HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (18)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mtunzi: Richard Mwambe
SEHEMU YA KUMI NA NANE
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
“Mamaaaaaaaa!” Anna akapiga kelele na kutereza vibaya, miguu yake ikaliacha daraja, Seidon akawahi kukaza mikono na kumzuia, lakini miguu yake tayari ilikuwa imeacha daraja na sasa ikining’inia chini ya daraja. Anna akalia kwa uchungu sana, akijua kuwa mwisho wake sasa umefika.
TUENDELEE...
“Jipe moyo Anna, tumefika mwisho sasa,” Seidon alipiga kelele hukumkono wake mmoja tu ukiwa umemshika Anna, “Shika kwenye daraja kisha jivute juu,” Seidon akatoa maelekezo.
“Seidon siweziiii !” Anna alilia.
Wakati huo maopambano makali katika ya Amatagaimba na Sherhazad yalikuwa yakiendelea, Amatagaimba alikuwa akimzuia Malkia wa majini kulifikia hilo daraja, pia alitaka Seidon amalize kazi hiyo kwani baada tu ya daraja lile kulikuwa na ngazi ambayo juu yake kulikuwa na sakafu kubwa na Klakos ilikuwa hapo.
Seidon akashindwa afanye nini, amuachie Anna na kwenda kurudisha lile fuvu au amshike Anna na achelewe kufikisha lile fuvu wakati huohuo hajui nini kitatokea.
§§§§§
Upande wa juu baada ya lile daraja kulikuwa na kitu kama jukwaa lenye ngazi zisizopungu ishirini na nne, na juu kabisa kulikuwa na kitu kama viti saba, vitatu upande wa kushoto na vitatu upande wa kulia, kisha kimoja kilikuwa mbele kabisa. juu ya hivi viti sita kulikuwa na viumbe sita vilivyokaa katika mtindo unaofanana, vyote vikiwa vimeweka viganja vyao magotini na sura zao zilikuwa zimenama na kuangalia chini. Kiti cha mbele kabisa kulikaa kiumbe kingine, hiki kilikuwa kikubwa zaidi ya hivi sita, hakikuwa na kichwa.
Viumbe vyote vilionekana havina uhai,ngozi zao zilisinyaa kabisa vikaonekana kama vimepakwa vumbi.
Sherhazad aliendelea kutembeza kichapo kikali kwa Amatagaimba ambaye alijitahidi kupigana kadiri ya uwezo wake. Sherhazad alionekana kuwa na nguvu sana ili kutimiza lengo lake. Amatagaimba aliona wazi kuwa wakileta mchezo hapo ndio mwisho wao kwani Sherhazad alikuwa anatumia mbinu kali za kichawi ambazo zilimfanya Amatagaimba kusahau kila kitu na kupumbazika.
“Seidon, Seidon!” aliita kwa taabu, Seidon akamtazama Amatagaimba aliyekuwa akitambaa chini.
“Muachie Anna, nenda kapachike hilo fuvu kwa kile kumbe kisicho na fuvu,” Amatagaimba alijitahidi kupiga kelele.
Seidon alimtazama Anna akiwa bado ananing’inia na huku amemshika kwa mkono wake mmoja ambao ulikuwa unavuja jasho na ukitetemeka kuonesha kuwa umefikia mwisho wa kustahamili, macho ya Anna yalijaa machozi nay a Seidon yaliakisi hali ile.
“Niache Seidon, niache uende, asante kwa yote,” Anna akafumba macho. Seidon hakuwa na lingine zaidi ya kumwachia Anna ili yeye amalize kazi iliyompasa kuifanya, hakupenda kumpoteza mwanadada huyo lakini ilimbidi.
“Seidooooonnnn!!!!” Amatagaimba aliita, sauti ile ilimgutusha Seidon asliyekuwa akimtazama Anna kwa huzuni, akamwachia ili atumbukie kwenye ule mto wa ajabu. Seidon hakubaki mahala pale, alivuta hatu na kulimaliza lile daraja akaanza kupanda ngazi kuelekea juu ambako Klakos ilikuwapo. Mara ghafla upepo mkali ukaanza kuvuma na kumfanya Seidon kushindwa hata kunyanyua mguu wake. Ule upepo haukukoma uliendelea kumpa shida Seidon, nay eye hakukubali alijilaza chini na kupanda zile ngazi huku akitambaa kama nyoka.
Wakati huo Amatagaimba alikuwa amesitisha mapambanao na Sharhazad ghafla baada ya kutoweka kwake, Sherhazad na Ujini wake lakini hakuwa na nguvu ya kupanda pale ilipo Klakos nah ii ilitokana na uovu mwingi uliomzunguka, hivyo alimwacha Amatagaimba na kuzunguka nyuma kisha kuanza kutengeneza upepo mkali kutoka katika kinywa chake kwa minajili ya kumpa kipingamizi, Seidon.
Ilikuwa bado ngazi chache sana Seidon afike kwa viumbe vya kwanza vile ambavyop kimoja kipo kushoto kinaitwa Aminus na kile cha kulia kinaitwa Sagitarius. Bado viumbe vile vilikuwa vimetulia kimya hata havikutikisika; ni utando wa buibui tu uliokuwa umewazunguka hapa na pale.
§§§§§
Anna alipoanguka baada ya kuachiwa mkono na Seidon, alijigonga vibaya kwenye moja ya nguzo za lile daraja, ivyo mwelekeo wa mdondoko wake ukabadilika badala ya kwenda chini akasukumiwa kushoto na kudondokas jirani na jiwe kubwa lenye kung’aa sana, alifumbua macho aliyokuwa kayafumba muda wote huo na kujikuta kama umbali wa meta moja kutoka kwenye ule mto ambao maji yake mazito yalikuwa kama uji mzito wenye rangi mchanganyiko.
Kizunguzungu kikamshika akajivuta pembeni na akulala kimya akipulizwa na ule upepo ambao hakujua hatima yake nini, maumivu makali yalikuwa katika eneo la mbavu zake ambapo alijgonga vibaya katika ile nguzo.
§§§§§
Amatagaimba akajibiringisha pale alipo na kujificha nyuma ya kitu kama ukuta mfupi, akachomoa uta wake mgongoni akautia mshale na kuuvuta kwa nguvu zake zote kuelekea kule ambako Cleopas alikuwa amekaa, alipouachia, ule mshale ukakata upepo kwa kasi na kuipita shingo ya Cleopas kwa nukta chache sana kambla haujapiga hewa na ule upepo ukakatika ghafla.
Seidon akanyanyuka haraka na kupanda kazi iliyobaki akakanyaga eneo lile la Klakos, mara alimwona Sherhazad akiwa na mshale uliochoma kinywani mwake akija hewani kwa kasi na papo hapo, lile fuvu likamtoka mikononi. Vile viumbe sita bikawa kama vimepata uhai baada ya Seidon kukanyaga Klakos. Macho ya vile viumbe Aminus, Petrius, Segidus, Sagitarius, Hesmspitus na Sectogamus yakaanza kung’aa na vichwa vyao vikageuka kwa Seidon kisha vikageuka kwa ghafla kuelekea kwa Cleopas na ndipo lile fuvu lilipotoka mikononi mwa seidon na kwenda kunasa moja kwa moja kwenye shingo ya Cleopas.
Viumbe sita vikainamisha vichwa vyao kama vinavyotoa heshima. Nukta hiyohiyo. Sherhazad alijikuta akipigwa na dharuba kali isiyoonekana, akapaisha juu na kujibamiza kwenye ukuta kisha akaanguka chini akihema, hakuweza hata kuvuta hatua.
Vitu kama milipuko vikaanza kutokea kona mbalimbali za lile shimo au pango, vitu anuai vilivyotengenezwa kwa dhahabu safi vikaanza kung’aa na kupendezsesha mle ndani. Seidon aslipiga magoti, Amatagaimba palepale alipo naye alifanya hivyo. Mara Sherhazad kutoka pale alipo aliinuliwa juu na kitu kisichoonekana akashushwa mbele ya Klakos kwa kishindo, alipotua tu, vazi lake alilovaa likaanza kugandamana na ngozi yake.
“Jostrutus, Jostrutus, loctus loctus, abilante sekretus …” yalikuwa maneno yaliyosikika kutoka kila kona lakini hakuna aliyeonekana kufungua kinywa chake. Sherhazad akatulia kimya sasa akiwa kiumbe wa ajabu kabisa, Seidon ambayew hakua mbali naye alikuwa akitetemeka kwa hofu.
“Jostrutus, ulikuwa una nia gani na viumbe hawa?” Aminus na Sagitarius walimuuliza Sherhazad ambaye jina lake katika ulimwengu wao alijulikana kama Jostrutus.
Hakujibu akabaki anathema, vile viumbe vikageuka kwa Cleopas ambaye sasa shingo yake ilikuwa ikinesanesa baada ya kupata uhai kwa lile fuvu.
“Miaka 500 umekuwa ukisumbua viumbe hawa, umekuwa ukiwapumbaza wasijue nini maana ya Klakos, ulikuwa na nia gani?” Petrius na Hesmepitus nao wakauliza kwa pamoja. Siri kubwa ya viumbe hawa walikuwa wakitumia roho moja kila viumbe viuwili vilivyotazamana. Upepo ukaanza kuvuma tena lakini mara hii ulikuwa ni upepo mtulivu, wale vioumbe wakainama vichwa vyao kumwelekea Cleopas.
“Cambialus Serpentus, Cmbialus Serpentus…” viumbe wale sita walianza kutamka kwa kurudia rudia maneno hayo.
Macho ya Cleopas yakang’aa sana na kufanya kama mwali wa moto uliotua moja kwa moja mwilini mwa Sherhazad ambao wao walimtambua kama Jostrutus. Ukelele wa ajabu ukamtoka Sharhazad na mara mwili wake ukaanza kugeuka na kuwa chatu mkubwa wa kutisha, na rangi ya vasi lake ndiyo ikawa rangi ya ngozi yake.
Seidon alihisi kuzimia lakini alijikaza akitetemeka, ule ukelele uliotoka katika joka lile sasa ulikuwa ukisikika hewani lakini haikujulikana ulitoka wapi, mara lile joka likatoka taratibu na kuingia katika ule mto wenye maji mazito, likaishia humo na yale maji yalionekana kama uji unaochemka kwa hasira. Mwisho wa Sherhazad ukawa ndani ya mto huo.
§§§§§
“Mmetoka wapi?” sauti ilitoka kwa Cleopas na kufanya mwangwi mkubwa ndani ya pango lile.
“Hamjui mlikotoka, lakini sisi tunajua mlikotoka, na kila mmoja atarudishwa salama kule alikotoka, lakini kila aliyefika mwisho wa mbio hana budi kupata zawadi,” ile sauti iliendelea. Mara vile viu,be vyote vikainama tena na mikono ta Cleopas ikatoka magotini na kuwekwa kifuani mwake.
“Neema zote za ardhi na mbingu nakurudishieni kila mmoja na alikotoka, mvua zitanyesha, mito yenu itajaa maji, mazao na mashamba yenu vitarutubika na njaa itaondoka katika uso wa nchi, vita na matatizo vitakoma, lakini na alaaniwe kila aliyejaribu kuvuruga mpango wa kuirudishia Klakos uhai. Sisi ni viumbe tunaowapa uhai wa mimea na ninyi pia,” mwangwi wa ile sauti uliendelea na mara hii radi kali ilipasua anga kuashiria mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha huko duniani.
Kisha Cleopas akaonesha ishara ya kuwaita pale juu wote watatu, Anna alihisi ghafla kutowekewa maumivu yake, akainuka na kufuatana pamoja na Amatagaimba na Seidon wakapiga magoti mbele ya Cleopas, katikati ya Klakosi.
“Wewe ni shujaa wa Hamunaptra, na Msindikizaji wako pia, safari hii ya hatari imewagharimu na kuwapunguzia sehemu ya maisha yenu, Mnataka niwape nini?” Cleopas akauliza kwa sauti yake yenye mwangwi ambayo ilisikika pande zote lakini yeye mwenyewe hakuonekana kufungua kinywa.
“Tunahitaji kurudi tulikotoka,” Seidon, Amatagaimba na Anna walijibu kwa pamoja.
“Fumbeni macho, msiwaze lolote vichwani mwenu,” Cleopas akawaambia nao wakatii,
Upepo Mwanana ulianza kuvuma, kila mmoja wao alijiona kama anapaa angani, hali ya utulivu ilitawala kwenye vichwa vyao.
Hospitali ya Dar El Shefa – Cairo, Misri
WAHUDUMU wa Hospitali walimshusha Anna Davis kutoka katika kitabda maalumu na kumlaza kwenye kitanda cha wosini, alikuwa hajitambui, fahamu zote zilimtoka kutikana na lile janga la kule kwenye mapiramidi. Wanafunzi wenzake walikuwa tayari wamekata tamaa ukizingatia mmoja wao alikuwa amepoteza maisha.
“Ataamka muda wowote huyu!” sauti hio ilipenya kwa mbali sana ngoma za masikio ya Anna, hakuelewa nini kinatokea, akili yake ilikuwa ikirudi taratibu kutoka katika safari ya mbali, kutoka katika ulimwengu wa chini kabisa.
Mara akakurupuka na kuanza kuhema kwa nguvu kama aliyekuwa anakimbizwa.
“Ameamka, ameamka!” sauti ya muuguzi ilimshtua mawazo Anna.
“Niko wapi hapa? Niko wapi? Amatagaimba, Seidon wako wapi? Wako wapi?” alikuwa akiongea kama mtu anayeweweseka.
“Anna, Anna tulia Anna, unanifahamu mimi?”
Anna akatulia kiasi na kumtazama mtu aliyekuwa mbele yake, “Ndiyo nakufahamu,” akajibu.
“Mimi ni nani?” yule mtu akauliza.
“Profesa Masati,” Akajibu, kisha akaanza kuwatazama mmoja baada ya mwingine, akamtambua na mwanafunzi mwingine aliyekuwa hapo.
“Inaonekana alikuwa kwenye maono mazito sana katika mzimio wake, labda baadae tutamuuliza kwa tuo ili tujue nini alikiona,” Daktari bingwa wa magonjwa ya akili ambaye aliwaambia tangu mwanzo kuwa kutoka na vipimo, Ubongo wake umepata shida kidogo hivyo anweza kuamka akiwa hana kumbukumbu au nusu kichaa.
Anna alilala kitandani, lakini mara alikuwa anacheka mwenyewe na mara alikuwa ananuna au kutajka majina ya vitu visivyoeleweka.
“Akae hapa kwa wiki zaidi ili nimwangalie namna ya kumsaidia” yule daktari akamwambia Profesa Masati na wakakubaliana hilo.
Jangwa la Uajemi
JUA kali lilikuwa likiwaka, vumbi lilitimka kama limetumwa. Watu wawili waliokuwa juu ya ngamia walitazamana bila kuongea, lakini baadae mmoja alivunja ukimya.
“Amatagaimba, Shujaa wa Msitu wa Solondo, Asante sana kwa kazi hii, Baraka za Klakos ziwe nawe,” Seidon akamwambia Amatagaimba.
“Nawe pia, Mpiga mbio, Shujaa wa Hamunaptra, kama zilivyo mbali Mashariki na Magaribi nasi nafsi zetu hazitaonana tena,” Amatagaimba akashuka katika Ngamia na Seidon akafanya hivyo, wakakumbatiana na kuagana kisha kila mmoja akaenda upande wake.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
MWISHOO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni