Notifications
  • MY DIARY (45)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA TANOTULIPOISHIA...Ndio niliona hipo haja ya kuokoka na kuishi maisha ya utakatifu kwa maana nishaishi maisha yote ya kuwa mbali na mungu. Nakumbuka nilipokuwa mdogo kipindi hicho naujua mlango wa kanisani tuisahawahi kufundishwa kuwa mtetezi wa kweli wa maisha ya mwanadamu ni Mungu.Na siku zote alaaniwe mtu yule amtegemeaye mwanadamu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Sio kazi ya…
  • MY DIARY (44)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA NNETULIPOISHIA...Yani alianza kutaka uhusiano na mimi tena uhusinao wa mapenzi.Mda wote alikuwa akiniganda kama luba.Na mimi nilikuwa mjanja sana maana nilijifanya sinywi pombe wala kuvuta sigara.Pia baada ya kugundua kuwa wahusika wengine walikuwa wanajiachia niliamua kujifanya mshauri wa mapenzi na mahusiano.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilikuwa nawasshauri sana mshiriki wa…
  • MY DIARY (43)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA TATUTULIPOISHIA...Wakati nabadilisha staili kwa kukichua kile kifaa na kukiweka vizuri huku nikibinya ile switch hili iongeze spidi Mark aliingia. Ni kweli nilimuona ila sasa sikuwa na jinsi ilibidi nimalizie furaha hiyo ya uwongo uwongo. Yaani wazungu jamani sijui walifikiria nini maana kile kifaa ukikiminya kwa juu kinakuwa kinajizungusha chenyewe.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (42)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA MBILITULIPOISHIA...Uzalendo ulinishinda ikabidi nimuulize ni kwanini bado wanatumia njia hiyo ya kizamani kutunza kumbukumbu wakati siku hizi kuna kitu kinachoitwa Human Resource Informaion system ambapo kumbukumbu zote za wafanyakazi kama waliochishwa kazi, wagonjwa, walioenda likizo ,waliopandishwa vyeo na taarifa nyingine muhimu uhifadhiwa kwa kutumia komputa.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (41)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA MOJATULIPOISHIA...Mark anashangaazwa sana na mwanamke huyo lakini kwa kuwa shida yake ilikuwa ni hela anaamua kuachana nae na kuanza maisha mapya hapo jijiini Dar es salaamMaisha yanaendela lakini Mark amekuwa tajiri na mtu mwenye mafanikio sana kiuchumi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Pamoja na mafanikio hayo ni mtu ambaye mapenzi bado yalikuwa yakimuumiza siku hadi siku.Filamu…
  • MY DIARY (40)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINITULIPOISHIA...Alikuwa akinyata kwa kweli. Kweli hata mimi nilimkubali tu siku ya kwanza ingawa bado nilikuwa sijajua ufanisi wake wa kazi.Nilikaa nae hapo kwangu kwa mda wa siki tatu huku asubuhi tukiamka na kuendelea na kazi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Ndani ya mda huo nikagundua kuwa alikuwa na uzorfu mkubwasana hivyo kazi hiyo alikuwa akiimudu kabisa.Hapo sasa nilimkubali sana…
  • MY DIARY (39)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TISATULIPOISHIA...Nilikuwa na furaha sana huku nikiamini kuwa ndoto zangu za kuja kuwa mtu maarufu zinaweza kufanikiwa hata kabla ya kuyapata yale madini. Sikutaka mbwembwe niliamua kuikopi na kuipesti hiyo stori kama ilivyo na kuifowadi kwa Mark.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Baada ya kama lisaa hivi Mark alipiga na kuniuliza kama kweli ilikuwa nai mimi nimetunga hiyo…
  • MY DIARY (38)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA NANETULIPOISHIA...Usiku nilishituka usingizini baada ya mbu kuning’aata na kunisumbua sana. Niliwachukia sana hao mbu kwa sababu walinikatisha ndoto yangu ambayo nilikuwa nikiota.Ndoto ilikuwa ikielezea jinsi harusi yangu na Mark itakavyokuwa. Ndoto ilikuwa tamu sana maana ilinipa taswira ya picha halisi ya maisha yangu ya mbeleni.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilishusha neti…
  • MY DIARY (37)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA SABATULIPOISHIA...Hapo alitulia tulii kama mtu aliyeaamia dunia ingine. Kimoyo moyo nikawa najisemeha kama amehamia dunia ingine na kuanza kuwaza ujinga sahuri yake mimi nipo kazini bwana acha nitafute hela. Ndio ni lazima nifanye kazi kwa utaalamu na utundu wa hali ya juu ili waendelee kusimuliana huko mjini ili niendelee kupata hela.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Wewe…
  • MY DIARY (36)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA SITATULIPOISHIA...Sasa wewe fikiria mimi niliyeletewa zawadi sikujua ni zawadi gani lakini yeye tayari alishafungua na kuchungulia na kujua nini kilifungwa huko ndani.Basi nikaendelea kumuhudumia yule mama huku na yeye akiniambia kuwa itabidi nikimmaliza hizo zawadi tusifungue hapo hapo na waniimbie wimbo wa happybirthday.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Tuliendelea na stori mbili…

AISEE KUMBE RAHA (19)

Mwandishi: Pablo

SEHEMU YA KUMI NA TISA
Maneno ya Baba yaliniacha nikiwa sina cha kusema nikajikuta nikibaki Namuangalia baba huku nikiwa siamini kama nimeweza kuwaelewesha baba na Mama bila ya kutumia Nguvu nyingi bila ya wao kunikazia sana.Na hakika sikuwa na La kuongea baada ya baba kuniambia nikaanze maisha mapya morogoro kwa sababu ya ile soo ya mimi kupigwa picha..............

SASA ENDELEA...
Harakati na safari ya mimi kuamia morogoro ikaanza haraka na sasa ile ile baba akaanza kuwasiliana na watu anaowajua ili wanatafutie Chumba cha kuishi katika madhari mazuri ambayo chumba kitakuwa karibu sana na Chumbani.Hakika yale yote yalioendelea sikuyategemea kabisa kwamba ingekuwa haraka haraka kiasi kile ambacho wala sikutegemea lengo la mimi kuamia morogoro haraka ni kuondoa hali ile ya mimi kudharirika katika jamii baada ya picha zangu kuwa zinazidi kusambazwa katika jamii picha ambacho mimi nilikuwa mtupu kabisa na kutangazwa kuwa mimi ni shoga na hata katika picha zangu nilizokuwa naziangalia picha ambazo zilikuwa zimeeditiwa huku zikiambatana na namba yangu ya simu.Hakika hata nilipoweka laini yangu katika simu mpya ambayo alininunulia baba bado messeji za watu na simu ziliendelea kumiminika ambapo watu wengi ambao kwa hakika walikuwa wamelaaniwa walikuwa wakinitumia messeji za mapenzi kuwa wananitaka na hata nilipojaribu kupokea baadhi ya simu habari ilikuwa ile ile hali ambayo ilipelekea mpaka hasira zinipande na kujikuta nikiitafuna ile laini kama pipi ya kifua.Hakika katika maisha yangu nikajikuta nikiweka bifu na suzan na kuapia kabisa kama nitakuja kuonana tena na suzan au chiku au catherini basi lazima ningewafanyia kitu kibaya ambacho kwa hakika hawatoamini katika maisha yao.Safari ya morogoro ikawadia kabisa na ilikuwa keshokutwa yake ambapo siku ya pili baba alienda Mjini kuninunulia vitu vya muhimu kama nguo mbalimbali ambazo zitaweza kunisogeza sogeza karibia hata miezi miwili au mitatu na kama nitazoea huko morogoro basi nitaweza kujitafutie nguo kali mwenyewe.Hata mama naye aliridhia mimi kuondoka licha ya yeye kunionea huruma na kujikuta mara nyingi akaniangalia kwa huruma na mara nyingi katika hiyo siku moja kila alipopata nafasi basi alikuja kukaa na Mimi na kunifariji.

"Mwanangu matatizo yamewekwa kwa ajili yetu sisi binaadamu kwa hiyo wala usijisikie vibaya mambo haya madogo tu sisi tunakupenda sana mwanetu ndio maana hata uliposema kuwa zile picha ulipigwa tukakuamini kwa sababu wewe mara nyingi umekuwa mkweli kwetu.basi mwanangu wewe sasa hizi mkubwa miaka 22 unaingia sasa kwanza punguza umalaya na achana nayo kumbuka huko morogoro kuna mambo mambo ya kiswahili sasa shauri yako ukienda huko na kuleta Mambo ya mapenzi mapenzi mwanangu watakuroga huko shauri yako."Yalikuwa ni maneno ya mama ambayo niliyakumbuka kwa wakati huo ambao nilikuwa tayari nishaingia katika gari ya baba ambaye licha ya uchovu wa kazi zake lakini akaamua kunipeleka morogoro mwenyewe kwa kutumia usafiri wake na kuniondelee kadhaa ambayo labda ningekutana nayo pale ningeamua kupanda mabasi yale ya mkoa.Safari yetu ikaanza kwa kasi na baba alikuwa akiendesha gari kwa kasi akiwa na lengo la mimi kuwahi na kilichonisaidia ni kwamba siku hiyo hakukuwa na foleni kabisa kwa maana hiyo tulikuwa tunateleza tu Barabarani na hata matraffic hawakuwepo katika baadhi ya sehemu nyingi barabarani.moyo wangu uliumia sana baada ya kuona naicha dar-es-salaam mji ambao nilizaliwa na kulelewa na kukulia pale nakuzoeana na watu kuwa nauacha kwa muda baada ya ujinga ambao niliusababisha mimi mwenyewe na hakuna hata rafiki moja niliyemuaga au kumuambia kuwa naondoka kwa sababu karibia marafiki zangu wote nao walikuwa wameona picha zangu ambazo nilikuwa mtupu kwa kweli.Sikutaka kabisa kukumbuka hali ile lakini cha ajabu ilikataa kutoka na kujikuta safari nzima nikiwaza inshu ile mpaka tunafika morogoro katika mishale ya saa sita mchana baada ya kutoka nyumbani saa moja Asubuhi.Tulifikia morogoro mjini mji kasoro bahari mji ambao sikuwahi hata siku moja kuwa ningefikiria kukaa.

"Daaa aisee kweli maisha yanabadilika."Yalikuwa ni maneno ambayo niliyatamka kimoyomoyo baada ya kushuka katika mji huo ambao udongo wake ulikuwa mwekundu kabisa.ila pilikapilika zilionekana kama zinataka kukaribia dar-es-salaam kutokana na mishe mishe na pilika pilika za watu waliokuwa wanafanya biashara za hapa na pale.Baada ya kushuka ndani ya gari la baba tukatoka nje nakuanza kuangalia madhari ya sehemu ile ambayo ilikuwa pale stendi ya mabasi yanayotoka sehemu kama dar,mbeya na mikoa mingine ambayo ilikuwa magari yake yapitie pale stendi ambapo palikuwa panaitwa msamvu.Baba taratibu akaingiza mkono wake mfukoni nakutoa simu yake ya mkononi kisha akabonyeza namba flani nakuipeleka sikioni.
"Eeee ndugu tushafika hapa msamvu...aaaaa kumbe ushafika basi njoo hapa wanapopaki magari."yalikuwa maneno ya baba ambaye baada ya kusema vile haikupita hata dakika tano akaja jamaa wa makamo ambaye kama ukimuangalia alikuwa na miaka kama ishirini na tano au ishirini na saba kuendelea thelathini.
"Haya nambie kijana wangu naona unapendeza tu."Baba akaanzisha mazungumzo na kumwambia yule jamaa ambaye aliachia tabasamu pana usoni wake.
"Shikamoo mzee wa magari naona upo na huyo ndio kijana wako.?? Anayekuja tuishi naye hapa Morogoro."
"Aaaaaa ndio anaitwa Pablo bwana."
"anhaa pablo aisee mwanao handsome boy hivi karibu sana Morogoro janja Huku kuna raha Aisee kuliko dar."....

Yalikuwa maneno ya yule jamaa ambaye aliponambia vile akanipa mkono kunisalimia na mimi nikaupokea.Baada ya kusalimiana mazungumzo yakaanza kuendelea na yule jamaa ambaye alionekana kabisa kupaelewa sana morogoro.
"Sasa kwa sasa hivi pablo Tutaenda nyumbani ambapo utakuwa wewe unaishi kisha kesho yake nitakupeleka kwenda moja kwa moja kuanza kazi katika duka la mpesa na tigopesa utafanya kwa muda mpaka vyuo vitapoanza kuchukua watu maana kwa sasa hivi Muda bado sasa nimeongea hapa mbele ya baba yako kuwa uwe muanifu katika kazi maana nimekupa duka langu hilo ambalo watu watakuwa wanatoa pesa na kuingiza pesa nahisi unajua wanavyofanyaga."yalikuwa maneno ya ya yule jamaa rafiki ya baba ambaye maneno yake yalisababisha niachie tabasamu baada ya kuniambia nitaanza kazi.Baada ya kuniambia vile Baba akaniachia kiasi cha pesa kisha akaniita twende katika gari lake kuna kitu anataka kuniambia na mimi sikuwa na budi nikamfuata baba ambaye naye alikuwa akimshukuru sana rafiki yake huyo
"Kijana wangu pablo dar-es-salaam umeharibu sitategemea upumbavu wowote huku morogoro nitakuua ujue wewe haya sitaki kabisa kusikia yani eti ujaenda kazini sitaki kazi rahisi sana uliyopewa fanya kazi kwa bidii mpaka muda wa chuo utakapowadia nakuomba sana uwe mtulivu huku.Sikukatazi wewe kuwa na mademu lakini angalia huku morogoro utarogwa yangu hayo nakutakia maisha mema lakini nitakuwa nakuja kukuangalia kila baada ya mwezi au safari zangu zikiianza tena utakuwa unaniona mwanangu."Yalikuwa maneno ya baba yaliyoniingia kabisa na kusababisha nitikise kichwa nikimdhihirishia kuwa nilikuwa nimeelewa sana kile ambacho alikuwa akikiongea.

"Sawa baba nimekuelewa Baba yangu na ahsante sana maana mpaka hapa siamini Ahsante sana baba yangu nakuomba ukija usisahau kuja na Mama namsalimie sana Mama yangu."Nikamjibu baba kwa kumsisitizia na kusababisha anisapoti naye kwa kutikisa kichwa taratibu akanipa mkono.
"Sawa mwanangu naomba umuheshimu huyu david nakuomba umpe heshima kama unavyonipa mimi maana mimi rafiki yangu tu ndio amefanya yote yani amekupangia chumba chenye umeme huku bila ya mimi kumpa chochote nakuomba umuheshimu pia nakuomba uache wanawake wanawake usije yakukuta mabaya kama haya."Baba alinisisitizia kwa maneno yake yale ambayo kwa hakika yaliniingia sana na kusababisha mpaka nijisikie hali flani ya upweke.Baada ya kumaliza kuongea baba akamuita yule rafiki yake ambaye alikuwa akiitwa david naye akaja na kuagana kisha naye baba akatoa kiasi cha fedha na kumkabidhi david ambaye alikataa kabisa kukichukia na kumuambia kuwa alikuwa ahitaji pesa na alimfanyia vile kama kulipa fadhila.Taratibu baada ya baba kumalizana na david akaingia katika gari kisha akanipungia mkono ishara ya kuniaga kisha akang'oa gari na kuondoka na kutuacha mimi na david huku mgongoni kukiwa na begi langu la nguo na lingine nikiwa nimelishika mkononi.baada ya gari lile kupotea machoni mwake david akaniangalia kisha akalichukua begi langu la mkononi na kulivaa yeye mgongoni.
"Twende kijana wangu."david akaniambia vile kisha tukaanza kuondoka pale tulipokuwepo na kuanza kunielekeza mitaa mitaa na majina yake.
"Pablo hii ndio Morogoro bwana si unaona inavyopendeza nimekaa hapa mwaka wa sita sasa kwa hiyo sasa naujua vizuri sana Huku bana kuna warembo balaa maana ninavyokuona unaonekana kabisa mzee wa totoz."
"Hahahaha hamna bwana anko mimi sio mzee wa totoz.".
"Aaaaa halafu pablo usinizeeshe mimi sio anko mimi naitwa david mdogo wangu."Hakika mimi na david damu zetu zilipendana ghafla kuliko nilivyotarajia kwa sababu muda mfupi tu kuongea naye akaanza kuniambia vitu vingi kuhusu maisha yake na vitu vingine niliviona vya siri lakini yeye aliniambia na kujikuta baadhi ya vitu ambavyo vilichekesha basi tulikuwa tunacheka wote.Hata mimi hakika nikamzoea haraka sana na kujikuta nikimkubali kwa muda mfupi na alionekana kabisa mienendo yetu inaendana kwa sababu kila tulipokuwa tunapishana na baadhi ya wanawake wazuri yeye alikuwa akiniambia.

"Pablo mwanangu hebu cheki yule manzi alivyokuwa na makalio makubwa hahaha Morogoro ujue kuna warembo mdogo wangu sema tu usiwe unasahau kinga pale tu utakapokuwa unapiga show."Maneno ya david yalizidi kunifanya mara nyingi niwe na tabasamu safari yetu ya kutembea ikaishia katika stendi ambayo tulipanda gari aina ya hiace gari ambayo tulipopanda sisi akaiachia mwendo na hata hatukakuaa sana katika gari kwa mwendo wa nusu saa tu tukafika sehemu ambayo tulitakiwa kufika.Hakika madhari ya Morogoro sehemu ambapo tulishuka na kuanza kutembea palionekana kama dar tu kwa sababu umeme ulikuwepo na vitu kama bar kumbi za kuangalia mipira ilisheheni kwa wingi miongoni mwa watu walionekana kucheka na kufurahi kwa pamoja hakika hali ya amani iliyokuwepo maeneo yale ambayo david aliniambia kuwa ndiye mitaa ambayo ndio karibia na sehemu ambayo nitakuwa nakaa hakika ilinifariji na kunitoa wasiwasi kabisa maana mara ya kwanza nilikuwa na waza sana.Safari yetu ya kwanza ikaaishia katika ofisi kubwa ya wakala wa tigo pesa na mpesa ambayo ilikuwa kubwa kiasi ofisi ambayo ilikuwa imefungwa.

"Sehemu ambayo utakuwa unafanya kazi ndio hapa kama unavyopaona watu wengi hapa biashara kama hii hapa ndio sehemu husika yani hapa ni mjini kuliko sehemu uliyokuwa unakaa hapa kitaani wote wananijua na ngoja nikakutambulishe na washikaji wakujue maana si unajua bwana kuna siku labda kuna weza kutokea vimatatizo lakini sitegemei."David akaniambia kisha akanipeleka kwa marafiki zake ambao walinichangamkia kwa sana na kuwaambia kabisa kuwa mimi ndio nitakuwa nasimamia ofisi yake na alinitambulisha kwa watu kuwa mimi ni mdogo wake wa damu kabisa.safari yetu ikaendelea mpaka katika nyumba ambayo ndio nitakuwa nakaa hakika nyumba ilionekana ni nzuri na kwa nje tu iliniridhisha lakini sasa ile tunaingia tukakaribishwa na Mwanamke mrembo ambaye alikuwa ndani ya kanga moja tu nakusababisha uchu unitoke kabisa hadi karoti yangu ikanyanyuka taratibu lakini nikajikuta nikijizuia pasipo kuonekana.
"Hee karibu david naona umetuleta mgeni ndio atakuwa anakaa huyu nini.??"yule mwanamke aliongea huku akicheka cheka na kuniangalia mimi kwa macho ya kuibia ibia lakini mimi nikampotezea na kujifanya kama simuangalia vile.
"Aaaa ndio bwana Rozinta huyu mtakuwa naye hapa mdogo wangu huyu tumefanana eee rozinta."
"Mmmh wala hata hamjafanana mwenzako huyo handsome boy wa nguvu."Maneno ya yule mwanamke rozinto yakasababisha mimi na david tucheke na kuingia kabisa ndani ambapo nikajikuta nikiganda kidogo na kushangaa baada ya kuwaona wanawake watatu wazuri sana ambao baada ya sisi kuingia na wao wakatutizama.
"Mmmmh humu nitapaweza kweli kwa hali hii??".......
Nikajikuta nikijisemea kimoyomoyo baada ya kuona hali ya pale nyumbani ambapo ndio nitakuwa nakaa kutokana na warembo wazuri waliokuwepo ndani kunitamanisha na kunipa uchu mkubwa wa mapenzi kila nilipokuwa nawaangalia.baada ya kuingia pale ndani tukakaribishwa vizuri kisha moja kwa moja mimi na david tukaenda mpaka alipokaa mwenye nyumba ambaye alikuwa amekaa na wale wanawake pale wakipiga story.
"Jamani karibuni Hamjambo vijana wangu wangu."
"Hatujambo mama shikamoo."wote wawili mimi na david tukamsalimia mwenye nyumba ambaye akatukaribisha tuketi pale naye katika mkeka na sisi hatukuwa na budi taratibu tukakaa.
"Enhe mama kama nilivyokuambia kuwa hapa sitakaa mimi atakaa huyu mdogo wangu kabisa alikuwa dar-es-salaam sasa kwa sasa amerudi na atakuwa na wewe hapa lakini atakuwa pia anafanya kazi katika ofisi yangu pale kwa hiyo naombeni mumpeni ushirikiano kwa sababu huyu ni mgeni hapa."yalikuwa ni maneno ya david yalisikiwa vizuri na kila mtu akiwepo yule mama mwenyenyumba ambaye alikuwa akiniangalia angalia kwa mtu ambaye alikuwa akionyesha kama ananitathimini flani hivi akiwepo na wale wasichana watatu ambao walikuwa nao wananitolea macho.

"Haya mwanangu nimekusukia na wewe kijana unaitwa nani vile??"
"Mimi naitwa pablo."
"Haya paplo eee pabilo majina mengine kama mizizi ya dawa kienyeji karibu mwanangu jisikie upo nyumbani kwanza nimekupenda unaonekana una heshima karibu je nikuulize swali??".
"Niulize mama tu usijali."
"Je humu kuna zamu za kufagia je utawezaa??"
"Heee mama yani mfagilishe kijana wa watu alivyompole mama tutafagia tu wala aache tu sisi tutagia."Ghafla kabla hata sijajibu swali ambalo nimeulizwa msichana mmoja akadakia na kujibu lile swali hali iliyosababisha wote waanze kucheka.
"Hahaha mama mimi naweza mbona."
"Haya mwanangu lakini siunaona warembo wanakutetea utakuwa haufagii mwanangu lakini karibu sana hii morogoro amani tu."Hakika nikajikuta nikijisikia hali ya faraja sana pale maana ukaribisho niliokaribishwa niliupenda kuliko maelezo baada ya kumaliza kuongea Mimi na david tukanyanyuka na haraka tukaenda katika chumba changu ambacho kilikuwa varandani na vyumba vingine vilikuwa uwani.Tukaingia katika chumba changu ambacho kwa hakika nilikipenda sana kilikuwa kina kila kitu cha muhimu hadi na tv na kilichozidi kunifurahisha ni kuwepo kwa umeme pale.

"Haya kijana naona warembo wanakutolea macho wameolewa wale wee haya."
"Hahahaha unasema ukweli.??"
"Hamna mwanangu pablo wewe wasughulikie tu wale lakini usisahau kutumia kinga maana mademu wa siku hizi vicheche."
"Aaaaaa kweli lakini kwa sasa mimi sihitaji mwanamke."
"Haya sasa hapa kuna inshu ya umeme lakini nahisi utaambiwa vizuri lakini hapa ndio kwako kwa sasa ukitaka kupika kuna jiko la gesi hapa na sufulia hizo kama unavyoona pia sokoni sio mbali ni pale si ulipaona."
"Ndio david"
"Haya sasa twende leo ukanunue chips pale halafu utakula sasa hivi then usiku utaenda tena kununua lakini ndio hivyo mimi nakuacha lakini sasa hivi naondoka nitakuja kesho Asubuhi nikakuelekeze kazi zinafanyajwe."yalikuwa maneno ya david ambaye alikuwa tayari kashasimama na kuvaa viatu vyake akiwa na lengo la kutoka nje.mwanaume nikanyanyuka kitandani pale nilipokuwa nimejiegesha kutokana na kauchovu wa safari kisha taratibu tukatoka mimi na david kuelekea sehemu ambayo tulikuwa tumekusudia.
"Hivi david wewe na baba mko vipi maana urafiki wenu sijaonaga aisee."Nikajikuta nikimuuliza david swali ambalo baada ya kulisikia akaachia tabasamu kidogo kisha akaniangalia na kuanza kusikitika.

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO



USIKOSE SEHEMU YA ISHIRINI

Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
4 Aisee Kumbe Raha Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni