Notifications
  • THE NIGHTMARE (9)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA TISAILIPOISHIA...“mmenifananisha, mimi ndio kwanza naigia ofisini mida hii.” Aliongea yule afande na kuigia kituoni.“sasa aliyekuwa anatuhoji ni nani kama sio huyo?”Alijikuta anajiuliza mwenyewe swali lililompa utata mkubwa kichwani mwake.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Wakati wakiwa hawajui hili wala lile, walishangaa kuona maaskari wakijazana pale na ambulance ikafika…
  • THE NIGHTMARE (8)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA NANEILIPOISHIA...Walipofika feri, walipewa nahodha mwingine tofauti na yule aliyemuota na boti ilikuwa ndogo tu ya kawaida tofauti na ile aliyoiota.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Sharji alijikuta anapiga makelele baada ya kumuona Balqis akiwa amejaa damu mdomoni huku ametoa makucha yake akimfata kwa nia ya kumdhuru.“AAAAAAAAAAAGH”Sharji alipiga kelele na kukurupuka.…
  • THE NIGHTMARE (7)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA SABAILIPOISHIA...“kha!!!!”Ulikua mshangao mkubwa kwa watu karibu wote baada ya kumuona Sharji akiwa na taulo akitoka chumbani kwa Balqis.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Wengine walicheka na kaka yake alionekana kutoifurahia hali ile.“sasa wewe unatutia wasi wasi bure, si ungesema tu kama unaenda kulala kwa huyu dada?” aliongea kaka yake na kukirudia kile chumba alichompangia…
  • THE NIGHTMARE (6)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA SITAILIPOISHIA...“toa loud speaker bwana.”Aliongea Balqis baada ya Sharji kubonyeza kitufe cha kupaza sauti.“kwanini hutaki nisikie maongezi yenu?” aliongea Karimu kwa sauti ya ukali kidogo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...“kwani kuna ubaya mimi nikiongea private na mdogo wako?” alijibu Balqis baada ya kuisikia sauti ya Karimu.“hakuna ubaya.” Alijibu Karim kwa sauti ya…
  • THE NIGHTMARE (5)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA TANOILIPOISHIA...Alijikuta outomatic akijisemea kwa mshangao baada ya kumuona dada mmoja mrembo mwenye asili ya kiarabu akiingia mule ndani. Hakuvaa ushungi kama alivyowazoea kuwaona waarabu wengi ambao alikutana nao. Huyu alivaa suruali ya jeanz nyeusi na juu akiwa na kikoti chake cheusi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Kati kati kulikua na nguo Fulani nyeupe iliyonakshiwa…
  • THE NIGHTMARE (4)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA NNEILIPOISHIA...Aliongea Khalidi na kuufungua mkanda wa suruali yake na kuanza kumtandika Karim.“unanipiga mimi?...utaona!”IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Aliongea Karim na kuondoka huku analia.*****************************Zilipita wiki mbili bila ya Karim kuonekana nyumbani kwao. Sabra alisikitika kidogo kutokana na kuwapenda sana watoto wake japokuwa huyo mtoto mkubwa hakuwa…
  • Fumanizi la Mchepuko Mwizi😂 | Comedy
    Mume amefuma viatu vya mchepuko wa mke wake mlangoni lakini akakosea kuingia ndani kabla aweke umakini kwenye hivyo viatu mwisho wa siku akaibiwa na vyake😂Hili tukio lazima lichukuchekeshe sana hata kama ulikuwa haujataka kuchekaItazame kisha nipe like na ukinipa maoni kwenye comment nitashukuru sanaUsisahau kubonyeza Subscribe kama haujajiunga na fungua #ChekanaZephiline kupata video zangu zote ambazo zipo mtandaoniNashukuru sana kwa wewe ambaye unanipa nguvu ya kuendelea kuwaletea kazi nzuri…
  • THE NIGHTMARE (3)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA TATUILIPOISHIA...Akiwa hewani akikata mawingu kurudi Tanzania, kichwa chake kilikua na mawazo mengi sana juu ya mume wake. Aliikumbuka siku waliyofunga ndoa.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Pia alijua kwanini mume wake alipendelea kufanya kazi uingereza na yeye kumfungulia ofisi huku huku Tanzania. Hakujua kuwa kazi anayoifanya mumewe ni ile ya kutembea na tajiri mkubwa…
  • THE NIGHTMARE (2)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA PILIILIPOISHIA...Khalidi alishangaa kuitwa na mtu asiyemfahamu. Alitoka na kwenda kumuangalia huyo mtu maana kiukweli hakua na ndugu aishie hapa Dar hata mmoja anayemfahamu..IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Alipigwa na butwaa baada ya kumuona Sabra pale.“ahsante mungu.” Aliongea Khalidi baada ya kumuona tu yule binti pale.“pole sasa kaka yangu, nisamahe mie.” Aliongea Sabra kwa…
  • THE NIGHTMARE (1)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA KWANZANi kipindi cha mvua za masika. Upepo mkali, na mvua kubwa iliendelea kunyesha kwa kasi kila kona ya nchi ya Tanzania.Ipo mikoa iliyofurahia mvua hizo kwa kuwa walikua wanaisubiria kwa hamu kwa ajili ya kilimo. Lakini ipo mikoa iliyokua inapata shida kwa uharabifu wa mazingira na mengineyo mengi.Moja ya miko hiyo ni Dar-es-salaam. Watu wanaoishi katika mkoa huo walichukia mvua mfululizo kutokana na sababu mbalimbali. Biashara nyingi…

CHAGUO LA MOYO (5)

Mwandishi: Michael Michael

SEHEMU YA TANO
Mzee wanao wanaendelea vizuri hasa yule mwanao wa kike ambae nafikiri atakua judith,yeye ameshapata fahamu na inawezekana wakamruhusu mda wa jioni, kwa upande wa michael nae hali ni nzuri japo sio sana na hii ni kutokana na kupoteza damu nyingi hasa kutokana na majeraha aliyokua nayo na nafikiri baada ya wiki moja hali yake itakua sawa,.

SASA ENDELEA...
Daktari yule alimaliza maelezo yake marefu ambayo alikua akimwambia mzee samwel,sawa nimekuelewa daktari ila nilikua na omba kama kuna uwezekano niende sasa hivi nikawaone wanangu na bila kikwazo chochote daktari yule alisimama na kumwambia mzee samwel amfuate ili ampeleke wodini ambapo wanae ndipo walikua wamelazwa,mzee samwel alitoka na kuongozana na daktari yule ambapo safari yao ya kwa kwanza iligomea katika chumba ambacho ndani yake ndipo alipokua amelazwa michael,mzee samwel alimuomba daktari huyo amsubiri hapo nje kwani anamaongezi ya siri ambayo alikua akihitaji kuongea na mwanae michael,daktari yule kwakua alikua ni muelewa alimruhusu mzee samwel aingie na yeye alibakia nje akimsubiri ili waweze kwenda katika wodi ambayo alikua amelazwa judith,mzee samwel baada ya kuingia katika chumba alichokua amelazwa michael alisogea karibu kabisa na kitanda ambacho alikua amelala michael na bada ya kufika alipiga magoti na kumuomba michael amsamehe kwa yote aliyomfanyia kwani anajutia kwa kila kitu,michael alitingisha kichwa kumaanisha kua alikua amemsamehe mzee yule na hii ni kutokana na kushindwa kuongea kwani alikua amefungwa nyaya katika mdomo baada ya taya zake kulegea kutokana na kichapo alichopokea kutoka kwa mzee yule,baada ya kumaliza maongezi yake na michael mzee samwel alitoka na kumkuta daktari akiwa bado anamsubiri na baada ya hapo waliongozana mpaka katika wodi ya wanawake na kuelekea katika chumba ambacho judith alikua amelazwa,baada ya kufika mzee samwel alimuomba daktari amsubiri hapo nje kwani pia alitaka kuzungumza na mwanae huyo jambo la siri ambapo daktari yule alimkubalia ombi lake,mzee samwel alifungua mlango wa chumba alichokua amelazwa judith kisha kuurudishia kwa ndani,alisogea mpaka karibu na kitanda ambacho judith alikua amelazwa,judith alimtazama baba yake kwa macho yaliyojaa chuki,alitokea kumchukia sana baba yake,alimuona kama mnyama kwa kitendo alichomfanyia michael,mzee samwel alilitambua hilo kupitia katika mboni za mwanae,alipiga magoti chini huku machozi yakimtoka na kumuomba mwanae amsamehe kwa ote yaliyotokea kwani ni shetani alikua amemtawala,judith huruma ilimuingia na akajikuta anamsamehe baba yake,baada ya kusamehewa na mwanae mzee samwel alisimama na kumbusu mwanae katika paji la uso na baada ya hapo alimnong'oneza judith kitu katika sikio lake,whaaaat... baba unasema kweli au unanitania,ni maneno aliyoyasema judith baada ya kupokea taarifa ile kutoka kwa baba yake,ndio mwanangu ngoja tusubiri apone maana madaktari wamesema baada ya wiki moja afya yake itakua imetengemaa,ila nataka asijue tumfanyie surprise.. aliongea mzee samwel kumwambia mwanae, judith alifurahi mno,taarifa aliyopewa na baba yake kwamba michael akishapona wataenda kufunga pingu za maisha kwa kuwa mke na mume kwake lilikua jambo kubwa sana,hakuamini kama ndoto yake ya kuwa na michael inaenda kutimia siku za hivi karibuni,hakika alifurahi mpaka akajikuta machozi ya furaha yakimtoka,nashukuru sana baba na mungu akubariki kwa kila jambo,aliongea judith kumwambia baba yake,usijali mwanangu ni jukumu langu kuhakikisha unakua na furaha muda wote,alijibu mzee samwel kumwambia mwanae..

Judith aliongea mengi sana na baba yake mzee samwel, na kila sikualikua akimuomba Mungu amsaidie michael apone haraka, hatimae baada ya wiki moja kupita michael aliruhusiwa hospitali na mzee samwel pamoja na judith walifika hospitali hapo kwaajili ya kuja kumchukua na kumpeleka nyumbani, hakika ilkua furaha sana kwa bibie judith hasa baada ya kumuona michael akiwa mzima tena, waliamua kukaa siti za nyuma za gari na kumuacha mzee samwel akiliondoa gari kwa kasi eneo hilo, michael alipatwa na mshtuko baada ya kuona gari haliendi muelekeo wa nyumbani na akahisi huenda judith ameshakubaliana na baba yake waende wakamuue kabisa, michael alipigwa na butwaa hasa baada ya kuona gari likipaki katika moja ya duka kubwa la nguo, hapo waliambiwa na mzee samwel washuke, michael pamoja na judith walishuka na mzee samwel akawataka waingie ndani ya duka hilo na kuwaambia judith achague shela na michael achague suti nzuri kwaajili ya harusi yao ambayo itafanyika sikuya jumamosi ikiwa imebaki wiki moja tuu kufikia siku hiyo,michael na judith walichagua nguo hizo na baada ya mzee samwel kulipia waliingia kwenye gari na safari ya kuelekea nyumbani ilianza, njia nzima michael na judith walikua ni wenye furaha na walikua wakipigana mabusu huku wakishikana shikana, michael uzalendo ulimshinda na akataka afanye mapenzi na judith humo ndani ya gari lakini judith alimzuia na kumuambia asubiri wafike nyumbani kwani wakifanya mapenzi humo watamkosea heshima mzee samwel, mzee samwel ni kama aliligundua hilo na aliendesha gari kwa kasi na baada ya dakika kadhaa waliwasili nyumbani, baada ya kushuka ndani ya gari, judith na michael walielekea chumbani huku wakimuacha mzee samwel akifanya taratibu za mwisho kwaajili ya harusi ya binti yake,michael na judith walipofika chumbani hakuna kilichofuata zaidi ya wawili hao kufanya mapenzi na kuziridhisha nafsi zao.....
*******************************************************
Ilikua siku ya jumapili ambapo barabara zote za mtaa zilikua zimefungwa, watu walijipanga katika barabara kubwa wakiwa wanaimba na kushangilia msafara wa gari aina ya VX 8 zipatazo kumi na mbili huku gari zingine zaidi ya thelathini zikiwa nyuma ya msafara huo, msafara huo ulikomea katika moja ya kanisa kubwa na baada ya gari hizo kupaki michael akiwa amevalia suti nyeusi iliyomkaa vyema aliteremka ndani ya gari na kufuatiwa na judith akiwa ndani ya shela jeupe ambalo lilimpendeza na kufanya aonekane kama miss world, waliongozana mpaka katika madhabahu ya kanisa hilo huku wakifuatiwa na nderemo na vifijo kutoka kwa kina mama waliohudhuria sherehe hiyo, mchungaji alifika na kuwafungisha ndoa michael pamoja na judith na wakawa mwili mmoja, baada ya harusi hiyo kuisha mzee samwel aliwakabidhi michael pamoja na judith baadhi ya miradi yake, nyumba pamoja na gari, huko maisha yaliendelea na kila siku judith huwa anamwambia mume wake michael kuwa anampenda sana na hatokuja kumsaliti ukizingatia magumu waliyoyapitia...
TUENDELEENI KUVUMILIANA SIMULIZI ZITAZIDI KUJA HIVYO NAJIPANGA KUWALETEA NYINGINE

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO



MWISHO

Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
10 Chaguo la Moyo Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni