MUWASHO (13)
Ukeni, wa Ngozi, Sehemu za Siri, Sehemu ya Kumi na Tatu
Zephiline F Ezekiel
2 min read
Mwandishi: Seif Jabu
SEHEMU YA KUMI NA TATU
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Baada ya kutawanyika binti huyo aliwatishia vijana wawili kwa bastora na kuwambia wamuingize kwenye gari yake,
Baada ya patashika za hapa na pale yule binti aliondoka eneo hilo akiwa na Seif ndani ya gari,
Scola, Monica na Dokta walifika eneo la tukio ila hawakumkuta Seif eneo hilo,
WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI
SASA ENDELEA...
"Atakuwa wapi?"
"Tuulize,"
"Si unaona watu wako makundi makundi tusogeye tusikilize wanayo zungumza,"
Waliwasogelea na kuanza kusikiliza watu wanachozungumza, walianza kufuatiria maongezi ili kuona kama watapata muongozo wa kumpata Seif,
"Kwa kipigo kile haponi mtu kabisa,"
"Lakini kaperekwa hospital anaweza kupona,"
"Aaaa.. Wapi si wakupona yule,"
"Yule hata akipona atakuwa na kirema cha maisha,"
"Hiyo ni kweli kile kipigo siyo cha mchezo,"
"Amshukuru yule Demu wa kihindi kumchukua na kumpeleka hospital,"
"Jamaa ana nyota huyo yule Demu sijui katokea wapi,"
Monica na wenzie walienda pembeni wakaanza kujadili Yale waliyoyasikia,
"Inaonesha kuna mtu amemchukua tena binti wa kihindi? wanajuana vipi?"
"Hatuwezi kujua wanajuana vipi? Ila cha mhimu ni sisi kujiunga na kuwa kitu kimoja tukamtafta,"
"Sawa,"
Upande wa pili Seif alifikishwa katika hospital ya Aghakan akapokelewa na manesi waliomkimbiza Chumba cha wagonjwa mahututi ila walipomfikisha mlangoni ilikuwa tabu kupokelewa,
"Kuna mgonjwa wa jinsia tofauti humu,"
Yule binti akahoji,
"Inamaana mnachumba kimoja tu cha wagojwa mahututi?"
"Hapana, kuna tatizo la kiufundi limetokea ndio maana tunatumia chumba hiki kimoja,"
"Kwa hiyo nifanyeje? Mtu wangu afie hapa?"
"Hapana ngoja tutoe gari ya wagonjwa wamuwahishe Regency Hospital,"
Wakiwa katika mabishano ya hapa na pale Dokta Sharihiya kutokea nchini India aliamuru Seif naye aingizwe humo ndani apatiwe matibabu,
"Muachane aingizwe humo, chukueni kitanda kingine mumuwe mgonjwa,"
"Sawa,"
"Arafu mwite Dk. Hamiyah aje amshugurukiye,"
"Sawa,"
Madaktari zaid ya kumi walijifungia humo ndani na kuanza kutoa huduma kwa wagojwa wote wawili,
Binti wa kihindi alikaa nje kusubiri kujua hatima ya Seif itakuwa nini kupona au kufa,
Akipoteza maisha nitafanya nini? Mwili nitaupeleka wapi simjui ndugu yake hata mmoja?
ila akiwa Muislam itakuwa rahisi nitatoa taarifa msikiti wowote ule watamzika,
ila kwa baadae ndugu zake wakijua si nitakuwa kwenye wakati mgumu?
Akiwa katika mawazo mengi Dokta Hamiya alitoka nje akauliza,
"Ndugu wa mgonjwa wa Mernah yuko wapi?"
"Nipo,"
"Na ndugu wa Seif?
" nipo,"
"Sawa tuwe hapo hapo Dokta Sharihiya anakuja kuwajuza hali za wagojwa wenu,"
"Sawa,". Wote waliitika.
Baada ya Dakika tano Dokta Sharihiya alitoka akiwa na madokta wote waliokuwemo humo ndani, ila sura zao ziriashilia habari mbaya,
"Ndugu zangu nasikitika kuwapa taarifa mbaya za wagojwa wenu siyo kosa letu kwani tumejitahidi kwa uwezo wetu ila tumeshindwa,"
"Tupe majibu acha kuzunguuka,"
MWISHO
Umeyaona Matangazo?
Yabonyeze Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Yabonyeze Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni