TANGA RAHA (28)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE
ILIPOISHIA...
Nikanyanyuka na kutoka nje na hatua ya kwanza nikachungulia dirishani kutazama ni nani anaye piga honi na kujikuta nikistuka na kajasho kembemba kakianza kunienda mbio,hii ni baada ya kuliona gari jeusi anina ya Land cruser likiwa limesimama nje kwangu huku likiwasha taa zote mbiliSASA ENDELEA...
“Nani huyu?”
Nilijiuliza mwenyewe kana kwamba kuna mtu pembeni yangu ninaye zungumza naye kumbe nipo peke yangu.Nikamshuhudi
Hilda akishuka ndani ya gari hilo na kuanza kupiga hatua za haraka kuja kwenye geti langu kidogo moyo ukanipata matumaini na kujikuta nikulifungua geti na
Hilda kwa ishara akamruhusu dereva wa gari kuliingiza ndani na nikabaki nikiwa ni nimeduwaa hadi gari linasimama akashuka jamaa mmoja mweusi kiasi aliye valia vizuri na kujikuta nikirudi katika hali ya kawaida baada ya jamaa kunisalimi
“AHaaa salama tuu kaka karibuni”
Nilizungumza huk u nikiliegesha geti langu na endapo kutatoke ishu yoyote niweze kukimbia kuepukana na msala uliopo ndani
“Eddy huyu anaitwa Rashid ni dereva wao Rahma”
“Ahaa karibu ndugu”
“Asante vipi huyo bibie yupo ndani?”
Swali la dereva nikajifanya kama sijalisikia na kuongoza ndani huku wao wakinifwata kwa nya-ma na mimi moja kwa moja nikaingia ndani na kuukuta
Rahma akiwa ametulia huku mapigo yake ya moyo yakienda taratibu kiasi kwamba nikabaki nikimtazama kwa muda.
Nikasikia sauti ya Hilda ikimuita Rahma huku akionekana kuja kwenye chumba chetu ikanilazimu kunyanyuka kitandani kwa haraka na kwenye kuufungua mlango na kumkuta akiwa amesimama mlangoni kwetu
Muambie huyo Rahma kwao wanamsubiria sana na ninampigia simu hapokei”
“Kwani kwao kuna nini?”
“Mimi wala sijui ila muambie kuwa kwao wanamsubira tena huyo dereva alitumwa kuja kwangu kumchukua kwa maana nilitoka naye nyumbani kwao”
Nikabaki nikimtazama Hilda huku nikikosa kitu cha kuzungumza hadi akaanza kuhisi kitu na macho yake yakanitazama kwa muda
“Eddy mbona una wasi wasi?”
“Eheee?”
“Mbona una wasi wasi?”
“Rahma ana umwa”
“Nini?”
“Rahma naumwa na hapa nilipo sijua ni uginjwa gani?”
“Mungu wangu yupo wapi sasa?”
“Humo ndani”
Halda akausukuma mlango na kumkuta Rahma kitandani akiwa amelala na kumshuhudia akianza kumwaga machozi na taratibu sauti yake yakulia ikaanza kuongezeka
“MIMI NINAWAAMBIA NINI WAZAZI WAKE JAMANI......EDDY UMEMFANYA NINI MTOTO WA WATU”
“Usilia sasa kwa sauti”
“Eddy acha nilie bwana umefanya nini mtoto wa watu mbona mimi sielewa?”
“Sasa wewe ukilia unadhani kutakalika humu ndani”
Nilizungumza huku nikianza kumvisha nguo Rahma na jasho jingi likazidi kunitiririka mwilini mwangu kiasi kwamba nihata uvishaji wangu nikajikuta mara kwa mara nikikosea kumvisha hadi ninamaliza kumvisha ni zaidi ya dakika kumi.
“Eddy Rahma ndio huyo amekufa unadhani mimi nitafanyaje na jaki ya MUNGU wazazi wake wakisema ni nani aliye fanya hivi mimi ninakutaja”
“Sasa hivo utakuwa unaharibu”
“Sio kuharibu”
“Kweli vile ni lazima niwambie na nitawaleta hadi hapa kwako”
Nikatoka sebleni na kumkuta dereva akiwa amesimama akionekana kama kusikilizia mazun-gumzo ambayo tunazungumza mimi na Hilda
“Kaka vipi kuna kitu gani kimetokea?”
“Ndugu yangu wewe acha tu kwa maana kuna ishu imetokea......Rahma ametokwa na mapovu na mwili wake umekakamaa sasa Hilda analia lia si unajua tena maswala ya wanawake”
“Haaa huo ni ugonjwa wake ambao humtokea kila baada miezi sita”
“Kweli?”
“Ndio”
“Ngoja basi nimlete huku”
“Usimtoe ngoja nimpigie simu mama yake kwa maana ugonjwa wake huu endapo utampata se-hemu alipo hapaswi kutolewa kwenye eneo alilopo na kuna shangazi yake ni mganga wa kihindi na kwa bahati nzuri yupo kwao wamerudi naye huwa ndioyo anamtibu Rahma”
“Hembu ngoja kwanza unataka umesema kuwa hapaswai kutibiwa sehemu yoyote zaidi ya se-hemu alipo pwatwa na ugonjwa huo?”
“Ndio na mukimuhamisha tu lazima anafariki?”
“Mungu wangu.....wewe umejuaje?”
“Ndugu ni mwaka wa 15 ninafanya kazi kwa kina Rahma na usinione hivi ni kijana ila umri wangu ni mkubwa na Rahma tangu yupo mdogo ninashuhudia matibubu yake yanakuwa hivyo na huo ugonjwa ameridhi kutoka kwa mama yeke”
Nikajikuta nikijibwaga kwenye kochi huku nikihisi nguvu za mwilini mwangu zikiniishia kiasi kwamba nikabaki nikiwa sina la kuzungumza na nikamshuhudia dereva akipiga simu na kuanza kuzungumza na mama wa Rahma na akaanza kutoa maelekezo ya sehemy alipo kiasi kwamba nikabaki nikitetemeka na akakata simu na kunitazama
“Wamesemaje?”
“Wamesema kuwa wanakuja na sasa hivi....Ila si wanakujua wewe?”
“MIMI.....?”
“Ndio wewe?”
“AHhhhhhaaaa”
“Ohoo basi vyema ukawa makini?”
“Makini na nini?”
“Yule mzee hana utani na mtoto wake na huwa hapendi sana watu weusi japo mimi nimepata bahati ya kufanya kazi kwake ila hataki hata kuniona ninazungumza na mwanae”
“Mmmm sasa..?”
“Hakuna cha sasa”
Akili yangu ikazidi kuchanganyikiwa na kusimama huku mapigo ya moyo yakianza kwenda mbio na sikujua hata ni nini nifanya,Nikaingia ndani kwangu na kumkuta
Hilda akiwa amekaa kitandani huku akiwa amemtazama Rahma huku akiendelea kulia na baada ya kuniona akanif-wata na kuanza kunipiga kifuani
“Eddy wewe ni katili umemuua rafiki yangu kwanini.....?”
Sikutaka kumjibu Hilda na kitu chochota na kumsukuma pembeni na kufungua kabati langu na kuanza kutafuta nguo ya kuvaa na kwa kiwewe nikajikuta nikichukua vesti na kuvaa na kabla sijatoka nje nikastukia Hilda akinishika vesti niliyo ivaa na kuanza kunivuta
“Hapa Eddy na kuambia hotoke na nimesha mpigia baba na kaseme anakuja”
“Wewe nimekuambia niachie nitakubamiza”
“Eddy nipige niue mimi badi sikuuachii kwani ukinipiga leo ndio mwanzo”
Nikasikia honi getini zikipiwa na moja kwa moja nikajau ni wazazi wa Rahma na kwa haraka nikamsukuma
Hilda na akadondoka chini na nikatoka ndani kwangu kwa haraka na kuufunga mlango kwa nje na kufika sembeli sikumkuta dereva na kwakupitai getini nikamuona dereva akijitahidi kufungua geti langu na gari moja ikaanza kuingia.Kwa haraka nikaingia jikoni kwangu na kumsikia Hilda akipiga makelele akiomba mkango kufunguliwa.
Katika sehemu ya juu ya jikoni kwangu kuna sehemu ipo wazi na kwaharaka nikapanda juu meza iliyopo jikoni na mikono yangu kuiingiza ndani ya sehemu hiyo na kujivuta kwa juu na nikafanikiwa kuingia ndani sehemu ya juu kwenye nyumba yangu japo kuwa kuna giza nikajipa moyo.Nikawasikia watu wengi wakiwa wanazungumza huku wakionekana kufuoka na kujiuliza maswali mengi.
Nikasikia wakifungua mlango wa ndani kwangu na Hilda akaanza kuropoka kwa kutumia Lghaya kiarabu huku mara kwa mara akilitaja jina langu la Edd
“Atakuwa ametorokea wapi?”
“Jamani nipeni nafasi ya kumuhudumia mgonjwa na acheni kelele kwani hali yake si nzuri”
Nikasikia machekeche kama ya wauza karanga za ketembeza yakipigwa na mama mmoja akaanza kupaza sauti yake huku akionekana kama mtu anaye pandisha mashetani.
Nikaanza kutembea taratibu huku nikikanyaga mbao za juu hadi kwenye sehemu ya chumba changu na kwa kupitia upenyo mdogo wa sehemu ilipo pitia feni la juu nikamuona Rahma akiwa amevuliwa nguo zake huku ndani ya ya chumba changu wakiwemo wamama watatu wa kiindi huku mmoja wao akiendelea kupiga machekeche yake huku kukiwa na vnyungu viwili vikiwa vinatoa moshi mwingi na kugundua harufu ya ubani.
Akaanza kumchunguza Rahma hadi kwenye ikulu yake na kumshuhudia akipiga chafya nyingi huku akitoa makelele mengi kiasi kwamba nikaanza kutetemeka
“ALIKUWA NA MWANAUME”
Mama huyo alizungumza kwa sauti nzito ambayo ni ya kiume na sikujua ni jini gani lililo mpan-da
“Huyo mwanaume ni wa aina gani?”
“HAAA NI MWAFRIKA ILA YEYE ANAWEZA KULETA MFARAKANO KATIKA FAMILIA YENU”
“Mfarakano gani mtukufu?”
“HHAHAAA YEYE ANAWEZA KUIFANYA FAMILIA YENU KUFILISIKA NA KUWA MASIKINI KABISA NA ISITOSHE RAHMA TAYARI AMAKIUMBA CHA HUYO MWNAUME TUMBONI MWAKE”
Moyo ukanipasuka na kwa haraka akili yangu ikapiga picha siku nikiwa gerezani kwani kitendo cha kumpa mwanafunzi mimba ni kifungo cha miaka 30 na mbaya zaidi mimi mwalimu sasa sijajua kama nitafungwa kwa miaka mingapi
“Mama wee kwanini huyu mtoto ameamua kunizalilisha kiasi hichi jamani ni nini jamani”
Nikajua mama anaye muhoji mganga huyo ni mama yeke Rahma na kujikuta nikizidi kumtazama kwa umakini na kila sifa aliyo kuwa nayo Rahma ameitoa kwa mama yeke
“USIPIGE KELELE NA ENDAPO MUTAKITOA HICHO KIUMBE BASI RAHMA MUTAMPOTEZA”
Mama Rahma akazidi kupaza sauti ya juu na kuuufanya mlango walio ufunga ukafunguliwa na akaingia mzee mwenye mwili mmkubwa na mama Rahma akanyanyuka na kwenda kumkumbatia mwanaume huyo na kuzungumza naye manneno ya kiarabu huku mara kwa mara mikono yake akimnyooshea Rahma aliyelele kitandani kama mtu aliye fariki huku mwili wake akiwa uchi kama alivyo zaliwa.
Gafla nikahisi kitu kiki nikuvutwa mguu kwa nyuma na nikageuza sura yangu nyuma kwa haraka kuangalia ni nini kilicho nigusa sikuona kitu cha aina yoyote na kujikuta nikitumia nguvu kujivuta mbele na kitu hicho kikaniachia na kustukia
Nikipoteza muhimili wa mwili wangu na kujikuta nikilala kwenye sehemu laini(signboard) ya juu kwenye chumba changu ambayo haiwezi kuhimili uzito wa mwili wangu na kujikuta nikipitiliza moja kwa moja na kuanguka chini ndani ya chumba changu na kutoa kishondo kizito
Kufumba na kufumbua sikuona mtu yoyote ndani ya chumba changu zaidi ya Rahma aliye lala kitandani akiwa hajitambui na nikasikia kelele na vishindo vya wanandugu wa Rahma sebleni kila mmoja akijaribu kuokoa maisha yake nikajua kwamba hawakutarajia kuuona uwepo wangu ndani ya chumba changu tena kwa mfumo huu wa kuanguka kutoka darini.
Nikanyanyuka japo sehemu ya mbavu za kushoto ninahisi maumivu makali ila nikajikaza na kuchungulia mlangoni sikuona mtu yoyote akitokea sebleni.
Kwa haraka nikaingia jikoni kwangu na kuchukua kifuko cha unga wa ngano na kujimwagia unga wote mwilini mwangu na nikausambaza vizuri usoni mwangu.
Nikachungulia sebleni nikaona vivuli vya watu wawili wakiwa wanakaribia kuingia ndani huku wakinyata wakitaka kuchungulia ni nini kilicho tokea
“Let’s go”(twendee)
Nilijisemea kwa sauti ya chini na kuchomoka kwa kasi jikoni huku nikitoa mlio wa pikipiki aina ya XL Baja na kuwafanya watu waliokuwa wakinyata mlangoni kukurupuka na kuanza kukim-bia kurudi walipo tokea huku baba
Rahma nikimpiga kikumbo getini na kumbwaga chini na kuwafanya wamama walio simama nje baada ya kuniona wakatawanyika kwa woga na kila mmoja akashika njia yake na kusababisha nao pia kuapiga kelele.
Breki ya kwanza nikasimama ndani ya maji kwenye fukwe almaarufu kwa jina la JET na sikujali watu wamenichukuliaje.
Japo kuwa siwezi kuogelea vizuri ila ikanibidi nipate ujuzi wa kupiga mbizi na kwenda mbali kidogo na ufukwe ulipo na nikakaa ndani ya maji huku nikiwa nimekiacha kichwa nje kwa ajili ya kuvuta punzi zaidi ya masaa manne hadi giza likatanda angani ndipo nikatoka ndani ya maji
Sikuwa na hamu ya kwenda nyumbini kwangu kwa maana nikahisi ni lazima watakuwa wananitafuta kwa udi na uvumba.
Nikapiga mwendo hadi nyumbani kwa madam Zena huku nguo zangu zikiwa zimelowa.
Nikagonga mlango kwa bahati nzuri akafungua madam Zena akiwa amevalia suruali na tisheti kubwa na akaonekana kunishangaa baada ya kuniona
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni