Notifications
  • MY DIARY (27)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA SABATULIPOISHIA...Alinamba eti hayo ya mimi kuolewa tuyaeke pembeni na kwa nini siku hiyo nisilale Moshi tukumbushie enzi zetu. Mwalimu John aliendelea kusema kuwa amenimiss sana na anomba nisahu yaliyopita na turudie yale maisha yetu ya zamani.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilijifanya simwelewi lakini ukweli ni kwamba nyota ya mwanaume huyu ilikuwa ni kali sana zaidi yangu na…
  • MY DIARY (26)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA SITATULIPOISHIA...Joyce alinambia yeye haendi kujipanga foleni kama makahaba wengine hivyo yeye hufanya biashara hiyo kitaalamu zaidi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Alisistiza pia kuwa eti huwa anatumia kinga kuwakinga wengine. Wakati mwingine alinambia acha awaambukize kwa sababu wanaume wangekuwa na akili basi wasingeenda kununua mwanamke. Anasema kuwa laiti biashara hiyo…
  • MY DIARY (25)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA TANOTULIPOISHIA...Sikuisha hapo pia nilimpongeza kwa kunijali na kunipenda na kuhakisha kuwa siingii kwenye majanga kama yake mara baada ya kutoka jela. Siku hiyo nilimuelewa sana Joyce na nilikuwa tayari kumsapoti kwa lolote ili mradi tu atimize athma yake hiyo ya kuzaa. Tuliongea mengi sana na baadaye alinionesha picha ya mtu ambaye alitaka kuzaa naye.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (24)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA NNETULIPOISHIA...Kwa kweli siku hiyo niliwaza sana na kutafakri vitu vingi. Wale wanachuo wenzangu wamenambia kuwa Msouth alikuwa kwa kimada mwingine na japo stori haikumalizikia ila ukweli ni kwamba alifumaniwa na kupigwa vibaya na huenda walimtupa mahali na ndio maana chanzo cha kifo chake hakieleweki.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilijaribu kuijikontrol ili nisiwaze kitu…
  • MY DIARY (23)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA TATUTULIPOISHIA...Alinisihi sana nisitoe niilee na yeye atatoa huduma zote lakini tuendelee kufanya siri ili tusije tukahatarisha ndoa yake na kusababisha familia yake kuyumba. Kwa kweli sikuweza maana ilikuwa ni kujipa tabu mimi na huyo mtoto atakayezaliwa. Bora ataa ingekuwa ni mimba ya ule mwalimu ambaye hajaoa.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilitamani nimchomekee hiyo mimba…
  • MY DIARY (22)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILITULIPOISHIA...Alitumia vizuri umbo lake la kimiss kutembea kimiss na kuweka mapozi ya maana. Na baada hapo alilala kwenye kile kigodoro na akachojoa vyote isipokuwa kufuli jeupe ambalo nalo alipewa hapo hapo kwa ajili ya kazi hiyo. IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi sikumpa nafasi Joyce niliingilia nafasi yake na kuchukua ule uume wa bandia nikamfuta yule dada.…
  • MY DIARY (21)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJATULIPOISHIA...Nilichomeka simu chaji na kuiweka hewani ili nione kama kutakuwa na sms yeyote iliyoingia.Hofu ilizidi kunitawala na wakati naendela kufikira simu yangu iliita niakzani labda ni Joyce na nilipoiangalia nilimkuta ni Msouth. Sikutaka kuipokea nikaiacha iite mpaka ikate yenyewe.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nikajiuliza kwani amepatwa na nini usiku huo mpaka…
  • MY DIARY (20)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINITULIPOISHIA...Nikamwambia kuhusu namba zangu za simu amuombe aliyemtuma anisaidie na kuhusu hilo la pili je hatuwezi kufanya kesho kwa sababu kuna mahali nilikuwa nikienda? Alifikiria kwa sekunde kadhaa na kuniambia kuwa hapana anaomba nimsaidie leo kama yeye alivyonisaidia mimi kwa sababu ningekuwa kwenye foleni nisingeweza kuondoka kirahisi hivyo kama ninavyofikiria.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (19)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMI NA TISATULIPOISHIA...Baada ya hapo niliendelea kumdadisi juu ya tukio lile lakini hakuwa tayari kufunguka zaidi ya kusema aliumia sana. Hapo nikaamua kuutafuta ukweli kwa kutumia mbinu za kike.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilimwekaa mikono begani na kumwambia pleaee dear naomba uniambie ukweli ili nijue nakusaidiaje? Basi Ramadhani akaanza kulalamika kuwa baba yake amekuwa akimwingilia…
  • MY DIARY (18)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMI NA NANETULIPOISHIA...Halafu eti akawasha simu na kuonesha zile picha alizotupiga kweli huyu rafiki yangu alikuwa hamnazo sio picha tu alituchukua video kabisa na sauti. Akanambia ngoja ampigie paparazi mmoja hivi aje ili atengeneze habari tupate hela. Kauli hiyo ilinikosesha amani na kunikera sana akanmabia eti kuna namna ya kufanya ili sura yangu isitokee.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…

MTAA WA TATU (59)

Mwandishi: Hafidhi J Ikram

SEHEMU YA HAMSINI NA TISA
Kesho yake yapata saa nne Asubuhi ndani ya uwanja wa ndege maeneo ya Kipawa tunamuona Hafidhi akiwa na wake zake
ijapokuwa bibiye Mariam alikuwa akijificha mara kwa mara

Ondoa hofu bibiye kila kitu kipo sawa,’’

NIOMBE SAPOTI, BONYEZA TANGAZO LINALOKUJA NA KUJAA KWENYE SIMU YAKO WAKATI UKIFUNGUA SIMULIZI AU LILE LINALOKUWA KATIKATI YA SIMULIZI ZETUKABLA HAUJAIFUNGUA NDANI, PIA KUNA LILE LINAKUJA NA KUNG'ANG'ANIA HAPO CHINI, BONYEZA WALAU MARA 3-4 HIVI HIYO NDIO SAPOTI YAKO KWANGU, TAFADHALI NIPE NGUVU NAKUTEGEMEA SANA MSOMAJI WANGU
SASA ENDELEA...
Hafidhi akajitahidi kumwambia bibiye Mariam asiwe na wasiwasi, baada kukamilisha taratibu zote hatimae Vivian akiwa kambeba mwanae na Mariam nae akiwa kambeba mtoto wake wakafanikiwa kuingia ndani ya ndege Hafidhi akabaki kuwaangalia tu na kuwapungia mkono wa kwaheli, nao wakampungia kila mmoja akitabasamu ndege ikaanza kuondoka na kuiacha aridhi ya Tanzania mwanaume akageuka na kusema sasa kazi moja tu kama familia yangu imeweza kuondoka wacha nikamilishe kazi kabla sijapotea katika dunia hii. Hafidhi aliongea hivyo huku akiondoka maeneo ya uwanja wa ndege lakini ghafla damu zikaanza kumtoka mdomoni na puani damu yake ilikuwa si yakawaida yani nyeusii utasema oil chafu, binafsi hakupenda kuonekana akakitoa kitambaa chake na kujiziba kuanzia puani hadi mdomoni kwa mwendo wa haraka akatoweka maeneo hayo. Siku baada siku hali ya Hafidhi ikazidi kuwa mbaya isijulikane tatizo ni kitu gani akawa ni mtu wa kushinda ndani amelala tu kwenye kijumba chake cha udongo.

“Hafidhi kijana wangu kwanza pole sana tambuwa kitu kimoja muda wako wa kuwepo hapa duniani umeshakwisha karibu kuzimu kwa maisha mengine mapya,’’ ilikuwa kauli kutoka kwa Ibnuwasi ambaye ndio baba yake upande wa majini. “baba mbona imekuwa mapema sana kwamie kuondoka kazi yangu bado sijaimaliza kingine nina watoto wadogo tu wataishi vipi bila mimi, nipeni muda niweze kucheza na wanangu nifurahi nao.’’ “sawa kijana tumeweza kukupa siku chache tu kuweza kukamilisha hiko ulichokiomba ikamilishe hiyo kazi haraka sana sisi tunakungojea kuzimu,’’ Ibnuwasi akapotea Ghafla mwanaume akaanza kujisikia yuko vyema, akainuka na kutoka nnje na kujisemea leo nitawafyeka wote kasha akapotea Siku hiyo ndani ya jumba moja hivi yalikuwa ndio makutano ya vingunge wote wenye kufanya mambo ya kishenzi katika nchi hii na nchi za jilani “sasa ndugu zanguni kwa mara nyingine tena tumeweza kukutania hapa kama ilivyo kawaida yetu kukutana kwetu basi ujuwe kuna jambo sasa basi tusitake kupoteza muda kwanza kabisa kila mmoja anatambuwa ndani ya dunia hii tuna adui mmoja tu na adui mwenyewe si mwingine ni kijana Hafidhi j Ikram tumefanya kila njia kila namna tuweze kumnyamazisha imeshindikana kila kukicha anazidi kutupukutisha sasa basi ghafla kuna kitu kilirushwa na kukita kwenye shingo yake akarushwa hewani alipotua chini yupo kimyaa damu tuu zinamtoka kwa wingi utasema kuku kishingo kachinjwa kila mtu akadata na kujiandaa kukimbia wakaangaza macho huku na kule kutaka kumuona huyo aliyekirusha kile kisu, si wakamuona Ninja short akiwa kasimama mlangoni huku kichwa kainamisha chini wote wakashtuka

Kila mmoja akabaki kushikwa na kitete vijasho vilianza kuwavuja kibaya zaidi Michael hakuwepo maana ndio mtu pekee atakayeweza kupambana na kiumbe hicho japo wanakumbuka vyema kule uwanja wa taifa nini kilitokea juu ya Michael. Walinzi wakaanza kumfata hakika ilikuwa ni sawa na kujiingiza mwenyewe kwenye tanuri la moto kitendo cha kumkalibia tu mwanaume akawa akicheza na shingo zao kwa kuwapitishia jambia na kufanya damu ziruke huku na kule hakika chumba kikawa ni kama bwawa la damu ndani ya dakika tano kila kitu kilikuwa kimekwisha kabaki mtu mmoja tu si mwingine ni Mzee Khatibu alikuwa kajikunyata akitetemeka utasema yule adui kubwa wa kihindi sema kwasasa hivi ni marehemu sijui anaitwa Amrish poor ni adui mwenye roho mbaya sema akidakwa na stering anakuwa mdogo kama vile kidonge cha pilitoni ndivyo ilivyokuwa kwa mzee Khatibu kifo kipo mbele yake atafanya nini tena zaidi akabaki kulia tu, baada Hafidhi kufanya mauwaji yale akapotea zake pasipo kufanya jambo lolote mzee Khatibu sijui kwanini labda atatuambia sababu ya kufanya hivyo wakati alikuwa na uwezo wa kummaliza. Binafsi mzee Khatibu hakuweza kuamini kama ameachwa hai kwa mara nyingine, akabaki palepale amejikunyata akiwa haamini kabisa akijuwa Hafidhi anaweza kumrudia kwa wakati ule. “hivi ni kweli nimeachwa mzima akaitoa simu yake na kumpigia Michael, “hallooo kijana, uko wapi wewe huku mambo yamekuwa sio mambo hivi ninavyoongea na wewe baba yako hatunae tena,’’ mzee Khatibu aliongea kwa pupa huku machozi yakimtoka. Hakika kijana Michael ndio akachanganyikiwa zaidi. Akaingia ndani ya gari yake aina ya suzuki njia nzima alikuwa analia na kuupigapiga usukani Hafidhi baada kupotea ndani ya mjengo ule safari yake ikampeleka mpaka kituo cha televisheni cha ITV kilichopo maeneo ya Mwenge hakika mwanaume alikuwa mnyonge sana hakuwa na uchangamfu wowote baada kufanya taratibu fulani hivi akaambiwa asubili kama masaa matatu nae hakuwa na kinyongo maana anafahamu fika siku zote vipindi vinaenda kwa muda tena vizuri zaidi kaambiwa angojee masaa matatu wakati wengine wanapewa wiki au siku. Baada kuvuta subira kwa muda kidogo kipindi chake kikawadia akaingia ndani na kukaa kwenye kiti huku camera kubwa ya kituo hiko ikiwa mbele yake. “sasa unaweza ukaanza kila kitu kipo sawa,’’ akaambiwa hivyo na mfanyakazi wa kituo hicho Mwanaume akakohoa kidogo na kuanza kusema.

(Maisha ni mzunguko siku zote siri ya mtu itabaki moyoni mwake usimuone mtu anacheka na kufurahi na wewe kumbe ndani ya moyo wake anakuwazia ndivyo sivyo leo hii nahitaji niuweke wazi ulimwengu kwa kutaja mabaya yote ya Vingunge wa nchi hii nchi ambayo wengi wanaiita nchi masikini. Kumbe sivyo wanavyo fikilia wao, unaweza ukajiuliza kwanini yule kawa jambazi au changudoa naweza kusema wapo watu ambao wameingia kwenye kazi hizo kwa kupenda wao wenyewe au kulazimishwa na watu fulani au mtu fulani. Muda mwingine unakuta wananchi wamemkamata mwizi pasipo kutaka kumuuliza sababu ya kuiba au kaiba nini wanampiga na kufikia hatua ya kumtia moto usikute kaiba chupa ya chai tu au kijiko. Binafs inatia uchungu sana hii kuona jinsi gani binadamu mwenzako akiuwawa kinyama namna hiyo ngoja niwaulize swali nyie Wananchi wakati mamillion ya pesa yakichotwa Richmond mlikuwa wapi? na kule Tegeta esco mlikuwa wapi? sijui kontena zimepotea bandalini mlikuwa wapi? Hamna majibu ya kunipa zaidi ya upimbi tu endeleeni kuuwana nyinyi kwa kwa nyinyi mkijiona wajanja kumbe wenye kukwapua kodi zenu wanazidi kuvimbisha vitambi. Sio kama wezi hamuwajui mnawajuwa sana tatizo ndani ya mioyo yenu mmejawa na uwoga kazi kuwaonea wanyonge. Au ndio mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, wakati Hafidhi akiongea maneno hayo kwenye kipindi kisichokuwa rasmi lakini ni kipindi ambacho kiliwafanya watu wengi wawe makini katika kufatilia kwa kumsikiliza kwakuwa ilikuwa ni siku ya wikiend yani jumapili wengi wawatu walikuwa majumbani mwao na kuweza kuangalia kipindi hiko hata wale wasiokuwa na wikiend walijazana kwenye viosk na mahoteli kuangalia taarifa hiyo kwenye baa napo kulifurika watu, wengi wakabaki kujiuliza maswali pasipo kupata majibu huyu kijana ni nani mbona anaongea maneno mazito namna hii si atasababisha kituo cha ITV kifungiwe maana nchi yetu hainaga jambo dogo,

“Msitake kujiuliza sana mimi ni nani mnaweza kuniita gaidi kutokana na hizi ndevu zangu kama wenye akili finyu mlivyoweza kukalili wenye kufuga ndevu na kuvaa kanzu na barakashia ni magaidi sio mbaya mkiniita hivyo mimi ndio Hafidhi j Ikram natokea Mtaa wa Tatu,’’ kitendo cha kulitaja jina lake tu wafanyakazi wakituo cha ITV wakaanza kushikwa na kitete maana wanafahamu fika huyo mtu si wamchezo kila mmoja akatoka nnje ya kituo wakimuacha yeye mwenyewe ndani akizidi kuongea kwanini niliuwa leo ndio nahitaji kuweka kila kitu wazi wakati nazaliwa mpaka kufikia hatua ya kujitambua sikuwai kufikilia kama nitakuja kuwa muuwaji. Leo hii Hafidhi mimi nimeuwa watu wengi sana, sijui nitaenda kujibu nini kwa Mungu baba kwa mara yakwanza nilimuuwa askari mmoja kwa bahati mbaya naweza kusema hivyo sababu nilikuwa katika hatua za kujitetea tu baada yeye kutaka kunipiga na fimbo yake nikafanya kumpushi ndipo akadondoka na kujibamiza kwenye nondo ya sero. Nilishtushwa sana kwa tukio lile nikaona sina jinsi ni kutoroka kwenye kituo cha polisi ili nisiweze kushitakiwa kwa mashitaka yale. Kuanzia hapo nikaja kukutana na msichana ambaye naweza kusema kwa namna moja au nyingine yeye ndio sababu ya mimi kutenda yote haya niliweza kupata document za siri nzito sana kuhusu watu kujitajilisha kupitia watoto yatima yani wanajifanya kusaidia na kuomba watoto wawili watatu waweze kwenda kuwalea kumbe sivyo wanachofanya wao ni kuwauwa kwa kuwatoa mioyo yao na kwenda kuiuza nnje ya nchi hakika niliumia sana nikajiuliza thamani ya watoto hawa iko wapi kutowa kwako sabuni au sukari ndio unajilipa kwa kuutoa moyo figo damu ya kiumbe kisichokuwa na hatia yoyote kisa upate pesa uwe tajili. Watoto wengine mnawachuna ngozi serikali iko wapi. Usiulize hivyo wakati serikali yenyewe inawalinda watu hawa laiti kama wangekuwa hawalindwi tungewatia moto kama tufanyavyo kwa mwizi wa jiko la mchina. Hakika risti ilikuwa ndefu sana mpaka mke wa muheshimiwa Rais alikuwepo naongea yote haya nikiwa na udhibitisho kamili kila kitu nimekuja kukikabidhisha leo nipo tayari kukamatwa mnifunge au mninyonge yote ni kheri kwangu ila nawaomba muweze kuyafanyia kazi yale yote niliowaeleza kuna vingunge sikutaka kuwauwa nimewaacha hai sheria ifuate mkondo wake. Habiba kazi uliyonipa nimeweza kuikamilisha. Wakati akizidi kuongea na kutoa siri nzito ambazo zilikuwa zimejificha nyuma ya panzia huku nnje polisi wasiokuwa na idadi waliweza kufika wakiwa na kikosi kizima cha FBI hawakutaka papala maana walifahamu kama watamuingilia kwa vurugu inaweza kuwaletea shida jamaa akagairisha kukamatwa na kusepa zake wakatulia nnje amalize kuongea na kutoka nnje kwa hiyali yake mwenyewe. Hafidhi aliongea maneno mengi sana yenye kuhuzunisha na kusikitisha wengi wawananchi walishindwa kujizuia na kuanza kulia hakika kuna kusamehe saba mara sabini lakini si kwa ushetani walioufanya watu hawa, kisha akasema kisa cha muheshimiwa Raisi kuuwawa na Undercover agent hapo sasa vilio vikazidi kuongezeka baadhi ya polisi walivua kofia zao na kujifuta machozi zikapita dakika kama ishillini na tano hivi wakimngojea ndipo akaweza kutoka ndani ya kituo hicho akiwa kaweka mikono yake mbele ishara yakwamba yupo tayari kukamatwa wamfunge pingu tu. Bibiye Mona ndio akaja kumfunga pingu ajabu wananchi walikuwepo maeneo hayo wakapinga vikali kitendo cha kukamatwa Hafidhi sio sahihi kabisa ikabidi polisi watumie mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi.

NAOMBA SAPOTI, KUNA MATANGAZO(ADS) YANAJITOKEZA KWENYE APP YETU, LIMOJA LINAJAA KWENYE KIOO CHAKO JINGINE LINANG'ANG'ANIA HAPO CHINI KABISA, BONYEZA JAPO MARA 2 AU 3 KILA UKIFUNGUA SIMULIZI HIYO ITANIPA NGUVU YA KUENDELEA ZAIDI NA SIMULIZI ZETU🙏🙏

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO



USIKOSE SEHEMU YA SITINI

Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
10 Mtaa wa Tatu Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni