MAMA MWENYE NYUMBA (48)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA AROBAINI NA NANE
Hapo jamaa mmoja aka kaa kusho kwake na mwingine kulia kwake moja aka kaa mbele na mzee Mashaka ambae ndie aliekuwa anaendesha gari, kitendo bila uchelewa gari likaondolewa “mzee simu yake hii hapa”SASA ENDELEA...
Alisema yule jamaa alie mnyang’anya simu Edgar, huku akimkabizi mzee mashaka ile simu, na mzee mashaka akaiweka kwenye mkebe wa gari pale kwenye dash board, “huyu ndie mshemshenzi anae jifanya kidume, yani demu amebadilika kishenzi, ata utamu ana nizungusha kwasababu yake” alisema mzee mashaka akikamata bara bara ya morogoro na kukanyaga mafuta kama gari la police lina fukuza mwizi, “ukaona aitoshi uka mcnganya na mwangu, yani wewe mb..o yako ina simama sana au?” aliongea tena mzee Mashaka kwa hasira kari, huku amekanyaga mafuta vibaya sana, gario lilikuwa lina karibia speed mia ishrini kwa saa, “jibu wewe mjinga,” alisema yule jamaa wa pembeni kushoto kwake, akimzibua na kofi la utosini
Hapo Edgar alihisi maumivu makali sana, “anajifanya bubu siyo” alisema yule alie kaa mbele akiinuka kidogo na kujigeuza, kisha aka rusha ngumi akiulenga uso wa Edgar, lakini Edgar akawa mwepesi na kukimga mikono yake yote miwili, akafanikiwa kuzuwia ngumi hisi tuwe usoni, “haaa aanajifanya kukinga siyo”alisema yule wakushoto akaanza kushusha makofi ya utosi mfurulizo, kwenye kichwa cha Edgar, “jamani mtaniua bule kwani kosa langu nini?” aliongea Edgar kwasauti iliyo jaa uoga, ni baada ya kuona hasipo tumia akili wata muua kweli, “wewe unazani kinachofwata nini?, hapa safari ni msitu wa kisopwa, tuna kufukia mzima mzima” aliongea mzee Mashaka, alafu wote wakacheka kwa kebei
“Hapa inabidi nifanye kitu ili kjiokoa” aliwaza Edgar akimtazama mmoja moja jinsi alivyo kaa, sasa walikuwa wamesha fika kibamba ccm wanakata kona kuifwata bara bara ya chuo cha sayansi natiba cha muhimbili, tawi la mloganzila, akajipapasa mfukoni, akaina kuna peni pekee, ‘inaosha” alijisemea kimoyo moyo, huku jamaa wakipokezana kumtwanga makofi ya kichwani, ikafikia kipindi akaanza kuona kichwaa kizito, “vijana fanyeni kazi, msijali ilibegi lina fedha nyingi sana kwaajili yenu kwanza wote mna kula million kumikumi, alafu malipo mengine atajuwa boss wenu” aliongea mzee Mashaka akiwasisitiza wale vijana, “kwani mimi kosa langu nini?” aliuliza Edgar akipiga mahesabu ya haraka, huku wa usiri mkubwa akijaribu kuichomoa ile peni mfukoni mwake, nakujaribu kuwa jaza hasira wale watu, asa mzee Mashaka ambae ndie dereva, maana aliona wanazidi kusonga mbele, tena kwenye eneo asilo lijuwa
“We msheninzi mkubwa yani ume tembea na mwanamke wangu, uka tembea na mwanangu, bado unauliza kosa lako nini?” aliongea mzee Mashaka akionyesha kushikwa na hasira, “kwani mzee mimi niliwatongoza?” aliongea Edgar makusudi akitafuta maneno ya takayo muumiza mzee Mashaka, “mbwa mkubwa wewe sasa kwani uliwabaka?” alidakia yule jamaa wakulia kwa Edgar akishusha kofi kikichwani kwa Edgar, “sikia mwe fala siyo una nipiga tu mimi sijawai kutongoza” alisema Edgar kwa sauti ya ukali, “ok! sophia sawa, unataka kusema atasuzane alikutongoza wewe?” aliuliza mzee Mashaka akijaribu kuzuwia hasira zake, maana alijuwa jukumu alilonalo lakuendesha gari alitaki hasira
Hapo Edgar alijuwa mpango wake unaweza kufeli, na walisha karibia maeneo ya shule ya msingi mloganzila akakulupuka na nakauri moja matata, “siyo Suzane tu! ata mama sophia pia alini lazimisha mwenyew...” kabla ajamaliza alistukia breck za ghafla, na lile gari liki yumba yumba kukosa mwelekeo, lika seleleka na kuelekea pembeni ya barabara, ikitaka kuvaa nguza za umeme kuu ziendazo mikoani, “yap hii ni saa ya huko mbozi” alisema Edgar kwa sauti kubwa, jamaa wa wa kushoto kwa Edgar baada ya kusikia kauli ya saa ya ukombozi, akamwona Edgar akiwa ana nyoosha mkono kufungua mlango wa gari, akamshika mkono, nakurusha ngumi usawa wa uso wa Edgar, laki aikiwa bahati yake maana ngumi iliishia njiani baana ya kuona mkono wa Edgar ukifyetuka na kutuwa usoni kwake usawa wa jicho lake la kulia, hapo yule jamaa akahisi kitu makama sindano kikiingia kwenye jicho lake, ikifwatia na maumivu makali sana
“Mama nakufaaa” huku wengine wakiwa wana mtazama mzee Mashaka akijitaidi kuliweka gari vizuri akisimamisha bembeni ya barabara, waliisikia sauti ile ya mwenzao, mwanzo wakazani ni uoga wa hajari, laki walistuka baada ya kuona Edgar akifungua mlango wa gari, “kamata huyu mshenzi anashuka” aliongea mzee mashaka, na yule jamaa wa kulia kwa Edgar akamdaka mguu Edgar, huku alie kaa mbele akifungua wake na kuzunguka gari kuwai ule mlango alio taka kutokea Edgar, hapo Edga ali jigeuza kigogo na kuachia teke moja languvu lililo tua usoni kwa yule jamaa aliemshika mguu, ambae alienda na kujibamiza kwenye kioo cha dirisha lililo pasuka kiasi cha kichwa chake mpaka maeneo ya shingo yapitilize na kuchungulia nje, na kusababisha vipande vya vioo vimchane chane huku kimoja kikizama kwenye shingo yake na kumkata kolomeo
Hapo hapo huyu jamaa akapoteza maisha, pasipo kuangalia kilicho mpata huyu alie mtwanga teke Edgar aligeuka na kumtazama yule aliekuwa amekaa mble, akamwona amesha karibia kwenye mlango aliotak akutokea, Edgar akarukia kiti chambele, alicho toka yule jamaa, nakusababisha awe jilani na mzee Mashaka, ambae alimshika Edgar kwenye shati na kumvutia kwake Edgar akamwona yule aklie zunguka kumzuwia akija mbio kule aliko yeye, hapo Edgar aka mgeukia mzee Mashaka, “niache mzee sipendi, nikuchafue” aliongea Edgar kwa sauti ya kirafiki kabisa, lakini mzee Mashaka hakuonyesha kutii amri “fanya haraka mshenzi huyu nime mkamat..”
Kabla ata mzee Mashaka hajamaliza alistukia ngumi nzito ikitua shavuni kwake, lakini kwa machungu aliyo nayo, akutaka kumwachia Edgar, tena ukizingatia ametamka kwa mdomo wake kuwa ametembea na mke wake pia, “bahati yako mbaya mzee”aliongea Edgar huku aki mkamata mzee Mshaka kichwani na kumpagza kwenye kioo cha mbele mala mbili mfululizo, nakummalizia kwenye kioo cha pembeni ambacho kilipasuka navipande vika tawanyika hu kimapomo kikimchana kwenye shavu, kisha akashindilia teke moja languvu lililo mkusanya mzee mashaka na mlango wa gari, wakatoka nje, na Edgar akifwatia, kwabahati mbaya wakti anatuwa akamkanyaga mzee Mashaka kwenye mguu na kufwatia sauti kama ya mti mkavu uki katika, yani mguu wa mzee mashaka ulivunjika pale pale, wakati Edgar akishangaa tukio la kutua kwenye mguu wa mzee Mashaka, akastukia ngumi nzito ikituwa shavuni kwake ..
Ile ngumi ilimpata Edgar barabara nakumrudisha ndani ya gari, na kujibamiza kwenyestearing (mshikanio) akasikia maumivu makali sana, usawa wa mambavu zake, akajaribu kujiinua, kabla ajafanya lolote, yule jamaa alikuwa amesha mfikia na kumkaba shingoni kwamikono yote miwili, hapo Edgar akajuwa hasipo fanya juhudi ataumia, maana alianza kuisi macho yake yakitaka kutoka nje huku punzi zikizidi kumkauka, Edgar akajaribu kuikamata mikono ya yule jamaa nakujipapatua lakini ata aikuonyesha dalili ya kupapatuka
Hapa Edgar akaona kifo kipo nje nje, akatawanya mikono yae kama mtu anae tapatapa kwa kutaka kukata roho, bahati ikakawa kwake, maana mkono mmoja ulipapasa kwenye kipande cha kioo, alicho kivunjwa mzee Mashaka ambae kwa sasa alikuwa chini anagaragara kwa maumivu makali ya shavu na mguu, Edgar alikikamata vizuri kile kioo na kukipeleka kwanguvu usoni kwa yule jamaa alie bakia, ambae alikuwa ame mng,ang,ania shingoni, na kioo kile kika pita pembeni kidogo yam domo wa yule jamaa na kuchana shavuni “mama..” jamaa alipiga kelele akishuhudia damu zikimchuluzika kama bomba lililo pasuka, huku akishuudia Edgar akijirusha mzima mzima kuelekea kwa yule jamaa, na kwa kutumia miguu yake yote miwili alituwa kifuani kwa muuaji wakukodi wa mzee mashaka, ambae alijibwaga chini akimwangukia mzee mashaka, ambae alikuwa anagaa gaa pale chini nakumwongezea maumivu mala dufu
Yule jamaa akajaribu kuya shinda maumivu, nakujaribu kuinuka, lakini alikutana ngumi mfululizo zausoni, ambazo hazikuchagua pakutua, nyingine zili tuwa kwenye kidonda kpya kabisa cha jamaa huyu, hapo alijikuta akienda chini kama gunia akitua tena kwa mzee Mashaka na kumsababishia mzee wawatu apoteze fahamu, huku jamaa nae licha ya kiwili wili chake kutuwa juu ya mzee mashaka, lakini kichwachake kiligonga chini na yeye akapoteza fahamu, hapo Edgar aka angalia huku na huku, pamoja na kuwaangalia watekaji wake, akaona wame tulia hawana atauwezo wakumsogelea huku mmoja alie jibamiza dirishani, akiwa katika dakika za mwisho za kukata roho
Hapo Edgar akaingia kwenye gari na kuchukuwa mkoba wa mzee Mashaka wenye fedha, kisha akaanza kuondoka taratibu akiifwata barabara waliyojia, huku nguo zake zikiwa na matonye machache ya damu, baada ya kutembea kama kilomita moja toka alipo liacha gari, akakumbuka simu yake, akaanza kurudi kuifwata, lakini alipo karibia akakwaona watu wamesha zunguka eneo la tukio, huuku wengine wakipiga simu polisi, kutoa taalifa ya tukio lile ambalo awakuli fahamu vizuri, maana watu wote walikuwa wana hali mbaya, wakati mmoja ambae alikuwa anaugulia maumivu ya jicho lake lilo toboka, wenzake walikuwa wame lala kimya, na mmoja wao amepoteza maisha kabisa, Edgar akaona bola asamehe simu aishie zake
“Hapa ni kuondoka kabisa Dar,” aliwaza huku akigeuka na kuanza kutembea kwa haraka sana, wakati ana karibia barabarani yani kibamba ccm, umbali wa kilometa mbili toka eneo la tukio, alishuhudia gari la polisi likipita kwa speed kuelekea alikotoka yeye, hapo Edgar akavuka barabara na kuelekea nyumbani kwa Suzan, alipo fika aliingia moja kwa moja chumbani kwake, kile alicho panga, akabadiri nguo zake haraka sana, kisha akatafuta peni na karatasi, kisha akaandika maneo fla ni kwa haraka sana, akaweka juu ya kitanda chake akawasha taa ya ndani, kisha akafungua begi la mzee Mashaka, nakuanza kuamisha mabulungutu ya noti za elfu kumi kumi na kuweka kwenye begi lake dogo la mgongoni, ambalo aliifadhia fedha zake nyingine, pasipo kuesabu yale maburungutu yafedha ambayo yalifikia kama hamsini hivi, aliyaamisha yote na alipo maliza akaweka nguo chache na viatu pea moja, ndani ya begi lile begi, akalifunga na kutoka nje akiwa na begi lake na begi la mzee Mashaka, ambalo lilikuwa na makaratasi muhimu ya mzee huyu
Alitembea mpaka, kwenye kiuo cha daladala za kwenda kibaha, yani upande wa morogoro, akaingia kwenye gari (coster) la kwenda msata, akakaa kwenye siti yap eke yake, na kuliweka lile begi la mzee Mashaka chini ya siti
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA AROBAINI NA TISA
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni