MUUZA CHIPS (1) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumatano, 17 Mei 2023

MUUZA CHIPS (1)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
📖 KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
😂 VIDEO za KUCHEKESHA
📑 MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA KWANZA
Jamani Simulizi hii, sio moja, bali zipo simulizi mbili ndani ya moja… Kuna simulizi yangu moja iliitwa MKE WA KAKA hio simulizi inaendana na simulizi hii ya MUUZA CHIPSI, hivyo sikutaka simulizi zangu ziwe zinajirudia, hivyo nimeiweka sehemu moja zote mbili, mana stori za simulizi hizi zinaenda.. Hivyo ukisoma jua kua unasoma simulizi mbili ndani ya moja… Ila simulizi halisi ni MUUZA CHIPSI ikifuatiwa na MKE WA KAKA ambayo nayo ipo humu humu ndani,. Na utaijua hapo itakapoanzia rasmi lakini mwanzo wa zote ndio, lakini pia MKE WA KAKA ina mwanzo wake huko mbele, hivyo nayo inaanzia hapa hapa……. Sasa ole wako uikose staki maswali mengi mana umekosa uhondo mwenyewe… Hivyo msije mkashangaa mke wa kaka kawa MUUZA CHIPSI….

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
MUUZA CHIPSI Ni simulizi inayomhusu kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la RASHIDI, Akiwa sambamba na kaka yake aitwae IBRAHIM kwa kifupi tutamuita IBRA, waliojaaliwa kupata mtaji wa CHIPSI jijini Arusha,… Ibra akiwa ndio kaka mkubwa katika familia yao aliikuwa akifanya kazi kwa bidii ili aweze kujikimu kimaisha na kuwatumia familia yake angalau kile kidogo akipatacho, Wazazi ama familia yake ilikuwa ikimuombea kijana ibra ili kazi ya mikono yake imuendee vizuri ili na wao waweze kufaidika, Kutokana na maombi ya wazazi kumuombea kijana wao,… Sasa Kijana ibara ambae ana umri usiopungua miaka 30 na alikuwa hajaoa bado, katka familia yao walizaliwa watoto watatu tu, Akiwemeo yeye mwenye umri wa miaka 30, Akifuatiwa na mdogo wake wa kiume mwenye umri wa miaka 22, Mama hakuishia hapo aliona ajaribu tena na tena na kufanikiwa kupata mtoto wa mwisho wa kike alioitwa HALIMA mwenye umri wa miaka 8 Sasa,.. Kijana Huyo ambaye ni mzaliwa halali wa mkoani Tanga katika mji uitwa PONGWE KIVUKONI huko mkoani Tanga,..

Ibra alichelewa kuoa kwasababu ya maisha hayajakaa vizuri katika upande wake, Ibrahim alikuwa ni kijana mpole sana na asiependa makuuu, Na biashara yake hio aliibuni sehemu nzuri kwani chipsi hizo zilikuwa zikiisha kwa kununuliwa na wanafunzi waliokaribu Na chipsi hizo,… Shule hio ilikuwa na wanafunzi weengi sana kana kwamba kijana ibra alikuwa akipika chipsi mara kwa mara, maana kuna muda wa wanafunzi na muda wa wateja wa kawaida, Alikuwa akipata shida sana kwakuwa alikuwa peke yake katika eneo hilo, na alikuwa akiuza vitu vingi kama vile, MISHKAKI, CHIPSI KUKU, CHIPSI MAYAI, NYAMA CHOMA, na vingine vingi ili kipato chake kiweze kumtosha yeye na familia yake ambayo inaishi mkoani Tanga tena kwa maisha magumu sana, kwani kijana ibra akiwa kakosa chochote cha kutuma nyumbani basi familia yote kule kijijini huenda vibaruani ili kujipatia kipato cha kujikimu kwa siku hio,..

Kijana ibra hakuwa akilala usingizi mzuri, kwasababu anafunga banda lake la chipsi mida ya saa nne au saa tano usiku, na kuamka saa kumi ya usiku au kumi na moja za asubuhi, kwa ajili ya maandalizi ya chipsi na vingine vingi ambavyo anavimiliki yeye mwenyewe…

Wateja wake walikuwa wakimiminika kila siku kuachilia wanafunzi, bado ana wateja ambao wanampa oda mbali mbali, labda mfano kwenye makampuni makubwa makubwa wafanyakazi na maboss wanataka baiti baiti, basi oda zote zinakuja kwa kijana ibra,.. Maisha yanazidi kwenda na anazidi kujizolea wateja wengi mana katika banda lake la chipsi palikuwa pasafi sana na paliimarishwa kwa ajili ya kazi hio,.. Kwa ndani ni sehemu ya kulia, kwa wale ambao wanakula papo hapo wana sehemu yao hapo hapo,.. Kila kiungo cha kuleta radha katika chipsi alikuwa nacho,.. Kijana ibra alikuwa hataki kuleta mchezo na biashara na alikuwa anajua kuihendo na kuwahendo wateja wake… Yaani hakuna aliokua anakula chipsi bure hata awe nani, haangalii uzuri wala umbo la mwanamke, kama unavyojua watoto wa kike kwa chipsi, heeeee balaa tupu yani,.. Haswa haswa huku mjini, lakini ibra yupo siriasi utafikiri hana viungo muhimu vya kuweza kushawishika na wanadada hao..

TUKIJA HUKU MKOANI TANGA, KATKA FAMILIA YA KIJANA IBRAHIM…

Tunaiona familia hio ikiwa juani tena ikiwa inalima shamba moja gumu sana lilionekana ni shamba la kibarua, yaani halikuwa lakwao bali lilikuwa ni la mtajiri mmoja alioajiri familia hio kuanzia mtoto mpaka baba,.. Lakini katika familia hii yupo kijana mmoja namuona, huyu sii mgeni sana machoni mwangu,… Anaitwa RASHIDI, tumemzoea kumuita Sharbiny au Sheby… Leo anaitwa Rashidi au ukipenda muite Chidi,.

Kijana huyu alikuwa akilima na familia yake lakini yeye peke yake ndie alieonekana kuwa na nguvu kuliko wote, na ni kweli mana alikuwa na mwili mwembamba kuasi chake, na mwili wake ulikuwa umegawanyika vipingili pingili haswaaa tumboni mwake,… Lakini ghafla tunamuona mschana mmoja aliobeba mtoto, akiwa anaelekea kule walipokuwa akina rashidi, mschana alikuwa ni mdogo na mzuri sana, lakini kachoka sana kutokana na maisha ya kijijini hapo, kijiji hicho kilihasiwa na mvua, hivyo kulikuwa kukavu kupita maelezo, yaan hali ya kijiji hicho ilikuwa ngumu sana,..

"mama na baba, chakula hiki hapa nimeleta"

Alikuwa ni huyo mschana sasa sijui ndio huyo rehema au vipi, mana rehema ana miaka 8 na huyu mschana hakosi kama miaka 18 hivi au hata 20..

Haikufika muda rehema ndio anatokea akiwa kabeba jagi la maji,.. Sasa huyo ndio rehema, je huyu mschana mwingine ni nani,..

Mama na baba pamoja na kijana Rashidi wanaacha kulima na kuja katika mti wenye kivuli na kuanza kula chakula cha mchana, ikiwa ni ugali tena ule wa dona jekunduuu, na bamia,…

"mzee tukimaliza kula hapa, tuhakikishe hii ungwe inaisha hii"

Ni sauti ya kijana chidi akimwambia baba yake ambae kidoogo wao ndio wana nguvu za kuifanya kazi hio, hao wengine kama mama, huyo anahamasisha tu lakini kwenye kulima hayupo kabisa..

"lazima iishe, kwani elfu 15 sio ndogo mwanangu inatutosha kabisa"

Ilikuwa ni sauti ya baba wa chidi akimjibu mwanae, wazee wa vijijini hao…

Unajua mzee mwenye miaka 50 huku kijijini ni tofauti na mzee wa miaka 50 kule mjini,… Kwanza wa kijijini amepigwa na maisha lakini ana nguvu, na yule wa jini itategemea na hali yake ya maisha, lakini nguvu hawezi kumkuta mzee wa kijijini,…

Kijana chidi walimaliza kulima kipande walichopangiwa, na kulipwa shilingi elfu 15 za kitanzania, yaa toka saa 11 asubuhi mpaka saa 11 jioni familia nzima inaingiza elfu kumi na tano, na hapo walipo wapo hoi, lakini ikitokea nyingine hawana budi kuifanya,… Famila ya mzee kingazi inarudi nyumbani ili kuweza kujipumzisha na kuangalia ya kesho,…

Maskini ya mungu nyumba yao iliokuwa ya nyasi tena mzee kingazi alijitahidi katika ujana wake, kwani alijenga nyumba ya tofari za kuchoma ila aliweka nyasi, kana kwamba hakuwa na uwezo wa kununua bati, kijana chidi alifika hapo nyumbani kwao na kuanza kuiangalia nyumba yao, huku akisikitika kwa hali ngumu ilioikumba boma lao,

Inaonekana vijana wote Ibrahim na rashidi wote walikuwa na uchungu wa maisha,…

Kila wanafikiria boma lao hua hawaba raha kabisa kwani wao ni tofauti na majirani zao, mana majirani zao nao wana watoto wao ambao wanawatunza wazazi wao, akiangalia nyumba za jirani zao zimejengwa kwa bati kasoro wao tu, na wengine wenye maisha duni kama wao,..

"mume wangu, maji tayari"

Ghafla saut8 inasikika ikimuita kijana rashidi aliokuwa akiyafikiria maisha ya hapo kijijini kwa, ni kijana mdogo sana aliozaliwa mwaka 1994 tena mwishoni mwa mwaka huo, hivyo hata miaka 22 yenyewe bado hajaitimiza,.. Lakini sasa mbona hapa kaitwa mume wangu, ina maana kijana huyu ana mke kabla ya kaka yake aliekuwa mjini,.. Na sheria ya Kisambaa huko tanga, inatakiwa aoe kaka mkubwa kwanza ndio aoe mdogo, sasa nashangaa kuona kijana chidi ana mke kabla ya kaka yake,… Na mke mwenyewe ndio yule tuliemuona kule shambani akiwa kabeba kapu la chakula, mschana mdogo na mzuri sana…

Mschana huyo alimshika kiuno mumewe ili kuweza kumfariji mana aligundua kuwa mume wake yupo katika dimbwi la mawazo mengi sana ya kimaisha,…

Mschana huyu alimuuliza mumewe kuwa

"baba king (kingazi) Kwanini upo hivyo mume wangu"

Alikuwa ni mschana huyo aliemtukuza mumewe kwa jina zuuri la mtoto wao

"Salma… Ivi haya maisha we huyaoni"

"nayaona sana tu, ila tutafanyeje na ndio haya haya, hayana mabadiliko tena"

Chidi alikasirika kuskia mke wake anamuambia hayana mabadiriko, kwani yeye chidi anaamini lazima maisha yabadirike,

Lakini chidi hakutaka kumuonyesha mkewe kuwa kakasirika kwa lile neno lake la kukatisha tamaa..

"salma"

"abee"

"ivi wewe apo ulipo una umri gani"

"lakini si unaujua baba king"

"yes.. Ila nataka unitaamkie wewe"

"ok.. Nina miaka 18"

"sasa miaka 18, kwanini unakata tamaa ya maisha kiasi hiki"

"nisamee mume wangu, labda nilikosea, na huenda nimekukatisha tamaa, naomba unisamehe sana"

"usijali… Yote ni maisha tu"

Basi kijana chidi anaingia bafuni kama alivyoambiwa na mke wake,… Kijana huyo alimaliza kuoga na kutoka nje ya bafu na kuanza kuliangalia lile bafu alilotoka kuoga muda sio mrefu,.. Aliliangalia kwa uchungu sana kwani lilikua bafu liliozungushiwa visalfeti na majani, yaani hali yao ilikuwa duni sana na inashangaza sana kaka yao anapiga bingo mjini alafu huku wanaishi hivi, daahh kweli inauma sana,……

*

"shika hiki kirungu, kakichomeke katika siri ya mke wako, na hio hirizi ilioishika nyota yako itatoka"

"heeeeeee mzeee rungu lote hili mzee na siri ya mke wangu ni ndogo sana"

"sasa bila hili rungu kuingia hio hirizi haiwezi kutoka kamwe na mtakuwa maskini mpaka kufa kwenu"

"ok hakuna dawa nyingine ya kuweza kuitoa hio hirizi bila kuingiza hili lirungu"

Kijana chidi alikua kalishika lile rungu lenye uwezo wa kuitoa hirizi iliomo ndani ya uke wa mke wake… Na rungu lilikuwa ni kubwa kupita kiasi,..

"kama huezi kazi hio, weka rungu langu chini na uondoke zako"

Mganga alipaniki na kumtishia kijana huyo..

"Nimekubali kuliingiza rungu hili katika siri ya mke wangu,.

Kijana chidi aliingia ndani ya kageto kake ambako kamejitenga kama hatua tano hivi kutoka nyumba kubwa ambayo ni ya wazazi wake, nae akajenga kadogo kwa pembeni,.. Mambo ya kijijini hayo, kwa wale walioshi kijijini kwa muda mrefu, huezi shindwa kujua haya mambo, lazima uwe na kageto kwa pembeni ya wazazi wako,… Geto ya kijana chidi ilikuwa imependeza kwa ndani kwani waliipamba kwa magazeti, na kuleta mwonekano mzuri,…. Mkewe alikwenda kupika nyumba kubwa nae akabaki anacheza na mtoto wake King au kingazi jina la baba ya rashidi,… Chakula kiliiva na mkewe alileta chakula huku geto kwao na kuanza kula…

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni