HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (13)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mtunzi: Richard Mwambe
SEHEMU YA KUMI NA TATU
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
“Nimeiona shida yako, nimesikia kilio chako lakini jambo moja ninaloweza kukwambia ni kwamba, nguvu zetu na nguvu za huku ni kinzani sana, nikikuahidi kukuvusha katika daraja la pepo nitakuwa mkaidi mbele ya watu wangu, kwa kukusaidia ewe shujaa wetu, nitakuonesha njia ya kuzunguka ambayo itakufikisha katika lango la Hamunaptra,
TUENDELEE...
ukishafika katika mlango huo, ingia bila woga, ijapokuwa Hamunaptra ni mji wa wafu, usiogope ndani yake kuna mji mkubwa sana ambao katikati ya mji huo kuna Clakos chini ya ardhi. Sasa shikeni njia mpita Mashariki kuzunguka milima mitano, baada ya majua mawili tu mtakuwa mmefika Hamunaptra, yeyote mtakayekutana naye njiani msiongee naye wala msimpa mkono, katikati ya njia mtapata shida kwa maana lazima mpitie mji mmoja katikati yake lakini mtavuka tu,” Baghoza alimueleza Amatagaimba.
“Ewe baghoza malkia wa majinni, tunamhofia Orion na Sharhazad, je tutafika?” Amatagaimba aliuliza kwa mashaka huku akiwa ameinamisha kichwa chake chini.
Baghoza akaizungusha fimbo yake katika pepo zote nne, kisha akamgeukia Amatagaimba.
“Orion haonekani, Sharhazad haweze kuwashambulia hapa kwani nayeye hawezi kuvuka daraja la pepo, nendeni msichelewe, jua la tatu litapatwa na mwezi, huo ni wakati mbaya sana kwetu, je vipi kuhusu ninyi?” mara ule upepo ukaongezeka, vumbi likatimka na baghoza akatoweka mbele ya Amatagaimba. Aamatagaimba akaitazama pete yake, kisha akainuka kutoka pale alipokuwa amepiga magoti.
“Amatagaimba umekiona kimbunga cha ajabu?” Seidon akauliza.
“Je wewe uliniona wakati wa kimbunga hicho?” Amatagaimba akamwuliza Sedon.
“Hapana,” Seidon akijibu kwa woga.
“Hakikuwa kimbunga, ila mimi nilikuwa ndani yake, Seidon, sasa twende hatua ya mwisho ya safari yetu,” Amatagaimba alipokuwa akisema hayo, mara matone ya mvua yakaanza kuwatonesha, Seidon aliachama kinywa chake na kuruhusu matone kadhaa yaingie ndani yake, kiu yake ikakatika na nguvu zikamrejea tena. Kisha wote wawili wakashika njia kuielekea milima mitano, Seidon alikuwa mbele na mfuko wake mweusi wenye fuvu ndani yake, Amatagaimba alikuwa nyuma yake, hakuna aliyeongea kila mmoja alikuwa akifikiri juu ya safari hiyo ya hatari.
Jua lilipokuwa likizama Amatagaimba alikuwa amechoka bila kificho.
“Tupumzike hapa na tupate chakula,” Amatagaimba akamwambia Seidon, wakaingia katika moja ya mapango yam awe yaliyokuwa eneo hilo na kuketi wakiangazwa kwa mbala mwezi. Seidon akafanya moto wa kuota maana baridi ilikuwa kali, wakatafuna masurufu waliyokuwa wamebeba, na wote wakapata usingizi.
§§§§§
Usiku wa manane, Amatagaimba na Seidon wakiwa wamelala katika pango hilo. Orion akiwa juu ya farasi wake mkubwa alivuta harufu na kuhisi kuna wageni pande hizo. Akamuongoza farasi wake kuelekea milima mitano ambako alipata hisia juu ya watu hao.
Upepo uliendelea kuvuma na kuufanya ule moto waliokuwa amekoka Seidon kuongezeka na kufanya joto kali ndani ya pango lile. Orion alifika na kusimama mbali, kila alipojaribu kuvuta harufu ile aliyoisikia mwanzo hakuipata badala yake joto kali la moto lilipenya pua zake na kumuumiza mapafu yake, akarudi nyuma zaidi na kusimama, hakuna ujanja.
KATIKA MJI WA SORIA
NDANI ya kasri kubwa la Shrhazad, kulikuwa na watu walewale, wazee wa kichawi waliojaribu kuisitisha safari ya Amatagaimba na Seidon wakashindwa. Sasa walikuwa wakisubiri muda ufike ili kupambana upya.
“Sikilizeni enyi wachawi wa Soria, Seidon na mwenzake wapo katika mapango ya Oregon, jirani kabisa na mji mtukufu wa Hamunaptra, lazima watavuka nchi ya Sharidan katika kijito cha Usoil, sasa na tuwasubiri pale kijitoni, mara hii tusikubali kabisa kulikosa lile fuvu maana ile ni neema ya Clakos, tukilipata tutaitawala dunia yote na itakuwa chini ya neno letu,” Sharhazad aliwaambia wachawi wake huku akitoka katika dirisha lake la ajabu. Akakiendea kiti chake cha enzi, kiti kilichotengenezwa kwa dhahabu safi na kung’azwa kwa moto mkali wa kuyeyushia chuma, vazi lake refu jeupe lenye mkia mrefu lilimfanya Malkia huyu kuonekana mkubwa kupita kiasi lakini alikuwa na mwili mdogo isipokuwa alikuwa na nguvu sana dhidi ya maadui wake, kila tawala iloimuogopa Sharhazad kwani alikuwa na uwezo wa kukugeuza chochote anachokitaka na usimzuie. Akakei juu ya kiti chake, na wale wazee wachawi wakainama mpaka chini kumpa heshima yake, kisha wakainuka na kuketi kwa kutumia magoti yao ilhali miguu yuao wameikunja kwa nyuma.
“Tufanyeje tuwaangamize wale watu?” akauliza Sherhazad.
“Mtukufu malkia, pete ya Amatagaimba ndiyo pekee inayotukwamisha kukamilisha ulilotutuma, ni lazima kwanza tuikamate pete ile kisha kazi inayobaki ni ndogo sana, kumbuka wakifika tu kwenye mstari wa Ikweta kamwe hatutawaweza tena kwani pale tayari Clakos itaona fuvu lake na nguvu za ajabu zitakuwa juu yao, tutafanya nini ee Malkia?” mchawi mmoja kati ya wale waliokuwepo pale akajibu huku akitetemeka kwa woga.
“Kwa nini u muoga sana wewe? Kwa nini unaonesha kukata tama wakati tama yenyewe imeijaza mioyo yetu sote, nitakupeleka kwenye ulimwengu wa wadudu watambaao kwa jinsi zao mara moja endapo utaonesha udhaifu wako tena,” maneno makali ya Sharhazad yaliyokuwa yakimtoka kinywani huku yakisindikizwa kwa radi kali yaliwafanya wazee wote wainame tena kumpa heshima Malikia.
“Ee malkia wa Soari uishi milele!!!” wote walisema maneno hayo.
“Fusha mafusho, ili majinni yote yakusanyike,” Sharhazad akatamka. Mchawi mmoja wapo akachuku kitu kama kibuyu kikubwa, akatia ubani mwingi na vitu vingine kama amdalasini, akasema maneno ya ajabu katika lugha ya kicawai lugha yao wanayoielewa wao wenyewe, mara moshi mzito ukaanza kutoka kwenye kile kibuyu, harufu izuri ya udi, ubani na manukato ya ajabu yalilijaza lila kasri zima. Sauti za watu wengi zikaanza kusikika kama watu wanaobadilishana mawazo ya jambo Fulani.
Kishindo cha kofi kali kikasikika, ukimya mkuu ukatawala, Sherhazad sasa likuwa kabadilika sura yake na kuwa Joka kubwa lenye vichwa vitatu, likiwa pale juu ya kiti, likanyoosha shingo yake huku na kule. Kisha likafungua kinywa chake na kuanza kuanza kunena kwa lugha yao.
“Umefika wakati wa kuitawala dunia na pepo zake zote nne, viumbe yabisi na viumbe hewa vyote view chini ya mamlaka ya Soria, nyote mnajua kwa karne nyingi tumekuwa tukilitafuta fuvu la Cleopas ili kupata neema za Clakos zenye wingi wa mamlaka juu na chini ya mbingu, viumbe wawili wanalirudisha fuvu hilo kwa Cleopas, na wamebakisha jua moja tu kufikia lango la Hamunaptra, nimewaita ili sasa sisi sote tuweze kufanya kila hila tulipate fuvu hilo kabla hawajaingia nalo ndani ya Hamunaptra, mimi na wengine wachache tutawasubiri katika kijito cha Usoil, lakini nataka ninyi mutangulie mbele kufanya hila ya kuwazubaisha,” Sharhazad aliongea na viumbe wake kwa sauti ambayo wewe mwanadamu wa kawaida ungesiki milio ya ajabu ajabu tu ikimtoka nyoka huyo.
“Ewe malkia mtukufu, sote tuko hapa kulinda na kuhakikisha utawala wako wenye nguvu hauanguki, yumkini hawa ni nani? Viumbe dhaifu vya dunia ya kesho hata vituzuie sisi ambao tuna nguvu, mamlaka na enzi kuikamilisha kazi yetu? Tunakuahidi kutekeleza na kuitawala dunia, kwa kuwa wale ni nyama na mifupa tutawapiga kwa magonjwa nao hawatakuwa na uwezo tena,” mmoja wale waliokuja pale aliongea.
“Aaaaaah! Wewe bado ni mchanga sana kati ya wachanga, kumbuka katika mbingu hii magonjwa hayana nafasi, sisi tunaweza kuwapiga kwa magonjwa wakiwa kwao duniani, lakini katika ulimwengu huu wa jinni ya jinnu hakuna hewa inayotembea hivyo magonjwa hayawezi, lakini tumieni sura na maumbo yenu ya kuazima ili kuwatia udhaifu wale,” Sharhazad akatoa maelekezo kwa viumbe wake, kisha kwa kupitia dirisha lake la ajabu akawaonesha Amatagaimba na Seidon mahali walipo. Lakini jambo moja liliwashtua wote waliomo katika kasri lile. Walimuona Orion akiwa kasimama juu ya farasi wake mweupe, farasi anayeweza kuchomoa mbawa na kuruka kama ndege wa kawaida ‘pegasus’. Sherhazad alijawa na hofu.
“Na huyu ni kikwazo kingine,” akawaambia.
“Ewe Malikia mtukufu wa Soria, Orion ametumwa na wachawi wa Misri ili apate fuvu lile na kuwapeleka kisha wao watampa maji ya uzima ambayo kwayo kamwe hatoweza kufika katika miisho ya maisha yake,” mwingine akasema na kumwambia Sharhazad, akahamaki kwa jibu hilo.
“Na tumuweke katika jalada la maangamizi kabla ya jua la mashariki ijayo,” Sharhazad akawaagiza na kisha moshi ule wa mafusho ukakatika ghafla, kasri likabaki tupu, kitini alikuwa yuleyule mwanamke mrembo, Sharhazadi, sasa katika umbo lake zuri la kibinadamu lakini alikuwa amelowa jasho mwili mzima.
§§§§§
“Seidon,” Amatagaimba alimwamsha Seidon, kisha wakajiandaa kwa safari, mbalamwezi ilikuwa ikitoa mwanga wake murua na kufanya vilele vya milima ile mitano kuonekana kama mtu aliyevaa kanzu nyeupe. Walipohakikisha kila kitu kipo salama wakaanza safari ya kumaliza ngwe hiyo. Wakiwa njiani, nyuma yao walisikia kwato za farasi akimbiaye, kabl;a hajatahamaki mfuko wa seidon ambao ndani yake kulikuwa na lile fuvu, ukanyakuliwa na Orion kisha Yule farasi akafungua mbawa zake na kuanza kuiacha ardhi, Amatagaimba alimshuhudia Seidon naye akinyanyuliwa kwani mfuko huo ulifungwa barabara kiunoni mwake.
Amatagaimba akauchomoa uta wake na kuuweka mshale wake utani, akavuta huku akibana meno kwa hasira na uchungu, akauachia uta huo nao ukasafiri kwa kasi. Amatagaimba akashuhudia farasi Yule akidondoka tena ardhini pamoja na Orion aliyekuwa juu yake. Vumbi kubwa likatimka, lile fuvu ilikachomoka kutoka kwenye ule mfuko, Amatagaimba na upanga mkononi akafika eneo lile, alipiga upanga lakini Orion akaupangua kwa wake, akauvuta na kupiga pigo linguine, Orion akaupangua kwa ustadi zaidi. Mara pigo la upanga la Orion liliikosa shingo ya Amatagaimba padogo sana, akaepa na kudondoka chale katika mchanga. Oriona akawa anakuja kwa kasi na upanga wake wa makalikuwili uliokuwa uking’aa sana mkononi mwake, akaruka kwa nguvu zake na kuelekea kutua juu ya Amatagaimba. Kwa haraka akauvhomoa upanga wake na kuukinga ncha yake ikatazama juu. Amatagaimba aliliona jitu la kutisha lililoachama domo lake ambalo lilikuwa likitoka joka kubwa, Amatagaimba akajawa na woga lakini hakuondoka, alifumba macho na kutulia. Upanga wa Amatagaimba ukapita katikati ya kifua kikavu kisicho na damu cha Orion, akalitupia pembeni jitu hilo, kisha akasimama na kuuchomoa upanga wa Orion mikononi mwake akakata shingo yake, Orion akaanza kuyeyuka na kupukutika kama kuwa vumbi.
Seidon alisimama kwa taabu, akaliendea fuvu lile lililokuwa chini katika mchanga, lakini kabla hajaliokota alibaki kinya wazi, pale lilipoangukia mchanga wote uliondoka na kufanya duara, kisha lile fuvu likaonekana likiwa juu ya kitu kama jiwe jeupe safi ambalo halikuwa na hata chembe ya vumbi.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni