Notifications
  • MY DIARY (30)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINITULIPOISHIA...Baada ya hapo Nnilimwomba mama mdogo ajikaze na kuwatarifu ndugu wengine habari hizo za msiba.Tulisaidiana hivyo hivyo maana sio siri kila mmoja alikuwa na uchungu sana kutokana na mazingira ya kifo hicho. Habari zilizidi kusambaa kwa kasi na majirani walianza kukusanyika hapo kwa mama mdogo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Msiba ni msiba tu na ukitaka kujua binadamu…
  • MY DIARY (29)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA TISATULIPOISHIA...Hapo sasa nikazidi kuchanganyikiwa ikabidi nimuulize mama huyo alikuwa akifanyia shughuli zake za kujipatia kipato sehemu gani.? Yule dada akanambia kuwa anafanyia soko la ndizi huko Korongoni. Sikuwa na jinsi nilimuomba anipeleke lakini na yeye alisita sita kwa madai kuwa alikuwa na kazi nyingi za kufanya na bado anatakiwa ampeleke mtoto shule.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (28)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA NANETULIPOISHIA...Sisi tumesomea mambo haya bhana waliendela kuzungumza wale walinzi huku wakishuka ngazi kwa polepole. Hapo na mimi nikawa nimejifunza kitu kuwa kumbe unaweza kuingia na mtu guest akakuzuru kisha akaondoka zake.Sasa sijui kwenye zile guest zetu za uswahilini kama wanalijua hili.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi nilala japo usingizi ulikuwa hautaki kuja kwa…
  • MY DIARY (27)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA SABATULIPOISHIA...Alinamba eti hayo ya mimi kuolewa tuyaeke pembeni na kwa nini siku hiyo nisilale Moshi tukumbushie enzi zetu. Mwalimu John aliendelea kusema kuwa amenimiss sana na anomba nisahu yaliyopita na turudie yale maisha yetu ya zamani.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilijifanya simwelewi lakini ukweli ni kwamba nyota ya mwanaume huyu ilikuwa ni kali sana zaidi yangu na…
  • MY DIARY (26)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA SITATULIPOISHIA...Joyce alinambia yeye haendi kujipanga foleni kama makahaba wengine hivyo yeye hufanya biashara hiyo kitaalamu zaidi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Alisistiza pia kuwa eti huwa anatumia kinga kuwakinga wengine. Wakati mwingine alinambia acha awaambukize kwa sababu wanaume wangekuwa na akili basi wasingeenda kununua mwanamke. Anasema kuwa laiti biashara hiyo…
  • MY DIARY (25)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA TANOTULIPOISHIA...Sikuisha hapo pia nilimpongeza kwa kunijali na kunipenda na kuhakisha kuwa siingii kwenye majanga kama yake mara baada ya kutoka jela. Siku hiyo nilimuelewa sana Joyce na nilikuwa tayari kumsapoti kwa lolote ili mradi tu atimize athma yake hiyo ya kuzaa. Tuliongea mengi sana na baadaye alinionesha picha ya mtu ambaye alitaka kuzaa naye.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (24)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA NNETULIPOISHIA...Kwa kweli siku hiyo niliwaza sana na kutafakri vitu vingi. Wale wanachuo wenzangu wamenambia kuwa Msouth alikuwa kwa kimada mwingine na japo stori haikumalizikia ila ukweli ni kwamba alifumaniwa na kupigwa vibaya na huenda walimtupa mahali na ndio maana chanzo cha kifo chake hakieleweki.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilijaribu kuijikontrol ili nisiwaze kitu…
  • MY DIARY (23)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA TATUTULIPOISHIA...Alinisihi sana nisitoe niilee na yeye atatoa huduma zote lakini tuendelee kufanya siri ili tusije tukahatarisha ndoa yake na kusababisha familia yake kuyumba. Kwa kweli sikuweza maana ilikuwa ni kujipa tabu mimi na huyo mtoto atakayezaliwa. Bora ataa ingekuwa ni mimba ya ule mwalimu ambaye hajaoa.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilitamani nimchomekee hiyo mimba…
  • MY DIARY (22)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILITULIPOISHIA...Alitumia vizuri umbo lake la kimiss kutembea kimiss na kuweka mapozi ya maana. Na baada hapo alilala kwenye kile kigodoro na akachojoa vyote isipokuwa kufuli jeupe ambalo nalo alipewa hapo hapo kwa ajili ya kazi hiyo. IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi sikumpa nafasi Joyce niliingilia nafasi yake na kuchukua ule uume wa bandia nikamfuta yule dada.…
  • MY DIARY (21)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJATULIPOISHIA...Nilichomeka simu chaji na kuiweka hewani ili nione kama kutakuwa na sms yeyote iliyoingia.Hofu ilizidi kunitawala na wakati naendela kufikira simu yangu iliita niakzani labda ni Joyce na nilipoiangalia nilimkuta ni Msouth. Sikutaka kuipokea nikaiacha iite mpaka ikate yenyewe.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nikajiuliza kwani amepatwa na nini usiku huo mpaka…

MTAA WA TATU (58)

Mwandishi: Hafidhi J Ikram

SEHEMU YA HAMSINI NA NANE
Hafidhi akiwa nchini Ufaransa
Aliweza kutambua kitu kimoja kama October 14 inakaribia basi
Bibiye Mariam anaweza kufanya kile ambacho aliwai kumueleza

NIOMBE SAPOTI, BONYEZA TANGAZO LINALOKUJA NA KUJAA KWENYE SIMU YAKO WAKATI UKIFUNGUA SIMULIZI AU LILE LINALOKUWA KATIKATI YA SIMULIZI ZETUKABLA HAUJAIFUNGUA NDANI, PIA KUNA LILE LINAKUJA NA KUNG'ANG'ANIA HAPO CHINI, BONYEZA WALAU MARA 3-4 HIVI HIYO NDIO SAPOTI YAKO KWANGU, TAFADHALI NIPE NGUVU NAKUTEGEMEA SANA MSOMAJI WANGU
SASA ENDELEA...
Akaona kama kweli atakuwa na lengo hilo itakuwa vigumu kutoka salama kwenye uwanja huo
Ndipo akafunga safari kuja kumzuia asifanye kitendo hicho.
Sema akawa amechelewa kufika na kukuta mauwaji yashafanyika bibiye kanaswa.
Chakufanya ni kumkomboa tu, mwanaume akafanya mambo na kuondoka nae.
Baada kuondoka nae akampeleka sehemu ya mbali yani kijijini, huko
Kwenye kijumba cha udongo juu kimeezekwa nyasi sijui ilikuwa nyumba ya nani, akamlaza kitandani na kuanza kumpatia huduma ya kwanza
Mariam alikuwa hajiwezi kwa chochote,
Mwanaume akawasha moto na kuchukuwa sufulia akaweka maji akatoka nnje na kuchuma majani fulani hivi akainjika jikoni
Dakika si nyingi dawa ikawa tayari akaanza kumkanda nayo kila sehemu yenye
Majeraha nyingine akatwanga na kumpaka
Sehemu yenye vidonda
“aaaaaaah"
Mariam alitoa sauti ya kilio kwani maumivu aliyokuwa nayo si madogo na ile dawa ndio ilikuwa kama inamchoma hivi,
“baby umzima?"
Hafidhi akauliza swali baada kumuona kipenzi chake kafumbua macho.

“ndio baby ni mzima ijapokuwa nasikia maumivu makali sana upande huu,"
Mariam akajibu hivyo
Basi ikawa kazi ya Hafidhi kumuangalia mpenzi wake mama chanja
Akaanda chakula yani viazi vitamu akavichemsha tu wakala. Usiku ukafika na kulala,
“Sijui atakuwa kaenda nae wapi dahaa simu zao zote hazipatikani,"
Vivian akabaki kujisemea hivyo akiwa kitandani na mwanae kipenzi Ikram
Hivi mtoto atakuwa kamuachia nani? Embu subiri nimpigie simu Khamisi, akaichukuwa simu yake na kubofya bofya akaiweka sikioni
Simu ikawa inaita hatimae ikapokelewa,
“halloo Khamisi ujambo?"

“sijambo Dada hofu kwako tu vipi kuhusu Dada Mariam mbona mpaka sasa hivi hajarudi nyumbani mtoto analia huku
anamtaka mama yake,"
Khamisi akaongea hivyo
“Mariam kuna matatizo yameweza kumtokea na mpaka sasa sijui yupo wapi ninachokuomba mlete Yusra kesho asubuhi,"

“Sawa sister"
Simu ikakatwa pasipo Khamisi kutaka kudadisi matatizo gani yaliyoweza kumsibu Dada yake.


Kesho yake asubuhi na mapema Khamisi aliweza kufika nyumbani kwa Vivian akiwa na mtoto basi akapokelewa na kuambiwa kila kitu kilichoweza kutokea ndani ya uwanja wa taifa kuwa dada yake ndio muuwaji wa Rais, binafsi Khamisi akapinga vikali sana na kusema hapana dada yake hawezi kutenda kitu kama hiko itakuwa kasingiziwa tu aliongea hivyo huku akilia, ikabidi Vivian ambembeleze na kumwambia asijali kila kitu kitakuwa sawa hakuna chochote kibaya kitakachoweza kumtokea dada yake. Kikosi cha jeshi la polisi waliingia kila sehemu ambayo walihisi wanaweza kumpata bibiye Mariam, yani ilikuwa msako mpaka nyumbani kwa Vivian sema kila kona mtu hayupo picha zake zikabandikwa kila maeneo kuwa mtu huyu anatafutwa kwa yeyote atakayeweza kufanikisha kukamatwa kwake zawadi nono itatolewa. Mwezi mmoja ukaweza kutimia pasipo kuonekana kwa Mariam wala Hafidhi hakika lilikuwa pigo kwa bibiye Vivian asiweze kufahamu hawa watu watakuwa wapi, akajitahidi kila njia kuwatafuta mwishoe akakata tamaa na kungojea ipo siku watakuja kuonana nae, kwakuwa watoto walikuwa wapo wawili ikamuwia vigumu kwa yeye kuwaangalia ukizingatia kazini anahitajika basi akatafuta mfanyakazi za ndani, siku moja Vivian alikuwa anajiandaa kwenda kulala wakati huo house girl ameshaenda kulala zamani tu na kumuacha Vivian sebuleni akiangalia season ya I miss you usingizi nao ukaanza kumnyemelea akazima tv na kupiga hatua kadhaa kuelekea chumbani kwake ghafla taa zikazima akajuwa labda tanesco washafanya yao akajongea dirishani kuangalia nyumba za jilani umeme upo “ohoo shit! Yani umeme nimenunua juzi tu leo hii umeisha mambo gani tena haya ile anageuka akajikuta anakabwa na kuwekewa kitambaa mdomoni akajitahidi kujinasua kutoka kwa kiumbe hicho sema hakuweza mwishoe akanyong’onyea na kupoteza fahamu hakuweza kutambuwa kilichoendelea. Baada bibiye kupoteza fahamu kiumbe kile kikapiga hatua za kunyata na kuingia chumbani kwa house girl haikumchukuwa muda mwingi kuwepo ndani ya chumba hicho akatoka na kuingia chumba cha Vivian akatoka akiwa kawabeba watoto. Ni asubuhi nyingine nyumbani kwa bibiye Vivian polisi waliweza kufika baada kupewa taarifa kuwa Vivian na wanawe wametekwa jana yake usiku na haijulikani wamepelekwa wapi,

Mona akachekecha akili na kutoa kauli moja tu, “itakuwa ni Hafidhi ndio aliyetenda kitendo hiki,’’ ndani ya kijumba cha udongo tunamuona bibiye Vivian akiwa amelala pembeni yake yupo Ikram sema sauti ya Ikram akilia ndio ikamshtua kutoka kwenye usingizi mzito akakurupuka huku akihema kijasho kilimtoka akazidi kudata baada kujikuta ndani ya nyumba ambayo haifahamu. Akaangalia kushoto na kulia akamchukuwa mwanae na kumkumbatia kisha akashuka kitandani si akaliona panga akawai kulichukuwa kwa mwendo wa kunyata akawa anatoka huku Ikram kambeba mgongoni ile anatoka tu ghafla akajikuta akidakwa mkono na kupokonywa panga nae akajizungusha kugeuka akapigwa na butwaa baada kumuona kipenzi chake yani Hafidhi ndio aliyemfanyia hivyo akafahamu amekuja kumkomboa baada kutekwa akawai kumkumbatia kwa nguvu huku nae akilia. Sauti ya makofi ikipigwa ndio ikamfanya Vivian ageuke kungalia ni Mariam, “baby mbona sielewi mbona niko huku kunanini huku na nimefikaje?’’

Vivian akauliza maswali akitaka kufahamu sema aliweza kufarijika baada kuweza kuwaona watu wake wa karibu akaenda kumkumbatia Mariam na kumuomba msamaha kwa kile alichoweza kumtendea kule uwanja wa taifa pia akamwambia hata Mona anaomba umsamehe,

“Vivian na Mariam naomba niwaambie vitu vya msingi sana kwanza kabisa tambuweni kitu kimoja nyie kuanzia sasa ni wake zangu nitakuja na shekhe hapa atie ubani ndoa ipite kitu kingine Mariam hutakiwi kuonekana tena mjini mpaka pale kila kitu kitakapokuwa sawa hata wewe Vivian swala la kwenda mjini sahau tutaishi hapa madamu pesa tunazo kila mahitaji muhimu mkihitaji mimi nitawaletea,’’ Hafidhi akaongea hivyo na kuwafanya wake zake watizamane na kutabasamu “hii sio haki kabisa yani mimi katika umri huu wa miaka 22 maisha yangu nimalizie huku kijijini si kujizeesha huku,’’ Vivian akapinga wazo la kuambiwa mjini apasahau. “hata mimi siwezi kuishi huku mbwinde kama kusakwa na polisi wacha wanisake ila mjini nitaenda,’’ Mariam nae akaunga mkono kauli ya mwenzake. “sikieni nyie wanawake binafsi hakuna ambaye nimemshika miguu nikamfunga kamba kumzuiya kwenda huko mjini mnaweza kwenda ila jichungeni sana,’’ baada mwanaume kuongea hivyo akanyanyuka na kuchukuwa panga huyo akaingia zake mashambani. “Mariam kwani hii sehemu mmeuziwa au mbona mnaonekana wenyeji sana?’’ Vivian akauliza swali, “mie hata sijui nakumbuka tu ile siku ya tukio baada kunitowa kule nikajikuta niko hapa,’’
Kusema kweli ndowa ya mabinti hawa ilipita kimtindo tu yani
Shekhe akaitwa na kutia ubani
ndugu pekee aliyeweza kuhudhulia ni Hamisi kaka wa bibiye Mariam
kwa upande wa Vivian kuna familia ikamuwakilisha kama ndugu
Leo kaolewa Vivian
Kesho kutwa Mariam watu walikula na kusaza wakaomba jamaa aowe kila siku,
saba za mwanzo zikapigwa sasa sijui saba gani wakati kawafunua wee kawageuza wee
Mpaka kuwazalisha leo hii anapiga saba
Pumbavu,
maisha ya
kijijini yalizidi kusonga mbele huku Vivian akipata nafasi anaenda mjini hata kwa bibiye Mariam nae ikawa hivyohivyo lakini siku moja wakati akiwa kwenye super markert moja hivi camera ikaweza kumnasa basi muhudumu akapiga simu polisi wakafika bila kuchelewa bibiye akanaswa mbele ya Michael kijana ambaye kajiunga kwenye jeshi la polisi kwa nia moja tu kumnasa Hafidhi wakati wale Maagent kutoka nchini Marekani baada kufika nchini iliwawia vigumu kumtambuwa Michael na kuamuwa kurudi nchini kwao. Taarifa za kunaswa kwa bibiye Mariam zilisambaa kama moto kwenye nyasi kavu watu wakaomba anyongwe siku hiyo hiyo, Wananchi wakaandamana wakimtaka muuwaji na kusema serikali inamchelewesha tu kama vipi wapewe wao waweze kumaliza kazi.

“Mama Ikram,’’ “abee mume wangu kipenzi’’ “mbona mama Yusra mpaka saa hizi hajarudi tu,’’ Hafidhi akamuuliza swali Vivian maana kigiza kinaingia sasa pasipo Mariam kuonekana pasipo kutambuwa mwenzao kanaswa usiku ule hakuna aliyeweza kupata lepe la usingizi kizuri zaidi Yusra kamzoea Vivian ndio kama mama yake vile, kesho yake asubuhi mwanaume akatoka kwenda mjini akarudi na jibu kuwa Mariam yupo gerezani,

(NADHANI TUMEWEZA KUFAHAMU KILA KITU KUHUSU MAMBO YALIYOWEZA KUTOKEA NDANI YA MIAKA MINNE TUNAKUMBUKA TULIHISHIA PALE BIBIYE MARIA KATOROKA GEREZANI NA KUMPIGIA SIMU HAFIDHI AKIWA KITUO CHA DALADALA GHAFLA AKAVAMIWA NA KIKUNDI CHA MAJAMBAZI NA KUTAKA KUMBAKA LAKINI MZEE WA KAZI AKAWAI KUFIKA NA KUPAMBANA NA MAJAMBAZI WALE NINI KILIENDELEA BAADA YA HAPO TUWEMO SOTE)

“Mwanaume akachumpa na kuachia double kick za ajabu jambazi mmoja akarushwa kule na kuwa kimya huku damu zikimchuruzika kwa wingi kwenye kichwa chake wengine wakaona mmh hii sasa balaa wakaamua kutimua mbio, kwakuwa bibiye alikuwa kapoteza fahamu baada kupigwa na kitu kizito kichwani akambeba na kuondoka nae.

Ndani ya usiku ule bibiye Vivian hakuweza kulala kabisa baada Hafidhi kupigiwa simu na kuondoka nae akainuka toka kitandani na kuanza kuzunguka huku na kule
Ndani ya chumba kile
Dakika si nyingi akashtukia mlango
ukifunguliwa akaingia Hafidhi akiwa kambeba bibiye Mariam
“ohoo Mungu wangu,"
Aliongea hivyo Vivian huku akimpokea
Mariam na kumlaza kitandani,
“sasa sikia nikwambie kitu Vivian itabidi kesho uongozane na mwenzako kwenda nchini Denmark
kumbuka kitu kimoja mnatakiwa muishi huko mpaka pale nitakapo wasiliana nanyi muweze kurudi,"
Hafidhi akazungumza hivyo na kutoa begi
Uvungu wa kitanda akamkabidhi
Vivian kwa kumwambia hiki ni kiasi cha pesa zipatazo billion 15
Za kimarekani

Bila shaka hizi pesa zitaweza kuwatosha kwa muda ambao mtaishi huko
Vivian muangalie sana mwenzako nilindie watoto wangu,"
Hafidhi aliongea maneno hayo huku mchozi ukimtoka ni jambo ambalo lilimshangaza sana bibiye Vivian,
“baby unamaanisha nini kuzungumza hivi?"
Vivian akauliza swali,
Sema Hafidhi akujibu kitu zaidi ya kumbusu kwenye paji lake la uso
Akafanya hivyo kwa watoto na kumalizia kwa Mariam,
Kesho yake yapata saa nne Asubuhi ndani ya uwanja wa ndege maeneo ya Kipawa tunamuona Hafidhi akiwa na wake zake
ijapokuwa bibiye Mariam alikuwa akijificha mara kwa mara

Ondoa hofu bibiye kila kitu kipo sawa,’’

NAOMBA SAPOTI, KUNA MATANGAZO(ADS) YANAJITOKEZA KWENYE APP YETU, LIMOJA LINAJAA KWENYE KIOO CHAKO JINGINE LINANG'ANG'ANIA HAPO CHINI KABISA, BONYEZA JAPO MARA 2 AU 3 KILA UKIFUNGUA SIMULIZI HIYO ITANIPA NGUVU YA KUENDELEA ZAIDI NA SIMULIZI ZETU🙏🙏

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO



USIKOSE SEHEMU YA HAMSINI NA TISA

Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
10 Mtaa wa Tatu Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni