MTAA WA TATU (60)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA SITINI
Bibiye Mona ndio akaja kumfunga pingu ajabu wananchi walikuwepo maeneo hayo wakapinga vikali kitendo cha kukamatwa Hafidhi sio sahihi kabisa ikabidi polisi watumie mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi.NIOMBE SAPOTI, BONYEZA TANGAZO LINALOKUJA NA KUJAA KWENYE SIMU YAKO WAKATI UKIFUNGUA SIMULIZI AU LILE LINALOKUWA KATIKATI YA SIMULIZI ZETUKABLA HAUJAIFUNGUA NDANI, PIA KUNA LILE LINAKUJA NA KUNG'ANG'ANIA HAPO CHINI, BONYEZA WALAU MARA 3-4 HIVI HIYO NDIO SAPOTI YAKO KWANGU, TAFADHALI NIPE NGUVU NAKUTEGEMEA SANA MSOMAJI WANGU
SASA ENDELEA...
Hapo Hafidhi akapakizwa kwenye gari safari ya kupelekwa kituoni ikaanza bibiye Mona alikuwa yuko makini sana kumtazama Hafidhi usoni ijapokuwa bibiye machozi yalikuwa yakimtoka binafsi Hafidhi kapitia hatua nyingi sana kwa kuifanya hii kazi ambayo hata kama wangepewa POLISI, FBI, USALAMA WA TAIFA, JWTZ, UNDERCOVER AGENT Hata kama wangekuwepo wote kwenye kazi hiyo sidhani kama ingefanyika kama alivyoifanya mtu mmoja tu, taarifa za kujisalimisha kwa Hafidhi ziliweza kujulikana nchi nzima huku mzee J Ikram akisema kile alichokifanya mwanae ni sahihi kabisa siku zote jambazi akamatwi kwa kufungwa kazi ni kuwauwa tu ili iwe fundisho kwa wengine kwani akifungwa si atatoka na kuja kufanya uporaji kwa mara nyingine akifahamu nikikamatwa nitaenda kula ugali wa bure ndio maana mwanae akawafyeka tu kama ufisadi ujambazi kula rushwa wakafanyie huko kuzimu, “sasa mume wangu utafanyaje kuhusu mtoto wetu ndio hivyo tena kajisalimisha na hukumu pekee ni kunyongwa tu,’’ Mama yake Hafidhi akaongea hivyo kwa sauti yenye kukata tamaa, “hapana haiwezekani mwanangu anyongwe kizembe wakati mimi nipo hai nitafanya kila namna asipewe adhabu hiyo, “sasa utafanyaje mume wangu?’’ “mke wangu embu ondowa mashaka kila kitu kitakuwa sawa kuhusu mtoto wetu kama niliweza kuvipanga vikosi vyema mpaka tukafanikiwa kumng’oa Nduli Idd Amini Dada, nitashindwaje kumkomboa mwanangu kwanza hakimu atakaye jalibu kufunguwa mdomo wake na kutamka ujinga sijui Hafidhi unanyongwa kudadeki nitamlipua palepale mahakamani,’’
Kukamatwa kwa Hafidhi ulikuwa kama vile msiba mkubwa kwa watanzania hasa waliokuwa wanyonge watu wakaandamana nchi nzima wakishinikiza mtetezi wao shujaa wao aweze kuachiwa kama wao wanauwa vibaka kwa kuwatia moto mbona hakuna hata mwananchi mmoja aliyekamatwa kwa kufanya mauwaji hayo je polisi hawafahamu kama Manzese, Tandale, Tabata, Buguruni, Temeke, na sehemu zinginezo mwizi akikamatwa anavishwa pira na kutiwa moto, basi wakamatwe wenye kufanya vitendo vile “muacheni’’,,,,shujaa wetu,,,,muacheni’’,,,shujaa wetuu,,,, yani barabara zilifungwa kutokana na watu kutapakaa kila kona ya mji wakiishinikiza Serikali kuachiwa kwa Hafidhi muuwaji wa kutisha baada Hafidhi kukamatwa akapelekwa moja kwa moja kwenye kitengo maalumu na kufungiwa kwenye chumba kimoja wapo huku ulinzi ukiwekwa vya kutosha, yote ilikuwa katika kumdhibiti yeyote atakayejalibu kutaka kumtorosha mtuhumiwa ndio maana hakupelekwa kituo chochote cha polisi wala gerezani. Hafidhi akiwa kajiinamia ndani ya chumba hicho ghafla akasikia sauti ya mtu akiimba na kupiga makofi kwa kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoweza kuifanya akanyanyuka kutoka kwenye kiti na kuangalia huku na kule hakuweza kuamini macho yake baada kumuona marehemu Habiba akiwa na bibiye Yusra wakimuimbia nyimbo nzuri embu tuisikilize
“Mtaa wa Tatu’’,,,,umetuacha gizani shujaa wetu yupo kifungoni’’,,,nasie tupo pembeni’’,,,hatuwezi kumuacha peke yake’’,,,hii kesi sio yake peke yake’’,,,niyetu sote’’,,hakika Mtaa wa Tatu usiwe na roho yakutu ukatutupia viatu,,,,Hafidhi’’,,,Hafidhi tunakupenda tunakujali tunakukubali japokuwa tupo mbali nawe shujaa wetu usipagawe hata kama Mtaa wa Tatu umekutengaaa’’,,,,,hakika ilikuwa nyimbo nzuri kutoka kwa mabinti hao ambao tayari washaenda mbele ya haki walikuja kimiujiza na kuondoka kimiujiza wakamuacha Hafidhi akiita na kupapasa ukuta “Yusra’’,,,,,Habiba,’’ akapaza sauti kuita sema sauti yake haikuweza kusikika popote pale zaidi ya kubaki humo humo ndani ya chumba “Hafidhi kijana wangu nini umefanya hiki? Yani kukupa muda wa kuimaliza kazi ndio ukaamua kuja kujisalimisha kwenye mikono ya wanadamu’’ ni sauti nyingine kutoka kwa Ibnuwasi ndio iliyomshitua Hafidhi na kufanya ageuke kumtazama baba yake kwa upande wa majini. “ndio baba yangu haya ni maamuzi yangu mimi natamani sana ninyongwe kama safari ya kuja kuzimu nije kwa style hii nahitaji kila mtu aweze kufahamu Hafidhi hayupo tena duniani,’’ “hahahaha’’ Ibnuwasi akacheka sana na kusema “Hafidhi wewe ni komando wa aina gani yani tulitaka kukupima tu uwezo wako uko vipi kwa kukulaza kitandani na kukuambia vile kumbe hakuna chochote kibaya kitakachoweza kukutokea kwanza tambua kitu kimoja vifo au kifo mpangaji wa yote ni Mwenyezi Mungu yeye ndio muweza wa kila kitu sasa basi fanya utoke’’,,,,,baada Ibnuwasi kusema hivyo akapotea “ha!ha!ha!,,,,tehe!tehe!tehe!,,,hahahaha’’ kwanza mwanaume alianza kucheka yani alicheka wee mwishoe akasema ndani ya usiku huu nawaacha soremba’’,,,,
“Ndani ya usiku huu sitoweza kubaki ndani ya chumba hiki, wacha niondoke lakini si nitakuwa nimevunja mkataba baina yangu na Serikali maana nimejisalimisha kwao kwa hiyali yangu mwenyewe kisha nikimbie. Hapana wacha nitulie nijuwe mustakabari mzima wa maisha yangu sijui nini kitanikuta katika kesi hii ya mauwaji ya haraiki ya watu. Hivi kwanini yule bibi akafanya kupandikiza mbegu ya kijini katika mwili wa mama yangu, mpaka nikazaliwa na homoni za aina mbili nusu Binadamu nusu Jini itakuwaje siku moja wazazi wangu wakaja kutambuwa hilo si nitatengwa mimi,’’ kitendo cha mimi kukamatwa bila shaka wazazi wangu washapata taarifa na wapo njiani kuja kuniona sijui itakuwaje kwa mzee J Ikram nahisi hatopenda kuona mwanae nikipatiwa hukumu ya kifo, sema itakuwa haina jinsi ni kukubali matokeo. Sasa kama mimi nusu Jini nusu Binadamu inamaana watoto wangu nao watakuwa ni hivyo hivyo,
Yote yalikuwa mawzo ya bwana mkubwa akiwa amekaa kwenye kiti kajiinamia akiwaza hili na lile kikomeo cha mlango kikawa kikitikiswa nae akainua kichwa chake kuangalia ni nani huyo anaekuja kumtazama kwa wakati huo. Mlango ukafunguliwa kwa taratibu akaingia kijana mmoja wakiume akiwakavalia mavazi ya kiuaskari ajabu alikuwa anatembea kwa mwendo wa kunyata kumsogelea Hafidhi pale alipokaa, nae hakutaka kuzubaa akamsoma yule afande na kumuona akichomoa kisu na kuja kwa kasi kwa nia moja tu ya kumchoma nacho cha shingo mwanaume akachumpa kutoka kwenye kiti na kukikanyanyua kile kiti akafanya kama ngao kisu kikaenda kukita kwenye kiti, ngreee,,,,ngwaaaa,,,ndio sauti iliyoweza kusikika ya kisu kile ikikikwanguwa kile kiti, Askari yule asieweza kufahamika ni nani na katokea wapi usoni alikuwa amevaa kitambaa cheusi kichwani amevaa kofia aina ya kapelo, viliweza kuiziba vyema sura yake asiweze kujulikana, basi ilikuwa akitaka kuchoma huku Hafidhi anazuiya kwa kutumia kile kiti yule afande akadanki kwa kuchumpa kwenye ukuta na kuachia mateke mawili double yaliyompata bwana mkubwa kifuani akayumba na kujibamiza ukutani huku kiti kikimponyoka mikononi mwake, nae akajiweka sawa baada kutambuwa kumbe huyu mtu si wamchezo kabisa, kwanza akahitaji kumfahamu huyu mtu ni nani. Njia pekee ni kumvua kile kitambaa jamaa akawa anakuja kwa kasi ya kimbunga mkononi kashikilia kile kisu barabara kitendo cha kufika tu nae akajikuta akipigwa teknik moja tu yani ngumi ya kumsukutua kidevu akarushwa hewani na kurudi alipokuwa kasimama awali huku kile kitambaa na kofia vikimvuka.
Dahaa kumbe alikuwa kijana Michael hapo sasa wamekutana mbona patamu, Hafidhi akatabasamu baada kuiona sura ya yule jamaa kisha akasema “ni kheri ungefanya kitu kimoja cha maana sana nacho si kingine ni kumzika baba yako kuliko kuja kulazimisha kifo chako sijui nani atamzika mwenzake,’’ “nyamaza mjinga mkubwa wee nawe tambuwa kitu kimoja huu ndio mwisho wa maisha yako, hivi unafikilia kitendo cha kujisalimisha kwenye mikono ya sheria ndio utasalimika sio,’’ Michael akaongea kwa hasira “sawa brother siwezi kuhukumiwa kwa hiki nitakacho kitenda leo hii juu yako siku zote mtoto akililia wembe mpe achezee ukimkata ndipo atakapo tambuwa kumbe hii ni hatari njoo sasa,’’ Hafidhi nae akaongea hivyo huku akimuonyeshea Michael ishara ya mkono asogee karibu yake. Binafsi Michael akaona kama vile anapoteza muda tu akamfata kwa kasi kisu kikiwa mkononi mwake kabla ya kumfikia upepo ukaanza kuvuma kwa kasi kitendo kilichomfanya Michael afunge bleak na kusimama huku akijitahidi kujizuia ule upepo usimyumbishe.
Kufumba na kufumbua Ninja short huyo hapo mbele yake yani Hafidhi akiwa kwenye mavazi hayo hakuna kinacho haribika juu yake nae mikononi kakamata zile silaha zake, sasa mchezo uanze Michael bila kusita wala kujiuliza akamfata na kuanza kupigana kwa kutumia silaha zao kila mmoja alikuwa mkali wa mapigo katika piga nikupige silaha ya Michael yani kisu chake kikamponyoka na kudondoka chini kibaya zaidi kimedondokea miguuni mwa mpinzani wake kila mmoja akabaki kumtazama mwenzake huku wakihema hakika vijasho viliwatoka maana ilikuwa piga nikupige. Hafidhi akaziangalia silaha zake na kuona haina haja ya yeye kuzitumia akazitupa pembeni na kukunja ngumi sasa ilikuwa kavukavu wanaume waonyeshane kazi wakati ndani ya chumba hiko mpambano ukiendelea kwenye chumba kingine kulikuwa na kikundi cha maafande na kikosi cha FBI mbele yao kukiwa na tv kubwa aina ya flat sicren nch 32 wakiangalia jinsi wanaume wa kazi wakionyeshana show kumbe ndani ya chumba alichofungiwa Hafidhi kuna camera.
Hafidhi alipigwa ngumi kama nne za haraka haraka akapanchi sema moja ikampata sawiwa kwenye korodani akayumba na kwenda chini kijana Michael alikuwa yuko shapu zaidi baada kumtandika ile ngumi bwana mkubwa kufumba na kufumbuwa kisu kikakita tumboni kwa Hafidhi yani Michael alichumpa na kuiwahi silaha yake ile Hafidhi ananyanyuka tu akakutana uso kwa uso na Michael kisu kikazama tumboni mwake. Michael akafanya kukishindilia kwa kukizungusha kisha akakichomoa na kutaka kumchoma tena Hafidhi akacheuwa damu ile jamaa anataka kumchoma tena tu akakidaka kile kisu kwa kushika kwenye makali. Ikawa huyu anakisukumiza mwengine anakizuiya japokuwa kilikuwa kikimkata mkononi mwake sema hakutaka kukiachia ghafla kisu kikavunjia kohooo’’,,,,
Michael akabaki na mpini huku bwana mkubwa akibaki na makali akatazama juu na kukirusha kile kipande kikaenda kutua kwenye camera na kuivunja mwanaume akazunguka kwa kasi kumfata Michael nae akajipanga kumpokea baada kumfikia akamwambia neno moja tu “kimbia huku yale majeraha yake yakijiunga, zile silaha zake zilikuja zenyewe kwenye mikono yake utasema sumaku na chuma
NAOMBA SAPOTI, KUNA MATANGAZO(ADS) YANAJITOKEZA KWENYE APP YETU, LIMOJA LINAJAA KWENYE KIOO CHAKO JINGINE LINANG'ANG'ANIA HAPO CHINI KABISA, BONYEZA JAPO MARA 2 AU 3 KILA UKIFUNGUA SIMULIZI HIYO ITANIPA NGUVU YA KUENDELEA ZAIDI NA SIMULIZI ZETU🙏🙏
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA SITINI NA MOJA
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni