DHAMANA (26)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mwandishi: Hassan O Mambosasa
SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Nakumbuka mara mwisho Faiz alimfuata Farida kisimani akalazimisha penzi na matokeo yake yalikuwa ni mabaya, kwani Farida alipiga kelele za kuwa anabakwa na sisi tuliokuwa karibu tukamvamia na kuanza kumpiga na baadaye watu waliongezeka hasa vijana wanaomchukia ambayo walimpiga sana kisha akapelekwa kwa kiongozi wa kijiji.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Wazazi wake waliitwa wakaelezwa juu ya hilo ambalo lilikuwa ni aibu kwao na jambo llililowakera, baada ya siku kadhaa kiongozi wa kijiji alimfukuza Faiz katika kijiji na ikawa ni furaha kwa vijana wa kijiji hicho pia huzuni kwa wasichana waliompenda kwani hakuwahi kuonekana hadi leo hii".
Hadi anafikia kituo kueleza juu ya hilo tayari Bi Farida alikuwa analia kwa kwikwi baada ya kubaini jambo alilofanyiwa na Shafii, Zayina naye alisikitishwa sana uovu alioufanya baba yake. Zalabain hasira zilimpanda zaidi hadi macho yakawa mekundu lakini hakufanya lolote juu ya hilo kutokana na kuzuiwa na mzee Mahmud, hasira zilipomzidi Zalabaun machozi yalimtoka na akawa anatetemeka hadi midomo ikawa inacheza.
Upande wa mzee Buruhan hasira zilimpanda kwa ujinga wa mwanae lakini alipotaka kuongea Mzee Mahmud alimzuia kutokana na masharti aliyowapa, mzee Mahmud alitazama hali za watu waliomo humo ndani na mwisho wake akayatuliza macho yake yaliyozungukwa na ngozi iliyofunyaa kutokana na uzee kwenye uso wa mzee Buruhan. Alimtazama mzee mwenzake halafu akasema, "mzee mwenzangu nadhani unakumbuka zaidi kile kisa nilichokusimulia nikitumia mafumbo pia nikiongeza chumvi ili usijue na nilikuambia muendelezo wake utaujua sasa usikilize huo muendelezo wake leo. Nilitia chumvi kukuambia hakuna aliyejua usiri wa penzi la Giguna ambaye ndiye huyu Farida na Mufeji ambaye ni Faimu ila ukweli ni kwamba kuna mtu mwingine ambaye alikuwa anajua ambaye ninampa Nikuza ambaye ni mdogo wa mwisho wa Nukeze au Shafii mdogo huyo ukipenda muite Ally. Haya Ally tusimuulie kile unachojua katika uhusiano wa Farida na Faimu".
Ally aliposikia maneno hayo alimtazama sana kaka yake kwa chuki kisha akamtazama Bi Farida kwa huruma sana halafu akafunguka kile anachokijua, "Baada ya mimi kuanza kupevuka tu tayari Faimu alikuwa ni mwenyeji ndani ya kijiji chetu na alikuwa ni rafiki wa huyo firauni wa kizazi hiki, Faimu namkumbuka kama mtu aliyenizidi umri ambaye alikuwa anapenda kukaa na mimi na hakutumia udogo wangu kwake kuwa sababu ya kunitenga kama ilivyo hao ndugu zangu.
Nilimpenda kutokana na uchangamfu wake na hata kunishauri mambo mengine katika umri huu wa upevukaji tofauti na wengine walioniacha nikacheze na watoto wadogo walionizidi umri kwa kisingizio kuwa sijakua, katika kipindi hicho niliomba ushauri kwake pia baada ya huyu Salma niliyemuheshimu kuanza kunitaka kimapenzi na alinishauri vizuri nimkatae. Siku moja nakumbuka niliwakuta Farida na Faimu wakiwa wamekaa kihasara sana niliyeambiwa ni shemeji yangu, iliniuma sana ila nilikuwa kawaida baada ya kujua juu ya uhusiano wao na nilipotambua kuwa hakuwa shemeji yangu kama nilivyoambiwa.
Niliukubali uhusiano wao kwa mikono miwili na niliufanya siri yangu kutokana na kaka zangu kutonihusisha katika yao, hata Salma alipokuja kuniambia juu ya kubaini hilo nilimuambia wamependana hivyo uwaache ingawa yeye alisema anaenda kumuambia mchumba wake na mimi nilipuuzia tu kwani namjua huyo ni mmoja kati ya wasichana walioenda nyumbani kwa mzee Mubaraka ili tu aonekane na Faimu kwakuwa anamtaka. Siku moja ndipo huyuhuyu Salma aliyekuwa ananitaka aliniletea taarifa ya uhusiano mpya wa Farida na Shafii ambao umeanza , nilienda kumuuliza Faimu juu ya hilo na akanibainishia kuwa Farida hamtaki. Sikutaka kuamini moja kwa moja nikamfuata Farida mwenyewe kwani alikuwa ananiheshimu na mimi namuheshimu, sikujali ndugu yangu kumpata ila niliangalia yule aliyenijali zaidi hata ya ndugu anavyonijali akiumia mimi iliniuma pia kwani nilimuheshimu sana.
"Farida umekuwa vipi? Si uliniambia wampemda Faimu wewe ni nini kimekupata?" Nilimuuliza Farida.
"Sikumpenda Faimu ila nilipotea njia ila sasa simronda(simtaki)" Farida aliniambia tena mwishoni akazidi kuniwekea msamiati wa kidigo akiniambia hamtaki.
"Farida kumbuka ulisema Faimu ndiyo chaguo lako leo umehamia kwa kaka yangu tena" Nilimuambia Farida nikiwa hata simuelewi.
"haaaa! Ally aaambiwa mimi huyo Farida mchetu(binti) wa Jumanne nimesema hivyo? Ally nampenda Shafii na sikumbuki Faimu nilimpenda vipi, niheshimu kama shemejio kwa kaka yako kama ninavyokuheshimu" Farida aliniambia neno hilo ambalo lilinichanganya na nikampelekea taarifa Faimu ambaye pia alionekana kuchanganywa ila zaidi yangu. Baada ya muda zilinijia taarifa za kutaka kumbaka Farida na nilienda kumshuhudia hiyo siku anayopigwa na roho iliniuma kutokana na jinsi alivyonipenda, baada ya kupona majeraha yake Faimu alikuja kuniaga akahama kijiji na sikumuona tena hadi leo hii na niliendelea kumuheshimu Farida kama alivyoniambia nimuheshimu. Baada ya...."
"Basi Ally ishia hapohapo kwa kusimulia unachojua juu ya kaka yako......Mzee mwenzangu umesikia hayo yanayosemwa nataka uujue muendelezo wa kisa chetu hadi mwisho. Salma wewe ueleze ukweli wote siku ya kwanza kumuona Faimu jua ukidanganya yatakayokupata shauri yako kuna nguvu kubwa hapa" Mzee Mahmud alimkatisha Ally kisha akamgeukia Mzee Buruhan akamuambua maneno machache, alipomaliz alimgeukia Salma akuambia asimulie na akamuonya juu ya usemaji uongo.
Salma aliposikia hayo maneno alijifikiria kwa muda mfupi kisha akaanza kusema, "Baada ya Faimu kuwasili kijijini kwetu nilimuona ni mstarabu kumbe ni mshenzi kupi...". Salma alishindwa kumalizia kauli yake baada ya eneo alilokaa kutokeza shimo kubwa kwa nyuma na nguvu kubwa ya upepo ikawa inamsukuma kuangukia kwenye hilo, alipiga kelele akijua wenzake wameona kule alichokiona kumbe alikuwa amekiona yeye, Mzee Mahmud na Zalabain tu. Kelele zake ziliwashangaza wengine wote waliomo humo kasoro waliiona kilichomtokea, Zalabain naye aliposikia kauli ya Salma hasirs zikampanda ila alishindwa kunyanyuka baada ya nguvu kubwa iliyopo hapo kumzuia. Mzee Mahmud alinyoosha mkono akatamka maneno yasiyoeleweka na lile shimo likapotea, hali ya kawaida ikarudi kama awali huku Salma akawa anahema kwa uoga.
"Kwanini unakuwa mbishi binti si nimekuambia uache kusema uongo unadhani hii ni sehemu ya kudanganya, nimekuambia kuna nguvu nzito hapa au huelewi? Sasa rudia tena iwe mwisho wa maisha yako" Mzee Mahmud aliongea kwa hasira halafu akamgeukia Zalabain akamwambia, "Huna nguvu ya kufanya hivyo bila nguvu zilizopo hapa kukuruhusu kufanya unachotaka kufanya hivyo tulia kwanza usiendekeze hasira mbele ya nguvu kubwa".
"Haya endelea kusimulia na uwe mkweli" Mzee Mahmud alisema.
Salma aliposikia kauli ya mzee Mahmud hakuwa na ujanja zaidi ya kusimulia yaliyompata akiogopa kufa na aliongea, "Urafiki wangu na Farida ni wa siku nyingi sana na yeye alinijua kama wifi yake mapema kabla ya waru wote kujua, hata shemeji Shafii alipoanza kumpenda alinisihi nimbembeleze ili akubali na mimi nilifanya hivyo lakini aliendelea kushikilia msimamo wake uleule wa kutokibali kuwa na Shafii.
Nilijitahidi sana mwisho nikachoka nikaamua kuacha na nikawa namuonea huruma sana shemeji yangu kwa jinsi anavyoumia, baada ya muda kidogo kupita ndipo familia ya Faimu ilipoingia hapo kijijini kwetu na nilipomuona Faimu kwa mara ya kwanza nilijikuta nampenda na nilitaka kuwa naye kwani nilishazoea kukaa na kutembea na wanaume mbalimbali na nilianza haya hata kabla sijampata Hamis na nilipokuja kumpata nilitulia ila nilijikuta nikiirudia tabia yangu hiyo kwa mara nyingine tena niliifanya kwa mara mbili tofauti. Mara ya kwanza nilianza kwa Faimu nikawa najipitisha sana kwao ili anuone nikijua nitamnasa tu kama nilivyonasa vijana wa hapo kijijini kumbe Faimu hakuwa kijana wa hivyo, uvumilivu uliponishinda niliamua kumuambia ukweli lakini pia nilimkosa baada ya kukataliwa na akanitishia kumuambia Hamis.
Mara ya pili niliirudia tabia yangu kwa kumtaka Ally baada ua uzuri wake kuonekana alipofikia kwenye balehe lakini pia alinikataa nikajikuta nazidi kumsumbua nikijua nitampata tu kwani ni mtoto yule bado akili haijapevuka zaidi ya kupevuka mwili tu, nilipoona nakataliwa sikuchoka na niliamua kuanzisha mazoea ya kawaida naye. Siku nilipokuja kuwafuma Farida na Faimu na wote wakakiri kuwa wana uhusiano ndiyo siku niliyoona ya kutumia sababu hiyo kwa njia mbili, kwanza ni kulipa kisasi cha kukataliwa na Faimu na pili ni kumteka Ally kiakili. Nilijua Ally ni bado ana akili za kitoto hivyo nilipanga nimuambie hii habari ili ajue ni jinsi gani nampenda hadi nikaamua kumuambia hiyo habari ili aamini moyo wangu upo kwake, pia nilitaka nimuambie mpenzi wangu juu ya usaliti wa rafiki yao kwao waweze kumfanyia kitu kibaya ili nimcheke na hata amkose Farida.
Sikutaka kurudi nyuma katika azma hii ambayo niliiweka na hapo ndipo nilipoona ni nafasi nzuri ya kuweza kujipa furaha niliyokuwa naitaka, nilianza kutimiza azma hii kwa kumuambia Ally juu ya uhusiano wa Farida na Faimu nikijua na yeye ataumia akisikia kaka yake ameporwa tunda alilokuwa akilitaka kila siku ili aweze kulimiliki katika mkono wake. Tena nilijifanya naongea kwa hisia zaidi ili nimteke akili zaidi kwa kuamini huyu bado ni mtoto, nilimuambia lengo la kumuambia hiyo habari ni kutokana na jinsi gani nampenda na sipendi aumie akisikia kaka yake ameumia kwani na mimi nitaumia pia kutokana na jinsi ninavyompenda yeye.
Nilizidi kuongea kihisia kwa kumuekeza ni jinsi gani namuamini mpaka ikafikia kumuambia hayo mambo kwani nilihisi ndiyo mahali salama ya moyo wangu, nilijivika ujasiri tofauti na watoto wengine wa kike nikiwa naeleza hayo maneno ambayo nilijua kabisa kwa mtu kama Ally mwenye kusumbuliwa na mihemko ya upevukaji basi nitaweza kumpata kirahisi jambo ambalo lilikuwa kinyume na nilivyotarajia.
Baada ya kutua maneno yangu yote niliyokuwa nimeyapanga kinywani mwangu Ally alinitazama sana kisha akaniuliza, "hivi watu wakipendana na wenyewe wakiridhiana kuna haja ya kuwafuatilia?"
Nilimjibu, "hakuna haja ya kuwafuatilia".
Jibu langu hilo nilimjibu kirahisi tu kwani bado nilimuona mtoto na ana itikadi za kitoto hivyo sikuhofia kabisa kama ataongea neno jingine kwa jinsi anavyompenda kaka yake, nikiwa nasubiri ni nini atasema kifua chake kilipanda na kushuka kuashiria anashusha pumzi ili aongee kitu ambacho niliamini kabisa atakuwa ameguswa na maneno yangu.
"Sasa kama hakuna haja ya wafuatilia basi Farida na Faimu nao wamependana haina haja ya wafuatilia waache na mapenzi yao na pia usitegemee nitaumia kwa jinsi kaka yangu anavyolazimisha kupenda kwa Farida ikiwa hatakiwi.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni