DHAMANA (8)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mwandishi: Hassan O Mambosasa
SEHEMU YA NANE
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Alipogeuka ili aone vizuri kwa kudhani labda anaona maruweruwe tu ndipo akajikuta akipokea kofi zito lililompeleka hadi chini, alipoinua uso wake alikutana uso kwa uso na yule mtoto ambaye aliwatokea Hisan na Hamid muda mfupi kabla hawajaiaga dunia.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
"Huna akili kweli yaani unataka kusoma dua chooni kisa umeniona mimi, toka lini jina la Muumba likatajwa chooni wewe na hata ungesoma unafikiri angekusaidia wakati muda unaingia chooni hukumkumbuka hata kidogo kwa kumuomba akulinde ukiwa humu" Yule mtoto aliongea huku akisikitika.
"sio mimi nisamehe" Hussein aliongea huku akitetemeka akiwa amekaa kitako kwenye sakafu ya maliwatoni hapo.
"Heh! Kwanini siyo wewe, inamaana huitwi Hussein Buruhan mtoto wa tano wa mzee Buruhan" Yule mtoto alimuambia Hussein huku akionekana kushangaa kwa jinsi anavyoongea.
"ndiyo mimi Hussein" Hussein alijibu huku akitetemeka kwa uoga.
"basi kama wewe ndiyo Hussein basi ndiyo wewe" Yule Mtoto aliongea kwa hasira kisha akamsogelea Hussein kwa kasi sana na alipomfikia alimkaba kooni hadi akawa hawezi kupumua vizuri, alimnyanyua juu akambamiza kwenye kioo kikubwa kilichokuwa kipo humo ndani juu ya masinki ya kunawia. Hussein alikatwa na vipande vya vioo na akajikuta akipiga kelele za kuomba msaada huku akimtaja mama yake kama ilivyo watu wengi wakiwa katika matatizo, kelele hizo hazikusaidia chochote kwani kipigo kiliendelea kama kawaida na alizidi kumtaja mama yake.
"Watu kama nyinyi ndiyo mungu hawasaidii hata kidogo, yaani unamkumbuka mama yako kwenye shida halafu unamsahau Mungu wako anayekupa pumzi hizo zinazokutia jeuri. Haya nipe upesi" Yule mtoto alimuambia Hussein.
"si.....sina" Hussein aliongea kwa tabu kutokana maumivu ya kipigo alichokipata.
"ohoo! Huna, basi utaenda kuonana na kaka yako Hamid huko roho yake ilipo" Yule mtoto aliongea kisha akajizungusha kama pia hadi kikatokea kimbunga kilichomzoa Hussein akawa yupo katikati, milio ya makofi ndiyo ilifuatia akiwa yupo humo ndani ya kimbunga hicho na makelele ya maumivu yakawa yanasikika. Kimbunga hicho kilipokuja kuisha Hussen alitupwa chini akiwa amevunjika sehemu mbalimbali za mwili wake, Yule mtoto bado alikuwepo na safari hii alikuwa yupo karibu yake zaidi na mkono wake wa kushoto ukiwa umekamata koo la Hussein.
"salamu zao kwa waliotangulia kabla yako" Yule mtoto aliongea kisha akalivuta koromeo la Hussein hadi akalitoa nje kiaha akalivunja akautoa mfupa wake akauweka pembeni, Hussein tayari alikuwa amekwisha maliza mkataba wake wa kuishi duniani hadi muda huo akiwa miongoni waaiokuwepo duniani kimwili.
****
KITUO CHA POLISI CHUMBAGENI
TANGA
Baada ya yule mama kuvamia mwili wa yule mwanaume aliyekutwa kwenye majani amekufa katika ajali ya gari ya Hamid, yule Inspekta aliamuru yule mama awekwe chini ya ulinzi kwa mahojiano zaidi na alipelekwa kituo cha polisi Chumbageni kusubiri Inspekta arudi ili afanye mahojiano naye. Inspekta yule aliporudi kituoni baada ya kumaliza kusimamia kazi kule barabarani yule mwanamke aliingiza kwenye chumba cha mahojiano, yule inspekta aliingia katika chumba cha mahojiano akiwa na maaskari waliokuwa wadogo kivyeo.
Naitwa Inspekta Ismail Mdoe, kulia kwangu yupo Sajenti Juma Shehoza na kushoto kwangu kuna Staff sajenti Dickson Mushi, sijui mama unaitwa nani?" Yule Inspekta ambaye ndiye Inspekta Mdoe aliongea huku akitoa utambulisho kwa wenzake.
"naitwa Mwanamkuu Jumanne" Yule mwanamke alijibu kwa unyonge.
"Ok Bi Mwanamkuu una umri gani, unafanya kazi gani na unaishi wapi?" Inspekta Mdoe alimuuliza.
"nina miaka 48 nafanya biashara ndogondogo, ninaishi hapahapa Chumbageni" Bi Mwanamkuu alijibu kwa unyonge, muda huo Sajenti Shehoza alikuwa akiandika kila kilichokuwa kinafanyika kwenye mahojiano hayo.
"wewe na marehemu mna uhusiano gani?" Inspekta Mdoe aliuliza.
"Marehemu ni mume wangu" Bi Mwanamkuu alijibu.
"ok, unaweza ukatuambia kilichokufanya utamke yale maneno kwenye eneo la ajali?" Inspekta Mdoe alimuuliza.
"afande chanzo cha kutamka maneno yale ni kutokana na mume wangu kuingilia mambo yasiyomuhusu na hatimaye akauawa" Bi Mwanamkuu alizidi kuongea na safari machozi yalikuwa yakimtoka.
"una uhakika gani na hayo unayoyasema? Hebu fafanua kauli yako" Staff sajenti Mushi alimuuliza kwa mara ya kwanza.
"muda mfupi kabla mume wangu alikuwa akiendelea na kazi zake za uganga, alipandisha maruhani yake akasema kuna mtu yupo hatarini kuuawa hivyo anahitaji kumsaidia. Akichukua vifaa vyake vya uganga akaenda huko, na sikumuona tena hadi niliona mnambeba" Bi Mwanamkuu aliongea huku akilia, maelezo hayo yaliwafanya maaskari hao waliokuwa wanamuhoji watazamane kwa muda wa sekunde kadhaa.
"Mama usituletee maelezo yasiyokuwa na uthibitisho wowote" Inspekta Mdoe aliongea akionesha kuchanganywa na maelezo aliyoambiwa.
"Afande hii siyo kiwango chenu naomba muiache na huyu mbaya wangu aliyeniulia mume wangu nitamkomesha" Bi Mwanamkuu aliongea kwa hasira kisha akaanza kuangaza pande zote za humo, alianza kunguruma kama simba akiashiria mashetani yamempanda. Maaskari waliokuwa wanaomuhoji walibaki wakimtazama tu wakionekana kuwa hofu nae, Bi Mwanamkuu aliposimama akionekana ana hasira kimbunga kizito kiliibuka humo ofisini kikamzoa na kilipotoweka naye alitoweka papo hapo.
****
Mfanyakazi wa kampuni ya Matro anayehusika na usafishaji vyoo na korido katika ghorofa la kampuni hiyo alianza kufanya kazi kama ilivyokuwa kawaida yake, alianza kufanyakazi katika ghorofa tofauti na mwishowe akamalizia katika ghorofa ya mwisho ambayo ndiyo inapatikana ofisi ya mmiliki wa kampuni hiyo. Kijana huyo anayeitwa Niko alianza kusafisha korido mbalimbali za ghorofa hiyo na hatimaye zamu ya kusafisha maliwato za ghorofa hiyo ya mwisho ikaanza, alianza kwa kusafisha maliwato ndogo na hatimaye akahamia kwenye maliwato kubwa ambayo ipo jirani na ofisi ya mmiliki wa kampuni hiyo.
Akiwa na kotoroli chenye vifaa ambacho alikiburuza hadi katika mlango wa maliwato hiyo kisha akaupa mlango mgongo akawa anakiburuza kitoroli ili aingie nacho ndani akiwa ameufungua mlango kwa kuusukuma na mgongo wake. Alifanikiwa kuingiza kitoroli hadi ndani akiwa anaimba kwa kuchangamka akiwa ameungalia mlango na ameipa mgongo sehemu ya ndani ya maliwato hiyo, akichukua fagio lenye nyuzi maalum kwa kufanyia usafi akaanza kufanya usafi kuanzia mlangoni na sehemu za pembeni ya mlango.
Baada ya kumaliza kufanya usafi maeneo hayo ndipo alipogeuka nyuma ili aendelee na usafi akakutana na hali isiyopendeza kutazamwa. aliuona mwili wa bosi wake mkuu ukiwa upo chini na koromeo lipo pembeni ya mwili huo. Niko alijikuta akitoa ukelelewa uoga kisha akakimbia kuelekea mlangoni, aliponyeza kitufe cha kengele ya hatari ya ghorofa kisha akakaa kitako akawa kama mtu asiyejielewa kabisa.
Mlio wa kengele ya hatari katika jengo lote ulisikika na kupelekea kundi kubwa la wafanyakazi litoke nje ili kuchukua tahadhari kama kuna uwepo wa jambo la hatari, walinzi wa kampuni wenye silaha wakaanza kupandisha wakiwa na tahadhari kubwa kwani kengele hiyo ilimaanisha jambo la hatari. Walinzi hao walipita kwenye ghorofa mbalimbali kwa tahadhari na hatimaye wakafika ghorofa ya mwisho, walitembea kwa tahadhari katika ghorofa hiyo hadi walipomuona Niko wakamfuata huku wengine wakiwa wanaangalia usalama. Walipomfikia Niko aliishia kuonesha kidole ndani ya maliwato ndipo maaskari hao walipoingia huku wengine wakimuuliza maswali ambayo hakuyajibu zaidi ya kutetemeka. Walinzi walioingia waliwaita wenzao wakajionea kilichotokea humo ndani ya maliwato, simu ilipigwa haraka kituo cha polisi ambapo polisi walifika ndani ya muda mfupi tu wakajionea hali halisi na wakachukua vipimo mbalimbali pamoja na kuuchukua mwili wa Hussein.
****
Maeneo hayohayo ya Raskazoni kwa upande mwingine kulikuwa kuna mzee wa makamo aliyekuwa akiangalia luninga sebuleni, alikuwa ni mzee wa miaka takribani hamsini na ushee ingawa alionekana kutozeeka sana. Wakati mwili wa Hussein ukiwa umeondolewa kule kazini na ukiwa tayari umeshafikiishwa hospitali ili kuhifadhiwa, mzee huyu aitwae Shafii Buruhan alipigiwa simu na alipoipokea na akasikia alichokisikia alizidi kuchanganyikiwa na akabaki akilia kwa sauti kama mtoto mdogo hadi mkewe akaja sebuleni akamuona mume wake akiwa katika hali hiyo.
"Baba Zayina kuna nini?" Mke wake aliimuuliza baada ya kumkuta akiwa analia kama mtoto.
"wadogo zangu Hamid na Hussein mama Zayina" Shafiu alijibu huku akilia kwa kushindwa kustahimili jambo aliloambiwa.
"wamefanyaje tena?" Mke wake aliuliza akionekana kutoelewa.
"hatunao tena duniani, wadogo zangu mimi jamaniii" Shafii alijibu huku akilakamika na mke wake akaanza kumbembeleza huku yeye mwenyewe akilia baada ya kusikia mashemeji zake wamefariki. Shafii alilia sana kama mtoto mdogo kutokana na vifo hivyo, mkewe naye alikuwa ana kazi ya kumbembeleza ingawa hata yeye alikuwa akitokwa na machozi.
"Baba Zayina jikaze wewe ni mwanaume" Mke wake alimwambia huku akimfuta machozi, muda huo mlango wa hapo sebuleni ukafunguliwa na akaingia mwaume alivaa kinadhifu.
"Ally mdogo wangu" Shafii akimuita yule mwanaume kwa jina lake halisi.
"Kaka kuna nini mbona unalia" Allu alimuuliza kaka yake.
"kaka zako Hamid na Hussein hatunao" Shafii aliongea kwa huzuni huku akitokwa na machozi, Ally aliposikia taarifa hiyo alijikuta akikaa chini kisha machozi yakaanza kumtoka ingawa hakutoa sauti kuashiria analia.
"Ally jikaze twende hospitali tunahitajika" Shafii aliongea akinyanyuka macho yakiwa mekundu kwa kulia, aliingia ndani halafu akarejea akiwa amevaa viatu na miwani ya jua ili kuficha macho yake.
"Farida sisi tunatoka, wewe baki. Ally twende" Shafii alisema huku akimnyanyua, kisha wakaondoka hadi nje.
***-
Taarifa ya kifo cha mmiliki wa kampuni ya Matro tayari zilishawafikia waandidhi wa habari na hadi anafikishwa katika chumba cha kuhifadhi maiti tayari waandishi wa habari walikuwa wamejaa nje ya chumba hicho wakisubiri kupata habari kamili. Hadi gari aina ya Cadillac la milango sita linawasili jirani na mlango wa chumba cha kuhifadhia maiti bado waandishi wa habari walikuwa wamejazana eneo hilo, dereva wa cadillac hilo aliposhuka kwenda kufungua mlango waandishi wa habari walikuwa wapo makini kujua anayeshuka katika gari hilo la gharama ni nani.
Shafii alipotangulia kushuka kamera mbalimbali za waandishi wa habari zilikuwa zikifanya kazi ya kumpiga picha tu, waandishi wa habari walikimbilia kumuuliza maswali mbalimbali lakini hawakupata ushirikiano.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni