MTAA WA TATU (62)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA SITINI NA MBILI
Video na picha zikasambazwa kwenye mitandao ya kijamii,
“mmh! Duhuu ebwana dahaa hakika huyu mtu hafai kabisa yani wafungwa walijuwa wakuja ehee
Wacha awaonyeshe kazi"
NIOMBE SAPOTI, BONYEZA TANGAZO LINALOKUJA NA KUJAA KWENYE SIMU YAKO WAKATI UKIFUNGUA SIMULIZI AU LILE LINALOKUWA KATIKATI YA SIMULIZI ZETUKABLA HAUJAIFUNGUA NDANI, PIA KUNA LILE LINAKUJA NA KUNG'ANG'ANIA HAPO CHINI, BONYEZA WALAU MARA 3-4 HIVI HIYO NDIO SAPOTI YAKO KWANGU, TAFADHALI NIPE NGUVU NAKUTEGEMEA SANA MSOMAJI WANGU
SASA ENDELEA...
Mmoja kati ya Askari akaongea hivyo.
Huku akisaidiana yeye na mwenzake
kuibeba miili ya vijana wale.
“Sasa vijana hili jambo nahitaji iwe siri yenu sitaki mtu yeyote afunguwe mdomo na kuzungumzia kitu hiki vinginevyo tutaonana wabaya,’’ Mkuu wa gereza akasema hivyo akiwa yupo sirius. “sawa mkuu tumekuelewa’’ askari wote wakaitikia na kutawanyika kwenda kuendelea na maswala mengine kesho yake asubuhi na mapema mkuu wa gereza akapokea ujumbe anahitajika makao makuu haraka sana iwezekanavyo afike huko nae hakuwa na hili wala lile akaingia ndani ya gari yake na kuelekea huko makao makuu. Akiwa njiani ndipo akaanza kujiuliza maswali mengi sana pasipo kupata majibu , “imekuwaje mbona nimeitwa kwa ghafla hivi au lile tukio la jana limeweza kujulikana nini? Sasa kama limeweza kufahamika nani kavujisha hii siri’’,,,Hafidhi mwenyewe au mmoja kati ya vijana wangu, haina shida wacha niende nitakuja kufahamu huko huko. Lakini kabla ya kufika makao makuu akapitia kwenye kibanda kimoja hivi aweze kununua gaazeti wakati akiwa kwenye kutupia macho vichwa vya habari vya siku hio akashtushwa na kuiona ile habari imetapakaa kwenye kurasa za mbele karibia magaazeti yote
“ohoo shiti upuuzi gani huu ulioweza kutokea nani kafanya hivi mkuu wa gereza akajikuta akiongea kwa hasira na kuupiga ngumi usukani wa gari na kuondoka eneo hilo hata kununua gaazeti hakutaka tena, akafika makao makuu kijasho kikimtoka “karibu sana bwana Msafiri’’ “asante sana mkuu nimeweza kukaribia naona asubuhi asubuhi tunaitana vipi kuna tatizo?’’ Bwana Msafiri akauliza swali huku akikaa kwenye kiti,
“hapana hakuna tatizo lolote kaka sema nimekuita hapa kutaka kukwambia yakwamba kuanzia sasa itabidi uamishwe gereza na kupelekwa kigoma,’’ mkuu wa kitengo akazungumza hivyo huku akiwa anatabasamu. “mkuu mbona umekuwa uwamisho wa ghafla hivyo na kwanini nahamishwa?’’
mkuu wa gereza akauliza kwa mshangao, “sikia nikwambie kitu bwana Msafiri siku zote usitake kuweka kila kitu wazi wakati wewe mwenyewe hukupenda kuliweka wazi cha umuhimu ni kujiandaa tu kwaajili ya safari kisha mengine yatafatia,’’ mpaka hapo Msafiri akawa keshaelewa kwanini anahamishwa kutoka gereza la segerea na kupelekwa sehemu nyingine, akainuka kwenye kiti na kuondoka zake hakukumbuka hata kuaga kibaya zaidi akajisahau kama alikuja na gari yake na kujikuta akielekea kituo cha daladala, “imekuwaje mbona bwana mkubwa kaiyacha gari yake hapa?’’ mmoja kati ya walinzi alimuuliza mwenzake, “labda itakuwa na hitirafu fulani au imeishiwa mafuta na ndio anaenda kufata,’’ nae akamjibu hivyo “hapana bwana kitu kama hiko hakiwezekani kwa mkuu kama yule lazima angeondoka na gari nyingine mara ngapi anakuja hapa hajawai kuacha gari!’’
Bwana Msafiri akiwa amekaa kwenye siti ndani ya daladala ndipo simu yake ikaita akaitowa na kuangalia mpigaji ni nani akaona jina la mkuu wa kitengo basi akaipokea na kusikika sauti ikimwambia “bwana Msafiri inamaana hili gari umeamua kutususia au?’’ nae akafadhaika si kidogo na kujiona kweli amedata yani amesahau gari yake na kupanda daladala,
“wee konda niache hapo’’ akapaza sauti kuomba ashuke, Yapata majira ya saa nne asubuhi ndani ya gereza la Segerea kwenye chumba kimoja wapo hivi kulisikika sauti ya kitu kikilia kwa kishindo kunzia Askari jela mpaka wafungwa wakabaki kushangazwa na kishindo hiko. Kwa mwendo wa kunyata baadhi ya askari wakajongea na kutaka kufahamu ni kishindo cha kitu gani, ile kufika tu hawakuweza kuamini baada kumkuta mwanaume wa shoka akipiga ngumi kwenye ukuta mpaka akatoboa tena akiwa yupo tumbo wazi mwili uliojengeka kimazoezi zaidi, “ebwana ehee huyu mtu au roboti mbona yuko hivi?’’ Askari mmoja akauliza swali sema hakuna aliyeweza kumjibu Mwanaume akaendelea na mazoezi yake japokuwa aliweza kuwaona watu wakimshangaa yeye hakujali kabisa, wakati walimu wake wakiwa katika harakati za kutaka kumgombowa ndani ya gereza mzee J Ikram akawaambia hivi Hafidhi sio kama anashindwa kutoroka anaweza sana sema hataki tu na yale ni maamuzi yake kwahiyo msijisumbuwe kabisa kwenda kumtowa muacheni. Kwakuwa ni kauli iliyotoka kwa baba yake na ni mkuu wa majeshi nao hawakuwa na jinsi ni kuachana na hilo swala’ kabla ya kufika siku ya hukumu watu wengi sana walienda kumtembelea “Hafidhi baba watoto wangu mbona unataka kuniacha mkiwa kwanini lakini umeamuwa kufanya hivi?’’ bibiye Beatrice aliongea hivyo huku akilia Hafidhi akamfuta machozi kwa kiganja chake cha mikono na kumwambia “siwezi kukuacha ukiwa mwenyewe siku zote nitakuwa nawe daima mwambie Sheira na Seiph baba yao nilikuwa nani naomba uwalee watoto wangu kwenye misingi iliyo bora,’’
“unaongeaje maneno hayo wakati umesema hutoniacha peke yangu tafadhali Hafidhi baki na mimi,’’ wakati wakiwa wanaongea wazazi wake Hafidhi na wao wamekuja kumuona mtoto wao sema walishangazwa kidogo kwa kumuona bibiye Beatrice akilia huku akiwa kawapakata watoto wawili baada salamu wakauliza basi Hafidhi akawaambia kila kitu binafsi wazazi wake wakafurahi na kuwabeba wajukuu zao. “Hakika nina furaha kubwa sana kwa kuitwa bibi kuonyesha jinsi gani furaha yangu imepitiliza huyu binti ambaye ni mkwe wangu nitaenda kuhishi nae pamoja kwani baba yako kanunua nyumba kubwa maeneo ya Mbezi beach,’’
Mama yake akaongea kwa furaha huku chozi likimdondoka, ni kesi iliyochukuwa takribani mwaka mmoja na nusu bwana mkubwa akiwa anasota ndani ya jera tokea afikishwe ndani ya jera hiyo hakihitaji kujenga urafiki na mtu yeyote yule muda mwingi aliutumia akiwa peke yake kesi ikawa ikisogezwa mbele tu hatimae siku ya hukumu ikafika ndani ya mahakama kulifurika watu kila mmoja akitaka kufahamu nini hatma ya Hafidhi j Ikram
“Baada kufanya safari ndefu yenye mirima na mabonde jangwa na makorongo, hatimae leo hii tumefika mwisho wa safari yetu, muheshimiwa hakimu ndio yalikuwa maneno yake yakwanza kuzungumza kisha akaendelea siku zote sheria ya nchi hairuhusu kitendo cha kuuwa iwe kwa bahati mbaya au makusudi. Sasa basi ndugu Hafidhi j Ikram yeye hakutaka kuiyacha sheria ifanye nini akajichukulia hatua kwenye mikono yake sasa basi ni kosa kisheria. Baada kuongea hivyo hakimu akanyamaza na kuweka miwani yake sawa, kabla mahakama haijakupatia hukumu je unalolote la kujitetea?’’ hakimu akamuuliza swali nae akatikisa kichwa kuashiria ndiyo analo la kusema, akaambiwa haya jitetee
“ndugu muheshimiwa hakimu kiukweli sina cha kujitetea isipokuwa nahitaji kuwaambia wazazi wangu wanitunzie watoto wangu,’’ baada kuongea hivyo akanyamaza na kumpa nafasi Hakimu atoe maamuzi “sawa kijana bila shaka wazazi wako wamekusikia ndugu Hafidhi j Ikram kutokana na kupatikana na kosa la kufanya mauwaji na kwenda kinyume na sheria ya mwaka 1961 kifungu number116 unahukumiwa kwenda jera miaka Nane,’’ watu wote mahakamani ahaa kila mmoja akajishika kichwa asiweze kuamini kwa ile hukumu hata Hafidhi mwenyewe akabaki kuduwaa mbona hukumu yenyewe imekuwa ndogo hivyo kila mmoja akamtazama hakimu nae machozi yalikuwa yakimtoka akavua miwani yake na kujifuta kwa kitambaa akanyanyuka na kushuka juu ya korti akapiga hatua kadhaa na kwa kusogea kizimbani ni kitu ambacho hakijawahi kutokea “nenda kijana katumikie adhabu yako nimefanya yote haya kwasababu mimi ndio mjomba ake marehemu Habiba nakumbuka vyema mke wangu alikufa kifo cha kinyama sana kwa kuitiwa kelele za mwizi’’
Yani aliuwawa mbele ya macho ya ndugu yake wa damu tena toka nitoke kisa kitu kidogo tu kumuuliza mbona siku hizi kaka yangu umebadilika mwanao wala humjali tena, unamuacha anapigwa bwana yule akamuitia kelele za mwizi. Mke wangu mpendwa akapigwa na kuvishwa pira hatimae wakamchoma moto mbele ya ndugu yake leo hii utasemaje damu nzito kuliko maji. Yani kauwawa haliyakuwa ana wiki sita tu tokea atoke kujifungua watoto wetu mapacha, akaniachia vichanga, Kijana nilitamani sana nikuachie huru sema nenda kijana utatoka tu,’’ baada kuongea vile muheshimiwa Hakimu akamshika Hafidhi begani na kuondoka zake akiwa anajifuta machozi, mpaka hapo kila mmoja akaweza kutambuwa kwanini hukumu imekuwa ndogo hivyo na kwanini alitoa hukumu ya kunyongwa kwa bwana Khatibu yeye na wenzake huku wengine wakihukumiwa kifungo cha maisha jela wapo baadhi ya watu wakasema kesi itakuwa imenunuliwa ile kwasababu baba yake ni mkuu wa majeshi haiwezekani aukumiwe miaka nane kwa mauwaji aliyoyafanya ni upuuzi mtupu. Ndani ya gereza watu hawakuacha kuja kumtembelea Hafidhi hasa wazazi wake na ndugu jamaa na marafiki kutokea mtaa wa tatu, “Hafidhi my baby ulisema utakuja kuniowa sasa upo gerezani je utaniowa kwa njia ipi?’’ alikuwa bibiye Smaiya mdogo ake marehemu Yusra akimuuliza Hafidhi siku ambayo alienda kumtembelea gerezani. Kabla ya kumjibu akamtazama na kumwambia “kama kweli unanipenda basi utaningojea kama ukiona miaka nane ni mingi chukuwa maamuzi mapema’’
“hapana sio mingi ningekusubiri hata ingekuwa miaka elfu na malaki,’’ Smaiya akaongea hivyo akiwa anatabasamu wakakutanisha ndimi zao na kupeana kitu roho inapenda siku zote Hafidhi hakuwai kumueleza yoyote kuhusu habari za wake zake bibiye Vivian na Mariam akabaki kimya tu wala hakuhitaji rafiki yeyote ndani ya gereza zaidi ya wale wanaokuja kumtembelea.
NA HAPA NDIO MWISHO WA SIMULIZI HII YA MTAA WA TATU, SEMA HAMNIPI NGUVU NITAKUJA NA KISA KINGINE ILA MNISAIDIE HATA VOCHA KWENYE NAMBA HIZO HAPO CHINI
NAOMBA SAPOTI, KUNA MATANGAZO(ADS) YANAJITOKEZA KWENYE APP YETU, LIMOJA LINAJAA KWENYE KIOO CHAKO JINGINE LINANG'ANG'ANIA HAPO CHINI KABISA, BONYEZA JAPO MARA 2 AU 3 KILA UKIFUNGUA SIMULIZI HIYO ITANIPA NGUVU YA KUENDELEA ZAIDI NA SIMULIZI ZETU🙏🙏
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

MWISHO
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni