MY DIARY (20)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mtunzi: __
SEHEMU YA ISHIRINI
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Nikamwambia kuhusu namba zangu za simu amuombe aliyemtuma anisaidie na kuhusu hilo la pili je hatuwezi kufanya kesho kwa sababu kuna mahali nilikuwa nikienda? Alifikiria kwa sekunde kadhaa na kuniambia kuwa hapana anaomba nimsaidie leo kama yeye alivyonisaidia mimi kwa sababu ningekuwa kwenye foleni nisingeweza kuondoka kirahisi hivyo kama ninavyofikiria.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
TUENDELEE...
Maneno hayo yalinigusa na sikuwa najinsi zaidi ya kumsaidia.
Tukaondoka na huyo dada na kuelekea bank na tukiwa njiani Joyce alinipigia na kuniuliza kama nilifanikiwa? Nikamwambia asante sana shoga yangu lakini Yule kaka ni nani maana alikuwa anaomba namba zangu za simu. Akanambia achana nae yeye ni mtu mdogo sana kwani yeye aliongea na Lecture wake na yeye alipewa oda tu. Hapo sikuwa na la kusema zaidi ya kumpa heshima yake maana yeye alikuwa akijulikana kila mahali. Basi tulivyofika bank nikamkumbuka Yule kaka aliyenisaidia kulipai ada lakini kosa nililolifanya zile namba zake alizonipa sikumtafuta kabisa.
Nikawaza haraka haraka kwa jinsi nilivyochoka na sikuwa tayari kupanga foleni niliamua kutumia ujasiri wa kumpigia. Huwa sipendi sana tabia ya kujitambulisha hivyo alivyopokea tu nilikata na yeye akapiga . Nilimwambia nipo kwanye foleni na nahitaji msaada wake. Dakika tano baadaye nilimuona kaunta akiaangaza macho huku na kule. Ilibidi nichukue zile hela kwa Yule dada na sikutaka kupoteza mda nilisogea nikamapa na akazipelaka kwa muhudumu mwenzake. Akanambia kwenye meseji nimsubiri kama dakiak 5 na baadaye nilimwambia Yule dada atoke kwenye foleni. Yule dada uvumilivu ulimshinda na kuniulizza nimejua huyo meneja wakati mimi ni mgeni.
Nikamjibu kuwa mimo sio mgeni na tulifahamiana siku niliyokuaja kulipa ada.
Akanambia kuwa makini mdogo wangu kwani hata yeye aliuwa akifahamiana nae lakini walikuja kugombana kwa sababu alimtaka kimapenzi. Sikumjibu kitu
kwa sababu hata mimi sikuwa na mawazo yoyote juu ya mwanaume huyo lakini pia sikushangaa kauli yake hiyo kwa sababu wanaume wa siku hizi ndivyo walivyo. Baada ya hizo dakiaka 5 tulifanikiwa na safari ya kurudi chuoni ilianza. Tulifika chuoni na mimi nikakamilisha swala hilo fasta na kurudi ghetto kwangu. Na Yule dada aliatambua mchango wangu akanipa elfu 10 kama ya asante. Sikutaka kudengua kwa sababu hata mimi sikujua kesho yangu.
Basi mimi nikawa nimeingia chuo kwa mtindo huo wa kuunga unga na kujitoa sadaka kuhusu mwili wangu. Maisha ya chuo yalizidi kuwa magumu kwangu kwani ilifika pahala mimi nikawa nakosa hata hela ya kula. Kwa bahati nzuri marafiki zangu wote niliowapata chuo walikuwa na mikopo hivyo siku moja moja wakawa wananisaidia. Uzuri wangu wa sura na umbo ulizidi kupotea siku hadi siku kutokana na shida nilizokuwa nazipitia.
Ni miezi mitatu sasa imepita na nilishaamua kupunguza mawasiliano kabisa na Joyce kwa sababu kazi zake za kujiuza na masoma ni vitu viwli tofauti. Hivyo hali ilizidi kuwa ngumu sikuwa na kipato chochote na sikuwa tayari kujiuza tena maana nilishabadilisha tabia. Nakumbuka siku moja kuna Lecture mmoja aliniita na kuniuliza kwa nini siku hizi najiweka rafu rafu tofauti na siku za mwanzoni. Sikutaka kumficha niliwambia ukweli wa mambo ili kama atapenda kunisaidia basi anisaidie. Yaaani kweli wanaume wa siku hizi ni penda penda kwa sababu mwalimu huyo alikuwa akinihudumia kwa siri lakini mwisho wa siku alinitongoza na kutaka kutembea na mimi.
Sikuwa na jinsi tukawa tunafanya mapenzi ya siri. Siri ilikua ni kubwa sana kwa sababu yeye alikuwa na mke wake. Tuliendelaea kusaidiana kimaisha na hata somo lake nilipata A. Huduma za mwalimu huyo zikanisaidia na uzuri wangu ukaanza kuonekana na nikawa napata maombi mengi sana ya kimapenzi kutoka kwa walimu na wanafunzi pia. Nilikuwa mjanja sana na wanafunzi wengi nilikuwa nikiwachuna tu. Lakini maji yalipozidi unga wapo wengine ilinibidi niwaonjeshe asali yangu niliyopewa bure na mwenyzi mungu.
Sikufichi ndugu msomaji hapa chuoni nilitembea na wanaume wengi sana hasa wale vinga’aninizi ambao pamoja na kuwaaambia na mchumba wangu hawakukomaa kunisumbua. Kwa hiyo nilikuwa siingii mikataba ya kudumu na mtu kwenye mapenzi zaidi ya siku moja au mbiili kama ikibidi. Hali hiyo ilinisababishia majanga makubwa sana kwani nakumbuka siku moja tulienda club na kjana mmoja raia wa South Africa. Kijana huyo alitokea kunipenda sana na alinisaidia sana kiuchmi. Siku hiyo lilitokea bonge la vurugu huko club kwani kuna kaka mmoja ambaye ndio Mr University alishaweka appointment na mimi siku hiyo lakini baadaye nili mblacklist akawa hanipati kwenye simu na hiyo ni mara baada ya rafiki yangu Joyce kuniambia anakuja Moshi.
Nilishindwa kubalance mambo hivyo sikuwa na jinsi zaidi ya kumfanyia hivyo. Wakati najiaandaa kwenda kumpokea Joyce msouth naye alikuwa akinisumbua sana. Siku hiyo kwa kweli ilikuwa ni ngumu sana kwangu kwa sababu chuoni kulikuwa na welcome freshers sherehe za kuwakaribisha wanafunzi wapya.
Siku hiyo huwa nzuri sana kwa wapendanao lakini huwa ni ngumu sana kwangu kwa sababu kila mtu alitaka kutoka na mimi. Mbaya zaidi mama ya tauni rafiki yangu Joyce alikuja na huyu akijaga huwa naua ratiba zangu zote. Kwa hiyo wakati natoka kwenda kumpokea Joyce nilikutana na msouth akija kwangu. Na kwa jinsi alivokuwa king’ang’anizi ilibidi niende naye na tayari Joyce alishatafuta chimbo akanambia nimkute huko. Tuliendelea kula na kunywa na cha ajabu Joyce siku hiyo alikuwa mwenyewe na hakuonekana kuwana ratiba ngumu kama ilivyokuwa siku za nyuma.
Baada ya kukaa kwa mda mrefu sehemu hiyo maaraufu kama Cash Mooney Pub, Joyce alinipa sigino kuwa leo kuna kazi ya wazungu kwa hiyo kama nipo tayari tuwaite waje hapo. Hali ikazidi kuwa ngumu hivyo nikatangaza kurudi ghetto mida hiyo jambo ambalo lilimshangaza Msouth ikabidi na yeye aendelee na ratiba zake. Basi Joyce alinambia tuende club ili hao wazungu watukute huko. Kumbe na Msouth naye aliamua kujiendea zake club mara baada ya kuona ratiba zangu kuwa zimekuwa ngumu.
Tulivyoingi club tuliamua kwenda kukaa kaunta tukiwasubiri hao wazungu waje. Baada ya mda mfupi tangia tuingie Msouth alikuja pale tulipokaa na hakutaka kuongea mambo mengi bali alisimama nyuma yangu na kunishika kiuno ishara ya kuonesha jamii kuwa mimi ni ake.Wote tulipigwa na butwaaa na kujiuliza huyu mtu amefikaje fikaje club wakati sisi tulimkimbia na kujua lazima atarudi chuoni kuendela na sherehe za kuwakaribisha wanachuo wapya (welcome Freshers). Nilimtoa mikono yake kiunoni mwangu na kumwambia haya tununulie bia.
Wakati akiendelea kutafakari ombi langu la kununuliwa bia Yule kijana ambaye ni Mr University alikuja na sijui na yeye alitokea wapi. Nilitamani kuyeyuka na kupotea eneo hilo maana nilijua kuna fujo zinaeza kutokea mda wowote. Huyu MR alikua na hasira sana na mimi na kilichomkera ni kile kitendo cha Msouth kunishika kiuno. Na kwa jazba alizokuwa nazo aliniuliza huyu ni nani yako akimaanisha Msouth?
Na mimi nilimjibu kwa dharau labda nikulize wewe kwan wewe ni nani kwanza? Kauli hiyo ilimboa na kunizaba kibao cha nguvu. Nikaona maluilui nikajianamia zangu chini na kuanza kuugulia. Joyce na yule Msouth waliamua kumshughulika vilivyo kitua ambacho kilizua zogo. Yule kaka alipewa kipondo cha maana na nilimsikia akisema niachieni nimfundishe adabu kwani hawezi kutuchanganya sisi. Ameshakula vyangu malaya huyu na kumbe leo amenikimbia ili aje kufanya umalaya wake huku aliendelea kusema Mr University. Kumbe na yeye alikuwa na kampani yake kubwa tu siunajua tena sharobaro huyo alikuwa ni marufu sana chuoni na alikuwa na vijehela.
Masikini ya mungu msouth naye aliwekwa kati na kupewa kipondo cha maana na alikuja kuokolewa na mabausa. Joyce nilikua simwoni maana sijui alichomokea wapi.Wale mabaunsa walikuwa kweli ni wababe kwani waliwachukua wote wawili na kuwaotoa nje na huko waliwafanyia ubabe sana kwani waliwamwagia maji mwili mzima.Mimi nikaendelea kumtafuta Joyce kila kona sio Chooni, sio kaunta sio stagini hakuonekana kabisa.
Ikabidi nitoke nje kabisa huko nikakuta mabwana zangu wawili yaani Msouth na Mr wakipewa funsisho kwani waliwekwa chini ya ulinzi na nilsikia wakiambiwa kuwa siku hiyo lazima wakalale ndani kwani haiwezekani kugombea mke wa mtu. Huyu si ni mke wa Lecture wenu kabisa sisi tunamjua alafu nyinyi manajifanya vidume wa kuleta fujo walisema wale mabausa. Ilinibidi nimwite bausa mmoja pembeni na kummuuliza habari za Joyce. Akanijibu kuwa ameondoka sa hivi na wazungu ebu mpigie.
Kweli siku hiyo nilikuwa nimechanganyikiwa kwa sababu nilikuwa sina wazo kabisa la kumtafuta kupitia simu.Nilijaribu kumpigia simu lakini cha ajabu simu yake ilikuwa haipatikani. Nikazidi kuchanganyikiwa nisijue nifanye nini.Ilinibidi niende kuongea na wale mabausa na kuwaomba wawasamehe wale vijana.
Walinielewa na wakasema suluhisho hapo ni kwamba kila mtu na kampani yake waondoke hapo watafute sehemu ya kwenda. Ilinibidi niongozane na wale mabausa mpaka ndani ili kuwatafuta marafiki zao.
Harufu ya damu ilikuwa ikinukia kabisa kwani nilihisi kuwa na mimi naweza kupigwa huko ndani mda wowote. Tuliwafanikiwa kuwapata marafiki wa kamapani zote mbili lakini ajabu tulipotoka nje hatukumkuta MR na kumbe alishaamua kupanda bodaboda na kusepa zake.Nikajisemea laity vurugu hizi zingetokea chuoni basi watu wange discontinue (wangefukuzwa chuo). Kwa hiyo Msouth aliruhusiwa kuendelea kufurahia huduma za club lakini kwa sababu mbaya wake alishaondoka nay eye aliamua kuondoka. Nikabaki hapo nje na bausa nisijue nifanyaje. Mbaya zaidi Joyce alikuwa ameondoka na pochi yangu.
Nilichanaganyikiwa kweli kweli kwa sababu nilikuwa sina hata nauli ya kupanda bodaboda
Niliendela kung’aa sharubu hapo nje na baadaye nilimwita bodaboda na kumwambia anipeleke ghetto kwangu.Nilijua kama ningefanikiwa kufika home ingekuwa nimesolve tatizo kwa sababu hata simu yangu iliisha chaji.
Siunajua tena hizi smartphone zetu hazikaai na chaji kabisa.Tulifika nikaingia ndani nikachuka hela na kumlipa dereva wa bodaboda akasepa zake. Sikuweza hata kubadilisha nguo kwa stess nilizokuwa nazo nikajitupa kitandani hivyo hivyo.Niliwaza sana kwanini Joyce aondoke bila kuniaga na hata kama alikuwa na watu wake kwa nini hasinipe taarifa.
Nilichomeka simu chaji na kuiweka hewani ili nione kama kutakuwa na sms yeyote iliyoingia.Hofu ilizidi kunitawala na wakati naendela kufikira simu yangu iliita niakzani labda ni Joyce na nilipoiangalia nilimkuta ni Msouth. Sikutaka kuipokea nikaiacha iite mpaka ikate yenyewe.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni