RANIA (7)
Zephiline F Ezekiel
3 min read
JINA: RANIA
SEHEMU YA SABA
ILIPOISHIA...
Rania, ninakitu naomba unisaidie...alisema Mfalme.Aaah...kumbe na wafalme hua wanaomba...alisema Rania huku anacheka kwa chini chini.
Mfalme ilibidi atabasamu tu maana hakua na cha kufanya.
Mfalme alimweleza ombi lake Rania...
Nini?...mimi?... Eti niwe....aah..hapana haiwezekani...alisema Rania baada ya kusikia ombi la Mfalme.
SASA ENDELEA..
Rania,hujajua Kwanini nimekuchagua wewe nikiwa najua kabisa huna hiyo taaluma...alisema Mfalme kisha akweka kituo.Hapana Mfalme, kwa vyovyote vile hii kazi siiwezi..nitawezaje kua mganga mimi?...nitaifanyaje kazi hii nisioijua?.. Alisema Rania.
Rania, hujajua kitu kimoja, naomba nikuelezee kwa mapana zaidi labda utanilewa...alisema Mfalme.
Mimi ni mfalme hapa..lakini naendeshwa sana na baadhi ya watu katika ikulu hii akiwemo mwanangu wa kumzaa mwenyewe.
Jukumu la kuchagua mganga ni langu kwakua watu wanaamini mfalme pekee ndio anaweza kupata maono ya kuchagua Mganga wa nchi kitoka kwa mizimu jambo ambalo kimsingi sio kweli.
Mimi tangu niwe Mfalme sijawahi kupata hayo maono.
Ingawa jukumu hilo ni langu, lakini kila mganga ninaemchagua anaishia kua kibaraka anaefuata anayoambiwa na mwanangu Azza pamoja na viongozi wanoshirikiana nae kwenye njama zao.
Maskini mwanangu hajui nia halisi ya watu anaoshirikiana nao...alisema mfalme kisha akanyamaza kwa muda mfupi kidogo.
Kila mganga hua anafuata mashariti yao maana hua wanampatia vitisho na wanamuonya kua akithubutu kusema kwa Mfalme atakufa yeye na familia yake kabla hajaonana na mfalme... Alisema mfalme.
Rania, naamini wewe ni jasiri sana,kama hukuniogopa mimi sizani kama utawaogopa wao.kwahyo nahisi hawataweza kukutumia kama walivyo watumia wengine maana wewe hutishiki..nakuomba kubali ombi langu..nchi hii itaingia pabaya sana kama wale nyang'au watafanikisha kuiteka...alisema Mfalme.
Mfalme, kwani mganga akiendeshwa na wao kuna tatizo gani kubwa sana?..aliuliza Rania
Tatizo lipo..katika nchi hii mganga ananguvu sana maana kila alisemalo watu huona limetoka kwa mungu..katika nchi hii mganga anakazi kubwa mbili ambazo Mfalme haruhusiwi kuzipinga..moja ni kuchagua mrithi wa kiti cha Mfalme endapo kuna wana wa mfalme wawili wanaolingana..hapo lazima mganga aiulize miungu.
Pili ni uchaguzi wa malikia mpya kama ikitokea malikia akafa..mengine yote nina uwezo wa kuyapinga hata kama mganga akijidai kutabiri...alisema Mfalme.
Azza anashirikiana na waziri mkuu wa hii nchi na wanatumia mganga ili kwamba aseme kua Azza ndo mrithi sahihi maana kuna mwanangu mwingine aliezaliwa siku moja na Azza
Azza anahofia kua ataikosa hiyo nafasi maana yeye no mtoto wangu lakini sio wa malikia na malikia ndo mweyr huyo mtoto anaelingana na Azza...alisema mfalme
Lakini mfalme, kwani mganga aliepo utamtoaje?..aliuliza Rania
Hayupo alipata ugonjwa mbaya akafariki...alisema Mfalme
Rania anomba unisaidie katika hili maana ninavyomjua Azza akiwa mfalme hii nchi haitadumu.. Alisema mfalme.
Sasa kwenye mambo mengine unazani itakuaje wakati sina ujuzi?..alisema Rania.
Kiukweli mganga aliekuwepo hakua akijua kitu chochote kuhusu uganga.. Nilidanganywa enzi hizo sijajua nia yao nikamchagua kua mganga..
Sasa Kumbe walikua wamemwandaa halafu mganga aliekuwepo kabla ya huyu aliekufa juzi juzi,walimkamata wakamfungia kwa siri ikasemeakana amekufa halafu wakawa ikitokea shida kwenye nchi wanamfuata na wanamuuliza na akisema wanatishia kumuua mke na watoto wake. Kwahyo ikajulikana kua huyu aliekufa juzi juzi ni Mganga mzuri kumbe muongo..
Sasa hao waganga wote wawili pamoja na huyo wa zamani wamekufa halafu mimi nina mganga wangu wa siri ndo atakua anakupa ufumbuzi wa matatizo . anaishi himu kwenye chumba cha siri.... Alisema mfalme.
Mmmh....humu ikulu kuna mambo jamani...alisema Rania
Rania alifikiria kwa muda kidogo kisha akakubali ombi la Mfalme wa Lazi.
Mfalme, nimekaa sana nikafikiri nikajua kwanini umefanya maamuzi ya kumfanya Rania mganga, nakukubali sana Mfalme, una maamuzi ya haraka na akili yako inafikiria mbali kwa muda mfupi... Alisema mlinzi wa mfalme wa Lazi akwa anaongea na mfalme
Mara ya kwanza nilimtaka Rania ili aje awe mke wangu sababu ua urembo wake,lakini baada ya kuiona tabia yake nikaona ni bora zaidi awe mganga kwa ajili ya mema ya nchi yetu.
Kesho yake Mfalme aliitisha kikao na viongozi wa nchi yake ili awatambulishe mganga mpya Rania.
Muda huo Rania alikua akivaa mavazi ya kiganga.
Mmnh.. Jamani hivi ntaweza kweli!!! Ngoja nijaribu..
Tdgi..tsjhhjs..shsusms . alisema Rania maneno ambayo hayapo eti hapo ni Mganga anapiga ramli
Mmmh jamani . mimi mrembo hivi niwe Mganga jamani.. Hata mzimu watanitongoza😂😂....mmh..Rania mie...alijisemea Rania kimoyomoyo.
Baada ya muda Rania alitambuliswa mbele ya baraza na viongozi wakatawanyika baada ya utambulisho..
Hivi Mfalme ameamua kuchagua mganga bila kutushirikisha!!!...alisema mama yake Azza.
Et anadai ameoteshwa....ameamua tu kutuzunguka...sijajua kwanini kamchagua binti ndogo vile.. Pole yake..hata huyo tutammiliki... Alisema Azza.
Azza fanya mpango haraka utafute wazazi wa huyo Rania wanaishi wapi..akikataa ushirikiano wetu tutawafanyia kitu kibaya....alisema waziri mkuu.
Hilo wazo liko vizuri sana nitahakikisha najua...alisema Azza huku anatikisa kichwa..NINI KINAFUATA?.
USIKOSE SEHEMU YA NANE
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni