Notifications
  • MY DIARY (41)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA MOJATULIPOISHIA...Mark anashangaazwa sana na mwanamke huyo lakini kwa kuwa shida yake ilikuwa ni hela anaamua kuachana nae na kuanza maisha mapya hapo jijiini Dar es salaamMaisha yanaendela lakini Mark amekuwa tajiri na mtu mwenye mafanikio sana kiuchumi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Pamoja na mafanikio hayo ni mtu ambaye mapenzi bado yalikuwa yakimuumiza siku hadi siku.Filamu…
  • MY DIARY (40)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINITULIPOISHIA...Alikuwa akinyata kwa kweli. Kweli hata mimi nilimkubali tu siku ya kwanza ingawa bado nilikuwa sijajua ufanisi wake wa kazi.Nilikaa nae hapo kwangu kwa mda wa siki tatu huku asubuhi tukiamka na kuendelea na kazi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Ndani ya mda huo nikagundua kuwa alikuwa na uzorfu mkubwasana hivyo kazi hiyo alikuwa akiimudu kabisa.Hapo sasa nilimkubali sana…
  • MY DIARY (39)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TISATULIPOISHIA...Nilikuwa na furaha sana huku nikiamini kuwa ndoto zangu za kuja kuwa mtu maarufu zinaweza kufanikiwa hata kabla ya kuyapata yale madini. Sikutaka mbwembwe niliamua kuikopi na kuipesti hiyo stori kama ilivyo na kuifowadi kwa Mark.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Baada ya kama lisaa hivi Mark alipiga na kuniuliza kama kweli ilikuwa nai mimi nimetunga hiyo…
  • MY DIARY (38)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA NANETULIPOISHIA...Usiku nilishituka usingizini baada ya mbu kuning’aata na kunisumbua sana. Niliwachukia sana hao mbu kwa sababu walinikatisha ndoto yangu ambayo nilikuwa nikiota.Ndoto ilikuwa ikielezea jinsi harusi yangu na Mark itakavyokuwa. Ndoto ilikuwa tamu sana maana ilinipa taswira ya picha halisi ya maisha yangu ya mbeleni.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilishusha neti…
  • MY DIARY (37)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA SABATULIPOISHIA...Hapo alitulia tulii kama mtu aliyeaamia dunia ingine. Kimoyo moyo nikawa najisemeha kama amehamia dunia ingine na kuanza kuwaza ujinga sahuri yake mimi nipo kazini bwana acha nitafute hela. Ndio ni lazima nifanye kazi kwa utaalamu na utundu wa hali ya juu ili waendelee kusimuliana huko mjini ili niendelee kupata hela.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Wewe…
  • MY DIARY (36)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA SITATULIPOISHIA...Sasa wewe fikiria mimi niliyeletewa zawadi sikujua ni zawadi gani lakini yeye tayari alishafungua na kuchungulia na kujua nini kilifungwa huko ndani.Basi nikaendelea kumuhudumia yule mama huku na yeye akiniambia kuwa itabidi nikimmaliza hizo zawadi tusifungue hapo hapo na waniimbie wimbo wa happybirthday.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Tuliendelea na stori mbili…
  • MY DIARY (35)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TANOTULIPOISHIA...Tatu niliambiwa kuwa ndugu zake na wazazi wake walihusika kwenye mipango hiyo hivyo walibariki kabisa huyo binti kuniacha mimi mumewe wa ndoa na kuamua mtoto wao aolewe upya. Nne ni kwamba huyo mzungu amewaamishia wazazi wake mjini na amewajengea nyumba ya kifahari.Kwa hiyo mimi ninavyowapigiana simu na kuwajulia hali kumbe wenzangu huwa wananichora tu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (34)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA NANETULIPOISHIA...Hapo nikakumbuka kuwa zile zana zangu za kazi nilikuwa nazo ni vile vifaaa vya kupimia ukimwi ambavyo huwa navitumia kabla ya kukutana na mwanaume yeyote nisiyemfahamu. Nikaamua kumkubalia huku nikiamini kuwa hiyo ndo kinga yangu pekee iliyobaki kama mwanaume huyo atataka kuzini na mimi usiku huo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi tuliondoka na kwenda sehemu…
  • MY DIARY (33)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TATUTULIPOISHIA...Nilikuwa nachanganya staili za kijamaika na hizi za kwetu, sikuacha pia zile za Nigeria hapo nikapata vitu vyangu vya tofauti kabisa. Basi baada ya kujihakikishia kuwa nipofiti kwa mastahili yangu hayo nilisubiri siku ya shindano ifike nikafanye yangu. Siku ya shindano ilifika na mimi nilikuwa miongoni mwa washiriki walioingia tatu bora.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (32)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA MBILITULIPOISHIA...Lakini kuchepuka kwangu na kuingia mgombani haikumaanisha kuwa sheria ingeniacha hivi hivi.Ilifika mahali ikabidi nizime gari na kutulia tulii kusikilizia nini kitafuata.Tayari nilikuwa nimezungukwa na mapolisi ambao walikuwa wakinifuatilia kwa kutumia pikipiki.Kwa bahati nzuri dereva wa lile gari na yeye alishafika hapo na alishawaambia polisi kuwa mimi naugua ukichaa na nilifufuka kutoka mochwari.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA…

MTAA WA TATU (24)

Mwandishi: Hafidhi J Ikram

SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE
FBI wenyewe wakabaki hoi washauwa
Laiya kama saba wengine tisa majeruhi.

Sema hawakutaka kuachwa kizembe ilikuwa mkimbize mkimbize mpaka hospitali ya muhimbili.

NIOMBE SAPOTI, BONYEZA TANGAZO LINALOKUJA NA KUJAA KWENYE SIMU YAKO WAKATI UKIFUNGUA SIMULIZI AU LILE LINALOKUWA KATIKATI YA SIMULIZI ZETUKABLA HAUJAIFUNGUA NDANI, PIA KUNA LILE LINAKUJA NA KUNG'ANG'ANIA HAPO CHINI, BONYEZA WALAU MARA 3-4 HIVI HIYO NDIO SAPOTI YAKO KWANGU, TAFADHALI NIPE NGUVU NAKUTEGEMEA SANA MSOMAJI WANGU
SASA ENDELEA...
Hafidhi nae alikuwa makini katika kuwakimbia FBI
ghafla
Mwanaume akapotea kwenye mazingira ya kutatanisha, polisi wakabaki kuzunguka kila kona mtu hayupo,
“huyu mtu au jini aisee mbona huku hakuna njia kabisa kapitia wapi
huyu nyau?"
Afande mmoja akauliza na kupiga ngumi ukuta.
“dahaa huyu kijana kusema kweli sio wa kawaida kabisa, yani hafananii na mambo anayo
yafanya kudadeki"
Afande mwingine akasema hivyo
ikawa ni kumtafuta huku na kule,
Ndani ya Yombo vituka tunamuona mwanaume akiwa anakata mitaa
Hana pikipiki sijui kaiyacha wapi.
“shit! Kudadeki kumbe hii nchi ina wakuda kishenzi yani hawajui kama wanauchokoza moto nitawachinja wote.
Hafidhi akaongea kwa hasira na kutokea balazani,
“wee kaka mambo?"
Kuna binti alikuwa akikaanga sambusa baada kumuona Hafidhi akampa hi
“powa tu mrembo niambie".....
Hafidhi akachukuwa sambusa moja na kuila,
“vipi shilling ngapi hizi sambusa?"

“mmh ushaanza kula ndio unaulizia bei haya shilling mia moja tu kaka yangu"

“ok! Isiwe kesi naomba niwekee kwenye sahani sambusa kama kumi kisha niletee chumba kile pale.
Nipo ndani nasubiri mchumba"...
Hafidhi huyoo akaongoza chumbani kwake
“sawa nakuletea sasa hivi usifunge mlango basi"

“Wee Nuiya yule kaka humjui akujui leo hii ushaanza kujipendekeza shauri yako usije ukavamia majini bule"....

“bwanaee haikuhusu fata yako nifate yangu kwanza ni mteja tu"...

“Ukisikia umbea ndio huo mtu kasema nimpelekee sambusa chumbani kwake ushaanza kuleta shobo,
kama vipi peleka wewe basi"
Nuiya akaongea kwa hasira kumwambia yule shogaake.
“sijakwambia nashoboka wala nini kumbuka
Mimi na wewe ni marafiki wakubwa tu, penye ukweli lazima niseme.
Yule kaka ndio kwanza kaja kutafuta chumba leo, tena kahamia bila kitu chochote ndani zaidi ya
Bagi tu!"

“bwanaee embu nitokee hapa kumbe ulitaka ahamie na wewe au?
Ndio maana nimekwambia haya kuhusu"
Nuiya akachukuwa sambusa na kumwambia yule shogaake,
“embu Rahma niangalizie hapo napeleka mzigo wawatu narudi sasa hivi"
Kisha huyo akaingia mpaka ukumbini na kubisha hodi chumbani kwa Hafidhi.
“hodii kaka yangu"..
“karibu Dada sukuma uingie mlango upo wazi tu"
Nuiya akaingia na kumkuta
Mwanaeme yuko kifua wazi kajilaza kwenye sakafu kichwa kaegemea kwenye bagi.
“nakuona umelala
mbona hakuna godoro au kitanda?"

“godoro na kitanda naenda kununua kesho si unajuwa ndio kwanza nimetoka kijijini huko
Msanga chole sina hata kijiko"..
Hafidhi akaongea uwongo tu.
“usijali kaka yangu kuna godoro nitakupa ulalie usiku huu maana Mimi silitumii lipo tu"

“nitashukuru sana Dada yangu"
Basi Nuiya akatoka dakika si nyingi akaingia akiwa kabeba godoro
Hafidhi akalipokea na kuliweka vizuri akapewa na shuka mbili mto wa kulalia na neti
“shukrani sana Dada yangu kwa kunipatia msaada"
Nuiya akatoka bila kuongea chochote.
Kufika ukumbini akajisemea
“duhuu huyu kaka ni handsome ana kifua kipana mwili uliojengeka kimazoezi yani mpaka raha kumuangalia,
sauti ya Rahma ndio akamshtua akimwambia
“wee Nuiya
Gube anachukuwa sambusa huku ataki kulipa"
Akaenda mbio na kufikia kumkunja huyo
Gube, “kudadeki zako nipe pesa yangu"....hivi unafikilia hizi sambusa nagawa bule sio?"

“sikia nikwambie kitu wewe Malaya hizi sambusa nakula na kulipa silipi kama polisi sijui kwa mjumbe nenda kashitaki bwege mkubwa wewe"..
Nuiya akasukumizwa na kudondoka chini. Kisha Gube akabeba deri la sambusa na kuondoka nalo.
Rahma akamuinua shost wake
na kumpa pole
“achana nae si anajiona mbabe sio kutudhurumu wanyonge.
Kwanza mimavi hiyo utakula utaenda kunya, hilloo,,,pyeee
Nuiya akaishia kuzomea tu.
Wakazima jiko na kuingiza vyombo ndani,
“huyu mamaye ni siku ya tatu hii ananitia hasara juzi kabeba jana kabeba leo tena ahaa siuzi tena"
Ghafla kuna kishindo kikasikika nnje akatoka mbiombio
Alikuwa ni Gube kavimba jicho na mdomo nguo zimechanika chanika,
“vipi tena mbabe kitu gani kimekusibu?"
Gube akaanza kuongea huku akiangalia kule alipotokea na kutetemeka vibaya mno.
“nisamehe Dada yangu shika hizi pesa zako na sambusa hizi hapa sijala hata moja wallahi tena,
Nisamehe basi mwenzako nisije kuuliwa Mimi.
Gube akazidi kuongea kama haitoshi akatambaa na kwenda kumshika miguu
Nuiya
“Rahma hivi unamuelewa huyu pimbi si mbabe yeye mbona analia kama mtoto"
Wakati huo
Hafidhi anatokea njia ile ile akiwa kashika chupa ya soda.
Akauliza
“vipi Dada kuna nini hapo?"

“si huyu jamaa kila siku anakuja kula sambusa bure anajifanya mbabe.
Nashangaa leo yuko hivi"
Nuiya akamjibu Hafidhi
“inawezekana kuna kitu kimemtokea embu muulize vizuri"
“sasa Gube niambie nini tatizo kitu gani kimekutokea?"
Gube akaanza kusimulia huku akilia maana maumivu mpaka kwenye nonino,
“huwezi kuamini aisee wakati naondoka na sambusa ile nakatiza pale kichochoroni kwa mpemba tu, ghafla nikakutana
Na yule kijana anaetafutwa na polisi
kwa kosa la mauwaji
Kabla sijakaa vizuri nikashtukia nakunjwa na kuanza kupigwa.
Nilijitahidi kupambana nae kumbe ndio nazidi kujichochea kuni kwani alikuwa anapiga vibaya mno
tizama jicho langu pua yangu.
mdomo wangu pia
jamaa kasema usipo nisamehe ataniuwa please Dada yangu nisamehee"
Hakika jamaa alijutia kitendo cha kujifanya yeye ni mbabe.
Nuiya akaona hiyo ndio nafasi ya kumaliza hasira zake kingine akajiuliza kwanini huyo Hafidhi j Ikram, amekuja kumsaidia amelijuwaje tatizo lake.
Akabaki kujiuliza maswali pasipo kupata majibu.
“sasa sikia wewe kifaurongo hizi pesa ulizonipa hazitoshi kabisa, maana juzi ulichukuwa sambusa za shilling elfu
Saba jana elfu sita leo hata kama hujazila.
Ni shilling elfu tisa
Jumla nakudai elfu hamsini, ajabu unanilipa shilling elfu kumi na tano tu!"

“sio hivyo Dada yangu hiyo ndio niliyokuwa nayo, nikipata nyingine nitakupa tu"
Ghafla Gube akaanza kupigwa vibao vya haraka haraka na
Nuiya zote hasira tu mpaka shogaake akaja kumshika kwa kumwambia,
“basi inatosha shost msamehe tu.
Samehe saba mara sabini".....

“mshenzi sana huyu kujifanya kutuonea watoto wa kike ndio nini inuka sasa upigane bwege mkubwa wewe.
Sasa nimekusamehe ole wako urudie tena potea haraka sana kabla sijabarisha maamuzi!!!
Gube akatoka mbio akiwa haamini.
Huku nyuma vicheko vya kishambenga vikasikika
“hahahaha hallooo
Ohooo,,,
“sasa shost! Itabidi umtafute huyo jamaa umpe zawadi yake kwa kazi nzuri aliyoifanya"

“ndio maana yake nitamkabidhi huu mwili na kumwambia wote wako ufanye unavyotaka.
Embu twende huko kitaa tunaweza kumuona"
Basi mtu na shogaake wakaongozana kwenda kumtizama
Hafidhi j Ikram
wakati mwenzao yupo hapohapo
sijui ana badilika vipi yani wee acha tu.
Ikiwa imepita wiki moja tokea Hafidhi afanye tukio la ajabu kule
Kaliakoo kusema kweli hali haikuwa shwali kabisa kwa mzee Khatibu
Akaagiza kikosi kutoka nchini Thailand kupitia.
kwa rafiki yake kipenzi bwana
Mark Henry
na siku hiyo ndani ya ukumbi wa Victory for
Kulikuwa na kikao kizito.
Ajenda kuu iliyokuwa ikijadiliwa na kupewa nafasi kubwa ni kuhusu kidudu mtu kuingilia kazi zao.
“nadhani wote tumekutana hapa kwa ajili ya kitu kimoja tu nakitu chenyewe si kingine ni kuhusu huyu
Mjinga
Hafidhi j Ikram kuingilia anga zetu
sasa basi haina budi atafutwe popote alipo ndani ya dunia hii au hata nnje ya dunia.
Apotezwe haraka sana, wengi walijalibu kutufatilia na kuishia pabaya"
Kiongozi wa mkutano huo akaongea kwa hasira,
“lakini mkuu huyu kijana yuko tofauti na watu wengine!"
“kivipi awe tofauti na wengine yeye ni mnyama au binaadamu?"
“hapana mkuu sijamaanisha kama yeye ni mnyama,
Tofauti ya huyu kijana
kwanza ni mkali wa mapambano kingine anajiamini kupita kiasi, embu fikilia mpaka anafikia kuuwa polisi
Kumi na moja si kitu kidogo hiko"
“Ha!ha!ha!ha
Bwana Joseph usitake kunichekesha kabisa
mbona mambo madogo tu hayo,
au kwasababu kakuvamia nyumbani
kwako na kuondoka na million mia saba
kumbuka kikosi chetu kinaweza kufanya yote hayo.
Cha umuhimu ni kujipanga tuweze kupambana nae sio kutaja sifa zake"
Muda wote bwana Khatibu ambaye ndio baba yake Habiba alikuwa kimya tu.
Akanyoosha mkono juu akiashilia kuna kitu anataka kuzungumza basi akapewa.
Ruhusa
“kwanza kila mmoja atambuwe ya kwamba huyu kijana si wamchezo kabisa
kama alivyosema bwana Joseph
kwanza tujiulize ametujuwaje
sisi mpaka kufikia hatua ya kumuuwa mwenzetu bwana
Jacob kisha akaondoka na Do comment za siri ambazo zina taarifa zetu zote
kwa kifupi kijana anafahamu kila kitu kuhusu sisi tofauti na sisi kutokufahamu chochote kuhusu yeye.
Mkuu naomba nikwambie kitu kimoja
tukusanye vikosi vyote
kwanza tuitafute familia yake ikiwezekana tuiteke.
Kabla ya kuendelea kuzungumza zaidi mwenzake akamkatisha kwa kumwambia
“wewe wee embu ishia hapohapo
unataka kusema tuingie vitani
na mkuu wa majeshi sio?
tutajificha wapi ni bora angekuwa mtoto wa Rais kweli tambua kitu kimoja hivi vita ni
Vya mtoto sio Baba yake huko mimi simo kabisa"
Kila mmoja akabaki kuduwaa baada kusikia kumbe Hafidhi j Ikram ni mtoto wa mkuu wa majeshi, ila mkuu wa kikao akasema
“tukumbuke tushajitoa sadaka bila kuhofia chochote sasa basi kijana atafutwe
Tukimpata tumchinje hadhalani
jamii nzima itutambuwe sisi ni kina nani"....
Wakati kikao kikiendelea
upande mwingine tunamuona
Hafidhi akiwa na ndoo ya maji akienda bombani kama ujuavyo uswazi maji yenyewe ya Shida basi bombani kulikuwa na foreni si mchezo,
Mwanaume akafika na kuweka ndoo zake mbili kwenye foreni, kama sio yeye vile
“Yusra umemuona mkaka yule ni bonge la handsome jamanii anavutia yule
kama"...
“Hivi Amina shogaangu kila mwanaume kwako handsome embu acha upimbi
bwana"
“lini nilikwambia kila mwanaume handsome
ushaanza kuleta nyege zako
utaniudhi ohoo!!!
“basi yaishe shogaangu haya yule kaka ni
Handsome ehee"...
Katika maeneo hayo watu walijazana waume kwa wanawake watoto kwa wazee,
Kuna vijana kama wawili hivi wakaja
Mmoja kati yao akaitoa ndoo iliyokuwa ikijaa maji na kuweka yakwake,
“wee kaka vipi utatoaje ndoo yangu,
wakati umenikuta"...
binti aliyotolewa ndoo yake akaanza kulalamika,
“binti embu kausha basi siku zote kutangulia sio kufika, wacha wanaume tuchukuwe maji tusepe zetu,
Kuna mama mmoja akaja na kuipiga teke ile ndoo ya jamaa ikaenda kule maji yakamwagika
yule mama akaanza kubwata
“Wee mtoto shika adabu yako kabisa umetuona sisi mazuzu sio tumekuja hapa muda tu tupo kwenye foreni
wewe unakujakuja na p***mbu zako hizo eti uwai kukinga
Kama una simamisha hata sisi wanawake tunadindisha pia au nikuonyeshe kama nimesimamisha"

NAOMBA SAPOTI, KUNA MATANGAZO(ADS) YANAJITOKEZA KWENYE APP YETU, LIMOJA LINAJAA KWENYE KIOO CHAKO JINGINE LINANG'ANG'ANIA HAPO CHINI KABISA, BONYEZA JAPO MARA 2 AU 3 KILA UKIFUNGUA SIMULIZI HIYO ITANIPA NGUVU YA KUENDELEA ZAIDI NA SIMULIZI ZETU🙏🙏

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO



USIKOSE SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO

Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
9 Mtaa wa Tatu Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni