELEE...
Akaishiwa pozi akanambia, nikombe kitu komoja kama hautojali… “kitu gani sema haraka mimi nasikia njaa nilimjibu kwa ukali” Alasema hapa nimenunua nyama kilo moja na kule ndani nina viazi unaonaje tukajiunga pamoja.Nikacheka kwanza na kumuuliza kwani wewe hujui kupika? Akajibu hapana wewe njoo bhana au hujiamni? Akaendelea ujue mambo ni kusaidiana na chakula anachopika mwanaume ni tofauti na anachopika mwanamke…
Hapo kimoyo moyo nilishakubali maana kuliko kushindia mayai mawili ya mia tano si bora kula rosti ya chipsi ya burebure.Ikabidi nimkubali huku nimtania kwa kumwambia umwogopi mkeo? Akacheka na akongoza njia mpaka chumbani kwake na sikuaamini macho yangu kwani ile naingia tu nilikaribishwa na harufu nzuri aliyopulizia kwenye chumba chake. Kwa kweli lilikuwa ni gheto zuri sana ambalo mwanamke yeyote akiingiz lazima angeshtuka kutokana na jinsi lilivyopangiliwa na usafi mzuri. Akanikaribisha kwenye sofa la ngozi na nilipokaa tu alienda moja kwa moja kwenye friji akachukua vinywaji vya aina tatu, juice, wine na soda za kopo. Akanisogezea kimeza cha kioo na kuniambia karibu.
Kwa haraka haraka na mbwembwe zangu za kitoto nikamuuliza hakuna maji, swali lilomshtua kwani yeye alijua kwa idadi ya vinywaji alivyoleta alikuwa kamaliza kazi. Niliamua kumsumbua tu lakini kiukweli niiitamani iloe wine huku nikukumbuka lile tukio la Mwalimu John. Akafungua friji akaniletea maji na bia za kopo mbili akimaanisha kuwa hataki tena usumbufu
Basi nikafungua nikanywa glass moja na kwa kuwa njaa ilikuwa ikinisumbua nikachukua juisi nikanywa tena glass moja. Akawasha flat sreen iliyokuwa mbele yangu kisha akaniletea remote akiwa na maana nichague nitakayo ipenda niendelee kuangalia.Sikumwelewa maana nilijua ataniletea viazi niendelee kumenya kwa kuwa nilimwambia nasikia njaa.Kama alikuwepo kwenye akili yangu ingawa hakuniletea viazi nimenye aliniletea matunda na karanga niendele kula. Kimoyomoyo usikute ananiwekea madawa anizimishe maana alionesha dhairi anapagwa natoto la kibantu.
Sikujivunga nikaendelea kula vitu taratibu, mara apple, papai na vingine sijui hiyo friji ilikosa nini.Basi nikachagua CD moja iliyoandikwa Asian Romantic nikaweka na kuanza kuiangalia na yeye alikuwa bize akikata kata nyama.Nilimwomba nimsaidie lakini aliktaa akasema nyie si mnafikirii wanaume hawajui kupika ngoja leo nikonyeshee.Kimoyomoyo nikasema afazali maana hata mimi uwongo dhambi nilkuwa sijui kupika vizuri ndio usishangae hii ni kutokana na malezi niliyolelewa na baba yangu.
Nyumbani mimi sikuwahi kupika na isingekuwa ile kozi ya mapishi niliyosoma kule o’level mbona ingekuwa kasheshe. Kaka wa watu aliendelea kupika na mimi kuangali movie ile niliyoichagua. Mara hee kumbe bhana ile CD huko mbele watu walikuwa wakichakachuana live(wakifanya mapenzi). Niliamua kupunguz asauti ili niendelee kufaidi ya duniani. Kumbe wahindi na wao wamo lakini nilivyoona naweza kuzidiwa na kuleta majanga niliamaua kubadilisha na kuweka CD ingine.
Japo yule alijifanya kuniuliza hiyo CD ni nzuri sana ungefoward tu hiyo sehemu na uendelee kupata love stories. Sikumjibu kitu maana niliona nia yake sio nzuri. Niliendelea kuangalia movie huku zile za season niliamaua kuziweka pembeni ili nikitoka nimwombe nikaziangalizie kwangu.
Nilikuwa free utazani huyu kijana tulijuana mda mrefu. Niliomba chakula kiendelee kuchelewa ili niendelee kufaidi kwani nilichoshwa sana na mimi kila siku kujifungia ndani kama mwali.Basi baadaye chakula kiliiva kikaletwa mezani nikajipakulia mwenyewe mtoto wa kike na kuendelea. Niliamua kujitoa ufahamu nikaacha maringo kwani nijilijua nikitoka hapo kukutana na chakula ni mpaka kesho tena. Tulikula huku tukipiga stori za hapa na pale.Kubwa zaidi ilikuwa ni kufahamiana.
Alijitambulisha kuwa yeye anaitwa Ally ni afisa wa wanyamapori huko TANAPA na mda mwingi yupo porini. Ila wiki hii alikuwa amechoka kwani walikuwa huko mikumi wakikusanya data kwani yeye yupo kitengo cha utafiti(research). Alijinadi vya kutosha na kutokana na sera zake ata mimi nililowana. Nikatokea kuvutiwa ghafla na kijana huyu anayeonesha kujitambua na kujua nini maana ya maisha.
Nilimwacha atawale mazungumzo kwani mimi siku zote sikupendaga mtu ajue historia yngu ya maisha. Basi baada ya kula aliweka filamu kali tukaanza kuangalia niliytamani kuaga lakini niende wa[pi na kufanya nini. Basi kwa kuwa na yeye alisema alikuwa hana pakwenda tuliendelea kukaa hapo mpka giza likaingia. Kila nikiaga alikua akikataa na kuniomba niendelee kumpa kampani. Na pia alitumia kigezo cha kusema subiri movie iishe wakati ni dhairi shairi hata ningesubiri kiasi gani ile movie isingeisha maana ilikuwa ni collection na labda uangalie kwa mda wa siku tatu mfulilizo.
Usiku ulivyozidi niliondoka na kuingia chumbani kwangu na kujitupa kitandani huku nikiendelea kutafakari mambo yaliyotoka siku hiyo, nikakumbuka jinsi kaka wa watu alivyochanganyikiwa baada ya kuniona nikiwa ndani ya kanga moja. Nikajisemea “ inaonekana ni mkarimu sana”.Basi nikaamua kupotezea mawazo hayo lakin kabal sijalala mara akanitumia meseji inayosema asante kwa kampani yako nimefurahishwa na wewe sana na ningeoenda urafiki wetu uendelee na ikibidi uwe zaidi ya urafiki. Niliielewa vizuri ile mesji lakini niliijibu kisanii “asante, karibu tena”> Kauli ambayo siku zote uwa inawachanganya wanaume wengi. Aliendelea kunichombeza kwenye meseji mpaka nikapitiwa na usingizi
***************************
Siku zilienda huku nikisubiri wikiendi ifike ili niweze kukutana na mwalimu John mawanume wa kwanza kuujua mwili wangu na kufaidi maungo mazuri niliyojaliwa na mungu. Ndio usishangae ndugu msomaji mwanamke ni tunda, pambo, mlezi, mshauri na mlezi. Sijisifii lakini mpaka sasa nasubiri matokeo ya kujiunga na chuo ni mwanaume mmoja tu ndo nilishawahi kukutana nae.
Ni ijumaa tulivu mida ya saa kumi jioni huku mji wa Moshi ukiwa umetawaliwa na kibaridi cha wastani hali ya hewa ambayo nilikuwa nikiipend sana
Nilikwenda stendi kwenda kumpokea mwalimu John. Alinambi alikuwa amepanda Bus la Kilimanjaro hivyo hawatashukia stendi bali kwenye ofisi zao.
Nilikuwa na hamu sana ya kumwona klwani nilimmiss sana.
Wakati naendelea kumsubiri kuna mtu alinigusa begani, nikageuka kwa haraka na kukutana na tabasamu kali la kijana mmoja ambaye alikuwa ni shombeshombe aliyefuga nywele utazani mtoto wa kike.Sikuongea kitu zaidi ya kumsilkiiza lakini chs ajabu na yeye hakusema kitu zaid ya kutabasamu hivyo nikaingia na hofu na kumuuliza samahani nikusaidie nini.? Akanipa hearphone zangu ambazo niliziangusha pembeni kisha akanambia “am Chriss”(naitwa Kris) nikamjibu thank u am Leah. Hatukuweza kuongea tena kwani gari tulilokuwa tunalisubiri lilikuwa limeshafika hivyo akaingia mfukoni na kutoa business card yake na kunikabizi.
Sikutaka kuikataaa, niliichukua nikaitupia kwenye pochi yangu na kumpa ishara ya kumwaga na kwenda kumkumbatia Mwalimu John. Alikuwa yupo simpo sana siku hiyo mpaka nikashangaa kwani alikuwa amevaa hizi kaptura za kisasa na kifulana cha kubana na sendo na mkononi na alikuwa na kibegi kidogo vile vya kimichezo. Kidogi nimsahau yaani yule mwalimu aliyezoea kuvaa suruali na kuchomekea mda wote leo hii amevaa kisharobaro. Basi nikajua ni zile mbinu zake anazotumiaga maana alishawahi kunielza kuwa eti yeye ni usalama wa taifa. Mimi huwa simwamini sana maana hawa watu nasikiaga eti hata wake zao huwa hawawajui. Tuliongea mawili matatu na kuniuliza tunaelekea wapi mwenyeji wangu?
Mimi sikuwa na jibu la swali hilo niliridisha mpira kwake “sema wewe boss wangu tunaeleka wapi maana mimi moshi bado mgeni”Tukaingia kwenye tax na moja kwa moja tulipelekwa Leorpard Hotel.Sikujua kwa nini alichagu hapo lakini palikuwa ni katikati ya mda.Tukaingia ndani na mwalimu John alibadilisha nguo na kwenda kuoga. Nikajifanya kama sijamwona na mimi nikaendelea kuangalia uzuri wa kile chumba, kwa kweli kilikuwa ni kizuri na kilikuwa na kila kitu mpaka huduma ya internet. Basi alitoka bafuni na kuvaa kibukta fulani hivi kizuri chenye rangi za kuvutia. Akaja kitandani tukakaa na kuanza kupiga stori, tuliongea mengi sana na zaidi zilikuwa ni lawama zilizoelekezwa kwangu kuwa kwanini sikumtafuta miezi yote hiyo na hili nilibadilisha namba na sikutaka kumwambia.
Kimoyomoyo nikajisemea ungejua ni hizi shida za masiha ndo zinanifanya nichanganyikiwe asingenilaumu.Hapa ngoja nikupe siri moja, ujue sisi wasichana wakati mwingine mwanaume anaweza kuwa anakupenda sana lakini usirizike kuwa nae.Huyu mwalimu mimi nilikuwa simkubali kihivyo sema faida aliyopata ni ile ya kuwa mwanaume wangu wa kwanza aliyenifundisha mapenzi ni nini. Lakini kitu kingine kilichonifanya nimtafute ni shida si unakumbuka nilikuwa nadaiwa kodi na niliomba nipewe wiki moja tu na siku hiyo ilikuwa ni ijumaa hivyo zilibaki siku mbili tu
Basi nilimwomba msamaha na kumwambia ni shida za maisha tu ndo zilikuwa zikinisumbua. Sikutaka kumweleza yote kwa haraka kwani angeshtuka sana hivyo nilienda nae taratibu.. Wakati tukiendelea na stori simu yake ilikuwa ikiiita sana lakini alikuwa hataki kupokea, kitu ambacho kitu ambacho kilinishtua nikamwambia “please pokea simu yako kabla hujanikera”Ilivyoita tena akapokea, nikatega sikio nisikie anaongea na nani siunajua tena wivu lazima. Kumbe walikuwa ni marafiki zake wa moshi, wakamwambia wanamsubiri mahali wakutane.
Basi alivyokata akanambia kuna club moja nasikia imefunguliwa huku Moshi inaitwa Club La Liga hivyo inazinduuliwa leo na marafiki zangu wanataka tuende.
Vipi tunaweza kwenda wote aliuliza John. Nilikosa jibu la swali hilo kwani sikujiandaa kwenda club si unajua tena kila sehemu na mavazi yake. Kipindi hicho nilikuwa bado ni mshamba hata club nilikuwa sijawahi kwenda na pia bado nilikuwa na akili za kitoto. Alinishauri sana tuende wote kwani kuwa na marafiki ni jambo zuri.
Akanambia kuwa wamemwambia wapo East Africa Pub na tayari wamaeshaagiza mkuu wa mbuzi. Mmmmhhhh kusikia mguu wa mbuzi mate yalinijaa mdomoni. Basi kwa harakaharaka nikamwambia naomba niende niende nyumbani nikachukue viwalo vya club kisha nitawakuta hapo.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni