SIKUACHI BABY (6)
Zephiline F Ezekiel
5 min read
Mwandishi: Juma Hiza
SEHEMU YA SITA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Kiukweli sikutaka kuamini kama kweli nilijizuia kiasi kile mpaka Samira akaweza kuondoka bila kufanya naye lolote. Hii haikuwa desturi yangu katika kumbukumbu za wasichana ambao waliingia ndani ya chumba changu hakuwepo mmoja wao ambaye aliweza kutoka salama, wote niliwarubuni na mwisho wa siku wakajikuta nimefanya nao mapenzi.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Samira alikuwa ndiye msichana wangu wa kwanza kuingia katika chumba changu na kutoka salama, mtarimbo wangu bado uliendelea kusimama huku nikianza kujilaumu kwa kosa kubwa nililokuwa nimelifanya yani kitendo cha kuzembea mpaka Samira akaondoka hivihivi bila kuuonja utamu wa vanila.
Tukio hilo hata nilipowasimulia marafiki zangu kijiweni walinicheka sana, hawakutaka kuamini kama kweli msichana huyo sikufanikiwa kufanya naye mapenzi. Nilihofia msimamo wake juu ya mwanaume aliyeniambia alikuwa anampenda sana lakini kwa wakati huo alikuwa nchini Marekani.
Baada ya kupita siku kadhaa nilimwambia kuwa nimeshapona na hivyo ningeweza kuendelea na kazi yangu ya kumpeleka kila siku kazini, alifurahi sana na kama nilivyomwambia ndivyo ambavyo ilikuwa. Niliendelea na kazi yangu hiyo huku kila siku ukaribu wetu ukizidi kukuwa.
Sikuacha kumwambia ukweli wa hisia zangu kwake kuwa hakukuwa na msichana mwingine niliyekuwa nampenda zaidi yake, nilipomwambia maneno hayo haraka aliwahi kubadilisha mada, hakutaka tuzungumze habari za mapenzi. Alizidi kunipa wakati mgumu sana mpaka kuna kipindi nikaanza kumchukia, nilihisi alikuwa akinifanyia makusudi.
Katika kitu ambacho naweza kusema nimenyimwa katika maisha yangu ni kumnyenyekea mwanamke, kumbembeleza kila siku kwa kitu kimoja hichohicho ambacho alionekana kutokukifikiria.
Kama uwongo niliutumia sana nakumbuka mbali na kumdanganya kuwa nilizidiwa na malaria kiasi kwamba akaonekana kujali lakini sikuishia katika maradhi peke yake, niliendelea kumdanganya kila siku lakini uwongo wangu haukuonekana kuwa na faida yoyote. Alionekana kuwa msichana mwenye msimamo sana, hakutaka kumuumiza mwanaume wake ambaye kila alipopata nafasi ya kuzungumza na mimi hakuacha kumsifia.
Niliacha kumsumbua na kitu nilichoamua kibaki ni kazi tu, nilibaki kubwa dereva na yeye alibaki kuwa abiria na huo ndiyo ulikuwa mwisho wa mjadala wetu. Alishangazwa na mabadiliko yangu hayo ya ghafla! kitu ambacho hakukitegemea, sikutaka kumficha niliamua kumwambia ukweli kuwa ule ndiyo ulikuwa mwanzo wangu na mwisho wa kumsumbua, niliamini alikuwa katika mapenzi na mwanaume mwingine na hiki ndicho kilikuwa kikwazo kikubwa cha yeye kutonikubalia ombi langu. Ama kwa hakika Samira alikuwa ni miongoni mwa wasichana wenye msimamo sana.
Baada ya kuacha kumfuatili Samira ambaye alionekana kuwa mgumu kama chuma cha pua niliamua kugeuza mashambulizi yangu upande wa pili, nilianza kuzitazama sketi zilizokuwa zikijipitisha mbele yangu. Sikujali alikuwa ni mzuri kiasi gani bali nilichokuwa nakiangalia ni kuona msichana huyo ninayemfukuzia anaweza kunikubalia na mwisho nafanya naye mapenzi.
Huo ndiyo ulikuwa ugonjwa wangu na tena kwa wakati huo sikuhitaji dawa yoyote, nilikuwa nimejawa na hamu sana ya kufanya mapenzi na msichana, kila nilipopata abiria msichana sikuacha kumchombeza, nilijikuta nikimtongoza katika mazingira ya ajabu sana.
Nilijivunia rangi yangu ya maji kunde iliyosindikizwa na muonekano wangu wa utanashati, mwili uliojengeka vyema kimazoezi, tatoo nilizokuwa nimejichora mwilini pamoja na mtindo wa nywele nilionyoa kichwani uliyokuwa ukifahamika maarufu kwa jina la kiduku, hakika ulinipendeza sana.
****
“Habari.”
“Nzuri.”
“Unaitwa nani mrembo?”
“Bianka.”
“Bianka jina lako zuri sana kama ulivyokuwa wewe.”
“Asante.”
“Vipi unaelekea wapi sasa hivi.”
“Nyumbani.”
“Nyumbani ni wapi?”
“Mtongani.”
“Naweza kukupa lift maana na mimi naelekea huko huko.”
“Asante.”
“Panda nikupeleke giza hili linaingia sasa hivi.”
“Nashukuru wewe nenda tu.”
“Sio vizuri hivyo halafu msichana mrembo kama wewe utatembeaje kwa miguu panda nikuwahishe fasta.”
“Mbona hatuelewani kaka angu nimekwambia asante nashukuru.”
“Mimi siondoki mpaka unikubalie.”
Yalikuwa ni mazungumzo yangu na msichana ambaye alijitambulisha kwa jina la Bianka. Nilikutana naye maeneo ya Temeke mwisho majira ya saa kumi na mbili za jioni muda huo nilikuwa tayari nimeshamrudisha Samira nyumbani kwake, wakati huo nilikuwa nikiendelea kutafuta abiria kama ilivyokuwa kawaida yetu sisi madereva bodaboda.
Alikuwa ni msichana ambaye alijaaliwa sura ya mvuto, rangi yake ya weupe ilizidi kuweka nakshi nakshi za kumshawishi mwanaume rijali kuhitaji kuwa naye lakini kuna vitu baadhi alinyimwa katika mwili wake. Hakuwa na shepu zuri wala wowowo, alipokuwa akitembea hakuonekana akiileta mitikisiko ya hapa na pale, kwa lugha ya kwetu uswahilini tunasema alikuwa amepigwa pasi.
Baada ya kumsalimia na kumuomba apande kwenye pikipiki yangu alionekana kugoma, kila nilipojaribu kumuomba nimpeleke nyumbani kwao hakutaka kukubali kirahisi. Sikutaka kuonekana kushindwa kirahisi niliendelea kumuomba mpaka pale maneno yangu yalipogeuka kuwa kero, alipoona nimezidi kuwa msumbufu mwisho akaamua kupata, tukaondoka mpaka kufika Mtongani.
“Ni hapo simama tumeshafika,” aliniambia huku akininyooshea kidole katika nyumba moja iliyokuwa upande wangu wa kushoto, haraka nilisimamisha pikipiki akashuka.
“Asante,” aliniambia.
“Usijali sisi ni watanzania na tumeumbwa kwa ukarimu, nimefanya haya kama msaada tu,” nilimwambia huku nikitabasamu.
“Nashukuru sana hapa ndiyo nyumbani kwetu,” aliniambia huku akiinyooshea kidole nyumba yao.
“Oooh! Ni nyumbani kwenu kabisa?” nilimuuliza.
“Hapana tumepanga,” alinijibu.
“Ok, vipi naweza kupata namba yako?” nilimuuliza.
“Ndiyo hakuna shida,” aliniambia kisha nikaitoa simu yangu mfukoni halafu nikampa akaandika namba yake, alipomaliza nilimbeep ili aweze kuipata namba yangu.
“Namba yako ndiyo hii inayoishia na 80?” aliniuliza.
“Yeah! ndiyo hiyohiyo,” nilimjibu.
“Hivi uliniambia unaitwa nani vile?” nilimuuliza huku nikionekana kusahau.
“Bianka,” alinijibu huku akitabasamu.
“Ooh! Sawa nimekumbuka ngoja niisave kabisa,” nilimwambia.
“Sawa ila hujaniambia jina lako.”
“Naitwa Metusela ila ukipenda we nisave Metu,” nilimwambia kisha sikutaka kuweka mambo yazidi kuwa mengi, nilimuaga halafu nikawasha pikipiki yangu nakuondoka.
Ubongo wangu ulitawaliwa na mapenzi kwa asilimia kubwa sana, hakukuwa na msichana ambaye nilikutana naye katika mazingira ya kazi yangu kisha nikaacha kumtamani.
Niliwatamani wasichana wengi sana ambao nilikutana nao na kati yao wapo waliyonikubalia na wengine walinitolea nje, sikutaka kujali sana wala kuweka mambo kuwa mengi, niliamini vya utamu kila siku vilikuwa vinazaliwa na hivyo sikutakiwa kuwa na mashaka yoyote.
Nilipokutana na Bianka kwa mara ya kwanza mpaka kufikia hatua nikampa lift nilijikuta nikimtamani sana, ingawa hakuwa na umbo zuri kivile lakini sura yake ya mvuto ndiyo iliyokuwa ikimbeba, sijui niseme nini kuhusu huyu Bianka lakini mapenzi ndiyo yalikuwa yamenitawala, sikumfikiria kwa kumuhonga pesa, kumjengea nyumba nzuri au kumnunulia gari la kifahari isipokuwa nilimfikiria kingono tu!
Usiku wa siku hiyo nilipokuwa ndani ya chumba changu akili yangu ikanipeleka mbali sana kimawazo, nikawaza jinsi ambavyo Bianka angeweza kuingia ndani ya chumba changu hicho kisha nikaanza kufanya naye mapenzi, mawazo hayo hayakukoma kunijia katika mawazo mpaka kuna muda nikajishangaa nilikuwa nimekumbwa na nini? Haikuwa kawaida yangu kuwa katika hali kama hiyo.
Nilikumbuka kuwa nilichukua namba yake ya simu, nilichoamua kukifanya niliichukua simu yangu kisha nikamtumia ujumbe mfupi, haichukua muda akaweza kunijibu kisha baada ya chatting fupi za hapa na pale nilimuomba kuonana naye.
“Unataka kuonana na mimi?”
“Ndiyo.”
“Wapi?”
“Popote pale.”
“Kwani kuna nini?”
“Hakuna kitu.”
“Ila?”
“Nataka tufahamiane tu! au hupendi?”
“Napenda ila.”
“Ila nini tena Bianka?”
“Mmh!”
“Mbona unaguna?”
“Kwani wewe unaishi wapi?”
“Mimi nipo Tandika Azimio.”
“Kumbe unaishi Tandika?”
“Ndiyo vipi itawezekana kuonana mimi na wewe?”
“Ndiyo itawezekana lakini nataka iwe sehemu open.”
“Usijali kwahiyo unapanga wewe au nipange mimi sehemu ya kukutana?”
“Panga wewe sehemu na muda.”
“Basi tukutane pale Tawheed.”
“Muda gani?”
“Saa kumi jioni.”
“Sawa nitafanya hivyo.”
Nilipomaliza kuchat na Bianka moyo wangu ulifarijika mno, nilihisi kuwa mshindi mpaka kufikia hapo. Nilitamani papambazuke ilimradi huo muda uweze kufika wa mimi na yeye kukutana katika mgahawa wa Tawheed uliyokuwepo mtaa ya Majaribio Tandika. Usiku wa siku hiyo nililala huku akili yangu yote ikimfikiria yeye.
****
Niliamka siku iliyofuata asubuhi na mapema, nilijiandaa kama ilivyokuwa kawaida yangu, nilipomaliza niliichukua pikipiki yangu kisha nikaenda kumpitia Samira nyumbani kwake nikampeleka kazini.
Siku hiyo sikuzungumza naye lolote zaidi ya salamu ya asubuhi niliyompa basi hakukuwa na kingine nilichokiongeza, alinishangaa sana lakini sikutaka kumpa nafasi ya kuniuliza lolote, uso wangu wa ukauzu niliyomuonyeshea uliashiria kuwa sikuwa sawa hata kidogo na hivyo hakutakiwa kunihoji lolote. Nilipomfikisha kazini kwake nilimuaga kisha nikaondoka.
Kimoyomoyo nilikuwa nilicheka baada ya tukio hilo kulifanya, niliamini nilimuacha katika wakati wa maswali lukuki ambayo yalikosa majibu katika kichwa chake, kama kunitesa alinitesa sana, nilitumia kila mbinu za kumpata mpaka nikafikia hatua nikawa namdanganya lakini kila nililokuwa nalitegemea kulipata lilienda kombo mwisho nikaamua niwe ni mtu wa kumfanyia visa bila sababu.
****
Baada ya kupita masaa kadhaa hatimaye saa kumi kamili iliweza kutimia, mpaka kufikia muda huo nilikuwa tayari nimeshafika katika mgawaha wa Tawheed uliyokuwepo mtaa wa Majaribio, niliagiza Juice ya embe na baada ya muda mfupi muhudumu aliweza kunihudumia kisha taratibu nikaanza kuinywa huku nikiusubiria ujio wa Bianka. Nilionekana kuwa mwenye shahuku ya kumuona msichana huyo kwa mara ya pili, macho yangu hayakutulia sehemu moja, nilitazama huku na kule mwisho nikaitazama pikipiki yangu niliyokuwa nimeiegesha pembeni na mgahawa huo uliyokuwa sehemu ya wazi sana.
Baada ya dakika kumi na tano hatimaye Bianka aliweza kufika katika mgahawa huo, alikuwa amevalia gauni refu la rangi ya nyeusi pamoja na blue lililokuwa limetawaliwa na maua kila kona, kichwani alikuwa amejifunga kilemba kilichoendana na rangi ya gauni lake.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni