AISEE KUMBE RAHA (12)
Zephiline F Ezekiel
7 min read
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
Nikajikuta nikipandwa na hasira za ghafla kwa catherini ambaye maneno yale nilikuwa na uhakika mkubwa kuwa ndie yeye ndio atakuwa amemwambia chiku habari zile. Nikajikuta nikinywea na kubaki nikiwaangalia chiku na yule jamaa na palepale nikajikuta nikiingia katika dimbwi zito la mawazo ya ghafla na kusahau kabisa kilichonileta.SASA ENDELEA...
"Wee msenge hebu ondoka kabisa maana umetuharibia starehe zetu kabisa."ghafla yule jamaa aliyekuwa na chiku ambaye naye mara ya kwanza alitulia kimya baada ya kugundua kama alikuwa amefumania akaniambia maneno yale ambayo yalikatisha mawazo yangu ya ghafla na kuibua hasira zangu na kujikuta nikimuangalia kwa hasira kali."Unasemaje wewe.??"mwanaume nikamuuliza kama vile sikusikia vile nilichoambia na safari ile nilikuwa kishari kabisa.yule jamaa akanyanyuka na kuvaa boxer yake iliyokuwa chini maana baada ya kuona mimi nimeingia alijiziba na shuka kisha kwa haraka akanisogelea na bila ya kuuliza swali akanitandika kofi zito ambalo lilisababisha nione nyota kutokana na uzito wa kofi hilo nakujikuta mpaka nikaguna kidogo nakushikilia shavu langu huku nikiwa na hasira.
"Umeona umenipiga.??"
"Fala kweli sasa unamuua nini?? Umetuingilia katika starehe zetu bado unajifanya unajua sana kuongea pumbavu wewe."yule jamaa akaniambia kwa kujiamini na mimi Hasira ndio sasa zilikuwa zimeshapamba moto bila ya kumtaarifu nikajikuta nikirusha konde zito ambalo lilienda moja kwa moja katika uso wake na kusababisha jamaa apepesuke mpaka kukivamia kitanda kile na mimi nilipoona hali ile nikamsogelea haraka nikiwa na lengo la kumkandamiza tena.lakini hali ikawa tofauti kabisa kuliko nilivyotegemea kabla hata sijamfika kwanza chiku akaanza kupiga kelele.
"Tumevamiiwaaa tumevamiaaaaa"ndio maneno aliyokuwa akiyaongea maneno ambayo kwa wakati huo sikuyasikiliza nilikuwa na hasira na yule jamaa ambaye kabla hata sijamfikia karibu ili nimkandamize makonde mengine yule jamaa akanyanyuka kiufundi nakunipiga mtama mkali ambao ulinipeleleka moja kwa moja mpaka chini na nilipojaribu kunyanyuka jamaa akaniwai kwa kunikalia juu akiwa na lengo la kunikandamiza ngumi lakini hali hiyo sikuiruhusu mwanaume nikatumia ujuzi wangu nakujikuta nikimbunia na mimi nikamkalia juu nakuanza kumshindilia ngumi ambazo nilimpiga tatu na nilipotaka kumpiga ya nne nikashikia kitu kizito kikitua katika kichwa changu nakujikuta nikiachia ukelele na kumtaja mama kisha nikaruka pembeni nakuanza kugalagala huku nikiwa na shika kichwa changu.
"Khaaaa kumbe chaliiii unafanya nini sasa khaaaa"alikuwa si mwingine bali ni yule jamaa ambaye alikuwa mapokezi katika ile gesti ndiye aliyenipiga fimbo ile kichwani.
"Huyu nashangaa ametuvamiaa tuu kwanza amevunja mlango nakuanza kutuvamia hapa kwanza na huyu ni mwizi."Bila ya kutegemea chiku akaanza kumwambia yule jamaa wa mapokezi ambaye alikuwa ameshika fimbo huku akiwa na Majamaa wengine kama watano ambao walikuwa wameshika silaha mikononi mwao wakiwa na shauku kubwa ya kunishangalia.
"Heee hebu chalii simama."bila ya kuchelewa mwanaume nikasimama baada ya kuambia na yule jamaa wa mapokezi na sikuwa na la kupinga nikanyanyuka huku mikono yangu ikiwa ni kichwani ambapo ilikuwa ni sehemu niliyopigwa fimbo na yule jamaa wa mapokezi.
"Nambie chalii umefata nini huku sasa wakati wewe umechukua chumba kingine??"
"Hamna sikia nikwambie chalii unajua huyu msichana mimi demu wangu sasa nimemfumania hap...."
"Weee muongo huyu nani demu wako wee huyu mwizi mimi simjui huyu."yalikuwa ni maneno ya chiku baada ya kusema Kuwa mimi sio demu wake nakusababisha nipadwd na hasira zingine za ghafla nakujikuta nikitaka kumvamia lakini yule jamaa wa mapokezi mwenye lafudhi ya kichaga akanizuia na kusababisha wale wengine watake kunivamia lakini yule jamaa wa mapokezi akawavuia.
"Chaliii wewe tusiongee naye sana la msingi tumepeleke polisi tu kwanza kituo si hapo sio mbali."yalikuwa ni maneno ya jamaa mmoja kati ya yale watano ambao walikuwa na mapanga mikononi.
"Kweli machalii wangu haya chalii twende kituoni."
"Aaaaaa jamani kituoni tena basi tuyamalize hapa hapa."mwanaume baada ya kusikia wale majamaa wanataka kunipeleka kituoni nikajikuta nikinywea ghafla nakuwaangalia wale majamaa kwa jicho la huruma........
"Oyaa chaliii nyanyuka basi twende."yule jamaa wa mapokezi akaendelea kuongezea na kuniambia ninyanyuke niende kituo cha polisi na kusababisha mwanaume nizidi kuoga nakuanza kulia lia.
"Jamani sisi sote wanaume yatupasa tuelewene eee hebu nambie chalii kiasi gani nikupe fasta"mwanaume niliendelea kujitetea mbele ya wale majamaa ambao mikononi mwao kulisheheni mapanga huku yule jamaa wa mapokezi ambaye alikuwa akifahamika kwa jina la chalii akiwa ameshika fimbo ndefu ya kimasai ambayo aliitumia vyema kuniponda kichwani pale nilipokua napigana na yule jamaa aliyekuwa akifanya mapenzi na chiku.
"Nyie mnasubiri nini mpelekeni polisi"hakika chiku alinishangaza kwa kiasi kikubwa kwa sababu alionekana kunichukia sana kwa muda mfupi wakati alikuwa apindui kwangu.kama ujuavyo mtoto wa kike akisimamia lake sikuwa na ujanja wale majamaa wengine watano hawakuwa na sababu ya kusubiri wakaninyanyua msobe msobe na kuanza kutoka katika kile chumba.
"Jamani nisameheni mimi kwa usumbufu ambao umejitokeza basi nawaombeni muhamie chumba cha pili muendelee na starehe zenu."yule chalii akawaambia chiku na yule jamaa ambao hawakuwa na kusema zaidi ya kutimiza kile kizuri walichoambia.Mwanaume nikapaki kimya huku machozi yakinilenga lenga hakika sikuwa na budi zaidi ya kuwaachia wale majamaa watano wakiongozwa na yule mwenye gesti ambaye alijulikana kama chalii kunikwida kiunoni nakunipeleka kituoni.
"Oya chalii yangu eee washikaji eeee mimi nitawapa mitonyo ya kutosha naombeni tu mniachie yani kituoni jau wale."mwanaume niliendelea kujitetea usikike bana kituo cha polisi kituo cha polisi tu lakini bila hata ya kunisaidia kiume wale majamaa wakafanya kweli hakuna aliyenijibu zaidi ya kuendelea kunipeleka puta kama nilikuwa nimeiba vile.safari yetu ikawadia nikaingizwa mpaka kituoni huku wakiwa bado wamenikwida kiunoni kama nilikuwa mwizi kweli vile.
"Haloo limefanya nini hilo lijizi nini??"ile tunafika tu tukakaribisha na sauti ya askari ambaye alionesha alikuwa akitaka kujua ilikuaje mimi kupelekwa pale.
"Afande huyu ni mfanyafujo na mwizi maana amevamia watu gesti wakiwa wanakula raha zao"jamaa kati ya wale watano akawa wakanza kujibu kama vile alikuwa mwenye gesti na kusababisha mwanaume nimkate chijo kali la hasira kwa sababu ndio huyo huyo ambaye alitoa ushauri wa mimi kupelekwa katika kituo cha polisi.
"Anhaa kumbe liahalifu eeew kamanda marungu kuna livamiaji hapo njoo kwanza ulitengeneze"bila ya kutegemea baada ya yule jamaa kumuambia polisi aliyekuwepo pale mapokezi tukio nililofanya bila ya kutegemea akamuita askari mwenzake ambaye alikuwepo katika chumba fulani na aliposikia anaitwa haraka akatoka mkononi mwake akiwa ameshika kirungu kile ambacho wanakuaga navyo maaskari.yule askari aliyeitwa akajitokeza na kumuangalia askari wa mapokezi ambaye hakusema kitu zaidi ya kuninyooshea mimi kidole kisha yule afande aliyeitwa akatikisa kichwa chake kuelewa kiukakamavu yule jamaa akanisogelea mimi kisha baada ya kunikaribia akawaambia wale majamaa walionishika waniachie.
"Sikia afande nikwambie eee mimi hawa wamenisingizia mimi sio mwizi mimi nilienda kumfumania de......"kabla hata sijamaliza kuongea nilichotaka kukiongea nikiwa na lengo la kujitetea huku nikiongea kwa hali ya kutetemeka ghafla bila ya kutegemea yule afande akanipiga mtama mkali ambao hakika sikuwai kupigwa duniani mtama ule ulisababisha nidondoke mzima mzima na kudondokea mbavu.
"Mamaaaaaaaa mbavu zangu iiii"nikajikuta nikiachia ukelele wa nguvu ambao ulisababishwa na maumivu makali ambayo hakika sikuwa kuyapata lakini cha kushangaza baada ya kupigwa mtama wale majamaa wakaanza kunicheka lakini vicheko vyao vikanyamazishwa na yule afande aliyenichota mtama.Niliendelea kulalamika kwa kupiga mayowe huku nikishikilia mbavu zangu ambazo hakika niliziona kama zimetoka kutokana na jinsi zilivyokuwa zinauma lakini makelele yangu nayo yalinyamazisha baada ya kutandikwa rungu kali la mgongo ikifuatia na sauti uliyosikika masikioni mwangu ikisema KIMYA.sikuwa na budi ya kuendelea tena kuugulia kwa kutoa sauti nikabaki kimya huku machozi yakinibubujika.
"Haya Afande Marungu muingize huyo livamizi katika chumba cha selo huku nikiwa namuandikia hapa na kuwaandikia na hawa"yule afande aliyekuwepo pale mapokezi akamwambia yule afande marungu kisha yule afande akaniambia nivue viatu na mkanda kisha nimpe hakika sikuwa na ujanya nikafanya kama nilivyoelekezwa kiunyonge kisha yule afande hakuishia hapo akaanza kunisachi mfukoni lakini akajikuta akiganda kidogo jambo ambalo lilinishangaza na kujikuta nikimshangaa.hapo ndipo taa yangu ya kufikiria ikawaka aliganda kidogo kwa kuwa yule afande aliziona zile pesa nilizokuwa nazo lakini jambo ambalo nilifurahi kuwa wala hakuzichukua akaniachia niingie selo huku nikiwa na simu na zile pesa.Hakika ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kuingia selo ambapo sio siri chumba kilikuwa ni giza tupu hewa ndogo na asikuambie mtu mbu ndio walikuwa wamejamaa kama nini.niliingizwa ndani ya selo mule kisha mlango ukafungwa na hakika sikuwakutegemea na nikamkuta na jamaa mmoja aliyeonekana kama mvuta unga vile ambaye naye baada ya kuniona akanisalimia na mimi nikaitika.Haikufika hata lisaa nikiwa ndani ya chumba kile cha selo yule afande ajulikanaye kwa jina la marungu akaja pale kwenye selo kisha akaniita na mimi sikuwa na budi nikanyanyuka na kwenda kumsogelea na kumsikiliza.
"Haya janja umejipangaje au unataka mpaka twende mahakamani kwa kesi hii"afande marungu akaniambia kwa sauti ndogo ya chinichini ambayo ilisikika vizuri katika tundu za masikio yangu na kusababisha nitake kutoa tabasamu lakini nikashindwa.
"Anhaa kweli kwani unataka bei gani afande."
"Aaaa kwa wewe hebu nipe elfu hamsini nigawane na mwenzangu elfu ishirini na tano elfu ishirini na tano"hakika kama ujuavyo pesa ndio kila kitu nikazama mfukoni na kuchukua zile pesa alizonipa mama chiku ambazo zilikuwa kama elfu siti na tano nikachukua elfu hamsini nikampa yule afande marungu ambaye
Alizopokea kwa furaha sana nakuanza kunipongeza eti nakusahau kama alinishushia kipondo bila ya hiyana akanifungulia mlango wa selo na mimi nikatoka kisha wakanikabidhi simu yangu na viatu vyangu na mimi sikuwa na muda wa kusubiri haraka nikatoka katika kituo kile cha polisi kisha haraka haraka nikachukua bajaj kuelekea nyumbani huku nikiwa ndani ya bajaj mawazo mengi yakanijia.
"Aisee yulee catherini leo hii kwanza facebook itamjua"nilijikuta nikijisemea mwenyewe ndani ya ile bajaj mpaka kusabababisha hadi yule mwenye bajaj kuniangalia.
"Vipi kaka kuna tatizo??"yule mwenye bajaj akaniuliza kwa mshangao baada ya kuona hali ile.
"Hayakuhusu endesha bajaj hiyo."nikajikuta nikimjibu kwa hasira baada ya kuniuliza swali lile ambalo sikulipenda na nikabaki nikiwa naendelea kuwaza na kuwazua huku nikiwa nashangaa maisha yangu yalivyokuwa na mikosi mikosi katika kipindi kile.kwa mwendo wa kama masaa mawili nikafanikiwa kufika nyumbani ambapo ilikuwa ni kama saa tatu au nne usiku mwanaume nikaingia ndani na kumkuta anaangalia tv nikamsalimia kisha haraka nikaingia katika chumba changu na moja kwa moja nikaenda mpaka ilipokuwa laptop yangu ambayo ilikuwa na zile picha za catherini akiwa uchi picha ambazo nilimpiga mimi.nikazingua zile picha na kuziangalia kwa uchu mkubwa huku hasira zikizidi kunipanda kila dakika nilivyokuwa naziangalia zile picha ambazo kwa muda huo hakika hazikunisisimua kimapenzi bali zilinisimumua na kunipandisha hasira kali ambazo sikuzitegemea.Hakika catherini ndio amesababisha mpaka chiku nimpoteze kutokana na kumuambia ukweli.
"Huyu mwanamke namchukia sana na Leo usikuu huu Facebook nzima itamjua na instagram"nikajisemea maneno yale kwa nguvu kama nimechanganyika na bila ya kupoteza muda........
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO


USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA TATU
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni