HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (16)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mtunzi: Richard Mwambe
SEHEMU YA KUMI NA SITA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Seidon alikuwa katika hali mbaya sana, kama ni kupambana basi alikuwa kapambana na jitu la kutisha linalowaka moto kila upande. Ilikuwa ni wakati wa kumaliza kazi aliyotumwa, akasikia radi zikipiga huku na huko, yule malaika wa moto akashtuka na akajua kwa vyovyote mvua itapiga hapo muda si mrefu, na kweli alipogeuka ulikotokea mlio ule.
TUENDELEE...
Malaika wa moto anayetegemewa na Sherhazad katika shughuli ngumu kama hizi huwa hatakiwi kuguswa na maji hasa mvua kwani mwili wake umeumbwa kwa moto hivyo akiguswa na maji ndiyo mwisho wa uhai wake. Mara moja bila kuuliza, akamgeuza farasi wake na kuondoka, na kweli mvua kubwa ikanyesha eneo lile na kukatika kwa muda mfupi. Mbele ya Seidon akatua mwewe mkubwa aliyeshika fuvu la Cleopas miguuni mwake, akatua na alipoliacha lile fuvu na kuondoka hakufika hata mita 10 mshale wa kichawi uliotumwa na Sherhazad ukampiga yule mwewe na kisha ukageuka nyoka aliyekuwa akijiviringa mwilini kwa yule mwewe. Yule mwewe akaanguka chini na vumbi likatimka eneo lile.
Seidon akalichukua lile fuvu na kuondoka mahala pale haraka, alikumbuka maneno ya yule mzee ambaye alikufa kwenye bonde la mauti, kuwa akifika katika mstari wa Ikweta basi nguvu zote za majini haziwezi kufanya kazi, hakuwa mbali na eneo hilo. Seidon akiwa na upanga wa Vernad mkono wake wa kulia na ule wa kushoto amelishikilia lile fuvu, sasa halikuwa kwenye mfuko lilikuwa wazi mkononi mwake, akaanza kutimua mbio kuielekea Ikweta. Nyuma yake alisikia sauti za watu wanaomkimbiza lakini kila alipogeuka hakuwaonaa, aliendele kukimbia lakini bado aliona hafiki wakati mahali penyewe palikuwa karibu. Mara hii alipogeuka nyuma aliona kundi kubwa la watu waliokuwa wakimfukuza kwa miguu na farasi. Seidon alikimbia kwa nguvu zake zote, akakaribia kabisa Ikweta, ndipo alipoanza kuona maajabu ya lile fuvu alilolibeba, akajikuta amekuwa mwepesi, anakimbia akikanyaga hewani na si ardhini kama ilivyokuwa mwanzo, wakati huo vishindo na kelele za radi zilikuwa zikisikika na anga lote lilikuwa likikatwa kwa miali mikali ya radi. Seidon aliendelea kukimbia na alipoingia Ikweta alijikuta akikimbia zaidi kuliko mwanzoni, mwisho wake akaingia ndani ya pango na kujificha, lile fuvu likatengeneza mwanga wa kutosha uliopitia katika matundu ya macho yake.
Seidon akawa anashangaa kila analoliona likifanyika sasa kutoka katika fuvu lile.
“Amatagaimba, uko wapi?” akanong’ona Seidon. Mara akasikia sauti za watu wawili wakiongea, sauti zao zilikuwa zikisikika kutoka chini. Seidon akasimama na kuangalia huku na huko lakini hakuweza kuona mtu yeyote isipokuwa aliendelea kusikia sauti zile mbili, ya kike nay a kiume.
Seidon akashtuka kidogo, kwani alikuwa akizisikia sauti zile kutoka chini ya ardhi, akapiga magoti na kutega sikio lake ardhini, akaisikia kwa uwazi kabisa sauti ya Amatagaimba.
“Inatupasa tutoke humu, namtafuta rafiki yangu Seidon,” ile sauti ikasikika.
“Amata gaimba!” Seidon akaita kwa sauti ya taratibu.
§§§§§
Amatagaimba akamzuia Anna kwa mkono wake wa kuume.
“Vipi?” Anna akauliza.
“Kuna mtu ananitafuta,” akamjibu. Baada ya kutulia kama dakika tatu hivi, akatazama kidole cha mkono wake, akaitazama pete ya ajabu aliyokuwa nayo kidoleni, akaongea maneno Fulani na mara upepo mkali ukavuma na kutimua vumbi jingi. Anna Davis kwa woga akajificha nyuma ya Amatagaimba akitetemeka kwa hofu.
Amatagaimba akanyosha mikono yake na lile vumbi likatulia, katikati ya vumbi lile kukabakia farasi mkubwa aliyesimama kimya akimtazama Amatagaimba. Akamshika mkono Anna na kumwelekea yule farasi.
“Mi naogopa kupanda farasi,” Anaa alikataa.
“Endelea kuogopa, utabaki hapo hapo ulipo maisha yako yote!” Amatagaimba akamjibu huku akimtazama, “Twende! Tena wewe una kazi ngumu sana ya kufika huko ulikotoka”. Amatagaimba akakwea farasi, akamtazama tena Anna bado akiwa amesimama palepale.
“Tazama nyuma yako!” akamwambia. Anna akageuka nyuma na kushuhudia moto mkubwa ukiwaka huku ukielekea kule walikosimama wao.
“Mamaaaaaaaa…. Amatagaimba nisaidie!” Anna alipiga kelele za woga, akakimbilia pale kwenye farasi, mkono wake ukashikwa na ule wa Amatagaimba na farasi akaanza kuondoka kwa kasi huku Anna akijiweka vizuri mgongoni mwake.
“Wanakuja Amatagaimba, watatuua wale kimbia!” Anna alikuwa akipiga kelele mgongoni mwa Amatagaimba. Farasi alikuwa akipiga mbio za ajabu, lakini Amata gaimba kila alipogeuka nyuma aliona jeshi lile linakuja kwa kasi kuliko yake. Vumbi lilikuwa likitimuliwa na miguu ya yule farasi, hakujali mchanga mwingi wa jangwani alizipiga mbio kwelikweli. Kwa mbali kidogo, Amatagaimba aliona kitu kama nyumba au mlima hivi hakuweza kujua haraka ni kitu gani kiuhakika.
“Huyo atakuwa Dherhazad na swahiba zake!” Amatagaimba aliendelea kuongea.
“Sherhazad?” Anna akauliza akiwa bado kamng’ang’ania Amatagaimba kiunoni.
“Ndiyo ni Malkia wa majini katika milki ya Soria,” akamjibu. Baada ya mwendo wa muda kidogo wakakaribia kabisa ule mlima, mara zikaanza kusikika kelele za watu, watu wengi kana kwamba kuna kitu wanakifukuza. Kelele zao zilikuwa zinaumiza masikio, mara nyingi Anna alikuwa akijiachia na kuziba masikio na kuataka kuanguka, kelele zilizidi sana, Amatagaimba hakujali.
“Anna!!! Jishike vizuri, tunaingia Ikweta!” Amatagaimba alipiga kelele huku akimwimiza farasi kupiga mbio, zile kelele sasa zilikuwa kali zaidi kiasi kwamba zilikuwa zikisumbua masikio ya wote. Alipogeuka nyuma aliona wale majeshi wanakuja na farasi wao tena hawakuwa mbali.
“Amatagaimba., wanatufikia, hawa hapa!” Anna alipiga kelele za woga.
“Tulia Anna, tukifika Ikweta tutakuwa tumekwishapona,” akajibu.
Mara ghafla yule farasi akawakama amejipiga kwenye ukuta au jiwe, wakaanguka chini wote wawili na farasi wao, tayari walikuwa wameingia Ikweta, lakini farasi yule aliishia pale ambapo Ikweta inaanzia kwa kuwa hakuwa farasi wa kweli bali wa kutengenezwa. Amatagaimba aliinuka nharaka na kumshika mkono Anna aliyekuwa amechafuka kwa vumbi la janagwani kisha akaanza kukimbia naye mpaka kwenye kitu kama mlango, akaupiga teke ukafunguka wakaingia wote wawili na kuufunga mlango nyuma yao, kisha wakasimama kwa kujibanza kwenye pango hilo lenye kiza kinene.
“Hamunaptra!” Amatagaimba alijisemea kwa sauti ndogo, kisha akaanza kufuatilia ngazi ndefu zilizokuwa zikiteremka chini.
“Amatagaimba” Anna akaita kwa kunong’ona.
“Shhhhhh!!!!! Usiamshe roho zimelala” Amatagaimba alaimwambia Anna. Amatagaimba akatazama zile ngazi zilizokuwa zikielekea shimoni, giza lilitanda, sauti ya vitu kama wadudu ndiyo iliyokuwa imetawala ndani humo, alikuwa akikanyaga kwa hatua za polepole ambazo hazikuwa zikitoa hata kelele, huku upanga wake ukiwa mikononi mwake barabara kabisa kwa hatari yoyote, mbele zile ngazi zikaisha pakabaki uwanda mkubwa lakini uliojazwa na giza totoro.
Mara sauti za milango ikifunguliwa zilisikika, Amatagaimba akasimama ilhali upanga wake ulikuwa mikononi mwake, mara kitu kama jiwe kilimpitia jirani na kugondokea upande wa pili. Mara kelele kama za watu waliokuwa wakija kumshambulia zikaanza kusikika, aliutwaa upanga wake na kuanza mapambano, ilikuwa ni kazi ngumu sana kwani alikuwa havioni viumbe anavyopigana navyo kutokana na giza lililokuwa mahala hapo.
Alijitahidi kuutembeza upanga wake wa nguvu zote alihisi kupiga vitu Fulani lakini hakuweza kuviona. Anna alibaki nyuma ya Amatagaimba akijikinga kupitia mgongo wake.
“Amatagaimba, nisaidie!!!” Anna alipiga kelele alipohisi mguu wake kama unafungwa minyororo, amatagaimba aligeuka kwa wepesi na kuona japo kwa taabu, mwiliwa Anna ukivutwa, akaruka sarakasi na kukata ule mnyororo. Kelele zilizodo kuongezeka na viumbe hivyo vya ajabu vilizidi kumiminika ikawa taabu.
Mara ardhi ya mule ndani ikaanza kuzunguka, taratibu na kueongeza kasi.
“Aiyaaaaaaa!!!!!” Amatagaimba alipiga kelele alipomuona Anna akitumbukia katika ufa mkubwa wa uliojitokeza ukutani na kufanya mwanga wa upande wa pili uking’aa, kwa haraka akawahi na kupenya katika ule ufa lakini kabla hajamaliza kuingia nguo yake ilibanwa na ule ufa.
Sasa kelele za radi zikaanza kusikika, mvua kubwa ikaanza kunyesha.
“Hapo sasa hauna ujanja, kama nilivyomkamata mwenzako sasa ni zamu yako,” sauti ya kike iliyoksikika kwa mwangwi ilikuwa inaongea sana, “Ingia, ingia wewe huko!” amatagaimba alianguka chini baada ya Anaa kukata ile nguo iliyonasa kwenye mwamba. Mara moshi mzito ukaanza kujaa mahala hapo.
“Aaaaaaa ha ha ha ha ha, Aaaaaa hahahaha, zama zenu zimekwisha nipeni hilo fuvu, niutawale ulimwengu wote wa juu na wachini,” sauti kali ya Sherhazad ilisikika na kufanya kile chumba kiwe na vitu kama radi katika kuta zake, ilikuwa ni hali ya kuogofya sana, Anna alikuwa akipiga kelele huku akiziba masikio yake.
Kwa mbali Amatagaimba akawa anasikia kana kwamba kuna ibada ilokuwa ikiendelea, kwani sauti za watu wengi zilikuwa zikisikika nkama watu wanaosali katika lugha isiyoeleweka.
“Krusum krusum, sontum sontum …” ile sauti ilizidi kukaribi akana kwamba waliokuwa wakisali walikuwa wakitembea. Kwa sekunde kadhaa hawakusikia sauti ya Sherhazad. Amatagaimba alizidiwa na moshi ule wakati huo Anna alikuwa chini kaishiwa nguvu, mara radi kali na mngurumo ikasikika mara moja.
“Amatagaimba… nifuate!” ilikuwa sauti ya Seidon.
“Seidonnnnn!” Amata naye aliita huku akimtazama Anna aliyekuwa hajiwezi kwa moshi ule, akamvuta kwa mkono wake na kumburuza mpaka pale alipomkuta Seidoni ambaye alisimama katikati ya ufa mkubwa wa ukuta ule wa jiwe akiwa juu ya farasi wa ajabu.
“Amatagaimba, pita!” akamwamuru, Amatagaimba akafanya hivyo, akapita na kutokea upande wa pili, nje ya lile shimo la mtego, Seidon akamwamuru farasi kurudi nyuma, naye alipoumaliza ule ukuta tu, ukajifunga kwa nguvu na kufanya mawe kutoka juu kuanza kudondoka huku na kule. Seidon akashuka juu ya yule farasi.
“Huyu ni nani shujaa wangu? Si unakumbuka huku hatutakiwi kufanya lolote na mwanamke” Seidon akafoka huku akipiga magoti kumwangalia Anna.
“Seidon, huyu ni mwnadamu sio jinni kama unavyofikiria, nimemkuta amenasa huko chini nikamsaidia kutoka, ni hadithi ndefu, tutaongea zaidi,” akamwangalia Seidon juu mpaka chini, “Fuvu liko wapi?” akamwuliza.
“Amatagaimba bora nimekuona nalikuwa nakutafuta kila upande wan chi hii, fuvu limenidondoka katika shimo refu sana hata sikuwa na uwezo wa kulichukua, twende twende mara moja,” Seidon akamwambia Amatagaimba.
Amatagaimba kabla ya kuondoka akachukua maji kutoka kwa Seidon na kumpa Anna, akayanywa kwa fujo na kuyamaliza. Nguvu zikamrejea. Anna akapanda juu ya farasi na Amatagaimba akatua nyuma yake, safari ikaanza.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni