DHAMANA (15)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mwandishi: Hassan O Mambosasa
SEHEMU YA KUMI NA TANO
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
"Vizee vingine bhana vinadhani kila gari ni ya kubeba watu masikini kama wao, akapande basi huko asinisumbue mimi" Falzal aliongea kwa dharau kisha akaongeza mwendo zaidi.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
"vijana wengine bhana wanadhani kila mali inaweza ikadumu bila kujali imepatikana kwa njia gani, wakatafute kupitia jasho lao wenyewe" Ilisikika sautu ikitoka kwenye kiti cha nyuma cha gari hilo na ikamfanya Falzal ageuke nyuma huku akiwa ameachia usukani, loh! Sallaleh alimuona yule mzee aliyempita pale barabarani akiwa amekaa kwenye kiti cha nyuma akiwa amekunja nne akiwa na mavazi yake machakavu aliyomuona nayo pale njiani wakati anampita. Falzal alizidi kupatwa na uoga sana kwani haiwezekani mtu akiyempita njiani tena kwa mwendo wa kasi amkute ndani ya gari yake, alibaki akimtazama huku akitetemeka kwa uoga hasa alipoona tabasamu la yule mzee.
"Kijana kamata usukani utagonga huoni kama tupo kwa Minchi tunaelekea kwenye ule mzunguko tena kuna tuta mbele, dereva gani usiyekuwa na umakini uwapo barabaranu wewe tena punguza mwendo maana tunaingia katikati ya jiji magari ni mengi" Yule mzee alimwambia Falzal huku akutabasamu na mahali alipomtajia Falzal palikuwa ni mahali ambapo ni mwanzo kabisa alipapita hata kabla hajafika Majani mapana.
Falzal alipoangalia mbele kweli aliona anakaribia kwenye tura na alipunguza mwendo haraka sana na akalipita tuta kisha akashika usukani vizuri akawa anaingia kwenye mzunguko wa kwa Minchi. Falzal alilizungusha gari kwenye mzunguko huo ili arudi alipotokea katika barabara kuu iendayo Segera, alipotaka kunyoosha tairi kisha akate kidogo aingie barabara ya hiyo ambayo alitokea kuingia mzunguko huo wa kwa Minchi alijikuta akishindwa baada ya usukani kugoma na hivyo akazunguka tena ule mzunguko na gari ikaingia katika barabara kuu iendayo Mombasa.
" Huwezi ukatoka nje ya Tanga hata kwa namna gani , ulidhani ukimaliza hiyo roundabout ya Kwa Minchi utaweza kurudi kule ulipokuwa unaelekea. Sasa umeula wa chuya kijana" Yule mzee aliongea huku akitabasamu.
"we...we.....wewe ni nani?" Falzal aliuliza huku akitetemeka na alikuwa akimuangalia huyo mzee pamoja na kuangalia mbele ili asipate ajali, uoga uliokuwa umeibugika nafsi yake ulimfanya ashindwe kutambua kama gari hiyo ilikuwa inaenda yenyewe kwa mazingira ya ajabu pasipo yeye kuiendesha.
"Achia usukani kijana maana unajisumbua gari hiyo inaenda yenye na si wewe unaiendesha na si unataka kunijua mimi ni nani sio?" Yule mzee aliongea kisha akaongea akajibadilisha akawa na sura ile ya mtoto ambayo iiliwatokea kaka zake muda mfupi kabla hawapoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha.
"Jamadin! Ha..pana siyo we..we" Falzal aliongea huku akitetemeka kwa uoga kwani hakutarajia kumuona aliyemuona hapo.
"Unashangaa kuniona mimi? Ha! Ha! Ha! Kwanini usijishangae kwa kuhusika kufanya maisha ya mwenzako aliyeumbwa kama wewe kuwa duni" Yule mtoto aliongea kwa sauti yenye kukwaruza tena alicheka kicheko kisichokuwa kinaashiria furaha kwani machoni alishaanza kutoa damu.
"Kutumia nguvu za wenzenu kujitajirisha mliona raha sana sasa leo ni zamu yako Falzal ambaye hupaswi kuitwa baba mdogo kwa mabaya uliyonifanyia" Yule mtoto aliongea huku akilia kwa machozi ya damu
"Si.....siyo mimi Jamadin ni kaka ndiyo aliyekukosea na ndiyo aliyepanga kila kitu" Falzal aliongea kwa uoga.
"Huna cha kujitetea kwa sasa kitachoweza kufanya nikusamehe wewe mwanaharamu, kwanza nipe ukitaka ufe kistarabu la si hivyo nakurarua kama Simba anavyorarua nyama ya swala" Yule mtoto aliongea kwa hasira hadi miale ya moto ikawa inamtoka mdomoni mwake.
"Ni...nikupe nini Jamadin?" Falzal aliuluza huku akiwa anazungusha macho yake kuangalia kama anaweza kupata upenyo wa kukimbia lakini hakukuwa na upenyo wa kutokea kwani milango ilikuwa imefungwa na vioo vimebanwa hadi mwisho.
"Mmmhu! Yaani hilo suala la kunitoroka usifikirie kabisa, nimesema nipe kile kinachowafanya muwe matajiri kila kukicha na kile kinakufanya uwe na bahati kila ukicheza kamari" Yule mtoto aliongea kwa hasira sana.
"sinacho mimi Jamadin anacho..." Falzak alijitetea na alipotaka kumtaka mwenye kitu kinachotafutwa na huyo mtoto lakini alijikuta akikabwa kooni baada ya huyo mtoto huyo kumnyooshea kidole.
"sijakuambia umtaje huyo aliyenacho, sasa nilikuambia nakurarua ukiwa huna na sitengui kauli yangu" Yule mtoto aliongea kisha akatoa makucha mikononi akaanza kumrarua hadi mwili wa Falzal ukawa ni damu tupu tu na vidonda kila sehemu ingawa roho yake haikuachana na mwili na maumivu ndiyo yalitawala mwili wake wote, alipiga makelele akilia kama mtoto mdogo lakini hakukuwa na mtu aliyesikia kulio chake kwa muda huo.
"Sasa wasalimie ndugu zako waliokuwa wametangulia kaburini nadhani watakuwa wanakungoja huko walipo" Yule mtoto aliongea kisha akatoa moto mkubwa wenye mlipuko mithili wa bomu ambao ulisambaa gari zima
Hadi muda huo tayari gari la Falzal lilikuwa limeshafika maeneo ya Kisosora kwenye matanki ya mafuta ya kampuni ya BP iliyopo jirani na bahari ya hindi, yule mtoto alipopuliza ule moto gari lote lilipuka na likarushwa juu hadi ndani ya maji na hu ndiyp ukawa mwisho wa maisha ya Falzal ndani ya dunia na ukawa mwanzo wa maisha mengine nje ya dunia hii katika ulimwengu usionekana kwa macho ya kawaida.
****
Hali ya Shafii kiafya iliendelea kuwa nzuri na hadi muda huo alikuwa tayari amesharuhusiwa na yupo nyumbani akiuguzwa na mke wake, huzuni kubwa ilkuwa ni sehemu iliyoutawala moyo wake hasa akikumbuka vifo vya wadogo zake. Hakuwa na la kufanya kwa muda huo kwani yeye alikuwa ni mtu wa kutembea na baiskeli ya walemavu kwani kiuno kilikuwa ni sehemu iliyopatwa na kadhia katika ajali ile iliyomkuta na ingemchukua muda mrefu mpaka kutengemaa na kuwa na hali ya kawaida kama ilivyokuwa hapo awali. Hadi muda huo si yeye wala familia yake waliokuwa na habari na jambo lililomkuta Falzal tangu alipowaaga anasafiri kuelekea Arusha akitumia gari binafsi, hawakujua akama falzal ni mmoja wa marehemu kwa muda huo.
Kusononeka, kuhuzunika na kuumia moyo ndiyo jambo ambalo lilikuwa likimsumbua Shafii kila siku hasa alipowakumbuka ndugu zake na jambo lile aliloambiwa na sauti asiyoitambua kuhusu mwanae wa pekee Zayina kuwa ametekwa na yupo chini ya adui yake ambaye hamtambui hadi muda huo aliwahi kumfanyia ubaya upi kwani hakuna dui yake mwenye ubavu wa kumfanyia mambo hayo kwa mujibu wa mganga wake marehemu Sauti ya radi kama alivyomuambia.
Alikuwa akimiliki cheni yenye kidani chenye kito kisichofahamika hapa duniani ambayo ndiyo ilifanya awe na nguvu miongoni mwa maadui zake na pia kidani hicho kilikuwa na uwezo wa kuwalainisha mioyo wanadamu wenzake ambao walitaka kufanya jambo baya kwake au kwa jamaa zake. Fikra zilizokuwa zipo kichwani ni kuwa adui aliyekuwa anamfanyia ubaya alikuwa ni mwanadamu wa kawaida na hakuwahi kuwaza kama kuna jini anayeweza kumfanyia hivyo kwani fikra zake zilimpa asilimia mia moja kuwa hajawahi kumfanyia ubaya jini katika maisha yake zaidi ya kuwafanyia ubaya wanadamu wenzake tu.
"ni nani huyu na ana shida gani na mimi kwani hata cheni niliyokuwa nayo inashindwa kumtambua hata kidogo.Jamadin,gasper,Hilson na wengine wengi niliowahi kuwafanyi ubaya tayari wametangulia mbele za haki" Shafii alijiuliza katika nafsi juu ya utata wa tatizo linalomsumbua la kuondokewa na watu anaowapenda.
"Eeeh! Mungu nimekosa nini mja wako nipo njia panda mja wako" Kwa mara ya kwanza Shafii alijikuta alijikuta akimtaja muumba baada ya kukaa kwa kipindi kirefu akimuasi mwenyezimungu kwa kumtegemea mwingine tofauti na yeye, maneno yake yalisikiwa nyema na mke wake ambaye alikuwa yupo nyuma yake akimtazama mumewe wake kwa masikitiko makuu jinsi anavyolalalmika kwa Mwenyezi mungu.
Bi Farida muda wote huo akimtazama mumewe kwa jinsi anavyolalamika alijua ni kutokana na vifo walivyokufa wadogo zake, wala hakutambua kama mumewe alikuwa akiteswa na sauti ya mbaya wake ambaye alikuwa hamtambui. Machozi yalipoanza kutiririka katika macho ya Shafii. Hali ya Shafii ilimfanya Bi Farida amkumbtie kwa nyuma kisha akambusu shavuni kwa upendo halafu akamwambia,"Baba Zayina kazi ya Mungu haina makosa yapasa kumshukuru katika kila hali kwani amekujalia uzima katika ajali mbaya uliyoipata, haipaswi kumlaumu kwakuwa ndugu zako wamepoteza maisha mpenzi wangu"
"Mke wangu inauma sana nahisi dunia yote nimeangushiwa mimi inauma.....inauma sana" Shafii aliongea huku machozi yakimtiririka machoni mwake.
"Ha! Ha! Ha! Ha! Nadhani unatambua ule msemo wa waswahili waliosema kwamba jeraha la kujitakia halihitaji pole, sasa usitegee pole kwa mtu ambye baadaye akija kukujua upande wa pili wa maisha atakuacha na janga lako mwenyewe. Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Mwanao Zayina najiandaa kuwapikia supu mbwa wangu wamle nikishamchinja" Sauti ileile iliyompa taarifa ya kuwa kuna jambo baya lnalotaka kutokea kwa mtoto wake ndiyo ilimpa taarifa iliyomfanya ashtuke
"He! Baba Zayina kuna nini mbona unashtuka hivyo hadi unanitisha mume wangu" Bi Farida aliuliza
"Nimejitonesha sehemu ya mgonogni mke wangu kutokana na kusononeka huku" Shafii aliamua kudanganya huku akiuma meno kwa maumivu kana kwamba alijitonesha kweli kumbe alishtushwa na sauti ya adui yake mkuu ambaye aliyewahi kumlea mwenyewe kwa mikono yake bila kujua ambye alimwambia jambo baya ambayo ameazimia kwenda kulifanya kwa binti yake kipenzi aliyempenda.
Laiti kama wanadamu tungalipewa uwezo wa kuona yaliyojificha katika mioyo ya wenzetu basi Bi Farida angeliomba talaka mapema sana lakini Mungu muumba hakutupa uwezo huo wa kuona yaliyo katika mioyo ya wenzetu ndiyo maana Bi Farida hakutambua jambo linalimtatiza. Ama kweli moyo wa mtu ni kiza nene zaidi hata ya giza nene lililotanda kwenye pori nene katika usiku mnene, mungu muumba alikuwa na maana yake sana kutuumba wanadamu kwa kuficha yaliyopo mioyoni kwani hadi muda huo tayari wanadamu tungekuwa tushafarakana kama tungebaini yaliyopo kwenye mioyo ya wenzetu.
****
"ngoja nikuwahishe ndani mume wangu ukanywe zile dawa na upumzike" Bi Farida aliongea huku akianza kuburuza kiti cha matairi cha mumewe huku akiita, "Jamali! Jsmali!".
"naam!" Sauti kutoka ndani ya chumba kimojawapo ilisikika ikiitika.
"njoo unisaidie kumuweka kitandani mjomba wako" Bi Farida alimuambia yule mtu aliyemuita huku akikisukuma kiti cha matairi kuelekea chumbani kwake, muda huo Shafii alikuwa bado ameuma akiweka maumivu yake ya kuigiza ili azidi kumchota mke wake akili ajue ni kweli ameumia.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni